Motisha wa Kazi nani Anapaswa Kutoa?

“Unatakiwa kutafuta sehemu ndani yako ambapo hakuna kisichowezekana” ~ Deepack Chopra 



Baada ya mapinduzi ya viwanda uko barani Ulaya mwishoni mwa karne ya 18, iliibuka na kujengeka dhana nzima ya kuajiriwa. 
Dhana hii ilikua kutokana na ukweli kwamba viwanda wakati huo vilihitaji sana nguvu kazi. Mabepari waliomiliki vitegauchumi walihitaji sana wafanyakazi, ilikuweza kuzalisha bidhaa na huduma mbalimbali. 

Kwa mtu ambaye amekulia kwenye ajira kila wakati akikasirika au akapata changamoto, katika fikra zake anakuwa anajua kuna bosi mkuu ambaye atamuonea huruma na wakati mwingine kumtia moyo….Hali hii iliendelea na hatimaye ikasambaa duniani kote hadi huku kwetu Tanzania. 

Dhana hii imekua kiasi kwamba hata wale waliojiajiri nao pia wanataka mtu wa kuwatia moyo, wanataka mtu wa kuwapa MOTISHA. 

Kila mtu anatafuta mtu wa kumtia moyo na akimkosa anakasirika matokeo yake anakata tamaa kwa jambo hilo alilokuwa analifanya. 

Dunia ya sasa imejaa watu ambao wanasubili mtu fulani aje kuwapa motisha ili kufanya kile wanachotaka kukifanya au wapate mafanikio wanayo tamani kuyapata. 

Habari mbaya ni kwamba “hakuna mtu yeyote wa namna hiyo ambaye anakuja kufanya kazi hiyo”. Ni asilimia 2% tu ya watu ambao wanaweza kufanya mambo yao bila kuhitaji usimamizi. Watu hawa tunawaita viongozi. Na wewe umeumbwa kuwa huyo mtu. 

Kwahiyo hivi sasa, watu ambao ni adimu ni wale walio tayari kujimotisha wenyewe. Utakapoweza kujimotisha mwenyewe, utaanza kuona wengine wakikufuata kwasababu utaanza kuonekana mtu wa tofauti lakini mwenye thamani. 

Katika KUJIMOTISHA mwenyewe simaanishi kucheza dansi bali namaanisha KUJIMOTISHA huku ukitengeneza thamani (zalisha bidhaa na huduma). 

Kwahiyo, wakianza tu kukufuata maana yake wanafuata na ile thamani unayozalisha na wewe hapo unakuwa na kazi moja tu! “kuwapa bill”. 

Ni kwa namna gani nitaweza kujipa motisha? 
Ili kuhakikisha unajipa motisha wewe mwenyewe lazima ukate shauli ya kufanya yafuatayo: 

Weka malengo: Yawe yanapimika na kutekelezeka. Njia nzuri ni kuwa na malengo ya muda mrefu (miaka 10 na kuendelea), muda wakati (miaka 3-5), na muda mfupi 

Badili mtazamo juu ya kushindwa: Chukulia kushindwa kama njia ya kuelekea mafanikio: tambua kuwa kushindwa kunatoa mafunzo muhimu ya namna gani usahihishe mipango, mikakati na namna nzima ya kujipanga, ili kufikia mafanikio tarajiwa. 

Kushindwa kufanikiwa kunakupa fursa ya kubaini na hatimaye kukupa ni hatua gani uchukue ili kupata matokeo chanya. 

Soma vitabu: Soma vitabu vya waliofanikiwa. Utagundua kuwa changamoto unazopitia ni marudio kuna watu wengine walishapitia na wakapata suruhisho na wameandika walivyotatua changamoto zao 

Kuwa karibu na uwapendao: Tumia sehemu ya muda wako na wale uwapendao; kumbuka usemi usemao kuwa “fanya kazi ili kuishi na siyo kuishi ili ufanye kazi” 

Shauku juu ya kazi: Shauku inakufanya kuwa na MOTISHA ulio juu muda wote. 

Fanya tafakari na mazoezi: Tafakari inaleta maelewano na amani kichwani. Mazoezi pia, yatakusaidia kuwa na nguvu muda wote na ubunifu. Kwa maneno mengine tenga muda kwaajili ya afya na hili litakulipa sana huko mbeleni. 

Anza leo maisha ya KUJIMOTISHA yanalipa sana kwa watu wote wenye KAZI na walioko kwenye AJIRA. 

Endelea kutumia maarifa kutoka MAARIFASHOP ili kujenga na kukuza uwezo wako wa KUJIMOTISHA. Kama unapenda kupata makala kila zinapochapishwa bonyeza kiungo hiki; TUMA MAKALA kisha sajiri barua pepe yako. 

Na pia unaweza kujiunga na kundi la WHATSAP kwa kubonyeza MAFUNZO, ili kupata mafunzo ya kila siku na pale makala zinapochapishwa.




Leo ni Siku ya Wafanyakazi au Siku ya Wenyekazi Duniani

Kwa miaka mingi tumekuwa na utamaduni wa kupumzika na kusherekea eti! “sikukuu ya wafanyakazi” kila ifikapo tarehe moja mwezi Mei ya kila mwaka. Lengo au ajenda kuu ya siku hii ya leo, imekuwa ni kudai uboreshwaji wa maslahi ya watumishi (waajiriwa) kutoka kwa waajiri (wenyekazi).

Kusherekewa kwa siku hii ya “Mei Mosi” kunathibitisha mambo makuu mawili, ambayo ni
ama waajiriwa wanafurahia maisha ya ajira au hawafurahishwi kabisa. Ukichunguza aina ya ujumbe ambao umekuwa ukiwasilishwa siku kama ya leo “Mei Mosi” na zilizopita, unapata kuona kuwa waajiriwa wengi mpaka sasa hawajaweza kupata furaha tarajiwa kwenye maisha ya ajira.

Kukosekana kwa furaha ndani ya Maisha ya ajira, siyo tu kunatokana na maslahi duni, bali ni kutokana na ukweli kwamba, ni vigumu mwajiri husika, kuweza kumridhisha kila mtu kwa jinsi apendavyo, bila mwajiri kuwa ameingilia maslahi yake (yeye kama mwenye kazi).

Kitendo cha waajiri wengi kushindwa kuwaridhisha waajiriwa (watumishi) wao, ndilo chimbuko la sisi waajiriwa kufikia kuamua kuungana kwa lengo la kujenga uwezo wa kupambana na waajiri katika kudai maslahi ambayo tanadhani tukiyapata tutafurahi au tutaridhika. 

Mara nyingi tumekuwa hatupati hicho tunachokidai na hivyo tumejikuta tukiwa ndani ya migogoro na waajiri wetu. Matokeo yake muda mwingi wa kutumikia ajira zetu tumejikuta tukiishi kwa misuguano mingi na mwisho wa yote tumeendelea kuishi Maisha duni na yasiyokuwa ya furaha.

Kwanini madai ya maslahi ni ya kudumu?
Suala la kudai maslahi ni la kudumu kwasababu sisi ambao tumeajiriwa ni kama vifaa vya kufanyia kazi kwa mwenyekazi (waajiri). Katika muktadha wa ajira, sisi waajiriwa ni sawa na komputa, gari, mashine n.k. 

Tofauti ni kwamba sisi ndiyo njia muhafaka ya kuwezesha vitendea kazi vingine viweze kufanya kazi. Ikiwa wewe ni mojawapo wa vitendea kazi, basi ujue kuwa yawezekana mtazamo wa mwajiri wako juu yako ni kwamba wewe ni sehemu ya matumizi au gharama za uendeshaji.

Kwahiyo, linapokuja suala la kukuboreshea maslahi wakati mwingine, inaweza kusababisha faida isipatikane au ikapatikana kidogo sana. Uzuri wa mwajiriwa ni kwamba hata akibaniwa maslahi leo hafi, ataendelea kufanya kazi japo chini ya kiwango, lakini baadae mambo yakiboreshwa ataweza kufanya kazi kwa kiwango cha juu.

Tofauti ya binadamu na nyenzo nyingine kama gari ni kwamba, gari likiishiwa mafuta, lazima pesa itafutwe kokote; nje ya hapo hakuna kitakachoendelea. Kwahiyo, mwajiriwa hasishangae sana kuona kila mwaka hapewi pesa ya likizo, lakini pesa ya kufanya ya magari na komputa hazijawahi kukosa!!

Leo, unaposherekea siku hii ya “Mei Mosi” ni vizuri ukafahamu kuwa kuna tofauti kubwa kati ya kazi na ajira. Hapa tunaona kwamba KAZI ni kitu cha kudumu, lakini AJIRA yoyote duniani ni ya muda. Kazi huwezi kufukuzwa, lakini Ajira unafukuzwa. 

Kwenye Ajira unapangiwa cha kufanya, lakini Kazi wewe ndiye unayepanga utaratibu gani utumike kuifanya. Kwa kifupi KAZI ni pale unapofanya jitihada za kuipatia dunia kitu bora na kizuri (bidhaa au huduma) na AJIRA ni pale unapoamua kuidai dunia ikupatie kitu bora unachokipenda (bidhaa na huduma).

SOMA; AJIRA SIYO KAZI NI AJIRA NA KAZI SIYO AJIRA NI KAZI

Ukitafakari pamoja na mimi juu ya suala zima la kazi na ajira, unakuja kuona kwamba, siku ya leo tunasherekea sikukuu ya wafanyakazi (Mei Mosi) tukidhani sisi (waajiriwa) ni wafanyakazi. Ukweli ni kwamba tunasherekea sikukuu ambayo siyo yetu. "Naona kana kwamba, wenye sherehe ya leo ni wenye-kazi (waajiri) na sio wenye-ajira (waajiriwa)".

Kwa jinsi hali ilivyo ni kama waajiri ndio wana kazi na sisi wengine ni kama tumewekwa kwa malengo ya kusaidia kazi zikamilike. Ndiyo maana tunaitwa waajiriwa (watumishi). Kwa maneno mengine tunaweza kusema; “waajiriwa ni watumishi wa kazi za wengine”.
Kuajiriwa ni vibaya?
Kuajiriwa ni jambo zuri na jema, isipokuwa unahitaji kujihoji juu ya suala hili zima la AJIRA. Mpaka sasa wengine tuko kwenye ajira LAKINI kwa mtazamo chanya. Kwetu sisi ajira ni awamu ya pili ya shule ya Maisha. Kwahiyo, tuko kwenye ajira kwa lengo la kusoma na kujifunza mambo muhimu yatakayotusaidia kufikia ndoto zetu kwa haraka na kwa urahisi.

Kutokana na mtazamo huo, ndio maana tumeamua kutumikia ajira kwa nguvu zetu zote, ili kujijengea tabia nzuri ya uchapa kazi na nidhamu ya kufanya yale tunayotakiwa kufanya. Tunafahamu fika kuwa pindi tutakapomaliza shule hii ya awamu ya pili—Yaani AJIRA, na kuanza kufanyia kazi ndoto zetu, vitu vikubwa viwili ambavyo tutavihitaji ni “kufanya kazi kwa bidii na kuwa na nidhamu”.

SOMA; HABARI NJEMA KWA WANAOTAFUTA AJIRA

Siku ya Mei Mosi ya leo, iwe chachu ya kutuchochea kutambua kuwa, kama tulivyosoma kwa bidii shule ya awamu ya kwanza (msingi—mpaka chou kikuu), na shule ya awamu ya pili kupitia AJIRA, tunatakiwa nayo kuisoma kwa juhudi na maarifa.

Tujitahidi na kuhakikisha tunafahuru kwa kiwango cha juu sana licha ya matatizo na changamoto tunazokutana nazo. Matarajio ni kwamba kama tukifanya vizuri kwenye AJIRA lazima na kwenye kutekeleza ndoto zetu pia tutafanya vizuri na hakika itafika siku tuanza kuishi Maisha ya ndoto zetu—hasa uhuru wa kipato.
Kwanini ni Muhimu Kuichukulia AJIRA Kama Shule? Tunasema AJIRA ni kama shule/darasa awamu ya pili kutokana na ukweli kwamba, ikiwa umeingia kwenye ajira kwa malengo hayo ni wazi unapata fursa hadimu ya kujifunza kwa vitendo na kwa undani zaidi na pia unapata uzoefu juu ya hicho unachofanyia kazi.

Wale wote watakaoamua kuichukulia AJIRA kama shule au darasa, ni muhimu wakatabua kuwa lazima ufike wakati wamalize shule (ajira). Inasemekana kuwa muda mzuri wa kusoma na kumaliza shule (ajira) awamu ya pili ni kuanzia mwaka 1—10. 

Baada ya hapo, kwa wale wanaopenda uhuru, kipato kikubwa, heshima, kuwa karibu na familia yako, kusafiri n.k. wanatakiwa au wanatarajiwa kuanza maisha ambayo unatakiwa kutengeneza kazi.

Ukianza kutengeneza kazi zako ni sawa na kufungua shule awamu ya pili kwaajili ya wengine. Kwasababu, ukishatengeneza kazi, lazima uwaajili watu wengine kwaajili ya kukusaidia kazi zako ziweze kukamilika kwa haraka zaidi. Wale wote watakaokuwa wameajiriwa na kazi yako, watahesabika kuwa ni sehemu ya gharama za kuendesha kazi yako. 

Ukifikia kuwa mtu wa kiwango cha kutengeneza kazi basi, ujue kuwa wewe hutakuwa mtu wa kulipwa mshahara tena, badala yake utaanza kuwa mtu wa kupokea kile kinachobaki baada ya kuwa umelipa gharama zote za uzalishaji na uendeshaji. 

Kwakuwa wewe ndiye unayepanga na kudhibiti kila kitu ni wazi kwamba utapata namna ambayo ni rafiki kwa wewe kuweza kuhakikisha kinachobaki ni kikubwa kulingana na nguvu na rasilimali utakazokuwa umewekeza. Ndugu msomaji wa mtandao huu: http://maarifashop.blogspot.com jitahidi sana kuitumia siku ya Mei Mosi ya leo kuwa siku muhafaka kwako kuweza kuanza kutafakari na kujihoji wewe mwenyewe juu ya mustakabali wa maisha yako.

Lazima ujiulize, hicho unachokifanya ni KAZI au AJIRA? Kama jibu lako ni kazi basi endelea kuifanya kwa viwango vya juu sana. Kama jibu lako ni AJIRA basi, tumia siku ya leo kubadilisha kwanza fikra na mtazamo wako juu ya ajira na zaidi anza kuichukulia ajira yako kama shule/darasa awamu ya pili.

Ukibadili mtazamo wako leo, hakika ndani ya muda mfupi utendaji wako kazini utaongezeka, kero zitapungua, utapata amani zaidi. Pia, kwasababu utaanza kuitumia ajira kama shule basi ni wazi kwamba utaanza kuwa mbunifu zaidi kazini—vyote hivi na mengine mengi vitakuweka kwenye nafasi nzuri ya kuweza kupata masilahi mazuri zaidi— na hivyo kukufanya uweze kumaliza shule yako ya awamu ya pili mapema iwezekanavyo.

NAWATAKIA SIKUKUU NJEMA YA MEI MOSI. Kuendelea kupata maarifa makubwa jiunge na mtandao wa MAARIFA SHOP kwaajili ya kujifunza zaidi.


Habari Njema Kwa Wanaotafuta Ajira

“Yatupasa kutambua kuwa, tabia mbaya unayoijenga ukiwa kwenye ajira ni mali yako na wala siyo mali ya mtu mwingine au shirika lililokuajiri” ~ Cypridion Mushongi
Lengo lako la kutafuta ajira ni nini? Je? Ni kutafuta kulipwa mshahara? kutafuta mtaji? Au ni kwaajili ya kujifunza mambo fulani kama sehemu ya maandalizi ya kufanya kitu fulani hapo baadae? Kimsingi maswali juu ya malengo ya kutafuta ajira ni mengi sana.

Lakini ukichunguza kwa undani unagundua kuwa lengo kuu la watu wengi kutafuta ajira ni kupata pesa kila mwezi na kuitumia. Lengo la kulipwa pesa kila mwezi likishakamilika, wengi ujaribu kutulia na kuridhika huku wakijaribu kubana matumizi ili kiasi kile kinachopatikana kila mwisho wa mwezi kiweze kutosha—japo kuwa huwa hakitoshi. Mshahara duniani kote huwa siyo zaidi ya asilimia 10% ya kile mtu anachozalisha.

Kwahiyo, mara nyingi tunajidanganya kila mara tunapodhani kuwa tutaweza kutimiza ndoto za maisha bora na endelevu kutokana na mshahara (ajira). Tukitaka kufaidi ajira yoyote, lazima tutambue kuwa ajira ni zaidi ya mshahara, huwe mdogo au mkubwa. Ajira yoyote ile inao uwezo wa kutupatia mambo mengine makubwa zaidi ya mshahara.

Ajabu na kweli ni kwamba, watu wengi kwenye ajira mbali na kupata mshahara, tunapata mambo mabaya ambayo kimsingi yamekuwa ni mwiba sugu kwa mafanikio yetu binafsi. Kwa waliowengi, ajira imekuwa ni sehemu ya kujenga tabia ambazo mwisho wake zinaangamiza badala ya kutujenga na kutuinua.
Mojawapo ya tabia mbaya ambazo watu uzijenga wawapo kwenye ajira zao ni pamoja na “kuchelewa kazini; kutegea kazi (uvivu); kulalamika; kupenda malipo ya papo kwa papo (kukosa uvumilivu), kila wakati kufanya vitu vinavyofanana na wenzako kazini (kukosa ubunifu); kupenda kufanyiwa kila kitu; kupenda kupongezwa n.k.

Wakati wote tunapojenga tabia za namna hii, tunadhani tuko salama na hatuoni madhara ya moja kwa moja kwetu, eti! kwasababu bosi wetu anaendelea kutulipa mshahara na marupurupu mengine. Ukweli ni kwamba, kwa tabia za namna hii, hatuko salama hata kidogo.

“Yatupasa kutambua kuwa, tabia unayoijenga ukiwa kwenye ajira ni mali yako na wala siyo mali ya mtu mwingine au shirika lililokuajiri”. Kwa maana nyingine ni kwamba wewe ndiye mmiliki wa tabia uliyoijenga ukiwa ndani ya ajira, iwe nzuri au mbaya ni yako tu.

Kila utakapokwenda utaambatana na tabia zako (mbaya na nzuri). Ikitokea ukahama shirika moja kwenda jingine, shirika unaloliacha linabaki salama, lakini endapo hutabadilika basi tabia zako zote unazihamishia kwenye shirika jipya—hili halitakuwa salama!

Hapa tunapata kujifunza kwamba, endapo tutaendekeza tabia mbaya tuwapo kwenye ajira, tusitegemee kubadilika pale tutakapoanza kufanya shughuli zetu binafsi. Kuna wakati ninaamini kwamba, Mungu anatuwezesha kupata ajira (kufanya kazi ya mtu mwingine), ili atuone na kutupima kabla ya kutupatia kazi (biashara) zetu wenyewe. Matarajio ni kwamba, kama unaweza kufanya vizuri kwenye ajira (kazi ambayo siyo yako), bilashaka utafanya kazi vizuri zaidi kwa kazi ambayo ni yako mwenyewe binafsi.

Umefika wakati sasa tutambue kuwa nafasi za ajira tulizonazo au tunazotarajia kupata, ni awamu ya pili ya SHULE. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, wengi tunapata ajira baada ya kumaliza awamu ya kwanza ya shule, mfano: “shule ya msingi, sekondari, chou” n.k. Kama ilivyo kwa awamu ya kwanza ya shule, awamu ya pili— “ajira”, inakutaka kusoma na kumaliza ndani ya miaka 5—10 kutegemea na kile ulichoajiriwa kufanya.

Ikiwa umejipanga vizuri, miaka 5—10 inakutosha wewe kuanza maisha ya kijiongoza mwenyewe. Ukiwa umeajiriwa huwezi kusema kuwa unajiongoza mwenyewe. Tunasisitiza maisha ya kujiongoza mwenyewe, kwasababu ukiwa bado kwenye ajira ni lazima kufanya kazi zile ambazo unaelekezwa na mmiliki wa ajira yako na siyo kwa mujibu wa unavyofikiri wewe binafsi.

Ni vizuri pale tunapofanya maamuzi ya kuingia kwenye ajira, tupange na kuamua ni muda gani tutatumikia ajira. Muda au miaka tutakayoipanga kukaa ndani ya ajira, lazima iwe inatosha na ituwezeshe kuwa tumekomaa, tumefuzu na kupata sehemu kubwa ya yale yote ambayo yanatuwezesha kuanza kujiongoza au kumiliki kazi.

Unapoona mtu ameamua kutumikia ajira yake kwa miaka mingi, basi ujue kuwa mtu huyo bado haichukulii ajira kama SHULE. Kwa mtu ambaye yeye haichukulii ajira yake kama shule, kwake yeye ajira ndiyo machimbo ya kudumu ya pesa, japo kiasi kipatikanacho huwa hakitoshi kuweza kuleta utajiri au kukutoa kwenye umaskini.

Kwa maneno mengine ni kwamba pesa tunayopata kama mshahara huwa ni kidogo na inasaidia tu kuvumilia umaskini na wala sikututoa kwenye umaskini. Kwahiyo, lazima ujitahidi kusoma kwa bidii na maarifa na umalize shule yako ya awamu ya pili (ajira), ili hatimaye uweze kustaafu mapema na haraka iwezekanavyo. 

Usifikiri kustaafu ajira ni lazima ufikishe miaka 60—hapana! Kustaafu ni pale unapoacha kutumwa kazi; kupewa maelekezo ya nini cha kufanya, muda gani ukifanye, na ukifanye kwa manufaa ya nani, pia kupata uwezo wa kujichagulia watu wa kufanyanao kazi n.k. Wito wangu kwa wote tulioajiriwa ni kwamba lazima tujitahidi kuwa na mtazamo chanya juu ya ajira zetu. Tuendelee kutumia vizuri muda wetu wote ambao tuko ndani ya ajira katika kujenga tabia za mafanikio. 

Kwa kufanya hivyo itatufanya kutoa matokeo makubwa kwa taasisi ambazo zimetuajiri, LAKINI pia tutapata fursa ya kujijenga sisi binafsi katika kila nyanja ya maisha yetu. Lazima tuhakikishe tunafanya kazi kama vile ni za kwetu na kikubwa zaidi, tuendelee kuziona na kuzichukulia ajira kama DARASA kama siyo SHULE. 

Nadhani umeelimika kiasi fulani kutokana na kusoma makala hii na endapo unapenda kuwa miongoni mwa timu ya mtandao wa https://maarifashop.blogspot.com kwa lengo la kuendelea kujifunza masuala yote ya pesa, mafanikio, biashara, ujasiriamali, uongozi na mengine mengi ni kubonyeza hapa: INGIA MAARIFASHOP kwa manufaa yako zaidi.


Fahamu Kwanini Tunasema Muda Siyo Tatizo!
“Kila mtu anatenga muda mwingi kufanya kazi anazotaka zifanyike na hatengi muda kabisa kufanya kazi ambazo hataki”.
Imekuwa ni kawaida watu wengi kulalamika kuhusu kutokupata muda wa kufanya shughuli fulani fulani. Nadhani ni mara nyingi umesikia kauli za kulalamikia ukosefu wa muda wa kufanya kazi fulani fulani. Malalamiko haya, yanatokana na.....
ukweli kwamba, watu kwenye fikra zao wanadhani muda haupo au uliopo ni kidogo sana. Jambo hili siyo kweli, kwasababu kitu MUDA ni kitu cha kutengenezwa na binadamu na hauhitaji kuutafuta kama unavyotafuta vitu vingine.

Binafsi nimekuwa nikisikia kwa watu wakisema “Nataka kufanya kazi au kitu fulani LAKINI tatizo ni MUDA”. Eti! mtu anadiriki kusema kuwa muda ni tatizo. Muda hauwezi kuwa tatizo kama ukiamua au ukiwa na nia ya kufanya kitu fulani.

Kauli nyingi za TATIZO NI MUDA zinaonyesha kuwa watu tuliowengi tunadhani na kuamini kuwa muda unajileta na kujipanga wenyewe. Ndiyo maana watu wengi wamejenga tabia ya kuhairisha mambo kwa matarajio ya kwamba ipo siku ambayo itatokea wakamilishe shughuli hizo za nyuma.

Ukweli ni kwamba kitu muda kinaendana na maamuzi ya kuchukua hatua. Kila utakapoamua kufanya jambo fulani, basi ujue muda utapatikana mara moja na endapo hutaamua kufanya, basi ujue kuwa muda hautapatikana!. Kuna usemi kwamba “Huwezi kukosa muda wa kufanya kitu unachokitaka”. Unapoona mtu anakwambia siwezi kufanya biashara au shughuli fulani kwasababu ya muda, basi ujue kuwa mtu huyo HATAKI KABISA kufanya kazi hiyo. Kinachotokea ni yeye kujificha kwenye kivuli cha KUKOSA MUDA.

Watu wengi tunapenda kutumia MUDA kama kisingizio cha kutofanya vitu ambavyo hatutaki/hatupendi kuvifanya, lakini wakati huo huo pia, hatutaki kuwaudhi marafiki zetu ambao wanataka tushirikiane katika kufanikisha mambo fulani.

Badala ya kumwambia rafiki yako HAPANA moja kwa moja, wewe unadhani atajisikia vibaya na atakuchukia, unaishia tu kumwambia “ningependa kufanya hivyo lakini TATIZO NI MUDA.

Ni wazi kuwa, tumekuwa na mahusiano ya KINAFIKI na watu ambao tunawaita marafiki zetu. Kwasababu kila wanapotutaka tufanyenao kitu fulani, moja kwa moja tunakimbilia kusingizia TATIZO LA MUDA. Hapa ni kwamba hakuna kitu kama “kukosa muda” bali ni kwamba tunaogopa kuwambia marafiki zetu HAPANA, jambo ambalo tunadhani litahatarisha mahusiano yetu na hao tunaowaita marafiki.

Kauli ya “TATIZO NI MUDA” ni mbaya zaidi kuliko mtu akikwambia “HAPANA”. Watu tunaojitambua, tunafahamu fika kuwa neno “HAPANA” lina maana nzuri na ni sawa na kusema “SIYO SASA HIVI”. Lakini kwa yule anayekwambia TATIZO NI MUDA, maana yake ni kwamba, haitatokea hata siku moja ambayo atatenga muda wa kujaribu kufanya hicho kitu ulichomwambia.

Watu wa “TATIZO NI MUDA” ni wengi, na wanafanya hivyo kwasababu, wanadhani kuwa MUDA ni kitu ambacho kinapatikana hivi hivi bila wao wenyewe kuwa wameamua kufanya kazi husika.

Ukweli ni kwamba, kitu kinachoitwa MUDA ni cha kufikirika tu na ni kitu ambacho kipo kwa wingi sana. Yaani ni rasilimali ambayo ipo kwa kila mmoja wetu, ni wewe tu kutumia vyovyote unavyotaka kulingana na kile unachotaka kifanyike.

Kwa taarifa yako ni kwamba, suala zima la muda linakuwepo kama binadamu anazo shughuli fulani ambazo anataka kuzifanya kulingana na mahitaji yake. Kwa maana nyingine ni kwamba, kama mtu akiamua kutokuwa na chochote cha kufanya, kwake yeye dhana ya muda haina maana yoyote.

Mtu ambaye hana kitu kinachomuhitaji kukifanya, kwake yeye dakika hazipo, masaa hayapo, siku hazipo na hata miaka haipo bali yupo yeye tu! Kadili unavyotakiwa kukamilisha shughuli nyingi kwa mara moja ndipo suala la MUDA linakuwepo na linakuwa na maana. Kwasababu watu wote ambao wana kazi za kufanya mara nyingi wanalazimika kuhesabu kila sekunde inayopita.

Maelezo yote hapo juu yanatupeleka kwenye falsafa mpya kuhusu muda; “Kila mtu anatenga muda mwingi kufanya kazi anazotaka zifanyike na hatengi muda kabisa kufanya kazi ambazo hataki”.

Falsafa hii ya muda inalenga kutukumbusha kuwa ukiona hujapata muda wa kufanya kitu fulani, basi ujue kuwa siyo muhimu kwa wakati huo na inawezekana hupendi na hataki kukifanya. Kwasababu, kila binadamu ni mtengenezaji wa muda au nafasi ya kufanya na kutenda kazi mbalimbali. Ukiamua kufanya kitu lazima muda upatikane na ukiamua kutofanya kitu muda nao hautapatikana.

Rai yangu kwako wewe unayesoma makala hii ni kwamba, uache kujiletea msongo wa mawazo yanayotokana na shughuli nyingi ambazo hujazikamilisha au hujazifanya.

Kwa shughuli zote ambazo ulihairisha kwa kisingizio cha kukosa muda wa kuzifanya, uamue kwa dhati leo KUTENGA MUDA na ufanye kila linalowezekana ukamilishe kazi hizo. Katika kutenga muda, unatakiwa uweke kwenye maandishi ambapo utakiri kwa kalamu yako huku ukiandika kuwa, kuanzia leo “NINATENGA MUDA KUFANYA 1,2,3………n.k….KUANZIA TAREHE HADI TAREHE…”.

Kuliko kila mara kulalamikia muda kana kwamba muda ni kitu halisi na chenye uhai. Lazima tufikie mahala tuache kutuhumu vitu ambavyo hata haviongei na wala havina uhai kama vile “Muda”. BINADAMU MUDA TUNAO MWINGI SANA, TUACHE VISINGIZIO, TUPAMBANE KWA KILA HALI, TUFIKIE KUISHI MAISHA YA NDOTO YETU. YETU



Je ni Kweli Uzoefu Unaleta Woga? 

“Kila kitu kipya ambacho unaweza kufikiri ni HALISI hata kama hakijawahi kuwepo” ~ Pablo Picasso ~

Uzoefu ni elimu au uelewa fulani ambao mtu anakuwanao kutokana na kufanya kazi mbalimbali lakini mara nyingi ni.....
kazi au shughuli zinazofanana kila siku. Kwa maana nyingine ni kwamba uzoefu unatoana na mtu kuzoea (mazoea) kufanya kazi kwa mbinu ile ile, ambayo unadhani ni muhafaka kwako. Kwahiyo, uzoefu unafanya akiri yako kutulia bila kujiangaisha kuwaza na kufikiria mambo magumu.

Utafiti umeonyesha kuwa, mtu anapofanya kazi ile ile kwa muda mrefu anapata kuielewa vizuri, japo hilo halizuii changamoto kutokea. Ni ukweli usiopingika kuwa, pamoja na kuwa na watu wengi wenye uzoefu lukuki hapa duniani, bado changamoto zinaendelea kuibuka kila kukicha.

Changamoto hizi zinakaa kwenye jamii husika kwa muda mrefu bila kupatiwa majibu ya uhakika, jambo ambalo linaendelea kusababisha umaskini mkubwa na hasa wa kipato. Kumbe hali hii inatufundisha kwamba changamoto nyingi zinapotokea, zinakuwa nje kabisa ya “Uzoefu” wa mtu alionao, kwanini, kwasababu kama zingekuwa ndani ya uzoefu, kamwe zisingekuwa changamoto na wala zisingeonekana.

Kwahiyo, inatosha kusema kuwa pindi changamoto zinapoibuka mahali popote haijalishi uzoefu ulionao, kwani na wewe mwenye uzoefu unakuwa na fikra zenye kiwango sawa mwanzoni kama yule ambaye hana uzoefu. Sana sana uzoefu unakusaidia kidogo kuwa mvumilivu na wakati mwingine kutokupaniki.

Changamoto zinapotujia sisi wote (wazoefu na wasiowazoefu), tunahitaji kuwa na nia, ujasiri, shauku na msukumo wa ndani wa kutaka kuondoa changamoto iliyo mbele yetu. Endapo nia, ujasiri, shauku na msukumo wa ndani havipo basi tujue kuwa uzoefu wetu tulionao kazini hautasaidia hata kidogo.

Inashangaza kuona kuwa watu wengi wanaamini kwa dhati kabisa kwamba “Uzoefu” walionao ndio kila kitu, na mpaka sasa hawana habari kuwa uzoefu wao huo, pengine ndio umekuwa kikwazo kikubwa cha wao kuendelea kuishi maisha duni.

Athari za watu kutumia zaidi uzoefu katika kuendesha maisha ni zipi?

Kuwa mpinzani wa mambo mapya: Watu wengi wanajivunia sana uzoefu, kiasi kwamba wanaona ndio kitu pekee cha kuleta mafanikio. Mtu akishajiaminisha tayari kuwa ana uzoefu wa jambo fulani anakuwa mgumu sana wa kupokea na kujifunza mambo mengi mapya na wala haoni sababu hata kidogo ya kufanya hivyo.

Kwasasa tutaendelea kushuhudia watu wachache wakizidi kufanikiwa na kuwa matajiri. Watu wengi wanaoamini katika uzoefu walionao, bado wanaendelea kutumia mbinu zile zile ambazo wamezitumia miaka yote kutatua changamoto mpya. 

Kutokana na kulewa sana Uzoefu mara nyingi wamekuwa wagumu kupokea na kujifunza mambo mapya. Ndiyo maana kwasasa wapo watu wengi ambao wao wamehapa kutokuijua Facebook achilia mbali kuitumia – hayo yakiendelea, wale watu ambao tuna uwezo wa kutengeneza picha nzuri ya jambo ambalo halijatokea, tunajitahidi kupokea na kujifunza mambo mapya ambayo tunaamini ni mazuri.

Mfano; tayari watu wengine tunatafuta masoko ya bidhaa na huduma mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii kama vile Face Book (FB). Ebu fikiria mwenzako anatumia FB kuwasiliana na wateja zaidi ya 1000 kwa dakika, wakati wewe siku nzima inapita bila hata kuwasiliana na mteja yeyote na wakati huo huo pengine unazo bidhaa nzuri sana na mpya.

Ni vigumu kutengeneza picha mpya: Wazoefu wengi wanadhani hawana haja ya kujifunza vitu tofauti na vile walivyovizoea. Wengine wanaamini wanajua vitu vingi kama siyo vitu vyote, wanaamini wameona mengi, na kwahiyo wanafanya maamuzi kwa kutumia uzoefu walioupata huko nyuma. Kwao suala la akiri yao kutengeneza picha mpya halipo; JAPOKUWA matumizi ya nguvu akiri katika kutengeneza picha mpya ndiyo huwasukuma na kuwafanya watoto na vijana kufanya maamuzi magumu na pia kuwa na ari kubwa wakati wakifanya kazi zao ili kutimiza ndoto zao za maisha bora.

Ukitumia zaidi uzoefu unakuwa mtu wa kulazimisha: Mtu aliyezama kwenye uzoefu, anapenda kutatua changamoto mpya kwa mbinu zile zile anazozijua siku zote. Watu wa namna hii, mara nyingi huwa hawakubali kujaribu mbinu madala hata kama mbinu zao wanazozijua hazifanyi kazi sawa sawa.

Ikumbukwe kuwa “Changamoto mpya siku zote zitaondolewa na mbinu mpya”, kwasababu kama mbinu za zamani zingekuwa bado zina uwezo wa kuhimili changamoto, basi hizo changamoto zisingeweza kujitokeza ~ Tunahitaji mbinu mpya!

Uzoefu unadumaza uwezo wa kufikiri: Ukiwa tayari umejikusanyia uzoefu kwenye eneo lako la kazi, motisha wa kufikiri, kuhoji na kubuni unakuwa ni mdogo sana. Hali hii ipo sana kwa waajiriwa. Mfumo wa ajira duniniani kote unajulikana kwa kuendeshwa kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu. Hii maana yake nini, ni kwamba, fanya yote ufanyavyo lakini hakikisha hauendi nje ya mipaka ya kazi yako.

Kwahiyo, waajiriwa wa mda mrefu tayari wao wamekariri sheria, kanuni na taratibu ndio maana tunaambiwa “wana uzoefu kazini”. Kwa maana nyingine ni kwamba, hutakiwi kufikiri nje ya miongozo na maelekezo kutoka juu, kwani kila kitu kilishafanyika, wewe unachotakiwa ni kutekeleza kila unachoambiwa kufanya.

Ukikaa kwenye maisha ya namna hii kwa muda mrefu unakuwa ni mtu ambaye huna jipya na kadiri miaka itakavyozidi kusoga mbele, thamani yako nayo itazidi kushuka kutokana na ukweli kwamba hutakuwa kitu kipya cha kuipatia jamii yako au dunia.

Siku zote thamani yako inapanda kulingana na mchango wako katika kutatua changamoto na kero mbalimbali za kijamii, hata kama ni kutatua kero za familia yako inatosha.

Kwahiyo, mjasiriamali hutakiwi kuiga mfumo huu wa maisha (kutumia uzoefu) kwani kwa jinsi mambo yako yalivyo haukufai hata kidogo. Kwa mfumo wa ajira, huo ndio utaratibu na hauwezi kubadirika isipokuwa kubadirika wewe binafsi!


Uzoefu unapunguza kasi ya kuchangamkia fursa: Mara nyingi fursa mbalimbali zinapoibuka, huwa zinakuhitaji wewe kubadirika ili kuendana na fursa hile iliyoko mbele yako. Hali hii inakulazimu wewe kubadirika na kutoka kwenye yale mazoea ya siku zote.

Pia, ili huweze kubadirika lazima utakumbana na changamoto ya kufikiri, kutafakari na kubuni, hali ambayo huleta ugumu kwa mhusika. Kutokana na ugumu huo, mtu anaona ni bora kuendelea na maisha yale ya zamani ambayo umeyazoea na unajisikia vizuri na salama kubaki ulivyokuwa. Kama una sifa zinazofanana na hizo nilizozitaja basi ujue unaelekea kwenye maisha ya kuishi kama bidhaa ambayo ikikaa muda fulani inaoza.

UZOEFU ni muhimu, lakini tusiutegemee kwa asilimia 100% na ikiwezekana, tutumie uzoefu angalau kwa asilimia 40% na asilimia 60% inayobaki tutumie picha mpya kutoka akirini mwetu hasa pale linapokuja suala zima la kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili jamii. Kumbuka kuwa “Yeyote atakayetoa suruhisho ya changamoto inayowakabili watu wengi ndiye atakayelipwa pesa nyingi”.

Picha mpya ndicho kitu pekee kitakacho kupa ujasiri wa kuamua hasa pale utakapopata changamoto na pale utakapolazimika kufanya vitu ambavyo hujawahi kuvifanya. Waliofanikiwa wanasema “huwezi kuwa mtu wa tofauti kwa kufanya vitu vile vile” Kwa maana nyigine, huwezi kuendelea kwa kutegemea mbinu zile zile zilizokufikisha kwenye hali unayotaka kuibadili, ni lazima ubadirike na kuwa mtu yule anayefanana na mafanikio unayoyataka.

Yawezekana hukubaliani na mambo fulani kwenye makala hii, basi nitaomba sana maoni yako ili yasaidie kuboresha uelewa wetu wote juu ya jambo hili. 

Endelea kushiriki mijadala mbalimbali kwa kubonyeza neno MAARIFASHOP au ujumbe kupitia mchumieconomist2009@gmail.com.



Wakati Unatafuta Ajira Fahamu Jambo Hili…..

“Maandalizi mazuri ya kazi nzuri ya kesho ni kufanya kazi nzuri leo”
~ Elbert Hubbard

Kati ya changamoto kubwa tunayopitia kwenye dunia ya sasa ni kwamba kila mtu ana fikra na maoni yake. Na kutokana na hali hii, watu wengi wamekuwa wakichukua maoni wanayopewa na kufikiri ndio ukweli. Lakini...

ukweli haupo karibu kama wengi tunavyodhania.

Watu wengi wanapindisha ukweli kwa manufaa yao binafsi. wanakupa maoni ambayo yatakufanya wewe kuchukua hatua ambayo itawanufaisha wao.
Ndiyo, maana umeaminishwa kwa miaka mingi kuwa bila ajira nzuri huwezi kupata maisha mzuri; bila mtaji huwezi kufanya chochote n.k.
Hivyo ni muhimu mara zote kutafuta ukweli, na ujiulize kila mara kama unachosimamia ni ukweli au maoni tu ya wengine.

Kabla hujafanya maamuzi yoyote makubwa kwenye maisha yako, hakikisha umetafuta na kujua ukweli kwenye jambo hilo. Kushindwa kuujua ukweli utajikuta kwenye changamoto kubwa sana baadae, na hii ni kwasababu ukweli huwa hauzikwi, unafichwa tu kwa muda, ila baadae utajitokeza wenyewe.

Na ifahamike kuwa kupata ukweli ni mchakato siyo kitu cha hapo hapo inabidi kwenda hatua kwa hatua ili kuweza kuupata ukweli halisi.

Moja ya hatua za wewe kuchukua katika kutafuta ukweli, ni wewe kuhoji kila kitu, hoji kila unachofanya, hoji kila kinachofanywa na wengine na hoji kila unachoamini.

Je kinasimamia ukweli? Au ni maoni tu ya watu ambayo wanataka na wengine wayaamini? Kwahiyo, ili uweze kuhoji sawa sawa ni lazima kutumia taarifa mbalimbali zitakazokusaidia kuchambua na hatimaye kufikia ukweli halisi.

Sasa Ukweli Kuhusu Malipo ya Ziada na Mshahara ni Upi?
Mwajiriwa anapofanya shughuli za mwajiri zaidi ya masaa yale ya kawaida, huwa analipwa pesa ya ziada au kwa lugha ya kiingereza “overtime”, wakati yule mwenye kazi (aliyejiajiri), akifanya kazi muda wa ziada anatengeneza uwezekano wa kupata faida ya ziada au tunaweza kusema kwa lugha ya kimombo “over-profit”.

Kwa utaratibu na kanuni za ajira, malipo ya ziada (overtime), mara nyingi huwa ni 5% ya uzalishaji ulioufanya kwa ule muda wa ziada wakati, wakati malipo ya faida ya ziada (over-profit), huwa ni asilimia 100% ya kile kilichozalishwa.

Kwa maana nyingine ni kwamba, mwajiliwa yeyote unapoweka bidii zaidi ya muda ule mliokubaliana ni sawa na kusema kuwa unamwendeleza au unamchangia mwenye kazi kwa asilimia 95% zaidi.

Kwa uliye na kazi (umejiajiri), unapoweka bidii zaidi ya ule muda wako wa kufanyakazi unakuwa umechangia kujiendeleza kwa asilimia 100% zaidi kwa chochote kilichofanyika katika muda huo wa ziada.


Kwa dondoo hizi unaweza ukaanza kujiuliza je, kuajiriwa ni vibaya? HAPANA; isipokuwa jambo la msingi unalohitaji kulitambua ni kwamba kuajiliwa ni uamzi kama maamuzi mengine ambao unafanywa na mwajiriwa katika kutumia muda na ujuzi wake kukamilisha shughuli au majukumu mbalimbali kama anavyopangiwa na mwajiri au mwenye kazi.


Unapokuwa umetimiza majukumu yako kama mwajiriwa, basi ndipo mwajiri anapochukua jukumu la kukugawia sehemu ya kile ulichozalisha na mara nyingi huwa siyo zaidi ya asilimia 10% ya kile ambacho umekizalisha, wenyewe wanaita “mshahara”.

Kama bado hujanielewa usihofu, kwani ninachojaribu kukupatia kupitia makala hii ni mwanga utakao kuongoza katika kuusaka na hatimaye kuujua ukweli halisi. Na ni wazi kwamba ukipata ukweli halisi basi utakusaidia wewe kufanya maamuzi sahihi na hivyo kujihakikishia mafanikio makubwa kimaisha.

Tunapomurika picha nzima ya ajira” tunasoma haya: Hata huwe na bidii kiasi gani, hakuna ajira iliyobuniwa duniani kukutajirisha au kukupa uhuru wa kipato. Kwahiyo, hata ujitetee vipi (kama ambavyo unajifikiria sasa hivi unaposoma mistari hii); hata ujifanye una ajira nzuri, utajiri katika mazingira ya haki sahau kabisa.

Uhalisia ni kwamba hata ukifanya yote ufanyayo, jifariji uwezavyo na ajira yako, ukweli utasimama pale pale kwamba maisha tunayoishi sasa hivi yanatulazimisha tutafute pesa zaidi ya kutegemea mshahara peke yake.

Kwasababu kokote kule hakuna mshahara unaotosha. Na wewe mwenyewe ni shaidi wa namna tunavyopigika siku chache baada ya kila mwezi tunapopokea mshahara.

Endelea kutukuza, kuabudu na kufurahia ajira, lakini elewa kwamba hututapata mafanikio ya maana sana kiuchumi, endapo tutaendela kutegemea mshahara na hizo “overtime’ peke yakeee! Na sasa hivi, wewe na mimi tunahitaji “gia mpya” ili kuinua hali ya maisha na hatimaye kufikia uhuru wa kipato.

Kama unataka kutumiwa makala mpya moja kwa moja kila zitakapochapishwa ni rahisi, unahitaji kufanya jambo moja nalo ni kubonyeza neno “MAKALA”, kisha weka e-mail yako tayari utakuwa umemaliza zoezi.

Weka maoni na tushirikishe mawazo yako. Endapo umejifunza chochote kutokana na makala hii, basi washirikishe marafiki zako kwa kuwatumia makala hii.

WASILIANA NAMI: WhatsApp: 0788 855 409.
E-mail: mchumieconomist2009@gmail.com. 


Chimbukola Umaskini kwa Waajiriwa ni Hili Hapa

  • Waajiriwa wengi wanauza nguvukazi ikiwa bado “ghafi”
  • Ukiuza nguvukazi ghafi umeuza “mtaji” na kuuza mtaji ni “kufirisika” jumla
Umaskini ndani ya kundi la wasomi unazidi kuingia kwa kasi ya ajabu kadili siku zinavyozidi kwenda. Kundi la watu ambao wako kwenye hatari kubwa zaidi ni hasa wale tulioko kwenye “ajira”. Ukweli ni kwamba watu wengi walioko kwenye ajira, kitu pekee wanachouza ili kupata kipato ni nguvukazitena ambayo bado ni “ghafi”.  

Uzoefu unaotokana na tafiti zilizofanywa, unathibitisha kuwa zipo sababu nyingi zinazosababisha waajiriwa na hasa wasomi wengi kuwa maskini. Lakini kubwa zaidi ni utamaduni wa wasomi kuendelea kuuza nguvukazi ikiwa bado ni “ghafi” (nguvukazi ambayo haijachakatwa). Katika ulimwengu wa “uwekezaji” nguvukazi ghafi ni mtaji muhimu sana, ambao ukichanganywa na mitaji mingine kama vile mashine, una uwezo wa kuzalisha bidhaa na huduma zenye thamani kubwa kwa watu wengine.

Ukiuza nguvukazi ghafi unakuwa umeuza “mtaji” wako: Waajiriwa wengi tumeendelea kukumbwa na adha kubwa ya umasikini kutokana na kushindwa kutambua ukweli kwamba mara nyingi kwenye maisha yetu ya ajira tumekuwa tukifanya zaidi biashara ya kuuza mtaji tulionao (nguvukazi) kwa matajiri wenye hitaji la mitaji.
Ikumbukwe kuwa, ili uweze kuzalisha bidhaa na huduma unahitaji mitaji ya aina mbalimbali ikiwemo nguvukazi ghafi. Ndiyo maana matajiri wengi wanapendelea zaidi kununua mitaji kwaajili ya kuzalisha bidhaa na huduma, ambazo huwapatia faida kubwa sana. 

Katika biashara yoyote duniani, kuuza mtaji ni kufirisika jumla. Kwahiyo, umasikini tulionao umetokana na kuuza mtaji wetu kila siku tunapotumikia ajira zetu. Kwa maana nyingine waajiriwa wengi tunafirisika kila siku ya Mungu tunapokwenda kazini.

Watu wanaouza zaidi nguvukazi ghafi wanabaki kuwa maskini kutokana na ukweli kwamba thamani ya nguvukazi ghafi huwa ni ndogo sana, kwasababu inapatikana kwa wingi na haina usumbufu kuipata. Kwa mfano: ukijifanya kutoza bei kubwa nguvukazi yako; waajiri wengi watakukimbia na chapuchapu watapata watu wengine wenye kuuza nguvukazi ile ile kwa bei nafuu sana.

Hivi ndivyo unavyouza nguvukazi ghafi: Unauza nguvukazi ghafi pale unapotumia nguvu yako kufanyakazi ya kuzalisha bidhaa na huduma ambazo siyo mali yako bali ni mali ya mtu aliyekuajiri (mwajiri). Unahitaji kufahamu kuwa, mwajiri amekuajiri ili umpatie (umuuzie) nguvukazi ambayo ni mtaji wa kuzalisha bidhaa na huduma ambazo ni mali yake binafsi. 

Kwakuwa bidhaa zinazozalishwa ni za thamani kwa watu wengine, basi ni wazi kwamba watu hao watampatia pesa mwajiri wako ili kupata bidhaa; LAKINI hawatakupatia pesa wewe, kwasababu wewe unayo nguvukazi peke yake, ambayo siyo hitaji muhimu kwa wateja wenye pesa zao. 

Ukiuza nguvukazi ghafi unauza “muda” wako: Kwakuwa umeajiriwa kwa madhumuni ya kutoa nguvukazi kwa mwajiri wako, basi thamani yako inapimwa kwa kuangalia muda unaoutumia kufanya kazi. Ili uweze kulipwa ni lazima kila siku ufike kazini na kusajiri muda wako. Usipoonekana kazini hakuna malipo yoyote, kwasababu muda wako utakuwa hujauwekeza kwa mwajiri. 

Kwahiyo, unapouza nguvukazi ghafi basi ujue umeuza “muda” na binadamu wa kawaida hawezi kufanya kazi zaidi ya masaa nane kwa siku. Masaa yote haya unafanya kazi bila kupumzika na kuzalisha vitu vyenye thamani kubwa kuliko mshahara unaolipwa na mwajiri wako. 

Haijalishi, thamani ya vitu vilivyozalishwa ni kubwa kiasi gani, mshahara wako unaolipwa unaendelea kubaki pale pale kila mwezi. Hali hii ndiyo inakufanya wewe mwajiriwa kukosa muda wa kufanya vitu vyenye kukuletea faida kubwa na mafanikio maishani, na hivyo kuzidi kuwa maskini kadiri umri wako unavyoongezeka.

Ukiuza nguvukazi ghafi huna cha kurithisha familia yako: Kama unauza nguvukazi ghafi siyo rahisi kuirithisha kwa watu wako wa karibu, kwasababu nguvukazi kama ilivyo haihamishiki kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Kama kitu hakihamishiki ni vigumu pia kukibadilisha kwa urahisi kuwa pesa.

Hali hii inazidi kutukumba wasomi na waajiriwa tuliowengi kutokana na ukweli kwamba unakuta umeajiriwa kwenye kampuni kubwa na una cheo kikubwa lakini ukifukuzwa au kufariki, haitokei mke au mtoto wako akapewa nafasi kama uliyokuwa nayo na wala familia haiwezi kutumia vyeti vyako vya elimu kuomba kazi. Lakini kama ungekuwa kwa mfano umeandika vitabu, hata ukifa hakimiliki ya kuendelea kuvichapisha na kuviuza inahamishiwa kwa warithi wako na wanaendelea kufaidi sawa na wewe ulivyokuwa ukifaidi.

Ukiuza nguvukazi ghafi unapata hasara: Hasara kubwa unayoipata kutokana na kuuza nguvukazi ni pale unapoishia kuuza kitu kimoja tu! Nacho ni nguvukazi. Hali hii inakubana kiasi kwamba unajikuta unalazimika kumtegemea mteja mmoja ambaye ni “mwajiri” na inakuwa siyo rahisi kubadilisha mteja kadiri unavyotaka.
Endapo ukiamua kuchakata nguvukazi yako na hatimaye kuzalisha bidhaa na huduma za thamani ni rahisi kupata wateja wengi, ambao ndio huleta mapato makubwa.

Hasara nyingine unayopata pindi unapouza nguvukazi ghafi ni kuendelea kubaki kwenye kundi la watu maskini ambao wanapata kipato hai (active income), yaani unapata pesa unapofanya kazi tu, ukiacha pesa hakuna. Endapo, ikitokea unaumwa au umesafiri basi ujue hakuna pesa itakayoingia.

Ndiyo maana unakuta mtu ni tajiri leo kwasababu anafanya kazi ya kibarua, lakini baada ya muda mfupi unakuta ni maskini na kwa waajiriwa ni hivyo hivyo wanakuwa na pesa wakiwa bado kazini LAKINI wanapostaafu ajira wanarudia kwenye hali ya umaskini jambo ambalo huwafanya watu wengi kufa miaka michache baada ya kustaafu.

Washindi dhidi ya umaskini ni wale walioamua kuchakata “nguvukazi” yao: Ukweli ni kwamba kila mchakato wowote lazima utoe matokeo. Matokeo ya kuchakata nguvukazi ghafi ni “bidhaa au huduma” zenye thamani kubwa kwa watu wengine. Kitendo cha kuchakata nguvukazi kinatokana na matumizi ya nguvu ya akiri pamoja na nguvu ya mwili kwenye rasilimali kama ardhi, maliasili, ujuzi, pesa n.k, kwa lengo la kupata mali au bidhaa kwaajili ya watu wengine. 

Ukishapata bidhaa zenye thamani (manufaa) kwa watu wengine, basi mara moja watakuletea pesa ili kujipatia bidhaa na huduma muhimu kutoka kwako. Kadiri utakavyotengeneza bidhaa nyingi na zenye thamani kubwa ndivyo utakavyopata pesa nyingi ambayo haina kikomo. 


Ni wakati sasa tuamke na tujibidishe sana kwa kuandaa mazingira yatakayotuwezesha hasa sisi wataka mafanikio kuuza “matokeo” ya nguvukazi badala ya utamaduni wa sasa wa kuuza nguvukazi ghafi. Ukweli ni kwamba, unapokuwa mtu wa kuuza matokeo ya nguvukazi ambayo ni bidhaa na huduma mbalimbali, tayari unakuwa umemaliza kazi, kinachofuatia ni kuendelea kuuza bidhaa hizo na wakati huo huo unakwenda kuwekeza muda wako huo kwenye kuzalisha vitu vingine, huku akiendelea kufaidi matunda ya kazi aliyoifanya mwanzo.

Kwa watu wote na hasa waajiriwa tunaotaka mafanikio makubwa, ni lazima kila mmoja wetu ajiwekee tarehe ya mwisho ya kuacha kuuza nguvukazi ghafi. Kila mmoja akifikia tarehe yake ya mwisho kuuza nguvukazi ghafi, mara moja aanze kujikita katika kubadili nguvu ya akiri na hisia kuwa bidhaa na huduma zenye kuwa suruhisho la kudumu kwa matatizo na changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wengine.

Kwakuwa utazalisha bidhaa na huduma zenye kuwa na manufaa makubwa kwa watu wengine, basi na wao watakupatia zawadi ambayo ni pesa, ili kujipatia kila kilicho bora kutoka kwako. Tukiweza kufanikisha azima hii, basi tutatajirika kutokana na ukweli kwamba watu wengi kwasasa wanataka bidhaa na huduma ambazo ni suruhisho ya changamoto zao. 
Wateja ni wengi ambao wako tayari kununua kila kitu kitakachozalishwa ilimradi kina thamani kwao ~ kwahiyo soko ni kubwa. Nchi yetu inapokaribia kuingia uchumi wa kati, mahitaji ya bidhaa na huduma zitokanazo na nguvu ya akiri/fikra zitazidi kuongezeka. 

Bidhaa zenyewe ni kama vile muziki, sanaa, vitabu, program za mafunzo ya ujasiriamali/biashara/afya/kilimo/majengo pamoja na machapisho juu miongozo mbalimbali ya uwekezaji katika mambo ya utalii, uwindaji, gasi, mafuta, madini, kilimo n.k.

Uchumi wa watanzania ukizidi kuongezeka na idadi ya wasomi ambao ndio wahitaji wakubwa itazidi kuongezeka huko tuendako ~ Kwahiyo ewe mtanzania mwenzangu, anza kuchukua hatua leo, wakati ni sasa.



Uhuru wa Kipato Unaletwa na Mchakato Siyo Shughuli
  • Ukifanya kazi ki-shughuli ni sawa na mtu anayesukuma mkokoteni kwa kulizunguka duara
  • Uhuru wa kipato (pesa) unawezekana tu kama utafanya kazi zako “Ki-mchakato

Watu wenye busara waliwahi kusema kuwa “maisha ni safari ndefu”, na kawaida ya safari ya maisha, ni pamoja na kukutana na vitu vingi njiani. Bila kuwa tumejipanga, vitu vingi tunavyokutana navyo safarini, vina uwezo mkubwa sana wa kutukwamisha na hatimaye kushindwa kufikia mwisho wa safari yetu.

Ili tuweze kumudu safari yetu maisha na hatimaye kufikia yale maisha ya ndoto zetu; kitu kimoja muhimu ni namna gani tunavyojipanga pamoja na mitazamo yetu juu ya kile tunachofanya kila siku.

Ukiangalia utaratibu mzima ambao watu wanautumia katika kufanya kazi zao, utaona makundi ya aina mbili. Aina ya kwanza ni kundi linalofanya kazi “ki-shughuli” na kundi la pili ni wale wanaofanya kazi “ki-mchakato. Kwa maana nyingine makundi haya mawili yanafanya kazi kwa kufuata mitazamo tofauti, ndiyo maana leo hii tuna watu wachache waliofanikiwa huku wengine wengi wakibakia pale pale miaka yote ya maisha yao.

Shughuli Hasa ni Kitu Gani? Shughuli ni kitendo kinachotakiwa kufanyika au kinachofanyika ili kukamilisha sehemu fulani ya kazi. Pia, shughuli inasimama kama kitu kimoja na ni cha kipekee, ikimalizika imemalizika, huna haja ya kuirudia. Ukiweza kufanya na kukamilisha shughuli moja peke yake haitoshelezi kutoa bidhaa husika. Lazima zifanyike shughuli zaidi ya moja ndipo bidhaa iliyokusudiwa iweze kupatikana.

Mfano: kama wewe shida yako ni kula chakula, lazima ujue kuwa, ili chakula chako kiwe tayari, lazima shughuli zaidi ya moja zifanyike, kutegemea mtu na mtu. Kuna mwingine ataanza kwa kununua mkaa, mwingine ataanza kwa kuwasha moto, na mwingine ataanza kwa kununua mchele n.k.; mpaka shughuli ya kupakua na hatimaye shughuli ya mwisho ya kula chakula.

Kwahiyo, endapo utakamilisha kufanya shughuli mojawapo na ukaishia hapo ni wazi kwamba hutaweza kula, kwasababu chakula kitakuwa hakijawa tayari. Kwa maana nyingine tunaweza kusema kwamba, hakuna bidhaa inayoweza kupatikana kwa kukamilisha shughuli moja peke yake, lazima shughuli zote muhimu zikamilike, ndipo matokeo au bidhaa tarajiwa ipatikane.

Kwa malengo ya kupata matokeo tarajiwa, inakubidi hujitahidi kukamilisha shughuli zako zilizopangwa, ili kupata matokeo tarajiwa. Endapo utaishia kukamilisha shughuli moja kati ya zote zinazotakiwa kufanyika, basi ujue kuwa hutaweza kupata au kuzalisha kitu chochote chenye thamani inayokusudiwa na wateja.

Mchakato Hasa ni Kitu Gani? Mchakato ni  mpangilio maalumu wa matukio au shughuli zaidi ya moja kwaajili ya kutoa/kuleta matokeo yanayokusudiwa. Ili mchakato uwepo, ni lazima shughuli husika ziwe na uhusiano wa karibu. Shughuli moja ikikamilika inakuwa ndio kianzio cha shughuli inayofuata na hatimaye kunakuwa na mwendelezo maalum hadi kufikia matokeo tarajiwa.

Kwahiyo, uzalishaji wa bidhaa yoyote unafuata utaratibu wa ki-mchakato. Ili uweze, kukamilisha kazi fulani au uweze kuzalisha bidhaa fulani, kunakuwapo na matukio au shughuli zaidi ya moja ambazo ziko kwenye aina fulani ya mnyororo. Na mnyororo huo ndio unakuwa na vipingiri pingiri ambavyo kila kipingiri, unaweza kusema ni shughuli au tukio moja. Kwa maana nyingine ni mchakato tu ndio una uwezo wa kukamilisha bidhaa.

Kazi ya kusaka mafanikio makubwa na hasa uhuru wa kipato (pesa) inawezekana tu kama utafanya au kuratibu kazi zako “Ki-mchakato  badala ya kuendelea na mfumo wa watu waliowengi, ambao utafuta eti! maisha bora “Ki-shughuli”. Na shughuli nyingi za utafutaji tunazofanya hazina uhusiano, mpangilio wala mwendelezo wenye tija.

Pia, shughuli hizi, hazina uratibu wowote wala uhusiano na ndoto zetu au malengo yetu ya muda mrefu. Matokeo yake tumejikuta tunapata matokeo hafifu, hali ambayo imeendelea kutukatisha tamaa na kudhania kuwa kupata uhuru wa kipato au pesa ni jambo ambalo haliwezekani na kama likiwezekana basi ni bahati.


Weka mpango wa kufikia malengo yako: Unapoanza safari yako ya kutafuta uhuru wa kipato (pesa) ni lazima ujipange, ikiwa ni pamoja na kufikiri kwa kina juu ya maisha yale unayotamani kuyaishi. Ukishajua ndoto yako ni ipi au mafanikio unayotarajia ni yapi, basi inakuwa rahisi kufahamu mchakato utakaopitia hadi kufikia kile unachotaka.

Ubainishaji wa mchakato kwaajili ya safari yako ya kwenda kwenye ndoto zako, unaambatana na zoezi la kuainisha shughuli zote muhimu zitakazotakiwa kufanyika hadi kufikia maisha ya ndoto yako. Pia, inakupa fursa ya kuweza kufahamu ni muda gani utautumia kufika hapo unapotaka kwenda.

Ukifanya kazi ki-mchakato ni rahisi sana kutathimini maendeleo ya kazi yako na unaweza kupima na kuona uko mbali au karibu kiasi gani na ndoto zako. Kwahiyo, inatosha kusema kwamba “mafanikio yoyote ni mchakato”. Na mchakato ndio unazaa mpango kazi, ambao ukifuatwa una uwezo wa kukutoa pale ulipo hadi pale unapotaka kwenda.

Ukifanya kazi ki-shughuli ni sawa na mtu anayesukuma mkokoteni kwa kulizunguka duara. Kwa mtu yeyote anayezunguka duara, siyo rahisi kufika anapotaka kwenda, kwani muda wote atakuwa anazunguka na kurudi aliko toka. Kwahiyo, maisha ya kufanya kazi ki-shughuli ni sawa na mtu anayezunguka mduara.  

Ndiyo maana unaweza ukakuta mtu kwa mfano anafanya biashara ya kununua na kuuza vitu na unakuta miaka nenda rudi yuko pale pale wakati kila siku anakwenda ananunua vitu na vinanunuliwa basi.

Sababu inayomfanya awe hivyo ni kwamba mtu huyo anafanya biashara yake kama shughuli na anajikuta kila mara anarudia shughuli ile ile miaka yote bila kupiga hatua yoyote. Yote haya yanatokea kwasababu “mtazamo wa biashara yako ni wa ki-shughuli badala ya mtazamo wa ki-mchakato”.

Unapoanza kufanya kazi au biashara yako kwa mtazamo wa ki-mchakato inakusaidia sana kupambana na changamoto. Lakini pia uvumilivu pale matatizo yanapojitokeza, ni rahisi kuvumilia kwakuwa unakuwa unafahamu ni wapi unaenda na utafanya kila liwezekanalo, ili kuweza kufikia malengo au ndoto zako. Ukiwa na mchakato wako ambao umeandikwa, unakusaidia kutokuangalia wengine wanachofanya badala yake, wewe unakomaa na jambo moja tu la kukamilisha mchakato wako.

Kufanya kazi Ki-mchakato kunahitaji umakini mkubwa sana, na umakini huu hauji hivi hivi, bali ni kwa kujenga tabia ya kujisomea vitabu na kujifunza kutokana na watu waliofanikiwa. Kama wewe ni mmojawapo wa wale wanaopenda kujifunza bonyeza KUJIUNGA NA PROGRAMU; kisha weka Email yako, tayari kwa kupokea makala nzuri za jinsi ya kupata mafanikio ya kifedha na kibiashara.

Kwa maelezo zaidi wasiliana name kwa namba:
WhatsApp: +255 788 855 409

KARIBU TWENDE KAZI PAMOJA




Sumu ya Umaskini ni Kufanya Kazi


Ni ukweli usiopingika kuwa umasikini ni kero kubwa hapa kwetu Tanzania na umekuwa kikwazo cha maendeleo ya watanzania kwa muda mrefu. Imefika mahali, watu wengine wamekata tamaa na wengine wanahisi kuwa labda Mungu ameamua wawe hivyo. Kosa kubwa lililofanyika na linaloendelea kufanyika ni tabia au utamaduni wa watu kuukubali umaskini na kuuona umaskini kama sehemu yao ya maisha.

Ndiyo maana hadi leo watu unawasikia wakisema na kujivunia wingi wao kama walalahoi au watu maskini. Kitendo cha kuukubali umaskni na kuufanya huwe kitu cha kawaida,  ndiyo sababu ya watu wengi kukosa ari, nguvu, ubunifu, shauku, juhudi na MAARIFA ya kufanya kazi ambazo matunda yake yatakuondolea umaskini. Kwahiyo, inatosha kusema kwamba, matunda ya kazi ndiyo yenye uwezo wa kipekee wa kumuondoa mtu yeyote kwenye mduara wa umaskini.

Lakini pamoja na hofu ya kushindwa kuondoa umaskini, dawa ni moja tu nayo ni kufanya KAZI. Ni vizuri kukumbuka kuwa tunaposema KAZI hatumaanishi ajira, bali tunamaanisha utumiaji wa akiri pamoja na nguvu ya mwili kwenye rasilimali kama ardhi, maliasili, ujuzi, pesa n.k.), ili kupata mali au bidhaa kwaajili ya watu wengine. Ukishapata bidhaa zenye manufaa (thamani) kwa watu wengine, basi mara moja watakuletea pesa kwa kubadilishana na bidhaa yako. Kadiri utakavyotengeneza bidhaa nyingi ndivyo utakavyopata pesa nyingi.

Wakati tunapofanya kazi, ni muhimu kufahamu kuwa, inahitajika kutumia nguvu zote mbili, yaani nguvu ya mwili na akiri (fikra). Mara nyingi, kwenye harakati za kupambana na umaskini, watu wengi tumeshindwa kupata mafanikio na sababu mojawapo imekuwa ni utumiaji wa nguvu ya mwili zaidi kuliko nguvu ya akiri (nguvu katika hali ya kufikiri na ubunifu).

Matumizi ya nguvu ya akiri katika KAZI yanahusisha zaidi kujitambua na kufahamu ni kitu gani unatakiwa kufanya na kwasababu gani, kutambua mahitaji ya watu wengine, kuongeza thamani na kufanya bidhaa kuwa bora zaidi, kuwa mbunifu kwa kila kazi unayofanya bila kujali ukubwa wake n.k.

Nguvu ya akiri na mwili ilibadilisha makapi ya ngano kuwa chakula cha mifugo: Miaka ya nyuma kidogo, kiwanda cha bia jijini Mwanza kilikuwa kikitupa makapi ya ngano kwenye madampo ya takataka, kutokana na ukweli kwamba hakuna aliyetambua na kuthamini hicho kilichokuwa kikitupwa. Watu wengi hawakuthamini makapi haya, kwasababu walikuwa hawajatumia nguvu ya akiri kuona makapi ya ngano kama kitu cha thamani.

Baada ya baadhi ya watu kutumia nguvu ya akiri, ndipo baadhi yao wakaanza kutengeneza chakula bora cha mifugo ambacho mahitaji yake kwa wafugaji ni makubwa sana. Leo hii tunashuhudia watu hawa wakitajirika baada ya kutumia nguvu ya akiri na mwili kugeuza makapi ya ngano (rasilimali) na kuwa chakula cha mifugo (mali) yenye thamani kubwa.

Mapanki ya samaki: Mwanzoni kabisa mapanki ya samaki, yalikuwa yanatupwa kwenye madampo ya takataka. Tofauti na makapi ya ngano, haya yalitoa harufu mbaya hasa pale yalipoanza kuoza na hali hii ilisababisha kero na uchafuzi wa mazingira hasa kwa wakazi waliokuwa wakiishi karibu na madampo hayo.

Lakini, watu walipoamua kuutmia nguvu yao ya akiri ndipo wakagundua kuwa kuna uwezekano wa kugeuza mapanki haya yakawa mboga (supu) au chakula kwa binadamu. Lakini zoezi la kubuni na kuongeza thamani halikuishia hapo, badala yake, watu walianza kutengeneza chakula cha mifugo hasa kuku.

Leo hii, watu walioajiriwa na kujiajiri kwenye bidhaa zitokanazo na mapanki ni wengi sana na wanapata kipato kwaajiri ya kuendesha familia zao. Kutokana na KAZI ya kuongeza thamani kwenye mapanki ya samaki, ni wazi kwamba wameweza kupunguza umaskini wao tofauti na huko nyuma walipokuwa hawajaanza kutumia nguvu yao ya mwili na akiri.

Kufanya kazi kunahitaji nidhamu ya hali ya juu. Mwanzoni mwa miaka ya sitini, Tanzania ilikuwa ina hali ya kiuchumi sawa na nchi nyingi za Asia; mfano: Singapore, Indonesia, Korea, China n.k. lakini cha ajabu ni kwamba leo hii nchi hizi ndizo zimekuwa wadau wetu wakubwa wa kutupatia misaada ya aina mbalimbali.

Tofauti ya maendeleo kati ya Tanzania na nchi hizi za Asia, ni nidhamu ya kufanya kazi. Wote tuliongozwa na siasa za ujamaa na umoja LAKINI sisi pamoja na kufanikiwa kuwa wamoja na wajamaa, tumekuwa na nidhamu ndogo ya KAZI, ambapo wengi wanategemea kupata huduma za bure kutoka serikalini bila wao kufanya kazi. Matokeo ya kutofanya kazi kwa bidii ni kwamba hapa Tanzania kila kukicha umaskini unaongezeka.

Wakulima wengi Tanzania wanakwenda shambani saa mbili asubuhi na kutoka kati ya saa tano hadi saa sita mchana. Kwa maana nyingine watu hawa kwa wastani wanafanya kazi masaa 3 hadi 4 kwa siku. Kuna wachache baadhi ya wakulima wanafanya kazi masaa 6 hadi 8 kwa siku. Hawa wanafanya kazi masaa matatu hadi manne zaidi ya wenzao. Wakulima wanaofanya kazi masaa mengi ni wazi kwamba wanapata mavuno mengi – na hapa wanaambiwa kuwa wametumia uchawi LAKINI kilicholeta tofauti ni yale masaa 3-4 waliyofanya kazi zaidi ya wenzao.

Kufanya kazi ni suala la mtu mmoja mmoja: Umaskini utaondoka kama kila mmoja atalichukulia suala la KAZI kuwa la binafsi badala ya kulichukulia kuwa ni la ujumla. Inatupasa kila mmoja, ajitathimni mwenyewe na ujiulize iwapo maisha anayoishi hivi sasa kama anayafurahia au la!.
Baada ya hapo kila mmoja kwa nafasi yake awekeza juhudi na MAARIFA kwenye kazi. Tukumbuke pia kuwa KAZI ni sheria ya Mungu na bila kufanya kazi hatuwezi tukaishi maisha mazuri.

Ili uweze kufanya kazi kwa malengo ya kuondoa umaskini, utahitajika kuimalisha na kuongeza nguvu yako ya akiri (fikra). Jambo hili linawezekana iwapo utajiwekea utaratibu wa kujifunza kitu kipya kila siku NA kama na wewe ni mmojawapo wa wale wanaotaka kujifunza bonyeza KUJIUNGA NA PROGRAMU  kisha weka barua pepe yako, na hapa utakuwa tayari kushiriki programu hii ya mafunzo juu ya mafanikio ya kifedha.
Mafunzo haya yatatolewa bure kuanzia 15-30/09/2015, kupitia barua pepe utakayosajiri. Ikiwa utashiriki mafunzo haya, basi tarajia kupata thamani kubwa sana, ikiwemo kubadili mitazamo hasi uliyonayo juu njia bora za kufikia uhuru wa kipato. Kama unafikiri hutapata muda wa kushiriki programu hii muhimu, basi mshirikishe rafiki yako, ambaye unamjua anapenda kujifunza.
Kwa maelezo zaidi juu ya programu hii ya mafunzo whatsApp: +255 788 855 409 au E-mail: mchumieconomist2009@gmail.com.
KARIBU TWENDE KAZI PAMOJA
 



Elimu ya Ajira Haiwezi Kukupa Kazi

  Mfumo wa Elimu Umetujengea Mtazamo wa Kutafuta “Ajira” Badala ya “Kazi”

Zaidi ya Asilimia 90% ya Watu Wenye Utajiri Mkubwa Walitafuta Pesa Nje ya Mfumo wa Ajira....MaanaWalitengeneza Kazi!.


Katika makala ya “Ajira Siyo Kazi ni Ajira na Kazi Siyo Ajira ni Kazi.... niliandika kuhusu tofauti iliyopo kati ya kazi na ajira, ambapo tuliona kuwa kazi” ni majumuisho ya majukumu mbalimbali uliyojipa wewe mwenyewe kazi, unajisimamia na kujiwajibisha mwenyewe kutimiza majukumu uliyojipa mwenyewe bila kutegemea kulipwa chochote mpaka matunda ya kazi hiyo yapatikane, hata kama ni muda mrefu (mwaka na zaidi). Na tuliona kuwa “Ajira” ni kufanya kazi ambayo siyo ya kwako, waweza kuwa unaipenda au huipendi. Kwa maana nyingine katika “ajira” unapangiwa majukumu maalum ya kufanya na mwenye kazi, ukiyakamilisha basi umemaliza kazi, zaidi ya hapo yanayobaki hayakuhusu.

Ukifuatilia kwa undani zaidi juu ya mfumo wa elimu duniani, utagundua kuwa mfumo huu umetujenga katika mtazamo wa kutafuta na kupata AJIRA badala ya  KAZI. Kama hivi ndivyo, basi tujue kuwa tumepata elimu ya yale tu! ambayo wenye kazi wanayataka na lengo lake likiwa ni moja tu “kupata watu watakaomudu majukumu ambayo watapangiwa na wenye kazi. Haijalishi  kama elimu hii inazingatia maslahi na matakwa yako, ukishindwa unatupwa nje na kubatizwa jina la huna akiri na wewe uliyepatwa na mkasa huu ukilikubali tu jina hili, umekwisha!.

Ukifahuru usijisifu sana na wala ukishindwa usijilaumu wala kuumia sana, kwani unapofahuru ni sawa na kusema “umekuwa mahili katika kujua yale tu kwa kiasi kikubwa wanayoyataka wengine”. Lakini tukumbuke kuwa yale wanayoyataka ni mambo machache sana ukilinganisha na yale yote unayoyahitaji ili kupata maisha ya ndoto yako. Unapokuwa umeshindwa tunasema husiumie sana kwasababu yawezekana yale uliyoyajua na kuyapenda kuyasoma hayakuwa mengi na hayakufundishwa kwasababu tu hayakuwa katika orodha ya yale wanayotaka wenye kazi. Kwahiyo, unaposhindwa mtihani usivunjike moyo bali huendelee kujiona kuwa wewe ni mwenye akiri nyingi na unaweza vitu vingi, isipokuwa vitu hivyo abavyo unaviweza, bado vingi haviko kwenye mitahala ya elimu rasimi ambayo umeshidwa. Habari njema ni kwamba, vitu hivyo unavyovijua vizuri, ukivitumia unaweza kutengeneza kazi kubwa yenye kukuletea matunda mengi sana, ambayo watu watakuletea pesa nyingi ili ujipatia matunda hayo.

Ukiwa wewe ni msomi, utakubaliana na mimi kuwa iwapo ukiamua kwenda nje ya mfumo wa ajira utagundua kuwa mambo mengi yaliyoko nje ya ajira ni tofauti kabisa na yale tuliyonayo vichwani mwetu na hasa sisi wenye shahada kutoka vyuo vikuu. Kumbe yale mambo ya nje ya ajira nayo yanahitaji kujifunza upya bila kujali kuwa wewe una cheti au shahada. Lakini, masomo ya nje ya ajira yenyewe hatuingii darasani bali tunajifunza kwa kuanza kufanya kile unachotaka kujifunza. Masomo ya mfumo wa nje ya ajira unanikumbusha maneno aliyowahi kuyasema mtaalamu wa zamani katika fani za hisabati na fizikia bwana Albert Einstein kuwa ELIMU ni kile kinachobaki baada ya kuwa umesahau yale uliyofundishwa shuleni”. Hapa kwetu Tanzania, hali ni mbaya kwa maana yale tuliyofundishwa shuleni na vyuoni mengi hayatumiki nje ya mfumo wa ajira. Matokeo yake tunajikuta tunasahau mambo mengi, huku tukibakiza elimu kidogo sana, kitu ambacho kinafanya wasomi wengi kuishi maisha duni ambayo siyo maisha ya ndoto zetu.

Ukizingatia maneno ya Bwana Albert Einstein ni dhahiri kwamba, elimu iliyobaki vichwani mwetu ni kidogo, kiasi kwamba haiwezi kututoshereza kukabiliana na changamoto nyingi ambazo ziko nje ya mfumo wa ajira. Kwahiyo, wakati ni sasa ambapo tunatakiwa kuwekeza nguvu nyingi kwenye kujifunza haraka mambo mapya ambayo mengi hatukuweza kuyapata shuleni na kwenye ajira. Aina ya mambo ya kujifunza yatategemea mtu mweneywe pamoja na kazi anayopanga kuitengeneza. Jitahidi kujifunza kwa wale wote ambao wamefanikiwa katika kile unachopanga kukifanya kama wapo. Ili uweze ujifunza kutoka kwa wazoefu unahitaji kujifunza mbinu mbalimbali za kujenga mahusiano na urafiki kwa watu wanaokuzidi au wanaishi maisha yale unayoyataka. Tunahitaji kujifunza kwa kuanza na usomaji wa vitabu na makala mbalimbali, vyote hivi vitakuhamasisha na kukujenga kifikra. Fikra sahihi ndizo zitafungua uwezo wa akiri yako kuona na kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi, ambazo zitakuwezesha kupata utajiri au maisha yale unayoyatamani siku zote.

Mwisho! Kumbuka kuwa, karibia asilimia 90% ya watu walio na utajiri mkubwa ni wale waliotafuta pesa nje ya mfumo wa ajira ...... maana walitengeneza kazi!.
 
AJIRA SIYO KAZI NI AJIRA NA KAZI SIYO AJIRA NI KAZI
Sasa hivi kuna tatizo kubwa sana la ukosefu wa ajira hasa kwa vijana. Ukosefu wa ajira ni jambo ambalo linazidi kuwawangisha  vichwa wadau wengi wa maendeleo na hasa serikali. Ni kweli serikali ina jukumu la kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na shughuli ya kufanya ili kujiongezea kipato. Lakini, wakati jitihada za serikali zikiendelea, sisi wenyewe tunaodai kukosa kazi tunayo majukumu makubwa zaidi ya kufanya kuliko kutegemea watu wakutupatia ajira. Kwahiyo, ni vyema tushughulikie kwanza yale yote yaliyondani ya uwezo wetu ambayo nina imani yanaweza kuchagia kwa asilimia 80% katika kutupatia suruhisho la kudumu juu ya kero hii ya kukosa kazi. Hivyo basi, hatua ya kwanza kabisa ni kutafakari na kufikiri kwa kina juu ya tofauti iliyopo kati ya kazi na ajira. Maana unaweza kujikuta muda wako mwingi unautumia kutafuta ajira ukifikiri ni kazi.

Kazi na ajira ni vitu viwili tofauti kabisa, na haviwezi kulinganishwa kwa kiwango chochote kile. Kazi inalipa sana na malipo yake mengine hayana kikomo, tofauti na ajira ambayo malipo yake ni kidogo na yanaweza kukoma muda wowote. Kitu cha ajabu kabisa ni kwamba watu wengi wanapendelea ajira kuliko kazi kwasababu, ulipohitimu elimu yako ulikaririshwa kuwa kazi inayotambulika rasimi ni ajira. Hii inatokana na mazoea ambayo tumeyajenga tokea tukiwa wadogo kuwa kazi yenye heshima ni ambayo umeajiriwa, ndiyo maana wale wote wanaofanya shughuli za kuajiriwa eti! ndio wanaitwa “Wafanyakazi”. Kwahiyo, wale wote ambao hawana ajira na hasa ajira rasimi, wanajiona na kujisikia kuwa hawana kazi na kutafuta njia usiku na mchana ili angalau siku moja waweze kuajiriwa. Hali hii, ya kushindwa kupata majibu sahii juu ya kazi ni ipi na ajira ni ipi. Matokeo yake kumeibuka makundi mawili ambayo ni kundi la wenye jukumu la kutoa ajira na kundi jingine ni la wenye kupata ajira. Kundi la wapata ajira ni wengi sana; Eti! Kazi yao ni kutafuta wapi ajira ilipo, na pale mtu anapotafuta ajira akakosa kwa muda huo, moja kwa moja anasema sina kazi! Hii inashangaza sana.

Ajira ni kufanya kazi ambayo siyo ya kwako, waweza kuwa unaipenda au huipendi. Watu wengine hawapendi kazi walizoajiriwa kuzifanya, lakini yawezekana  wanaendelea kufanya kazi hizo kwasababu wanalipwa pesa. Kutokana na hali hii, watu wengi hulazimika kutafuta kazi nyingine pale tu malipo yanapokuwa hayatoshelezi mahitaji ya muhusika. Mwenye kazi “mwajiri” anapokuwa amekuajiri kwenye kazi yake ambayo “siyo ya kwako”; wewe moja kwa moja unahesabika kuwa ni sehemu ya gharama za uendeshaji wa kazi au kampuni! Hii ni sawa na kusema kuwa waajiri wengi wanawaona wafanyakazi (waajiriwa) kama gharama za uzalishaji!. Hii haina maana kwamba waajiri hawawathamini waajiriwa wao, bali wakati wa kufanya tathimini ya maendeleo ya kazi inawabidi kufanya hivyo, ili kupanga mipango mikakati ya kuwezesha matunda ya kazi husika yapatikane kwa gharama nafuu.

 Kazi ni majumuisho ya majukumu mbalimbali ambayo kwa mwenye kazi unajiwajibisha mwenyewe katika kuyatimiza hayo uliyojipa mwenyewe, bila kutegemea kulipwa chochote mpaka matunda ya kazi hiyo yapatikane. Unapofanya kazi siyo lazima alipwe, kwasababu mara nyingi kazi inakuwa ni mchakato wako wa maisha na haupangiwi na mtu yeyote, wewe mwenyewe unajipangia ni nini ufanye, kwa malengo yapi na ni nani unamlenga kunufaika na matokeo (matunda) ya kazi yako. Iwapo matokeo ya kazi yako yanatoa suluhisho la matatizo au kero zilizopo kwenye jamii husika, basi ujiandae kulipwa malipo ambayo hayana kikomo, kwasababu watu watanunua matunda ya kazi yako, ili kukidhi mahitaji yao, hivyo ni rahisi wewe kuweza kutajirika kutajirika kupitia utatuzi wa kero na matatizo mbalimbali. 

 Kutokana na maana pana ya “kazi” tunaona kwamba kazi inaweza kupatikana popote lakini ajira haipatikani kila sehemu. Kazi ni nyingi sana ajira ni chache sana, hii inamanisha kwamba watu wanapenda vitu ambavyo vimeishapikwa tayari, kazi yao ni kupakua na isitoshe hata kwa kupakua tu! unalipwa na mwenye kazi. Kazi ni ya kudumu wakati ajira ina ukomo; kwenye kazi hakuna bosi, isipokuwa bosi wako ni malengo na ndoto zako lakini kwenye ajira kuna bosi ambaye anayo madaraka ya kuamua juu ya nini kifanyike na wakati mwingine kifanyike vipi na huyu ndiye anamiliki na kuongoza hatima ya mafanikio yako
na hasa ya kiuchumi. Kwenye kazi unachukua muda mrefu kuanza kulipwa tofauti na ajira ambayo, ukianza tu ajira yako unaanza kulipwa maramoja au mwisho wa mwezi huo huo. Pengine tofauti hii ya muda wa kulipwa kati ya mwenye kazi na mwenye ajira ndiyo inayowafanya watu wengi na hasa wasomi wa fani mbalimbali kupendela “ajira” kuliko “kazi”.

Kutengeneza na kufanya kazi kunahitaji kujitoa, ubunifu, kufikiri sana, kuvumilia na zaidi ya yote, kazi inahitai ujasiri na ninadhani ujasiri huu wa kufanya kazi bila kulipwa kwa wakati huo ndiyo mzizi mkuu wa neno Ujasiriamali. Kwenye ajira kila kitu ambacho unakifanya unadai ulipwe, kwahiyo, kama hakuna malipo hicho kitu au shughuli haiwezi kufanyika. Kwa uhalisia ni haki ya mwajiliwa kudai malipo ya kila nguvu anayowekeza kwenye ajira yake kwasababu, mwajiriwa kama mwajiriwa yeye hana umiliki wowote wala hisa juu ya matokeo au mapato yote ya  kile kilichozalishwa bali mwenye kumiliki hicho ni mwenye kazi. Waajiriwa hupewa sehemu ndogo sana ya kile chote kilichozalishwa. Makampuni mengi, kila mwisho wa mwaka huwa wanafunga mahesabu na kupima wamepata faida kiasi gani lakini siyo rahisi kwa mwenye kampuni kutoa gawio (dividend) kwa wafanyakazi wake kwasababu, wafanyakazi (waajiriwa) wote, wanahesabika kama sehemu ya gharama na siyo sehemu ya faida, na faida hii ndiyo motisha na kichocheo kikubwa cha yeye kuendelea kuwekeza na kutengeneza kazi nyingi ambazo zinaweza kutoa ajira kwa watu wengi zaidi. 

Kwakuwa kazi unajipatia mwenyewe, ni wakati muhafaka sasa wa kujipa kazi badala ya kusubili kupewa kazi (ajira). Tusisubili wale wakutuletea kazi, kwa maana hatujui wataleta lini na kwa malengo yapi. Tuzidi kukumbuka kuwa ajira haziwezi kuwa nyingi kama kazi zinazotengenezwa ni chache. Tuzidi kujipa kazi kwani chochote tutakachozalisha, watu wako tayari kununua, ilimradi kina manufaa kwao. Anza leo, kuanza kujitenga na watafuta ajira, pia jiepushe na tabia ya kulalamikia watu wengine kwa mambo ambayo ni majukumu yako. Kwahiyo, bila kujali umesomea nini, anza leo kufikiria ni kitu gani unaweza kukizalisha ambacho kina uwezo wa kutatua kero na changamoto mbalimbali katika jamii. Kwakufanya hivyo, utakuwa umepata suluhisho la kudumu juu ya kero ya muda mrefu ambayo ni ukosefu wakazi”.






SURUHISHO PEKEE LA KUWEZA KUPATA MAFANIKIO MAKUBWA KWA KILA JAMBO UNALOFANYA NI KUFANYA VITU VICHACHE AMBAVYO NI MUHIMU
Kwa sasa, watu wengi duniani wanakabiliwa na tatizo la msongo wa mawazo katika maisha, sababu mojawapo ikiwa ni pamoja na tabia ya kuendekeza kufanya kila kitu kila wakati. Tabia hii inatokana na hulka ya walio wengi kutaka kila mara kufanya kazi ili kumfurahisha na kumridhisha kila mtu, jambo ambalo limekuwa likichangia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza sana ufanisi na ubora wa kazi tunazofanya kila siku na hivyo kutumbukia katika umaskini. Endapo una tabia ya kufanya kazi kwa kumridhisha mtu ni rahisi sana kuwa “mbabaishaji”; kwasababu kila kazi yenye kuhitaji uharaka, utarundikiwa wewe na ukiweza utapewa motisha au posho nyingi. Mwisho wake ile nguvu yako unaitawanya kidogo kidogo katika kukamilisha kazi zote zinazokujia. Ukiwekeza kidogo kidogo kwa kazi nyingi zitakazokujia, mwisho utapata matokeo ya kiwango cha chini sana! Na huu utakuwa mwanzo wa wewe kuitwa “mbabaishaji. 

Tabia ya kutaka kufanya kila kitu, inatokana mafundisho tokea utotoni, ambapo uhamasishwa kusema “NDIYO” kwa kila jambo. Kumbe ni muhimu tangu mwanzo watoto wetu tuwafundishe kusema "HAPANA" na siyo kuwapongeza kila mara kwa kusema "NDIYO" peke yake. Mara nyingi hata watu wazima, unapofanya kazi ukapongezwa anavutiwa na kuhamasika sana na hivyo kuingia kwenye mtego wa kutaka ufanye na kumaliza kila kazi iliyopo mbele yako. Kutokana na tabia hiyo ya kuvutiwa na pongezi unajikuta kila kazi unaikubali hata kama ulikuwa unafanya kazi nyingine za muhimu. Kwahiyo, ni vizuri ujifunze tabia ya wachapakazi hodari ambapo wao uhamini sana falsafa ya “kidogo lakini kizuri” (Less but Better).

Watalamu wanatwambia kuwa ili mtu aweze kufanya kazi kwa kiwango cha juu, ni lazima ajifunze au tujifunze na tuache tabia ya kufanya shughuli nyingi tena ndogo ndogo. Kwani, hii Ndiyo sababu watu wengi anaposhirikishwa fursa Fulani Fulani za Biashara mara nyingi hutoa visingizio vya kuwa hawana muda (busy) au utasikia mtu anakwambia nina mambo mengi sana. Kwa watu walio wengi, hili la kuwa na kazi au mambo mengi sana wanalichukulia kama ni sifa ya uchapakazi na uwajibikaji hodari. Kwahiyo, wanatumia U-Busy kama kipimo cha utendaji bora wa kazi hata kama vitu wanavyofanya havina tija.

Watu waliopata mafanikio makubwa kwa njia halali, mara nyingi wanashauri kwamba, mafanikio makubwa yanahitaji sisi kuwekeza katika vitu vichache ambavyo inakuwa rahisi kuweza kuvipa muda wa kutosha na kuvifanya kwa ufanisi mkubwa. Na katika kulitekeleza hilo, wanatuhasa pia, tuanze mara moja kujijengea utamaduni wa kuweka vipaumbele katika maisha, kwani tusipo fanya hivyo, mtu mwingine atatuwekea vipaumbele ambavyo tutapoteza muda wetu kutekeleza vipaumbele hivyo ambavyo hatuvipendi.

Mara nyingi unapokabiliwa na suala zima la kutekeleza vipaumbele vya watu wengine ni wazi kwamba utafanya kazi hiyo huku ukiwa huipendi na kama huna mapenzi ya dhati kwa hicho unachokifanya basi itakupelekea kufanya kazi hiyo chini ya kiwango. Na iwapo utaendelea kufanya kazi zako chini ya kiwango ni lazima uwe maskini, kwasababu kwa muda mrefu ambao utafanya kazi chini ya kiwango ndani mwako itajengeka tabia ya uvivu hasa ule wa kufikiri. Ukiwa na uvivu wa kufikiri, huwezi kuwa mbunifu na matokeo yake mbinu zako za kupambana na changamoto za maisha zinakuwa zimepitwa na wakati. Kwahiyo, safari yako ya kuelekea umaskini wa kutupa inakuwa imeanza hapo. Ewe mtanzania jitahidi kuwa mjasiri, ili uweze kufanya maamuzi magumu juu ya vitu vichache ambavyo ukiwekeza nguvu zako zote utaweza kufikia haraka maisha ya ndoto yako.

KARIBU TWENDE KAZI PAMOJA




HII NDIYO SABABU YA WATU WENGI KUKOSA KAZI KATIKA NCHI YENYE KAZI NYINGI
Nadharia ya kutafuta kazi eti! Inayoendana na mapenzi yako Ndiyo chanzo cha watu wengi kuchagua kazi na kuishia kukosa kazi. Wataalam wa masuala ya kazi na Ujasiriamali wanasema kuwa, Katika ulimwengu wa kazi kuna makundi makuu mawili yote yakitofautiana kulingana na mtizamo juu ya “kazi” . Kundi la kwanza lina mtizamo wa kujiuliza swali la “dunia inaweza kumpatia mtu kitu gani kinachoweza  kumridhisha au kumfurahisha”? (Passion Mindset) na kundi la pili lina mtizamo wa kujiuliza swali la “Mtu anaweza kuipatia dunia kitu gani kitakacho wafurahisha au kuwapendeza watu”? (Craftsman Mindset).

Katika Utafiti uliofayika duniani imekuwa ni vigumu sana watu wa kundi la kwanza kuweza kufanya kazi kwa bidii na kuishi kwa furaha. Kukosekana kwa furaha kazini, siyo tu kumetokana na maslahi duni bali ni kutokana na ukweli kwamba, ni vigumu kampuni husika kuweza kumridhisha kila mtu kwa jinsi apendavyo bila kuingilia maslahi ya kampuni hiyo, kwa hiyo kinachotokea ni ni huyo mtu kuanza kupambana na mwajiri kwa kudai mambo ambayo yanaweza kumfurahisha au kumridhisha kama yeye binafsi. Na iwapo mambo hayo hayapati basi migogoro na mwajiri inaanza mara moja, matokeo yake mtu anaanza kuishi kwa misuguano mingi na mwisho wa yote anaishi bila furaha kila anaposhindwa kupata maslahi aliyotarajia kipindi kile alipo wazia dunia itampatia nini.

Kutokana na mtizamo wa “dunia itakupatia nini” mtu huendelea kujaribu huku na kule akiwa ujatulia kabisa, huku ukitafuta chochote cha kupata kutoka kwenye dunia. Mara nyingi, maisha ya namna hii, huwa ni ya kubahatisha au kujaribu jaribu. Katika kubahatisha, mtu anafika mahala dunia inampatia fursa ya kazi (ajira) kutoka kwa watu wengine waliotengeneza kazi, hapo ndiyo hujenga matumaini na matarajio makubwa ya kukidhi furaha yake na tamaa zake nyingine kutoka kwenye ajira aliyopewa. Baada ya kipindi kifupi, mtu huyu ghafla unashangaa hapati kile kilichokuwa kinamfurahisha kwenye kazi ya ajra aliyopewa miaka miwili iliyopita.

Hali ya kutopata kile alichotarajia mwanzo, humfanya huyo mtu kutafuta suluhisho la haraka, ambalo huwa ni ni kutafuta sehemu nyingine yenye kumpatia furaha na maslahi mazuri zaidi na hapo anafurahia kwa muda na baadae tena kero mpya zinaibuka upya. Kwahiyo, inakuwa ni mzunguko ambao unakuwa maisha yenye furaha kipindi kifupi na kipindi kirefu cha kero nyingi; hali ambayo husababisha kiwango kidogo sana cha ufanisi, ikiwa ni pamoja na uzalishaji chini ya kiwango inachotegemewa. Watu wengi katika kundi hili la kwanza, hawapendi kazi wanazozifanya, isipokuwa wanaendelea kufanya kazi kwasababu wanalipwa pesa.

Kutokana na kuhamahama kwa watu ambao tayari wana kazi (ajira) kutoka mwajiri mmoja kwenda mwingine, ndiyo sababu ya kuongezeka kwa kundi la watu wanaotafuta ajira. Kwani kunakuwa na kundi la vijana ambao ni wapya (walio hitimu karibuni) na kundi la zamani wote wakishindana kupata nafasi chache zilizoko kwenye soko la ajira. Kundi la watu wa zamani, ambao kimsingi ni wazoefu, wanatumia kigezo cha uzoefu ujuzi kazini kuwashinda wapya hasa katika nafasi zinazosemekana zina marupurupu makubwa.

Kwa upande wa kundi la pili lenye mtizamo wa “Mtu anaweza kuipatia dunia kitu gani kitakacho wafurahisha au kuwapendeza watu?; Mtizamo huu unafanana sana na mtizamo watu wa sanaa na maonyesho kwa ujumla. Kundi hili kwa kuongozwa na mtizamo huu, kila mara lina jaribu kuumiza vichwa vyao kufikiri na kutafakari ni kitu au vitu gani waifanyie au waipatie dunia!. Kwakuwa kundi hili linashughulika tu na kufikiria cha kufanya, linajikuta swala zima la kazi siyo tatizo kwasababu ni watu wa kundi hili wanaoibua na kutengeneza kazi. Kundi hili linapokuwa limeibua na kutengeneza kazi ndipo linajikuta likikabiliwa na majukumu mengi yaliyopo mbele yake katika kufanikisha kazi hizo. Hili kukabiliana na majukumu hayo, kundi hili hulazimika kutafuta watu waliobobea katika fani mbalimbali, ili waweze kusaidia katika kutimiza na kufanikisha malengo ya kazi husika. Mfano chukulia ‘Wasanii wa muziki na firamu za kitanzania’ ukitafiti watu hawa utagundua kuwa wanaipenda sana kazi yao, na kutokana hali hiyo kupenda kazi yao, wemeweza kuwekeza nguvu na maarifa yao yote na matokeo yake, wameweza kutegua kitendawili cha ajira , jambo ambalo linaonekana kuwaelemea sana wasomi wengi hasa wanaotoka vyuoni.


Katika nchi zote duniani, wanaomiliki uchumi wa nchi huska ni wale tu walio na utashi na uwezo wa kutengeneza kazi, na hii ni kutokana na ukweli kwamba faida yote inayotokana na kazi husika mara nyingi inachukuliwa na yule tu! aliyetengeneza kazi, waliobaki bila kujali idadi yao kwenye kazi husika, wanaendelea kuhesabika kama sehemu ya gharama za uendeshaji. Kwa hapa Tanzania, wasomi wengi tunayo nafasi nzuri zaidi ya kuweza kutengeneza kazi kuliko wale ambao hawakusoma, kwasababu, wasomi ni rahisi kupata ujuzi na habari za mambo mbalimbali yaliyoko duniani na kuzitumia katika maamuzi ya kutengeneza kazi mbalimbali ambazo zingeweza kuvuta maendeleo ya haraka hapa nchini. Cha ajabu kabisa, hapa Tanzania, wale ambao hawakubahatika kuedelea na shule, ndio wengi wao waliamua kutengeneza kazi na wemejiendeleza Kiasi cha kubobea katika kazi hizo hizo walizozitengeneza. Kwasasa, watu hawa ndio wanaendesha uchumi wa nchi huku wakitoa pia ajira kwa wasomi ambao wangeweza kutengeneza kazi nyingine nyingi zaidi.

Watu wengi katika kundi hili linaloongozwa na mtizamo wa “nitaipatia nini dunia”? wanapenda sana kazi zao ambazo wamezitengeneza wenyewe. Na kwasababu hiyo; wanazifanya kwa moyo, umakini, kujituma na kwa juhudi na maarifa. Mambo yote haya, ni nadra sana kuyakuta kwenye kundi la kwanza ambalo ni la wenye mtizamo wa “dunia itanipatia nini”?. Kundi hili la pili, ndio wanaotoa ajira kwa wale wanaoitwa “wasomi” na hii nikutokana na ukweli kwamba, wale ambao hawakusoma walijikuta wakilazimika kutengeneza kazi ili waweze kuishi. Mfano ni wakulima, wasindikaji; wavuvi, wafugaji; wasanii, wafanyabiashara, mafudi n.k. bila watu hawa mambo hayaendi na serikali inategemea sana kundi hili kupata pesa za kugharimikia huduma za jamii.

Mwisho nipende kusema kuwa, kazi zinazo subili kutengenezwa zipo nyingi sana hapa Tanzania, lakini ajira ambazo zinatafutwa na watu wengi ndizo chache sana. Kwa maana nyingine, ajira haziwezi kuwa nyingi kama kazi zinazotengenezwa ni chache sana. Ewe mtanzania jiunge na mtandao wa watengeneza kazi, ili uweze kufanikiwa na kuishi maisha yenye furaha. Kuanzia leo, acha kulalamikia watu wengine kwa mambo ambayo ni majukumu yako na jitenge kabisa na watafuta ajira. Bila kujali umesomea nini, anza leo kufikiria ni kitu gani unaweza kuwapatia watu wakafurahi kwa kukidhi mahitaji yao, na iwapo utafanya hivyo, basi utakuwa umepata suluhisho la kudumu na hivyo kuweza kutegua kitendawili cha “kazi” maisha yako yote.
~TWENDE KAZI PAMOJA~



MAFANIKIO YA KWELI YATALETWA NA KAZI SIYO AJIRA

Siku moja nikiwa naangalia kipindi maarufu cha “Tuongee Asubuhi” kinachorushwa kila siku na kituo cha televesheni cha StarTV. Mada kuu ilikuwa ni hali ya umaskini Tanzania, ambapo ilionekana kuwa, umaskini nchini, una husiano wa moja kwa moja na vitu viwili, ambavyo ni “kazi” na “ajira”. Mjadala huu uliniwezesha kutambua kuwa, kuna tofauti kubwa sana kati ya kazi na ajira; nilipoendelea kudadisi juu ya mtizamo wa watu kuhusu mambo haya mawili, niliweza kugudua kwamba walio wengi wanadhani ni kitu kile kile na wanaamini kwa dhati kwamba ni lazima wapate ajira, kwani kwa mawazo yao ni kwamba usipokuwa na ajira, basi wewe huna kazi!!.

Wakati nikiendelea kutafuta majawabu ya tofauti kati ya kazi na ajira, ndipo mmoja wa wachangiaji mada, akasema kwa sasa “watu wengi hasa waliosoma wanaacha kazi kutafuta ajira”. Baada ya kusikia kauli hii, nikatafakari kwa undani zaidi juu ya dhana nzima ya “ajira” na “kazi”, ndipo nikapata kufahamu kuwa ajira ni shughuli ambayo mtu upewa na mtu mwingine au mwenye kazi (mwajiri) kwa makubaliano ya kulipwa ujira au mshahara. Kwahiyo, ni jukumu la mtu yeyote aliyepewa ajira, kuhakikisha anafanya kazi aliyopewa kwa umakini mkubwa na hii ni kutokana ukweli kuwa unalipwa kwa kazi hiyo. Mtu akiajiriwa ni lazima aingie mkataba na mwajiri wake na lazima awajibike kufuata kanuni na sheria za kampuni husika, sheria ambazo, mwajiriwa hukushiriki kuzitunga.

Kwa maana rahisi “ajira” ni kufanya kazi ambayo siyo ya kwako, waweza kuwa unaipenda au huipendi. Watu walio wengi hawapendi kazi walizoajiriwa kuzifanya,  wanaendelea kufanya kazi hizo kwasababu wanalipwa pesa Ndiyo maana masilahi yanapopungua wengi hubadilisha na kuhamia kampuni nyingine yenye masilahi maubwa zaidi. Kwakuwa mwajiri amekuajiri kwenye kazi yake (kazi siyo ya kwako),  basi wewe unahesabika kuwa sehemu ya gharama za uendeshaji wa kampuni! Ebu jifikirie, mwanadamu anavyoogopa gharama, kila wakati anataka aishi au aendeshe miradi kwa gharama nafuu. Kwahiyo, kadili mwajiri atakavyojitahidi kupunguza gharama, ndivyo mwajiriwa utakavyo athirika kiuchumi na kimaisha kwa ujumla. Na nyongeza ya hapo kila mara mwajiri anapokuona au kukufikiria, hakuoni/hakuwazii wewe, isipokuwa anaona au kuwazia gharama tu basi!.

Kazi ni majumuisho ya shughuli mbalimbali ikiwemo kutumia nguvu au ubongo kufikiri, kwa lengo la kukamilisha au kuzalisha vitu au huduma fulani.  Kwa maana iliyopana kazi ni shughuli zote ambazo mtu ufanya, yaweza kuwa kitu chochote mtu anachokifanya ili kutekeleza majukumu kwa familia kama vile kupika chakula, kufanya usafi wa ndani n.k. Tofauti na ajira, ukifanya kazi siyo lazima alipwe, kwasababu mara nyingi kazi inakuwa ni mchakato wako wa maisha kwa maana bila ya kupangiwa na mtu yeyote, wewe mwenyewe unajipangia ni nini ufanye, kwa malengo yapi na ni nani unamlenga kunufaika na matokeo ya kazi yako. Iwapo matokeo ya kazi yako yanatoa suluhisho la matatizo au kero kwenye jamii husika, basi ujiandae kulipwa malipo ambayo hayana kikomo, kwani watu watanunua kitu au Huduma ili kukidhi Mahitaji yao, na kwa kufanya hivyo unatajirika kwa kutatua kero za watu.

Ewe mtanzania unayejitambua anza leo kufikiria ni kazi gani unaweza kuifanya ukaondoa au kutatua kero mbalimbali zinazowapata watanzania wenzako. Kwani kwa kufanya hivyo, utakuwa umesaidia watu walio wengi kuondoa umaskni walionao na wakati huo huo utakuwa ukilipwa bila kikomo.
~TWENDE KAZI PAMOJA~

2 comments:

Unknown said...

Chezea mshahara siyo kazi, umeona piga kazi kwanza kisha pata cha kukazia!!!!!1

Gerd Ulrich said...

Maisha yangu Maajabu yanashangaza ushuhuda, Jinsi nimepata kisanduku chenye nguvu sana ambacho sasa ni pesa yangu mara mbili kutoka mia hadi elfu ya pesa ndani ya masaa 24, na pia jinsi nimerudisha mpenzi wangu wa zamani, sababu kuu niliwasiliana na Dk Lomi kwa msaada mimi kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, basi ananisaidia ni nguvu kubwa ya kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, na ananipenda na ananithamini sasa, basi mimi na Dr Lomi tukawa marafiki, baada ya mazungumzo kadhaa namuuliza ikiwa kuna njia anaweza kuniganga ili nipate pesa, hapo ndipo aliponiambia juu ya sanduku hili la uchawi, akaniambia kuna aina na saizi tofauti ya sanduku, aliniambia aina zote za sanduku, ningeweza kumudu ndogo tu ya sanduku, baada ya maombi muhimu anayofanya kwenye sanduku, ananipeleka kupitia huduma ya kujifungua, aliniambia niweke pesa ndani, niliweka ndani ya sanduku 100 euro baada ya masaa 24 nikagundua ilikuwa elfu 10 euro ndani, na nimekuwa nikitumia sanduku kwa miezi 7 sasa, mimi na mchumba wangu tunaishi maisha bora, ikiwa unahitaji b ack mpenzi wako au pesa spell wasiliana na Dr Lomi kwa barua pepe: lomiultimatetemple@gmail.com au WhatsApp namba +2349034287285 unaweza pia kumwandikia kupitia Jina la Mtumiaji la Snapchat: drlomi20 atakusaidia nje, asante kwa kusoma,

Kwaheri Gerd Ulrich