“Sababu ya watu wengi kuendelea kubaki wadogo kibiashara na kimaisha ni kwamba kila wakati wao utatua matatizo yale tu wanayoweza peke yao” ~ Cypridion Mushongi.
kutokana na watu wengi kuendelea kuamini na kushikiria tafsiri isiyo sahihi juu ya maana halisi ya ujasiriamali.
Mtazamo wa watu wengi ni kwamba “mjasiriamali” ni mtu anayeonekana kuhangaika sana, mtu ambaye anajifanyia shughuli zake yeye mwenyewe, aliyejiajiri na kufanya kazi zote za kila siku peke yake. Mtazamo au tafsiri kama hii, ndiyo inapelekea kuona kama vile Tanzania ina wajasiriamali wengi sana. Hatahivyo, ukweli ni kwamba, nchi yetu ndiyo inaongoza kwa kuwa na wajasiriamali wachache katika nchi za Afrika Mashariki.
Kwahiyo, mjasiriamali ni nani?
“Mjasiriamali” ni yule mtu anayeona fursa (siyo kutazama fursa), akaweka timu ya watu pamoja, akajenga biashara ambayo inatengeneza faida kutoka kwenye fursa husika”.
Mwingine unapomwambia maana halisi ya mjasiriamali anakuuliza maswali mengi, kwasababu anaona maana unayompa inamtupa nje ya kundi la wajasiriamali. Kwa mfano mtu anakuuliza hivi….. “Ikitokea nimeona fursa ambayo naweza kufanya kazi peke yangu na bado nikapata faida bila kuhitaji nguvu ya watu wengine, nitakuwa siyo mjasiriamali?
Katika kujibu swali hili ni kwamba, endapo ukiona fursa, na ukaona kwamba unaweza kufanya kazi peke yako, basi ujue kuwa wewe ni mfanyabiashara mdogo sana na wala siyo mjasiriamali.
Tofauti kati ya mfanyabiashara mdogo na mjasiriamali ni kwamba, mfanyabisahara mdogo ni mtu ambaye anaweza kuzalisha bidhaa au kutoa huduma kwa nguvu yake binafsi. Kwa mfano: daktari wa tiba ya meno anaweza kufanya kazi hiyo peke yake.
Mjasiriamali wa kweli hawezi kufanya yote anayotakiwa kufanya peke yake. Lazima avute pamoja watu wazuri wenye utaalam na ujuzi mbalimbali na kuhakikisha wanafanya kazi pamoja, ili kutimiza malengo ya pamoja.
Kwa maneno mengine, mjasiriamali ujenga timu ambayo kwa pamoja uzalisha bidhaa fulani ambayo haiwezi kuzalishwa na mtu mmoja peke yake. “Sababu ya watu wengi kuendelea kubaki wadogo kibiashara na kimaisha ni kwamba, kila wakati wao utatua matatizo yale tu wanayoweza peke yao”.
Kwahiyo, tofauti na watu wengine, mjasiriamali ujishughulisha zaidi na majukumu yanayohitaji timu ya watu zaidi ya mmoja.
Mjasiriamali/mfanyabiashara mkubwa, huwa halipwi mpaka timu yake ifanye kazi inayotakiwa kufanywa pamoja kama timu. Waajiriwa wengi na wale waliojiajiri, mara nyingi ulipwa kulingana na nguvu binafsi au nguvu ya mtu mmoja.
Mjasiriamali huwa halipwi mpaka timu yake ifanikiwe. Kama alivyo mkandarasi wa jengo, utumia wajenzi kama vile fundi bomba, umeme, seremala na wanataaruma wengne kama wasanifu majengo, wahasibu n.k. katika kujenga nyumba. Mjasiriamali naye utumia watu mbalimbali, mafundi mchundo, wanataaruma/wasomi kumsaidia kujenga biashara.
Kwahiyo, ni muhimu tukatambua katika akiri yetu kuwa, mjasiriamali ni kiongozi wa timu, japo inawezekana asifanye kazi moja kwa moja kwenye timu. Kadiri utakavyoongoza timu ya watu makini, wenye elimu na uelewa mkubwa bila ya kuwa wewe umefanya kazi kama sehemu ya timu, ndiyo itakuwa vizuri na ndivyo utazidi kuwa mjasiriamali wa kweli.
Mjasiriamali wa kweli unaweza ukakuta anamiliki kampuni nyingi, lakini hafanyi kazi yoyote ndani ya kampuni hizo. Ndiyo maana unakuta mtu anatengeneza pesa nyingi na kufanya vitu vingi zaidi bila ya kutakiwa kufanya kazi. Ndiyo sababu ni vizuri tukatambua sasa kuwa uongozi ni ujuzi muhimu sana kwa mtu yeyote anayetaka kuwa mjasiriamali.
Je uongozi ni taaruma ambayo unaweza kujifunza?
Ndiyo, nimegundua kuwa sisi wote tuna ujuzi fulani wa uongozi. Tatizo la watu wengi, ni kwamba tunatumia muda mwingi wa maisha yetu katika kuendeleza taaluma au fani tunazoamini kuwa zinatufanya tuwe waajiriwa wazuri. Na hii ndiyo sababu kubwa ya taifa kuwa na kundi kubwa la wasomi walioajiriwa na wasio na uwezo wa kujitegemea.
Nchini Tanzania, kuna idadi ndogo sana ya watu ambao utumia muda wao mwingi kuendeleza taaluma ya uongozi amabayo ndiyo uhitajika kuendesha biashara kubwa.
Kwahiyo, kwakuwa inawezekana kujifunza uongozi, ni vizuri na ni muda muhafaka sasa kwa wale wote ambao wanataka kuwa wajasiriamali wa kweli kujikita zaidi kwenye kuendeleza taaluma ya uongozi na ujuzi katika masuala yote yanayohusu elimu ya mawasiliano na mahusiano na watu.
Watu wengi wanasema siasa, biashara na ujasiriamali ni vitu vigumu kuvifanya kwasababu, vyote vinahitaji ushiriki wa watu zaidi ya mmoja. Kwa maana nyingine ni kwamba, huwezi kufanikiwa kwenye dini, siasa, biashara na ujasiriamali, kama uko peke yako. Na vitu vingi vyenye kukuletea mafanikio makubwa, mara nyingi huwa vinahusisha watu wengi ---.
Kwa wewe unayesoma makala hii sasa hivi, naomba ujisemee maneno haya kwa sauti: “Mimi kama mjasiriamali wa kweli nimeamua kuimarisha elimu yangu ya uongozi, ili kuunganisha watu, kwa lengo la kufanya kazi pamoja hadi kufikia uhuru wa kipato na maisha bora”.
Ujuzi katika uongozi unaendelezwa kwa kujifunza kila siku kupitia kujisomea vitabu, makala mbalimbali ambazo nyingi zinapatikana hapa MAARIFA SHOP. Waweza pia kuwa karibu na blog hii kwa kubonyeza “NAJIUNGA” ili kujipatia makala nzuri moja kwa moja kupitia barua pepe yako.
No comments:
Post a Comment