HUU NDIO MUUJIZA WA VYAKULA VINAVYOISHI
“Siri ya kufanya kazikwa bidii bila kuchoka ni kula vyakula vinavyoishi”~ Cypridion Mushongi
Wewe
kama binadamu anayejitambua na kujipenda, unahitaji kufahamu kuwa wewe ni
matokeo ya kile ulacho kila siku. Kwa kufanya mageuzi katika lishe yako,
unaweza kabisa kubadili maisha yako kuanzia muonekano, nishati/nguvu ya mwili
hadi uchumi. Wengi wetu tayari tunafahamu juu ya ulaji wa kunenepesha mwili au
kupunguza mwili, lakini ni watu wachache sana ambao wanatambua jinsi ya..
kutumia
chakula katika kufungua nguvu ambayo mara nyingi upotea kutokana na kutumika
katika kusaga na kulainisha baadhi ya vyakula ambavyo havisagiki haraka mfano nyama
n.k.
Mikakati
yote ya kukuza uchumi, kuleta utulivu wa akili na mbinu binafsi za ustadi wa
maisha hazitakusaidia kama hautakuwa na nguvu na afya ya kufanya yote yale
yanayohitajika ili kufikia maisha ya ndoto yako. Makala hii ni juu ya muujiza
wa chakula ambacho uwekwa mwilini mwako. Kwa kujali zaidi kupitia lishe sahihi,
unapata uhakika wa kuishi maisha marefu na uwezo wa kufikia ndoto zako za
maisha bora. Kwa kuliacha suala nyeti la chakula na lishe lijiendee vyovyote,
ni wazi kwamba ndoto zako nyingi zitavunjikavunjika na kamwe hutaweza
kuzitimiza hata siku moja.
Katika
nchi ya India ya kale, watu wake waliamini kuwa akili na ubongo imara ni vitu
vilivyo na uhusiano wa moja kwa moja na aina ya chakula na lishe ya mtu husika.
Vyakula vyepesi na ambavyo siyo vya asili ya nyama kama vile mbogamboga na
matunda, walivipendelea zaidi. Watu hawa wenye asili ya India na Asia, walikuwa
wakiamini kuwa kutiririka kwa nguvu binafsi na nishati mwilini ni kitu
kilichokwamishwa zaidi na ulaji wa nyama. Utafiti wa kisayansi wa hivi karibuni
umedhihirisha kuwa utendaji kazi hafifu wa mtu unahusishwa moja kwa moja na
hali yake ya akili na mwili. Wito kwako msomaji ni kwamba ni muhimu ukahakikisha
unajali sana hali ya akili na mwili wako na kwa kufanya hivyo utatengeneza
maisha mazuri unayostahili.
Ulaji vyakula vinavyoishi: Hatua
kubwa kupata afya na mwili imara!
Watu
wa kale kutoka jamii ya “yogis” huko milima ya “Himalayas” ni watu wanaotoa
somo zuri sana juu ya suala zima la kuishi maisha marefu, nishati/nguvu ya
mwili na uimara wa mwili na akili. Wengi wao tunaambiwa ni watu wanaoweza
kuishi maisha ya zaidi ya miaka 100 na kudumisha uwembamba na miili imara yenye
nguvu sana maisha yao yote, na kuweza kufanya shughuli nzito zinazohitaji
ujasiri mkubwa vizuri kwa kile wamarekani wanachoita miaka ya mwisho. Watu hawa
wanaweza kukaa hadi zaidi ya wiki moja bila kula chakula na bila usingizi. Pia,
ni watu wenyekuwa na uvumilivu wa kipekee ambao wanaweza kuvumilia maumivu
makali sana. Ni siri gani iliyopo juu ya
maisha marefu na ya ujana kwa watu hawa? Jibu ni rahisi kwamba, huwa
wanajitahidi kula chakula kiasi na wanafuata utaratibu wa kula vyakula
vinavyoishi au hai na vya asili.
Kwa
taarifa ni kwamba vyakula vinavyoishi ni vile ambavyo vimekuwepo au vimetokana
na njia ya asili ambayo ni muunganiko wa nishati ya jua, hewa, udongo na maji. Lishe
yenye vyakula vya namna hii, inasisitiza matunda (na juisi zake), mbogamboga na
nafaka. Kwa kuweza kufanya mabadiliko na kuhakikisha asilimia 70 ya lishe yako inakuwa
ni matunda, mbogamboga na nafaka, utakuwa umepiga hatua ya kwanza kuelekea uimara
wa mwili na maisha yenye hamasa kubwa.
Hapa
ni baadhi tu ya faida zilizothibitika ambazo utazipata endapo utaanza kutumia
vyakula vinavyoishi ni pamoja na kuongezeka
kwa kiwango kikubwa cha nguvu zako na stamina; kuongezeka kwa utulivu wa akili na
ubunifu; kupungua kwa kitambi na mafuta mwilini; kulainika kwa ngozi; kupungua
kwa mahitaji ya usingizi, chakula kusagika kwa urahisi; kuongezeka kwa
uchangamfu wa akili; kuwa na kumbukumbu nzuri; maisha marefu na athari kidogo
za magonjwa; kuwa na hali ya kujisikia utulivu utokanao na kuwa na hali nzuri
kiafya kwa ujumla.
Lishe
ambayo imesheheni mbogamboga, nafaka na matunda, ndio hasa asili yetu ililenga
kutupatia sisi binadamu. Kwa mfano, meno yetu na utumbo wetu unatofautiana sana
na ule wa wanyama wanaokula nyama kama mbwa, LAKINI meno yetu yanafanana na wanyama
wanaokula matunda. Kutoka kwenye nyama kama vile ya ngombe, mbuzi, kuku n.k
utupatia lishe ambayo ni ya daraja la pili kwa umuhimu mwilini. Nyama inakuwa
kwenye daraja la pili kwasababu inapatikana kwa myama anayekula nyasi,
mbogamboga na matunda ya asili.
Kimsingi
bidhaa kama nyama imeonekana kuwa na matokeo hasi mwilini na pia inakosa kiasi
kikubwa cha vitamini na madini muhimu katika ustawishaji wa mwili wa binadamu.
Madini na vitamini ni viasili ambavyo vinahitajika mwilini ili huweze kufanyakazi
vizuri na kwa ufanisi mkubwa. Jambo lingine muhimu kulifahamu ni kwamba, nyama
ni chakula kigumu kusagika tumboni, na kwa maana hiyo ni chakula kinachosagwa
kwa kuhitaji kiwango kikubwa cha nishati. Matokeo yake, kusagwa kwake kunamaliza
kabisa ile nishati/nguvu yote iliyohifadhiwa mwilini na ambayo kama isingepotea
kusaga nyama, ingeweza kutumika kufanya kazi nyingine za uzalishaji mali. Ebu
jaribu kulinganisha jinsi ujisikiavyo mara baada ya kula nyama steki, na mara
baada ya kula mbogamboga na matunda au saladi?
Vyakula
vya asili kama vile matunda vinasagika kwa urahisi sana tumboni na vinatumia
nishati kidogo sana. Maana yake ni kwamba, ulaji wa vyakula hivi unauachia
mwili kiasi kikubwa cha nishati ambayo inakuwepo kwaajili ya kufanya shughuli
nyingine muhimu, hasa zile za uzalishaji na shughuli nyinginezo za kutimiza
ndoto zako. Siri mojawapo ya kufanya kazi kwa bidii na bila kuchoka ni uwepo wa
hifadhi kubwa ya nishati mwilini. Unaweza ukawa unawahi shambani, ofisini, na
mahala pengine, lakini kama huna hifadhi ya nishati ya kutosha mwilini ni kazi
bure. Maana utakuwa unachoka haraka kila unapoanza kazi za siku husika. Kwa
wale tunaofanya kazi maofisini ni mashahidi wa sisi wenyewe au marafiki zetu
wanaosinzia ofisini na kwenye vikao – tatizo hili linasababishwa na uhaba wa
nishati mwilini ambayo kila mara inatumika zaidi kusaga vyakula kama nyama
n.k.
Kama nyama ni kitu kibaya kwetu, kwanini
tunaila?
Watetezi
wengi wa ulaji wa nyama wanadai kwamba, ulaji wa mbogamboga hautoi protini
inayotakiwa mwilini. Lakini, hiyo tunaweza kusema kuwa ni kejeli kwasababu,
wale walao nyama siku zote upata protini isiyokuwa bora kwa binadamu. Ukweli ni
kwamba protini ya kutoka kwenye nyama ina tindikali (acid) hatari mwilini aina
ya “Uric acid” ambayo lazima ivunjwevunjwe na ini jambo ambalo linaweza kuleta
athari za kiafya siku za mbeleni.
Mbogamboga
na matunda pamoja na bidhaa zingine za wanyama kama vile; maziwa ni chanzo cha
protini yenye ubora wa hali ya juu (daraja la kwanza) kuliko ile itokanayo na bidhaa
za nyama. Ushahidi uliopo ni kwamba unahitaji kuangalia mnyama mwenye nguvu
nyingi duniani. Tembo, Faru, Nyani – (wanayama hawa wananguvu mara 30 zaidi ya
binadamu), na wote wanaweza kuishi kwa kutegemea majani, mbogamboga, na
matunda. Matunda na mbogamboga vitakupatia protini unayohitaji ambayo ni ya
daraja la kwanza.
Sehemu
kubwa ya makala hii imetokana na maudhui ya kitabu cha Bw. Robin S. Sharma
ambacho kinajulikana kama “MEGALIVING! 3O DAYS TO A PERFECT LIFE:
The Ultimate Action Plan for Total Mastery of Your Mind, Body & Character.
Kama unapenda kupata nakala tete (soft copy) ya kitabu hiki bonyeza neno KITABU; na kisha weka barua pepe yako, nitakutumia
kitabu hicho ndani ya masaa 48. Kama uliwahi kusajiri barua pepe yako hapa MAARIFA
SHOP; basi wewe nitumie
tu majina yako kwa whatsap no: 0788 855 409.
Endelea
kunufahika na http://maarifashop.blogspot mpaka utakapohisi umefanikiwa bila kikomo.
BILA "MABORESHO" IMANI YAKO INAWEZA KUKUANGUSHA
- Kila binadamu anapendelea kufanya kitu kadiri anvyotumwa na imani yake
- Imani Mbaya = Matokeo Mabaya
Uzoefu katika maisha ya binadamu
umeonyesha kuwa kile unachoamini zaidi ndicho ukuletea mafanikio uliyonayo.
Siku za nyuma kidogo nilichukua likizo yangu ya mwaka, wakati nikiwa likizo
nilibahatika kwenda Entebbe Uganda, nikiwa huko nilitembelea hoteli ya Imperial
Botanical Beach, lengo langu lilikuwa ni kuamsha upya mwili na fikra zangu
ndiyo maana niliweka jitihada za kuuzuria mafunzo ya jinsi ya kujenga na kutunza
afya ya mwili. Hakika nilipata nilipata somo la thamani kubwa kwa maisha yangu yote.
Kila binadamu anapendelea kufanya
kitu kadiri anvyotumwa na imani yake: Siku ya kwanza nilipokutana na mtaalamu
wa mazoezi ya viungo na afya, aliniuliza kuhusu tabia na utaratibu wangu kwa
ujumla juu ya ulaji wangu wa chakula kwa siku. Nilimwambia kuwa, mara nyingi huwa
ninakula milo miwili kwa siku; yaani kifungua kinywa na au chakula cha mchana
na usiku. Wakati nikimueleza hayo nilifanya hivyo huku nikiangalia saa yangu ya
mkononi, ndipo nikashitukia ni saa kumi na mbili jioni na baadae kugundua kuwa
sijala chochote kwa siku nzima. LAKINI bado nilijisemea kimoyomoyo “Kwangu mimi kula siyo kipaumbele ”.
Baada ya mtaalamu kusikia kuwa
huwa na kula mara mbili kwa siku aliniangalia na kuonyesha kusikitika kidogo,
lakini aliendelea kusema, “Unatakiwa kula
milo mitatu kwa siku.”
Kusikia hivyo nilimjibu kwamba,
habari hiyo ya milo mitatu kwa siku nilikwishaiskia kabla. Lakini pamoja na
kusikia habali hiyo, mimi imani yangu ni kwamba, iwapo nitakula milo mitatu
kila siku, unene wangu utaongezeka sana.
Mtaalamu wangu alicheka, na
akazidi kusisitiza kuwa ninatakiwa kula zaidi wakati wa mchana kwasababu mwili
unakuwa unafanya kazi sana. Kwahiyo, miili yetu uhitaji chakula cha kutosha nyakati
za asubuhi, na mapema kabla ya saa za mchana (adhuhuri), na pia tunahitaji
chakula kidogo nyakati za usiku, kwani muda wa usiku mwili unakuwa na kazi
kidogo sana kwa maana nyingine unakuwa umepumzika.
Niliambiwa kwamba kwa mtu ambaye
bado yuko vizuri kiafya, asipokula chakula cha kutosha ni kwamba badala ya mwili
kuunguza mafuta, mwili utaunguza misuli na ikitokea hali hii basi ujue hutakaa
huwe na kiwango cha uimara wa mwili unaoutaka.
Mimi nilikuwa ninaendelea kupigana
na imani yangu iliyozidikuniambia kuwa, milo mitatu kwa siku itaongeza kilo moja
ya uzito. Lakini kwakuwa nilienda kwa mtaalamu kwaajiri ya afya yangu, nilijifikiria
na kuamua kufuata ushauri niliopewa na mtaalamu.
Wasikilize wataalamu: Kwa
muda wa siku sita, nilianza kufanyia kazi imani mpya na kuanzia siku ya kwanza
nikaanza kupata milo mitatu kwa siku. Niliamua kufuata masharti kama
nilivyoelekezwa na mtaalamu kwa kuanza kula milo mitatu kwa siku. Kitu kimoja kilichojitokeza
ni kwamba nguvu ya mwili iliimarika zaidi. Kuanzia nyakati za asubuhi, nilijisikia
mwenye nguvu ya kutosha siku nzima. Niliendelea na mpango huu mpaka mwisho wa
siku ya sita, siyo tu kwamba sikuongezeka uzito, bali badala yake nilipugua
kilo kadhaa.
Kitendo cha kuamua kuachana na
imani yangu juu ya idadi ya milo kwa siku, na kuamua kumsikiliza mtaalamu, kilinisaidia
sana kufikia malengo yangu ambayo nisingeyatimiza hata siku moja kama
ningeendelea kufanya yale niliyoamini miaka yote.
Imani mbaya = matokeo mabaya:
Hoja muhimu juu ya stori hii ni kwamba, nilikuwa na imani potofu ambayo ilijengeka
siku nyingi na imani hii kimsingi ilinizuia kusonga mbele na hatimaye kushindwa
kutimiza malengo yangu ya kiafya. Pamoja na kwamba nimesikia tangu nikiwa mdogo,
kwamba mtu mzima anatakiwa kupata milo mitatu kwa siku, sikuwahi kuamini kama
faida zitokanazo na kula milo mitatu kwa siku zilikuwa za kweli. Nilikuwa na
taarifa, lakini, faida hizi sikuzipata mpaka pale nilipoamua kufunguka na
kuamua kujaribu yale niliyoelekezwa na mtaalamu —ndipo nilipopata uzoefu na
elimu ya kweli juu ya kile kilichoonekana kufanya vizuri kwangu.
Kwa vyovyote vile, ukweli huu ni
rahisi na unaweza kutumika kwenye hali yoyote katika maisha. Sasa swali kwako,
“ni imani zipi zinazokurudisha nyuma kiasi cha kushindwa kufikia mafanikio ya kipesa
au ndoto zako? Na utafanya nini kuondoa imani hizo?
Iwapo utapenda kujifunza jinsi
ya kutambua na kuondokana na imani ambazo siku zote zimekurudisha nyuma pale
ulipojaribu kutafuta uhuru wa kipato na mafanikio kimaisha, bonyeza; http://eepurl.com/bkXr3r kuweka
barua pepe yako, ili kujiunga na
programu ya mafunzo juu ya mafanikio ya kifedha.
Mafunzo haya yatatolewa bure kupitia barua pepe utakayosajiri
hapa: http://eepurl.com/bkXr3r.
Mafunzo yataanza tarehe 15/Septemba/2015 hadi
30/Septemba/2015. Kwa kujiunga na
mafunzo haya utapata thamani kubwa sana, ikiwa ni pamoja na kubadili mitazamo
hasi uliyonayo juu ya kupata pesa. Pia utapata kujua mbinu na njia za uhakika utakazozitumia
kufikia maisha ya ndoto yako kwa uhakika na kwa muda mfupi zaidi. Kama
unafikiri program yetu haikufai huko sahihi; LAKINI bado ninakushauri ujitahidi
kutafuta mtu, ambaye atakufundisha na kukupa mwongozo wa jinsi ya kufikia uhuru
wa kipato.
Kwa maelezo zaidi juu ya prograu hii ya mafunzo whatsApp:
+255 788 855 49 au E-mail: mchumieconomist2009@gmail.com.
KARIBU TWENDE KAZI PAMOJA
CHIMBUKO LA PESA NI HILI HAPA
- Afya Bora Ndiyo Machimbo ya Kudumu ya “Pesa” tuliyonayo!
- Watu Wengi Bado Wanaamini Kuwa Kitu Kinachoitwa “Afya” Kitajileta Chenyewe!
Katika
maisha ya siku hizi inashangaza sana kuona kuwa pesa tunazotafuta zimekuwa zimekuwa
adui yetu mkubwa wa miili na afya yetu kwa ujumla. Ndiyo maana leo hii, watu
wengi “wanakula dawa kama chakula badala
ya kula chakula kama dawa”. Maana yake ni kwamba, watu wengi wanayo pesa
lakini, Asilimia kubwa inatumika kununua dawa ili waweze kusogeza maisha yao
mbele. Mwanaharakati mmoja kutoka bara la Asia aliyejulikana kwa jina la “Dalai Lama”, alipoulizwa kitu ambacho
kiliwahi kumshangaza zaidi kuhusu ubinadamu, alijibu kuwa ni Binadamu:
“Kwasababu,
binadamu anatoa afya yake sadaka, ili kutafuta pesa. Alafu anatoa pesa yake
sadaka, ili kurudisha afya yake. Na sasa anaanza kuhofia juu ya mstakabari wa
maisha yake ya baadae (future), kiasi kwamba anashindwa kufurahia maisha
yaliyopo wakati huu; Matokeo yake ni kwamba mtu huyu hawezi kuishi wakati huu
(uliopo) au ujao; anaishi kama vile hatakaa aje kufa na alafu anakufa kama vile
hakuwahi kuishi”
Maono
ya mwanaharakati huyu yanatuonyesha kwamba, muda mwingi wa maisha yetu
hatufanyi kitu chochote kinachohusu afya zetu isipokuwa tunaelekeza nguvu,
ujuzi, maarifa na rasilimali nyingine kwenye mambo tu ya kutafuta pesa peke yake.
Fikra za waliowengi ni kwamba bado wanaamini kuwa kitu kinachoitwa “afya”
kitajileta chenyewe, ilimradi uwe na pesa, na wengine wasiojua wanaamini katika
“Pesa Kwanza na Afya Baadae”.
Kwa
sasa hali ya afya kwa waliowengi siyo nzuri, na hii ni kutokana na kutokuwa na
malengo na mipango inayohusu afya. Mipango mingi inalenga zaidi kujiendeleza kiuchumi,
kielimu, kujenga nyumba nzuri, kuongeza uzalishaji, kununua magari n.k. Ni watu
wachache wenye kuwa na malengo na mikakati ya kujenga na kuimalisha afya zao. Mara
nyingi, watu wanakumbuka kujali afya zao pale wanapougua au kuanza kusikia
maumivu. Wataalam na wadau wengine wa masuala ya afya, wanatwambia kwamba, pale
unapoanza kujisikia maumivu ndani ya mwili au kuumwa kabisa, basi ujue kuwa umechelewa
kula chakula kama dawa.
Mara
nyingi, imekuwa ni kawaida kuletewa chakula bora pale tunapokuwa tayali tunaumwa
na kulazwa hospitalini, ndiyo maana ukitembelea wagonjwa, unapishana na watu
wakipeleka machupa makubwa ya jwisi na matunda ya kila aina. Vyakula hivi ambavyo
tunaletewa tukiwa wagonjwa, hakuna mtu anayeweza kukuletea tena nyumbani kwako
ukiwa mzima, kwasababu, ni matarajio yetu kuwa, ukisharudia hali yako nzuri
kiafya, utachukua jukumu la kuendelea kujali afya yako wenyewe. Lakini, cha
ajabu, hatufanyi hivyo mpaka tunapoletewa vyakula kwa mara nyingine, pindi tunapougua
tena!. Ukweli ni kwamba, jambo la kuimalisha na kulinda afya zetu
tumelichukulia la mzaa sana. Kwahiyo, ni muhimu sana tukatambua kuwa mafanikio
makubwa tunayotafuta kwasasa yataweza kufikiwa kwa haraka iwapo tutazipa afya
zetu kipaumbele namba moja, nje ya hapo maisha bora yatabaki kuwa ndoto ya
milele.
Ukitafakari
kwa kina sana, utagundua kuwa afya bora ndiyo machimbo ya kudumu ya “Pesa” tuliyonayo. Afya bora ndio
utupatia rasilimali “nguvukazi”na
pindi nguvu kazi yetu tunapoiwekeza kwa ufanisi hasa katika shughuli za
uzalishaji ndipo tunapata bidhaa au huduma ambazo watu wengine utoa na kuleta pesa
kwetu, ili kujipatia bidhaa/huduma husika. Pesa ndiyo utuwezesha kupata mahitaji
yaliyo mengi kwa muda tunaoutaka na hatimaye kufikia maisha bora ambayo ndiyo
ndoto yetu ya muda mrefu.
Kwakuwa,
pesa tuipatayo, chimbuko lake ni afya bora, ni muhimu kwa kila shilingi ya pesa
tunayoipata, mgao wa kwanza uelekezwe kwenye kuimalisha na kulinda afya.
Tunasema suala la matumizi ya pesa kwenye afya, liwe ndio kipaumbele namba moja
kwasababu afya ndiyo kisima chetu cha pesa. Unapoamua kutenga pesa kwaajili ya
afya yako, maana yake ni kwamba unazifanya pesa zako kuwa rafiki mkubwa wa
mwili wako. Pesa zinakuwa rafiki yako pale unapozitumia kujenga, kuimalisha na
kulinda afya yako kwa ujumla. Pesa haziwezi kuwa rafiki wa mwili wako, kama
hazijatumika kulisha chembe hai za mwili kupitia ulaji wa vyakula na
virutubisho muhimu. Nje ya hapo, chembe hai za mwili wako hazina uhusiano na na
pesa yako iliyoko mfukoni, benki au kwenye miradi yako ya biashara.
Wito
kama unataka mafanikio makubwa anza sasa kuweka malengo ya kupata afya njema na
kipato. Ni muhimu vitu hivi viwili viende pamoja kwasababu katika maisha ya Ujasiriamali,
vinategemeana sana na vinapoungana ndiyo tunapata furaha ya kweli. Kwahiyo,
jitahidi sana kujali afya wakati wote wa safari yako ya kusaka mafanikio ili
ukifika maisha ya ndoto yako uwe una afya njema na hapo utafurahia zaidi kuliko
anayeumwa kwasababu aliunyima sana mwili wake wakati wa safari ya kusaka
mafanikio.
MAAMBUKIZI KUPITIA NJIA YA MKOJO (UTI) YANAATHIRI WANAWAKE WENGI TANZANIA
Wanawake wanapata ugonjwa wa UTI kwa
urahisi sana kuliko wanaume kwa sababu mirija ya mkojoya mwanamke ni
mifupi ambayo huruhusu bacteria kuingia kwa urahisi tofauti na ya mwanaume. Katika magonjwa yanayosumbua
wanawake wengi na watoto nchini hivi sasa ni ugonjwa unaoathiri njia ya mkojo
yaani U.T.I (Urinary Tract Infection). Wakati wanawake wengi wanaougua
ugonjwa huu wakihangaika kila siku kupata tiba yenye usahihi, wataalamu wa afya
wanasema UTI inapojihimarisha mwilini kwa muda mrefu huathiri figo pia.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya
Wanawake na Afya ya Uzazi kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dk. Cyriel
Massawe anasema, tatizo hili hujitokeza pale mlango wa njia ya haja ndogo
unaposhambuliwa na bakteria ambao husambaa na wasipotibiwa mapema, huenea hadi
kwenye figo na athari zake ni mbaya.
“Bakteria hawa hupatikana ndani
ya sehemu za siri za mwanamke, bakteria hao wakiwa ndani ya uke hawana madhara
kabisa, lakini pindi uke unapopata mchubuko bakteria hawa huanza kuathiri
kibofu cha mkojo na mtu kuanza kupata madhara,” anasema na kuongeza: Wanawake wanapata UTI kwa
urahisi sana kuliko wanaume kwa sababu mirija ya mkojoya mwanamke ni
mifupi ambayo huruhusu bacteria kuingia kwa urahisi tofauti na ya mwanaume.
Vyanzo vya UTI
i.
Matumizi ya maji machafu wakati wa kujisafisha au kuoga huweza kuweka
bakteria kwa urahisi na mwanamke kupata UTI.
ii. Uchafu wa vyoo umetajwa kuwa sababu nyingine,
kwani matumizi ya vyoo ambavyo ni vichafu huweza kusababisha mwanamke kupata
UTI kwa sababu ndani ya choo kuna bakteria wengi ambao wanaweza kusababisha
UTI.
iii. Kufanya ngono mara kwa
mara ni tatizo kubwa ambalo ndilo linafanya wanawake wengi kupata UTI siku
hizi, kwani wakati wa ngono msuguano huwa mkubwa ambao hufanya bakteria kutoka
kupitia majimaji ya ukeni na kuingia katika njia ya mkojo. “Mwanamke ambaye anafanya ngono mara kwa mara yuko kwenye hatari ya kupata UTI
kuliko yule ambaye hafanyi ngono mara kwa mara.
iv.
Matumizi ya nguo za ndani za
mitumba bila kufua husababisha kwa urahisi mwanamke kupata UTI,” anasema.
v.
Matumizi ya vipodozi na sabuni
zenye "KEMIKALI" Ambazo zinawaathiri wanawake wengi siku hizi,
kutumia sana kemikali hasa kwenye vipodozi na sabuni ambavyo kemikali hizi kwa
kuwa ni sumu huenda hadi kwenye kibofu na kuchubua kibofu na hapo ndipo tatizo
hilo huanza.”
vi. Tabia tabia ya kubana mkojo kwa muda mrefu, lakini matokeo ya tabia
hii ni kupata UTI:
No comments:
Post a Comment