Kwa jinsi binadamu tulivyo, tunaweza kuona vitu vyote ambavyo havionekani mbele ya macho yetu. Ukifuatilia kwa undani unagundua kuwa vitu ambavyo tunaambiwa na kuamini kuwa havionekani, kiuhalisia vitu vyote vyaweza kuonekana endapo ukiamua. Kwa mazoea, wengi tunafikiri kwamba kama kitu hakionekani mbele ya macho yetu ya kawaida, basi tunasema...
Ajabu na kweli ni kwamba, mtu asipoona kitu kwa macho yake ya kawaida,
basi udhani kwamba kitu hicho hakionekani na wengine ufikiri kwamba kitu hicho
hakipo kabisa duniani. Kumbuka kuwa kuendelea kufikiri na kuamini kwamba kitu
fulani hakionekani au hakipo haina maana kwamba hakionekani kwa wengine! Wewe
usipoona wengine wanaona.
Tunapodhani kwamba kitu fulani hakipo duniani, wakati kipo, moja kwa
moja tunapoteza uwezo wetu wa ndani na nje wa kukifanya kile kisichoonekana
kionekane mbele ya macho ya wengi.
Kwa binadamu ni akiri yake pekee iliyo na uwezo wa kuona vitu vyote
vinavyoonekana na visivyoonekana. Unapofikiri kwa kutumia akiri (ubongo), hapo
tunasema kuwa umeona kwa macho ya akiri au ubongo. Pia, kile uonacho kupitia fikra
zako, ndicho ambacho ukusukuma wewe kutumia rasilimali zilizopo, ili kukiweka
katika uhalisia.
Kitu kikishakuwa kwenye uhalisia, basi hapo tutasema “umefanya kwa
vitendo au umetenda”. Ukisha tenda, maana yake ni kwamba, unakifanya kile
ambacho kilikuwa hakionekani mbele ya macho yetu ya kawaida, kionekane sasa machoni
mwa wengi. Endapo watu wataona kile ulichotenda, wasijidanganye kuwa “wameona
BALI wajue wametazama”.
Kuna tofauti kubwa sana kati ya “kuona”
na “kutazama”. Kutazama siyo kuona, na
kuona ni zaidi ya kutazama. Dhana nzima ya “KUONA” ni pale tunapoweza kutumia
akiri kuota ndoto, halafu tukapiga picha, halafu tukapanga, tukaamini, na kisha
tukatenda.
Kwa maana nyingine ni kwamba, akiri (ubongo) ni kiwanda na karakana
ya kuzalisha mambo mapya. Lakini pale tuonapo picha ya kitu kutokea nje (kwa
macho ya kawaida), basi huko siyo “kuona” bali ni “KUTAZAMA”.
Binadamu wengi tunao uwezo wa kuona kila kitu endapo tunataka kufanya
hivyo. Pamoja na uwezo mkubwa tuliopewa, bado hatuutumii katika kuona fursa za
kujiondoa kwenye majanga ya umaskini.
Watu waliofanikiwa mara nyingi wanatwambia
kila siku kuwa popote tulipo Tanzania tumezungukwa na fursa nyingi. Kwanini
sasa watu wengi ni maskini katika nchi iliyo na fursa nyingi? Jibu ni moja tu
nalo ni “watu wengi hawaoni fursa
bali wanatazama fursa”.
Utajiri wa uhakika hautapatikana kutokana na watu wengi kutazama fursa
BALI ni pale tu watu watakapoweza kutumia akiri zao kuona fursa na kisha kuanza
kuchukua hatua za maksudi ili kuzifikia fursa hizo.
Kumbe watu wengi tumekuwa ni watu wa “kutazama” fursa na siyo “kuona”
fursa. Unapoona fursa unakuwa na ujasiri, nguvu na shauku ya kutenda ili
kufaidi fursa husika. Lakini unapotazama fursa, mara nyingi unajawa sana na
uoga, hofu inayotokana na wewe kukosa majibu muhafaka ya maswali unayojiuliza
baada ya kuona kwa macho yako kile kilichofanywa na wenzako.
Unapotazama kitu kilicho mbele ya macho yako, mara nyingi utajiuliza
maswali mengi bila majibu juu ya jinsi kilivyotengenezwa. Unapokosa majibu
sahihi ya mswali yako, mara nyingi utapata hitimisho moja tu! Nalo ni “HAIWEZEKANI”.
Ukishajiridhisha kuwa haiwezekani, basi unaamua kwenda kutazama fursa nyingine
ambayo nayo utapata hofu na woga wa kuifanyia kazi. Mwisho wake unaishia kuwa
ni mtu wa kutazama na kuongea tu! Huku ukizidi kuandamwa na maisha ya taabu na
umaskini.
Watu wenye kuona fursa ndio wenye “maono”. Maono ni ndoto kujumlisha na
ukweli wa mambo. Ukiwa na maono yafanyie kazi. Tumia macho ya akiri au ubongo
kuona fursa.
Ukitumia macho ya ubongo au akiri, utaweza kuona vinavyoonekana na
visivyooekana. Fursa za uhakika hazionekani kwa macho ya kawaida.
Usipoona
fursa machoni mwako haina maana kwamba fursa hizo hazipo! ni uhamuzi wako tu!
ukiamua zionekane na ziwepo basi, itakuwa hivyo.
Lakini, ukiamua zisiwepo basi,
hazitakuwepo wala hazitaonekana mbele ya macho yetu ya kawaida. Jambo hili
aliwahi kulisisitiza mwanafalsafa wa Kifaransa aliyejulikana kama Henri Bergson
kuwa “Jicho
linaona kile ambacho akiri iko tayari kukiona au kuelewa”
Kutokana na maneno hayo ya Bwana “Henri Bergson”, tunajifunza kwamba fursa
ambazo hazionekani machoni mwako, ni lazima uziite wewe mwenyewe ndipo zitakuja
kwako na usipofanya hivyo watu wengine watafanya hivyo, mwisho wake fursa ulizotakiwa
kuzifaidi wewe, utabakia KUZITAZAMA kwa jirani. Endapo jirani au watu wengine
wasipoziita fursa hizo, basi zitaendelea kubakia katika hali yake hiyo ya
kutoonekana, mpaka zitakapoitwa na vizazi vijavyo.
Leo hii Tanzania kama taifa tunaishi maisha duni kutokana na ukweli
kwamba watu wengi wanaanzisha miradi ya biashara baada ya kutazamia kwa
wengine. Ni bora ukaona mradi anaoufanya mwingine kuliko kuutazama.
Watu wengi
hasa Tanzania, huwa hawaoni miradi bali uitazama tu basi. Kwa maana nyingine ni
kwamba, unapoona mwenzako akijishughulisha na mradi fulani wa kibiashara na
wewe ukafanya kama anavyofanya bila kuongeza kitu chochote kipya, basi ujue
kuwa mradi huo “haujauona” BADALA
yake “umeutazama” tu!.
Ni
nini faida za kufanya mradi ambao umeuona?
Kimsingi nchi inapokuwa na watu wengi ambao tunafanya miradi tunayoiona
kwa macho ya ubongo au akiri zetu, ni wazi kwamba tutakuwa na uwezo mkubwa wa kutatua
changamoto na kero nyingi ambazo zinasababisha maisha magumu kwa jamii tunayoishi
nayo.
Pili, tutaweza kutengeneza bidhaa na huduma za thamani kubwa kwa watu wa
Tanzania na dunia kwa ujumla. Tatu, tutasaidia katika kuharakisha ukuaji wa
uchumi wetu binafsi na taifa letu kwa ujumla.
Watu wengi tukiona na siyo kutazama miradi ya maendeleo, tutaweza
kutegeneza bidhaa nyingi ambazo ni tofauti tofauti. Tukiwa na bidhaa nyingi
zenye ubora wa hali ya juu, ni wazi kwamba tutaweza kuvuta pesa nyingi kutoka
kwa watu wengine hasa nje ya nchi. Watu wenye pesa zao, watapenda watume pesa
zao kwetu, ili kupata bidaa na huduma na hivyo kutufanya sote tuwe na pesa
nyingi.
Kwa ngazi ya kitaifa ni kwamba watu kutoka mataifa ya nje watapendelea
kutuma pesa zao Tanzania ili kununua suruhisho tulizonazo juu ya changamoto
walizonazo kwao – hali hii ndiyo itachangia uwepo wa ajira na hatimaye nchi
kuwa na uchumi mkubwa.
Hili
tuwe na uwezo wa kuona miradi tufanye nini?
Katika hili hakuna namna na hakuna njia muhafaka ZAIDI ya kuzidi
kuwekeza sana kwenye fikra. Ninaposema kuwekeza kwenye fikra ni zaidi ya watu
kusoma hadi vyuo vikuu au kubobea kwenye taaluma fulani.
Uwekezaji mzuri kwenye fikra ni ule ambao unajifunza kila siku kwa
kutumia njia mbalimbali, kama vile kujenga tabia ya kuwa mdadisi wa kila jambo/kitu
na hasa yale yanayohusu kile ambacho unakifanya au unatarajia kukifanya.
Kabla ya kuanzisha mradi wako hakikisha unafanya utafiti wa kero na
changamoto zinazowakabili watu waliokuzunguka au wengine wa mbali --- kwa
kawaida kero inayo wapata watu waliokuzunguka mara nyingi huwa inawapata pia watu
wengi walioko mbali na wewe.
Uzuri wa uwekezaji katika fikra hauna usumbufu na wala hauitaji gharama
kubwa. Kinachohitajika ni nidhamu ya kufanya kile ulichopanga kukifanya hata
kama ni kigumu. Kwahiyo, huu ni uwekezaji ambao unaweza kufanywa na karibu wa
aina yoyote, ilimradi mtu awe anajua kusoma na kuandika.
No comments:
Post a Comment