Vitabu

Ugonjwa wa Kuchoka Unatumaliza!

KITABU CHA "MEGALIVING! 30 DAYS OF PERFECT LIFE
 “Chanzo kikuu cha ugonjwa wa kuchoka ni watu wengi kufanya kazi ambazo hawazipendi” ~ by Cypridion Mushongi.
Ugonjwa ni hali ya kutojisikia vizuri, na wakati mwingine hali hii uambatana na maumivu makali sana. Katika ulimwengu wa afya, magonjwa yamegawanyika katika makundi makuu mawili. Kundi la kwanza ni magonjwa ya kuambukiza, mfano: kipindupindu, malaria, ukimwi n.k.

Kundi la pili ni
magonjwa yasiyo ya kuambukiza, kama vile shinikizo la damu, kisukari, tezi dume n.k. Lakini mara zote tumekuwa hatuoni au tumeshindwa kutambua ugonjwa wa “kuchoka” ambao nao kimsingi upo kwenye kundi la magonjwa yale ambayo siyo ya kuambukizwa.

Tunaweza kusema kuwa ugonjwa huu wa “kuchoka” ni ugonjwa sugu na umekuwa hatari kwa maisha ya binadamu kwa muda mrefu sana. Watu wengi hasa hapa kwetu Tanzania wanaugua sana ugonjwa huu.
 

Chanzo kikuu cha ugonjwa wa kuchoka ni watu wengi kufanya kazi ambazo hawazipendi. Watu wengi wanafanya kazi za ajira siyo kwasababu wanazipenda bali ni kwasababu ndiyo njia pekee ya wao kuweza kujihakikishia usalama wa chakula basi!

Unapofanya kazi ambayo huipendi, mara nyingi unajikuta kila unapoanza kufanya kazi unakuwa na wasiwasi na mawazo mengi nje ya kazi hiyo unayoifanya. Kwahiyo, wasiwasi na mawazo hasi ni visababishi vikubwa vya “kuchoka”.

Akiri inayoshangaa itakufanya kila wakati uchoke sawa na kukimbia umbali wa kilomita 15. Akiri ya binadamu ni sawa na betri yenye moto asilimia 100%. Unapoamka asubuhi au unapoanza siku yako, betri yako inakuwa imejaa moto au “charge” kwa asilimia 100%.

Unapofika ofisini na kukaa kwenye kiti, mara unatumia nguvu kuwazia jinsi rafiki yako alivyokusema vibaya juzi kwenye kikao, hapo unatumia asilimia 20%. Mara unawazia ujaenda kijijini kwenu siku nyingi na hujapeleka watoto kuwaona bibi na babu yao, lakini hapa unagundua kuwa huna pesa kwasababu, kazini kwako huwa hawalipi pesa ya likizo japo unastahili kulipwa, hapo unatumia asilimia 30%, mara unawaza kuwa binti wa kazi anavyomshindisha njaa mtoto wako, hapa asilimia 20% zinapungua; unawazia jinsi ulivyopata hasara kwenye mradi wako wa boda boda ambayo ulinunua kimya kimya kwasababua ofisini wakijua wataanza kukuzonga hapo asilimia 15% zinakweda.

Unapokuja kushituka kuanza kazi rasimi za ofisi, betri yako inakuwa imebakiwa na moto kidogo kama asilimia 15%. Kwa maana nyingine ni kwamba unafanya kazi kwa muda wa saa moja hadi mbili, moto unaisha na baadae kuzima kabisa—kuchoka!

Unaporudi nyumbani jioni unajisikia umechoka sana, wakati kiuhalisia hujafanya chochote cha maana. Mara nyingi hata watoto wako hutaki kabisa wakusemeshe, eti kwasababu una uchovu kwasababu ya kazi za ofisi. Lakini, cha kushangaza, ukifika tu nyumbani unawasha TV kwa kisingizio cha kutuliza uchovu ulionao.

Ebu niambie kwa maisha ya namna hii FURAHA itatoka wapi? Na kama furaha haipo nguvu ya kufanya kazi ili tupate pesa za kutosha itatoka wapi?

Mafanikio ya mtu yoyote yanatokana na kukamilisha yale uliyopanga na ulipaswa kuyafanya. Hakuna furaha utakayoipata maishani kwa kukumbuka jinsi ulivyoangalia runinga (TV) mwaka mmoja uliyopita, au jinsi ulivyoshindwa kwenda likizo na familia kwasababu ya kukosa nauli. Lakini, utapata furaha na amani sana moyoni utakavyoanza kukumbuka jinsi ulivyomaliza kujenga nyumba yako mwaka jana, utakumbuka jinsi ulivyo mwezesha hadi akapata mafanikio makubwa.

Ili kupata furaha na nguvu ya kufanya kazi—hatimaye pesa, lazima tuone kuwa athari za ugonjwa wa “kuchoka” dhidi ya uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla ni kubwa sana. Kwasasa, tunaweza kusema kuwa ugonjwa wa “kuchoka” ndio kisababishi namba moja cha umaskini na ufukara kwa watanzania waliowengi.

Kwahiyo, kama ugonjwa wa “kuchoka” ni hatari namna hii, tunadhani ugonjwa huu unahitaji tiba au dawa ya haraka. Habari njema ni kwamba, tiba yake imo ndani ya mtu mwenyewe (binafsi), kwasababu “kuchoka” ni ugonjwa wa kujitengenezea mwenyewe,

Ili tiba ya kuchoka ambayo imo ndani yako, iweze kukutibu ni lazima uwe tayari kujifunza mfumo mpya wa Maisha, lakini pia uwe tayari kutekeleza yale uliyojifunza kwa vitendo. Njia muhafaka na ya uhakika kuweza kujifunza jinsi ya kutibu ugonjwa wa “kuchoka” na kupata mfumo mpya wa maisha ambao ni wa kimafanikio zaidi ni kusoma vitabu.

Nashauri, usome hasa kitabu cha MEGALIVING! 30 DAYS TO A PERFECT— “The Ultimate Action Plan for Total Mastery of Your Mind, Body & Character” By Robin S. Sharma. Kama wewe unayesoma makala hii sasa hivi unataka kutibu ugonjwa wa “KUCHOKA” na kubadilisha mfumo wa Maisha yasiyokuwa na mafanikio, bonyeza maandishi haya: NITUMIE KITABU, ili kwa kuanzia uweze kujipatia nakala ya kitabu hicho hapo juu na vingine vingi kulingana na mahitaji yako.
Nimeamua kujikita kwenye UPENDO...Chuki ni mzigo mkubwa sana kuubeba” ~ Martin Luther King Jr.
Unapoona watu wanatembea, wanaongea na wanacheka, usidhani wengi wana furaha ya dhati. Ukweli ni kwamba watu wengi wana chuki, hasira, kinyogo na kero nyingi ndani yao. Kubwa zaidi ya yote ni kwamba..
muda mwingi hawana furaha. 

Hali hii ya watu kukaa muda mrefu bila kuwa na furaha, inatufanya kukosa msukumo na uwezo wa kufanya kazi kwa bidii na maarifa. Matokeo yake wanapata magonjwa na umaskini usioisha. Chanzo cha chuki na hasira miongoni mwetu ni kutokana na uwepo wa hisia hasi au mtazamo hasi ndani ya fikra zetu. 

Kimsingi kuna aina nne zinazosababisha hisia hasi au mtazamo hasi. Katika kitabu cha “In Search of the Miraculous: Fragments of an Unknown Teaching” cha Bwana Peter Ouspensky kutoka Urusi anasema kwamba, vyanzo vya mitazamo hasi ni pamoja na 1. Kuhalalisha matendo; 2. kujitambulisha binafsi au kujishikiza; 3. Kujari sana wanavyokuchukulia watu wengine; 4. Kulaumu watu wengine. 

Mpendwa msomaji wa MAARIFASHOP leo nitakushirikisha ili uweze kufahamu na kuelewa tabia ya “kuhalalisha matendo” ni kitu gani na unaweza kufanya nini ili kuondokana na kisababishi hiki cha mtazamo na hisia hasi ulizonazo hivi sasa kwenye maisha yako. 

Kuhalalisha matendo ni mojawapo ya kisababishi kikubwa cha chuki na hasira kwa watu walio wengi. Kitendo cha kuhalalisha matendo ni kama vile ambavyo huwa unafanya pale unapokuwa na visingizio au kutengeneza sababu ya hasira yako. Unajiambia wewe mwenyewe na watu wote wanaokusikiliza jinsi ambavyo hujatendewa haki. Wakati mwingine unajiambia jinsi ambavyo umetendewa vibaya sana au jinsi ambavyo watu wengine walivyofanya mambo ambayo hayakuwa ya kistaarabu/kiungwana. 

Kwahiyo,unaendelea kurudiarudia hali ile iliyotokea ndani ya akiri yako. Unarudia sababu zote zilizokufanya ujisikie vibaya. Kila mara unapojaribu kufikiri juu ya mtu yule unayesema amekutendea vibaya, ghafla unakasirika. Unajisikia na kujiona kama vile unastahili kuwa na hasira; unajiona kana kwamba jambo hili limekughalimu sana, na wewe katika kukadiria kwako unajiona ulikuwa mtu mzuri au muungwana sana. 

Je nitaondoaje tabia ya kuhalalisha matendo? Unaweza kuondokana na tabia ya kuhalalisha matendo na kuhakikisha unakataa kujihusisha nayo: 

1. Acha kuhalalisha matendo: Unapoacha “kuhalalisha matendo” maana yake ni kwamba, unatumia vizuri akiri yako kufikiri sababu halisi iliyotokea, na siyo kuhalarisha hisia hasi au hasira zako.
  Kumbuka kuwa hasira na hisia hasi, hazikufanyii jabo lolote jema, badala yake zinakuharibu kabisa. Hisia hasi na hasira, hazimdhuru mtu mwingine na wala hazibadili hali iliyopo au iliyojitokeza, BADALA yake zinadhohofisha furaha yako, zinapupunguza uwezo wako wa kujiamini. Kitendo cha wewe kuwa mnyonge na dhaifu kinakufanya kuwa na ufanisi kidogo sana katika utendaji wako wa kazi au nyanja zingine za maisha. 

Badala ya kuhalalisha hasira na hali yako ya kutokuwa na furaha, unatakiwa kutumia uwezo wako wa kufikiri na kupiga picha ndani ya akiri; Ili kuondoa lawama kwa mtu mwingine, au kuachana na hali ile ya kuchukia au kutokuwa na furaha. 

Kwa mfano: ukiwa unaendesha gari na ghafla mtu akakuingilia upande wako barabarani, badala ya kuchukia na kuwa na hasira, unatakiwa kusema, “haina shida ninatakiwa kuwa mwangalifu sana siku nyingine”, “ninadhani siku ya leo siyo nzuri kwake” au “lazima atakuwa anawahi ahadi muhimu kwake”. 

2. Ondoa lawama kwa watu wengine: Kwakuwa akiri ya binadamu inao uwezo wa kushikiria jambo moja baada ya lingine, ni kwamba kadili utakavyoanza kuondoa lawama kwa watu wengine ndivyo utakavyoanza kupunguza nguvu au mafuta ambayo hisia za hasira na chuki uzihitaji ili kuendelea kuwepo na kufukuta. 

Unarudisha uwezo wa kujihami. Unajiweka mpole na kujipa mtazamo chanya. Baada ya muda mfupi, hali hii ya sintofahamu huweza kupita na wewe kusahau yote yaliyotokea. Kwa kubadilisha fikra hasi, maana yake unaziondoa kabisa hisia zako hasi hata kama ni kubwa kiasi gani. 

Kama unayo matatizo makubwa kimaisha, kama vile mambo ya taraka na mkeo, kupoteza kazi au hasara kutokana na uwekezaji ulioufanya, njia ile ile ya kudhibiti hasira na chuki utumika. Acha kujiambia wewe na mtu mwingine yeyote anayekusikiliza kuhusu kwanini unastahili kuchukia au kutokuwa na furaha. 

Ondoa lawama kwa watu wengine kila mara unapofikiria hali fulani inayokunyima raha mpaka ile hali hasi ipotee. Pindi ule moto wa kuwa hasi unapoisha au kupungua, sasa unaweza kuelekeza nguvu yako kwa kitu kingine ambacho ni chanya. 

Kanuni mojawapo muhimu ya mafanikio na furaha ni “usiwe na hasira au kuwa na wasiwasi wala kuhofia kitu chochote ambacho huna uwezo wa kukibadilisha au huwezi kufanya chochote juu yake”. Usirumbane na kumlaumu mtu yeyote kwa kitu ambacho hana uwezo wa kukibadili. Sheria maarufu inasema kwamba, “Kama hakuna suruhisho, hakuna tatizo”
  3. Usiwekeze nguvu yako kwa mambo yaliyopita: Katika maisha huwa kuna vipindi viwili muhimu, yaani kipindi kilichopita na kipindi kijacho. Kipindi kilichopo ni kifupi sana, na kinatoweka haraka mara tu kinapotokea. 

Uamuzi ni wako, unaweza kuamua kuweka nguvu yako kwa mambo ambayo yametokea tayari, lakini huwezi kuyabadilisha. Au unaweza kuweka nguvu kwa mambo yajayo ambayo yanawezekana na unao uwezo kiasi fulani wa kuyafanya yatokee. 

Tatizo lililopo ni kwa watu wengi kutumia sana nguvu ya hisia zao kuchukia au kuwa na hasira kwa mambo ambayo yamekwishatokea. Niseme kuwa hii ni bahati mbaya, kwasababu nguvu yote hii inapotea bure. 

Hakuna jambo lolote zuri linaloweza kutokea kwa kuendelea kulalamikia mambo ya nyuma. Kibaya zaidi ni kwamba nguvu unayotumia kufikiria mambo mabaya yaliyopita inakupunguzia nguvu ambayo ungeitumia kufikiria jinsi ya kubadilisha au kuweka sawa hali ya maisha yako ya baadae.
  4. Acha liende: Watu wengi ambao hawana furaha ni kutokana na wao kurudishwa nyuma na mambo ambayo yalitokea na ambayo hawataki kuyasahau au kuyaacha yaende zake. Bado wana chuki, hasira na wanajisikia vibaya juu ya kile walichowahi kufanyiwa na watu wengine.
  Wana chuki na wazazi wao, ndugu, mahusiano mabaya ya ndoa, bosi au mahusiano mabaya ya kibiashara. Ukweli ni kwamba, maisha yako yatakuwa ni mwendelezo wa matatizo, changamoto, ugumu na kushindwa kwa muda. Haya yote ni mambo ambayo hatuyatarajii, japo muda wowote yanaweza kutokea na hayakwepeki. 

Kubadili fikra na kubadilisha maisha, lazima ufanye maamuzi ya kukabiliana na changamoto au matatizo yaliyopo, bila kujali ni makubwa kiasi gani. Mpaka utakapochukua hatua ndipo utakoma kuwa mtumwa wa mambo yote ya nyuma yanayokukwaza na ambayo kwa vyovyote vile huwezi kuyabadilisha. Fanya maamuzi leo kwamba kuanzia sasa na kuendelea utaondoa maneno yote ya kama isingekuwa hivi.....kwenye maisha yako. 

5. Kutafsiri matukio kwa njia tofauti: Mwandishi na mzungumzaji maarufu aitwaye “Wayne Dyer”, anasema hujachelewa kuwa na furaha ya wakati wa ujana”. Alimaanisha kwamba, muda wowote unaweza kutafsiri tukio lolote lililokuudhi au kukuchukiza siku za nyuma katika hali au njia ambayo ni chanya. 

Unaweza kujaribisha sheria ya kubadilishana, ambapo unaondoa kibaya na kuweka kitu kizuri na kuanza kuwazia kizuri badala ya mabaya yaliyowahi kutokea huko nyuma. 

Unaweza, kujikita juu ya ni jinsi gani jambo baya lingeweza kukufanya huwe bora zaidi, au mwenye busara zaidi. Kimsingi unaweza kuwa mwema kwa watu wote wale waliowahi kukukwaza huko nyuma, kwasababu, wameweza kukufanya huwe imara zaidi kwa wakati huu ulionao. Na kwa vyovyote vile, isingeweza kutokea vinginevyo. 

Wazazi wako hawakuwa na uzoefu wa kulea vizuri watoto. Na nyongeza ya hapo, walikuwa ni zao au matokeo ya jinsi wao walivyolelewa. Kama ilivyo kwa binadamu yeyote yule, waliingia kwenye malezi wakiwa na matatizo pamoja na udhaifu wao sawa na jinsi ulivyo wewe leo hii. 

Hatahivyo, walijitahidi, walifanya vizuri kile walichoweza kwa uwezo waliokuwa nao. Walifaya kazi jinsi walivyo na wasingeweza kukulea tofauti na wao walivyokuwa. Ni kutokufikri vizuri kuendelea kutokuwa na furaha kwa vitu ambayo walifanya au hawakufanya vile ambavyo hawakuweza, hawakuwa na namna ya kuvifanya tofauti.

Ngoja viede hivyo hivyo na wewe uendelee na maisha yako. Mpendwa msomaji wa makala hii yawezekana unapenda kusoma zaidi kitabu hiki “In Search of the Miraculous: Fragments of an Unknown Teaching” cha Bwana Peter Ouspensky: Weka e-mail yako kwa kubonyeza maneno haya: “NITUMIE KITABU” . Baada ya hapo nitakutumia nakala tete ya kitabu hicho ambacho mimi binafsi kimenijenga sana.
  KARIBU TWENDE KAZI PAMOJA

 

Jitahidi Upate Kusoma Kitabu Hiki

“Mimi siyo zao la hali yangu ya maisha BALI ni zao la maamuzi nifanyayo kila siku”. ~ Stephen Covey ~

Ukibahatika kupata na kusoma kitabu cha “Are you fully charged?” Utajifunza mambo makubwa sana ambayo yatarahisisha kazi yako ya kusaka mafanikio makubwa.

Kutoka katika kitabu hiki na mimi nimejifunza mambo mengi sana LAKINI nimeona nikushirikishe mambo 5 kama sehemu ya mambo niliyojifunza kutoka katika kitabu hiki: Mambo 5 niliyojifunza mimi binafsi ni….

Ushindi katika maisha: Binadamu wengi wanadhani vitu pekee vinavyoweza kuwaletea ushindi mkubwa ni vile vikubwa tu! Lakini, mwandishi wa kitabu hiki cha “Are you fully charged?” anasema kuwa kitu kinacholeta ushindi mkubwa ni wewe kutengneneza maana kwa ushindi mdogo mdogo. 

Unahitaji kujiuliza ni kitu gani hicho ambacho utakifanya leo kilete utofauti? Hata kama ni kidogo. Utofauti mdogo mdogo ndio unapelekea utofauti mkubwa, hivyo hivyo ushindi mdogo mdogo ukikusanyika kwa pamoja ndio unaleta ushindi mkubwa. 

Usipuuzie jambo dogo ukadhani unapolifanikisha litakua halina utofauti mkubwa, HAPANA si kweli. Cha msingi ni wewe kuhakikisha kila unachofanya hata kama ni kidogo unakifanya vizuri ili kuleta maana. Siku zote maana inaletwa kwa kuunganisha ushindi mdogo mdogo na kisha kuwa ushindi mkubwa.

Hamasa ya kazi: Fanya vitu kutokana na msukmo wa ndani au hamasa ya ndani kuliko hamasa ya nje. Hamasa au msukumo wa nje huwa sio endelevu, hivyo ukiutegmea siku zote utapotea tu! Na huwa siyo wa kudumu. Hamasa ya ndani hua ni ya mtu binafsi.

Hamasa ya ndani ya mtu binafsi, ndio inayompa mtu nguvu ya kufanya zaidi na zaidi, hata anapokutana na vikwazo. Mfano kama unafanya biashara, hamasa ya nje inawezakuwa ni kutengneza faida kubwa, na hamasa ya ndani ikawa ni kuwafanya wateja wako kuwa na furaha au kutoa suruhisho la matatizo yanayowakabili wateja.
 

Faida ya kutambua mahitaji ya jamii/dunia: Unatengneza maana pale uwezo wako na vile unayovipenda vinapokutana na mahitaji ya jamii. Kufahamu vipaji vyako na kile upendacho katika maisha ni muhimu, lakini hilo halitoshi maana hilo ni nusu tu katika mlinganyo kuzalisha na kuhitaji vitu na huduma.

Kitu ambacho kinaweza kuwa cha muhimu zaidi ni kufahamu jamii yako au dunia inahitaji nini kutoka kwako na jinsi gani unavyoweza kutumia vipaji na uwezo wako katika kuzalisha kile unachopaswa kutoa kwa jamii au dunia.
 

Furaha katika Maisha: Katika safari ya maisha, tunatakiwa kusafiri na furaha muda wote na siku zote Kwa maana nyingine furaha siyo tukio la muda fulani bali inatakiwa kuwa sehemu ya maisha. 

Lakini, kwenye kitabu hiki tunakumbushwa kuwa ili huweze kuwa na furaha ya kudumu ni vyema ukaacha kutafuta furaha kama furaha na badala yake ujikite katika kutafuta “Maana”.

Utafutaji wa maana ndio unaofanya maisha yawe ya thamani na sio utafutaji wa furaha. Watu wanaotumia muda mwingi katika maisha kujitafutia furaha yao binafsi, huwa hawaipati. 


Furaha pasipo maana ni sawa na maisha yenye ubinafsi. Watu wanaoishi maisha yenye maana huwa wanapata furaha kubwa sana kwa kuwapa watu wengine.
 

Simamia vizuri muda wako: Matakwa ya wengine katika zama hizi za leo ambapo kuna taarifa kibao zisokuwa na kikomo. Pia kuna vizuizi vingi visivyoisha, ni rahisi kutumia muda mwingi katika mabishano na majibizano. 

Ni rahisi sana kukosa umakini katika kazi kwasababu ya simu au radio, runinga n.k. Matakwa ya wengine yanayokuja kwako lazima yatatumia sehemu ya muda wako wa siku.

Mfano wapo watu watataka kuchati na wewe, kukupigia simu muongee, wapo watakaotaka mtoke wote n.k. Ila baada ya miaka kadhaa vitu utakavyokua unajivunia havitatokana na matokeo ya kufuata matakwa ya wengine. 


Kitu kitakachokupeleka mbele katika maisha yako ya baadaye ni kile ulichoanzisha leo na sio ulichoanzishiwa. Usiishi maisha yako kwa kuwa mtu wa kujibu yanayoendelea kutendeka badala yake huwe ni mtu wa kuazisha vitu ambavyo baadaye utakua unajivunia.

Mambo hayo matano ni baadhi tu ya busara nilizozipata ndani ya kitabu hiki cha “Are you fully charged?” Kama unapenda kupata kutumiwa kitabu hiki kwa lengo la kukisoma kwa undani zaidi, basi bonyeza NITUMIE KITABU. Ndani ya masaa 48 utatumiwa kitabu hicho mara moja.




3. KUTOKA Kitabu cha "Tough Times Never Last, But Tough  People Do!" cha bwana Robert H. Schuller.
Ni kitabu kizuri kukisoma ili kufahamu jinsi ya kumudu changamoto za maisha ambazo ujitokeza karibu kila siku. Katika kupitia kitabu hiki kwa mara ya kwanza niliweza kubaini yafuatayo:
Ø  Siri ya kukusaidia kutokushindwa jumla ni wewe kuendelea kujaribu bila kuacha
Ø  Kila mtu huwa ana matatizo, na hakuna ambaye yuko huru.
Ø  Watu wengi wanapoteza udhibiti (control)  ya maisha kwa kuwaachia uongozi wao kwa watu wengine.
Ø  Kila mtu unapaswa kujua kuwa hapo alipo anaweza kutoka na kwenda sehemu nyingine.
Ø  Watu wengi waliofanikiwa mara nyingi huwa ni mwiko kwao kuachia matatizo kuwa visingizio vya kufanya mambo makubwa.
Ø  Hakuna tatizo ambalo ni la kudumu isipokuwa mtu ndiye wa kudumu
Ø  Tatizo la mtu mmoja ni fursa kwa mwingine.
Ø  Kila wakati unapokabiliwa na matatizo kuna muhitikio (reaction) hasi au chanya.
Ø  Matatizo ni kama mimba yasipopatiwa ufumbuzi yanakuwa mpaka kuweza kuonekana na kusababisha madhara makubwa
Ø  Ili uweze kutatua matatizo ni lazima ujenge utamaduni wa kutodharau matatizo eti kwasababu ni madogo.
Ø  Kama unataka kutatua matatizo yako usimungoje mtu mwingine kumaliza matatizo uliyonayo.
Ø  Ni wewe mwenyewe uliye na uwezo wa kulifanya tatizo liwe dogo au kuliendeleza na kuwa kubwa.
Ø   Kwenye maisha, dalili za wewe kuanza kushindwa kukabiliana na matatizo ni pale tu unapoanza kulaumu watu wengine kwa matatizo yako.
Ø  Kila kikwazo kinaweza kuwa fursa
Ø  Usiruhusu ukosefu wako wa pesa leo ukubadilishe ndoto zako



2. UKISOMA KITABU CHA "THE $100 STARTUP: Reinvent the Way you Make a Living, Do what you Love, and Create a New Future"
By ~ CHRIS GUILLEBEAU~
Katika kitabu hiki, tunaambiwa kuwa, kuanzisha Biashara ni rahisi sana kiasi cha kwamba  unahitaji vitu vitatu tu yaani: bidhaa, kundi la watu na  njia ya kulipwa tu! Mambo mengine ni nyongeza tu. Mwandishi anabainisha kuwa, ili kufanikiwa katika Biashara unahitaji ujuzi, kuipenda kazi unayofanya, pamoja na chochote chenye manufaa kwa watu wengine.
Bwana CHRIS GUILLEBEAU anatufundisha kuwa Biashara yenye tija ni ile itakayoendana na uhitaji wa watu, kwahiyo, ni muhimu kuangalia ni bidhaa ipi inahitajika ndipo uizalishe na kila utakapotoa jibu lenye kutatua kero za watu, tegemea malipo maradufu.
Mwandishi anatoa mambo mengi yanayohusu mafaniko katika Biashara, lakini anazidi kusisitiza kuwa, si elimu kubwa ya biashara inayoweza kumpa mtu mafanikio, bali kikubwa ni ufahamu na bidii katika kufanya biashara.
Hiki ni kitabu kizuri sana, hasa kwa wale wanaopenda kujitenga na kundi la wasaka ajira na kuanza mchakato wa kujiunga na “MTANDAO WA WATENGENEZA KAZI” jitahidi ukipate
KARIBU TWENDE KAZI PAMOJA

KUTOKA KATIKA KITABU CHA "Essentialism" The Disciplined Pursuit of Less"
By   ~ McKeown ~
Ukisoama kitabu hiki utajifunza mambo mengi hikiwa ni pamoja na haya machache!

1.      Msongo wa mawazo katika maisha hutokana na sisi kutaka kila wakati kufanya kila kitu. Kufanya kazi ili kumfurahisha na kumridhisha kila mtu kunapunguza sana ufanisi na ubora wa kazi tunazo fanya.
2.      Ili tuweze kufanya kazi kwa kiwango cha juu lazima tujifunze kukubobea katika kufanya shughuli nyingi tena ndogo ndogo.
3.      Tukiwekeza katika vitu vichache itakuwa rahisi kuweza kupiga hatua kubwa na kupata mabadiliko makubwa katika maisha.
4.      Tusipojijengea utamaduni wa kuweka vipaumbele katika maisha yetu, mtu mwingine atatuwekea vipaumbele, jambo ambalo litatupelekea kutekeleza malengo ambayo hatuyapendi na hivyo kushuka kwa kiwango cha utendaji kazi.

5.      Ni muhimu sana tangia mwanzo watoto wetu tuwafundishe kusema "HAPANA" na siyo kuwapongeza kwa kusema "NDIYO" peke yake.

6.      Ukiwa na tabia ya kufanya kazi kwa kumridhisha mtu ni rahisi sana kuwa MBABAISHAJI; Na hii ni kutokana na ukweli kwamba, kila kazi yenye kuhitaji uharaka, utarundikiwa wewe na ukiweza utapewa bonus/reward nyingi. Mwisho ile nguvu yako unaitawanya kukamilisha kazi zote zinazokuja. Hatimaye kila kazi una-invest kidogo kidogo mwisho utapata matokeo ya kiwango cha chini sana! A.K.A Mbabaishaji.

7.      Watu wengi wanatumia U-Busy kama kipimo cha utendaji bora wa kazi hata kama vitu wanavyofanya havina tija.

8.      Mtu akipongezwa anavutiwa na kuhamasika sana na hivyo kuingia kwenye mtego wa kutaka afanye na kumaliza kila kazi iliyo mbele yake. Kumbe wafanisi katika kazi wanalitambua hili "Less but Better"

9.      Katika maisha yetu ya kila siku, Kazi kama vile kufikiri, kutafakari, kupumzika, kulala (sleeping) n.k. Havipewi muda wa kutosha kama vitu muhimu; mara nyingi vinatengewa muda kidogo sana na wakati mwingine hakuna kabisa.

10.  Kama hujaelewa vizuri dhumuni na lengo lako katika maisha. Unapoteza sana muda wako kwa kujaribu kuonekana vizuri kwa kujilinganisha na watu wengine. Ndiyo maana tunavipa thamani ya juu sana vitu kama vile gari, nyumba au vitu visivyo shikika kama  vile idadi ya followers kwenye facebook n.k. Matokeo yake tunaacha vitu muhimu kama Mazoezi, kuspend muda na family n.k.

11.  Kama watu hawana ndoto au dira katika maisha; Mara nyingi watu hawa watapendelea kufanya vitu vyenye kuleta matokeo ya muda mfupi na bila kujua vitachangia kwa namna gani kwenye ndoto husika.

12.  Ili kuchagua vitu muhimu vya kufanya tunahitaji Ujasiri (courage).

13.  Mara nyingi watu wanaosema ndiyo kwa kila jambo huwa hawana tabia ya kutafakari matokeo. Matokeo yake wanaacha vitu muhimu ili kufanikisha majukumu mapya.

14.   Kwasababu binadamu tuna tabia ya kutothamini vitu ambavyo hatuvimiliki, hata kama ni vya muhimu maishani. Ndiyo maana mali za umma, ndugu na marafiki zinatumiwa na kuharibiwa bila kujali

No comments: