Saturday, April 30, 2016

Umuhimu wa Kutafuta Pesa Bila Sababu ni Huu


“Unashindwa kupata pesa nyingi kwasababu unatafuta pesa kulingana na shida unazotegemea kupata siku zijazo” ~ Cypridion Mushongi
Siku moja nilikuwa naongea na rafiki yangu ambaye aliwahi kuniuzia kiwanja siku za nyuma. Baada ya mwaka mmoja tangu rafiki huyo aniuzie kiwanja, tulikutana mjini Bukoba na hapa aliniuliza juu ya mpango wangu wa kukiendeleza kiwanja hicho. Jibu langu kwake lilikuwa...

Friday, April 22, 2016

Siri ya Watu Kupenda Mikate Imefichuka



“Kama pesa ni kazi iliyoisha, wewe pesa yako kazi yake imefanywa na nani?” ~ Cypridion Mushongi
Jumapili ya tarehe 17/04/2016…nilikuwa nyumbani nasikiliza mziki wa injiri, mara tu ukapigwa wimbo wa “Mikate” ambao umeimbwa na “AIC Chang’ombe Vijana Kwaya”. Katika wimbo huu waimbaji wanasikika wakiimba kuwa “Watu Wanapenda Mikate” . Wimbo huu umebeba ujumbe mzito na unaeleza.....

Tuesday, April 12, 2016

Pesa ni Matokeo Nifanye Nini?



Matokeo ni kitu kizuri kwani kinapendwa karibu na kila mtu. Matokeo ni kitu cha mwisho kutokea baada ya hatua mbalimbali na shughuli nyingi kufanyika. Kwa maana nyingine tunaweza kusema kuwa pesa ni hitimisho. Matokeo yana sifa moja nayo ni...

Tuesday, April 5, 2016

Wewe au Pesa Nani Kashuka Thamani?


“Bei ni kile unacholipa. Thamani ni kile unachopata” ~ Warren Buffet
Wimbo ulioenea kote nchini sasa hivi ni “kushuka thamani ya pesa au shilingi ya Tanzania”. Watu wengi tunashusha lawama kwa watu waliopewa madaraka hasa ya kuongoza taasisi za kifedha. 

Lakini nimetafakari sana jambo hili. Fikra na imani yangu vinanituma kuamini kuwa....