Wajasiriamali




Ukweli Kuhusu Mwekezaji ni Huu
“Usitegemee kipato kutoka kwenye chanzo kimoja peke yake BALI wekeza ili kutengeneza chanzo cha pili” ~ Warren Buffet
 
Birashaka wewe unayesoma makala hii, umesikia mara nyingi maneno kama “uwekezaji, mwekezaji n.k. Pengine niseme kuwa, kwa nchi kama Tanzania ambayo iliwahi kuongoza na kuendesha siasa zake pamoja na uchumi wake kwa kufuata falsafa na kanuni za mifumo ya ujamaa na hata ukomunisti, neno “uwekezaji na wawekezaji” ni vitu ambavyo ni vigeni na vinachukuliwa kuwa ni kazi ambazo ni maalum kwa wazungu!. Watanzania wengi bado hawaamini kama mtanzania tena ambaye ni mweusi anaweza kuwa mwekezaji”.

Unaposikia kuwa mtu fulani ni mwekezaji, mara moja akiri yako inakutuma kuwa huyo lazima atakuwa ni mtu mkubwa sana mwenye majumba, viwanja, viwanda, magari, pesa nyingi n.k. Pengine inawezekana picha uliyonayo kichwani mwako kuhusu mwekezaji ndiyo imekufanya uogope kuwa mwekezaji.

Sasa swali linakuja huyu mtu anayeitwa mwekezaji ni nani? Unaweza ukashangaa jinsi jibu lake lilivyo rahisi. Watu wengi huwa wanajiweka mbali na uwekezaji kutokana na sababu kwamba uwekezaji ni kitu ambacho ni kigumu sana na kinahitaji mchakato mrefu sana au wanafikiria kuwa, ili kuwa mwekezaji ni lazima uwe na pesa nyingi.

Njia rahisi ya kuelezea dhana nzima ya uwekezaji ni kama vile; kununua kitu kwa matumaini kwamba ukikiuza utapata pesa zaidi ya ile uliyonunulia. Mfano halisi mwingine ni kumfikiria mkulima anavyofanya shughuli zake za uzalishaji.

Tuseme kwamba mkulima amenunua mbegu ya mahindi na kuzipanda kwa matumaini ya kwamba muda mfupi mbegu moja tu itampatia punje nyingi za mahindi. Kwa maana nyingine ni kwamba; tayari mkulima huyu atakuwa na zaidi ya kile alichokipanda ardhini.

Kwahiyo, inatosha kusema kwamba mkulima ni “MWEKEZAJI”.

Mfano wa kilimo cha mahindi hapo juu unaweza kulinganishwa na ununuaji wa hisa, ambao nao unaweza kuelezeka vile vile kama kitendo cha mkulima anayepanda mbegu moja kwa matumaini ya kupata mbegu nyingi zaidi ya kile alichopanda. Kama wewe ni mwekezaji, unatenga pesa kununua hisa kwenye kampuni fulani kwa matarajio ya kupata faida au pesa zaidi ya hizo ulizotumia.

Kiukweli ni kwamba, “uwekezaji siyo mchezo wa kamali au kubahatisha”. Kwasababu, kamali ni kile kitendo cha kuweka pesa katika hatari ya kubahatisha matokeo yasiyojulikana na ambayo hayatabiriki kwa matumaini kuwa utaweza kapata pesa zaidi. Sehemu ya mkanganyiko huu kati ya uwekezaji na kamali (bahati na sibu), unaweza kutokana na jinsi ambavyo watu wengi wanavyotumia pesa zao kuwekeza. Wengi tumekuwa na tabia ya kuwekeza kwenye miradi ambayo tumesikia na kuona juu juu eti! Inalipa sana!

Kwa mfano: unaweza kusema kwamba mtu anayefanya maamuzi ya kununua hisa kwa kutumia tu maneno aliyosikia mitaani, kimsingi ni sawa na kutumia pesa yako kucheza kamali au bahati na sibu kwenye kumbi za starehe. Mwekezaji wa kweli na ambaye ni makini, huwa hatupi tu pesa yake kwenye mradi wowote unaopita mbele yake.

Kujifunza na kubobea kwa maana ya kuzijua na kuzielewa vizuri kanuni za uwekezaji inachukua muda au inahitaji uwekezaji wa muda mrefu kwenye elimu juu ya mambo ya fedha na uwekezaji.

Kufahamu na kuelewa vizuri mambo yote ya msingi juu ya uwekezaji, itakuwezesha wewe kuanza uwekezaji bila woga. Unaelekea wapi baada ya hapo ni juu yako. Hii ina maana ya kwamba; aina ya mwekezaji na kiwango gani cha uwekezaji utakachokuwa nacho ni juu yako.

Jinsi yakuwa mwekezaji aliyefanikiwa itategemea zaidi elimu yako. Kutokana na utofauti huu wa elimu juu ya biashara na uwekezaji, ndiyo maana kuna wawekezaji wadogo na wakubwa.

Sasa wakati umefika wa wewe kuacha woga wa kuwa mwekezaji. Anza kuchukua hatua moja baada ya nyingine kwa kuanza taratibu kujifunza kanuni na mbinu madhubui za uwekezaji. Kumbuka kuwa maisha mazuri na uhuru wa kipato vyote vitawezekana endapo utaamua kwa dhati kuanza mara moja safari yako ya uwekezaji.

Endapo unataka kuwa mwekezaji mkubwa, jitahidi sana kujifunza kupitia mtandao wa MAARIFA SHOP. Acha kufanya maamuzi ya uwekezaji kwa kutumia taarifa za mitaani badala yake soma vitabu na makala hasa zinazohusu masuala mazima ya uwekezaji na ujasiriamali kwa ujumla. Bonyeza neno “KUJIUNGA” ili kujipatia makala nzuri moja kwa moja kupitia barua pepe yako, kila mara zitakapochapishwa hapa - http://maarifashop.blogspot.com

Kwa Ushauri na Mafunzo, Tumia:

WhatsApp/Telegram: 0788 855 409


Unapata Faida Gani Kwenye Woga?
 
"Kitu pekee tunachoweza kuogopa ni woga wenyewe" ~ Franklin D. Roosevelt


Jiulize leo: “Ni faida kiasi gani unaweza kutengeneza kutokana na woga?. Na hii ndiyo sababu ya kwanini nimelazimika kuangalia moja kwa moja kwenye macho ya “WOGA” bila woga.....

Neno woga...
linasikika mara kwa mara kuliko "imani na matumaini ya mambo mazuri".

Mwanaume na mkewe wanashirikishana neno “woga” ili kutoshereza hali ya mashaka waliyonayo kwa siku za baadae au mbeleni…


Wapenzi ambao ndo wameanza kupendana, mara nyingi wakati wa mahaba wanashirikishana zaidi “woga” kabla ya kukubaliana…

Wafanyabiashara nao pia wanaongelea sana juu ya WOGA wa kupata hasara zaidi bila sababu…...


Kwahiyo, WOGA ni nini?: Tunaweza kusema kuwa “woga” si kitu chochote zaidi ya hali ya muamko wa hisia za fikra ambazo zinahitaji marekebisho madogo ya mtazamo wa mhusika. Ni hivyo tu basi ndugu yangu!

Muamko wa hisia unatengenezwa ndani ya fikra au akiri yako, na unapewa nguvu na kuruhusiwa na sisi wenyewe.

Sasa tujiulize, ni watu wangapi waliwahi kufanikiwa kwa kujikita zaidi kwenye “Woga”?

Ebu tuchukulie watu wawili maarufu ambao walikuwa mawakala wa mabadiliko makubwa yaliyokuwa chanya:

Wa kwanza ni Thomas Edison: Kama mtu huyu angeangalia woga wake wa kushindwa mara 999 kabla ya kufauru ; leo hii wote tungekuwa bado kwenye giza mpaka leo.
Lakini pamoja na kushindwa mara 999; bado aliendelea kuamini na kujiamini kuwa anaweza kufanikiwa.

Ndiyo maana katika nukuu zake aliwahi kusema kuwa: “Sijashindwa, isipokuwa nimegundua njia 999 ambazo haziwezi kufanya kazi na wala haziwezi kufanikisha ndoto yangu”.

Kwasababu hakukata tamaa na hakuusikiliza woga wake unamwambia nini, leo hii wote tunaona na kufurahia mwanga wa umeme.

Wa pili ni Henry Ford: Huyu ni mtu mwingine ambaye ni mfano wa kusisimua abaye aligundua magari; Kama angekata tamaa na kuacha kutimiza ndoto zake, nani anajua pengine leo hii tungekuwa bado tunatembelea ngamia au farasi.

Lakini kwasababu, hakukubali “woga” umtawale, leo hii tunashuhudia watu wengi wakiendesha magari mazuri.

Kwasababu bwana Thomas Edison na Henry Ford hawakukata tamaa na wakaendelea na kazi ya kutimiza ndoto zao, leo hii tunafurahia mwanga wa umeme unaotuwezesha kuona wakati wa usiku huku tukiendesha magari yetu ...

Mpendwa msomaji wa mtandao wa Maarifa Shop, ukweli ni kwamba watu wote tunazo ndoto kubwa. LAKINI ni kwa namna gani tunaweza kuzitimza?

Je? Kukaa tumeangalia na kufikiria zaidi woga kutatufikisha karibu na ndoto zetu? Bilashaka jibu sahihi ni HAPANA!!!

Lazima tubadili fikra na mitazamo yetu kama kweli tunataka kushinda na kupata mafaikio.

Hakuna wakala wa mabadiliko aliyewahi kushinda kwakuwa muhahirishaji wa mambo...

Hakuna wakala wa mabadiliko aliyefanikiwa kwa kuangalia zaidi mambo hasi au kwa kuangalia zaidi juu ya namna gani na kwanini mambo hayatafanikiwa….

Tunahitaji tudanganye woga wetu na tuangalie zaidi kile kitakachozidi kutusogeza karibu na ndoto zetu kuliko kukaa tumeangalia zaidi yale tunayodhani hayawezekani.

Somo tunaloweza kujifunza kutoka kwa Thomas Edison na Henry Ford ni kuwa na tabia ya kuushinda woga.

Kuzidi kujali WOGA hakuwezi kutupeleka karibu na ndoto zetu. Kama ni lazima tushinde, lazima tuwe tayari kudanganya WOGA wetu leo.

Nitawezaje kuushinda “woga” unaonizuia kuwa mjasiriamali?

Suka upya ubongo wako: Kuusuka upya ubongo wako ni njia ambayo ni ya uhakika katika kukabiliana na woga ulionao na kujenga ujasiri unaohitajika ili uweze kwenda huko unakotaka kwenda. Jaribu kuadika maneno ya kiapo cha ushindi na ujiambie maneno hayo kila siku. Kiapo cha namna hii kinakujenga kuwa juu na kuongeza uwezo wako wa kujiamini. Pia, jisomee vitabu na machapisho mbalimbali ambayo yanakusaidia kuingilia kati sauti na mazungumzo hasi ambayo yamekuwa yakiendelea ndani ya akiri yako.

Tagu tukiwa watoto wadogo, tumeambiwa vitu ambavyo hatuwezi kuvifanya, hatuwezi kuwa navyo n.k. Kama hutafanya jitihada za kusuka upya ubongo na fikra zako kwa ujumla, woga utafanya kazi hiyo na matokeo yake yatakuwa mabaya kwako na jamii inayokuzunguka.

Tengeneza mpango wa kufanya yale unayohitaji kufanya: Mara nyingi huwa tunakuwa na woga hasa pale tunapokuwa hatuna taarifa na mpango madhubuti wa kile tuachotaka kukifanya. Weka malengo yako bayana yakiambatana na mpango madhubuti wa utekelezaji. Baada ya hapo chukua hatua kwa kuanza kufanyia kazi yale uliyoyapanga hatua kwa hatua. Kuchukua hatua dhidi ya malengo yetu kunatupunguzia msogo wa mawazo na kutukinga dhidi ya kuchanganyikiwa kunakochochewa na woga wa kushindwa.

Fanya kitu kimoja kila siku ambacho kinakutisha: Kuendelea kukukaa kwenye ukanda wa kujisikia vizuri au hali uliyoizoea, siyo njia nzuri ya kuishi. Bila kufanya vitu ambavyo vitakushitua kunaongeza uwezekano wa woga ndani yako kuwa mkubwa na baadae kuchukua sehemu kubwa ya maisha yako. Kinaweza kuwa kitu kidogo ambacho unakifanya kila siku, lakini fanya kitu kila siku ambacho kinakutisha.

Unapojenga tabia ya kufanya kitu cha kukutisha kila siku, taratibu taratibu ujasiri wako wa kushinda woga unaongezeka siku hadi siku. Muda si mrefu vizuizi ambavyo hapo mwanzo vilikuzuia kusonga mbele, vitapotea na uwezo mkubwa uliopo ndani yako utajitokeza kwa kiwango cha juu sana. Kitendo cha kufanya maamuzi ya kutoruhusu woga ukurudishe nyuma tena, ni mojawapo ya maamuzi bora sana ambayo unaweza kuyafanya ili kuhakikisha mafanikio makubwa mbeleni.

Kufanya maamuzi ya namna hii siyo kitu kinachoweza kutokea kwa siku moja, lakini kuchukua hatua za makusudi na kuukimbia woga wako kila siku, inakupa matumaini ya kupata matokeo mazuri siku za baadae.

Kila kitu kizuri unachotaka maishani kiko nje ya ukanda wako wa kujisikia vizuri au mazoea. Usiruhusu “woga” kuwa ndiyo sababu ya wewe kuishi maisha duni na yasiyokuwa huru. Kwa mbinu hizi tatu hapo juu,pamoja tutamshinda adui “WOGA”.
Endelea kuwa karibu na mtandao wa MAARIFA SHOP Kwa kubonyeza neno “KARIBU”, Kama njia muhafaka ya kujifunza kuushinda “woga”.



Elimu ya Ujasiriamali Haipo Chuoni Iko Wapi?
“Usione aibu kutokana na kushindwa, jifunze kutokana na kushindwa na uanze tena” ~ Richard Branson, mwanzilishi wa kampuni ya Virgin Group.

Mara nyingi shuleni tulifundishwa kutii sheria na taratibu kama siyo kanuni; kufanya vitu kwa kutumia vitabu na kama ukionekana ukikaa mbali na kundi, haraka haraka unasukumwa tena kwenye tanuru ambalo hasa ni......
mfumo wa elimu rasimi, ambao siku zote utuweka na kutuandaa ili tufanane wote. “Shuleni siyo sehemu muhafaka kwa mjasiriamali”.
Mjasiriamali ni mtu anayefikiri tofauti na kiukweli; kila mmoja anafikiri na kujifunza tofauti. Ndiyo maana mfumo wa elimu rasimi ambao unalazimisha watu wote kufikiri sawa unaua kabisa roho na fikra za ujasiriamali. 
Wajasiriamali ni watu ambao wanafanya vitu tofauti na wanakwenda kinyume na mazoea au mtazamo uliozoeleka kwa watu wengi. Mara nyingi, wajasiriamali ukataa kulazimishwa kuishi maisha wanayoishi watu wengine na pia ukataa kufikiri sawa na watu wengine, haijalishi ni wengi kiasi gani.

Mfano: Watu wengine wanaambiwa hakuna kuuza mahindi kuna baa la njaa linakuja, LAKINI kama mjasiriamali yeye hawezi kukaa akaamini yale aliyoambiwa na watu wengine, badala yake atafikiri na kutenda tofauti na alivyoambiwa. Hapa yeye ataamua kuuza mahindi yake na pesa itakayopatikana anaweza kununua mbuzi wenye mimba ambao baada ya miezi kadhaa watakuwa wamezaana na kuongezeka maradufu, pia watakuwa wamepanda thamani kwa kiwango kikubwa wakati huo, kuliko ambavyo angeendelea kutunza mahidi.

Mjasiriamali huyu ukimfikiria haraka haraka unaweza kudhani ni mtu mkorofi, lakini ukimfikiria kwa mtazamo wa kiujasiriamali utamuona ni mbunifu wa kuigwa. Kwa kifupi ni kwamba mjasiriamali ni mtu ambaye anapenda kutengeneza, kuumba, kutenda, kuibua kitu kinachojibu changamoto za wakati huo; siyo kufuata misaafu ya vitabu vya kanuni zilizotengenezwa na mtu mwingine.

Ujasiriamali ni nadra kufundishwa darasani: Leo hii, elimu inabadilika. Wakati watoto wengi katika shule za msingi na sekondari bado hawajifunzi “Pesa na Biashara”; vyuo na hasa vya biashara, vimeanza kufundisha kozi mbalimbali za ujasiriamali kwa wale wote ambao wana malengo ya kujenga na kukuza biashara zao. Jaribio lolote la kuendeleza na kukuza ujasiriamali ni la msingi sana na la kuigwa; lakini kuwa mjasiriamali aliyefanikiwa ni nadra sana kufundishwa darasani. Wajasiriamali lazima wawe ni watu ambao wako tayari kubadilika haraka kulingana na hali au changamoto zilizopo. Lazima wawe na roho ya ujasiri wa kupambana na changamoto kadiri zinavyoibuka bila kukata tamaa. Mambo yote haya hayawezi kutoka shuleni.

Wajasiriamali wanapata elimu wapi? Kama uliwahi kukutana na mjasiriamali aliyefanikiwa, birashaka utakuwa uligundua kuwa huwa hawapendi kupoteza muda hata kidogo. Muda wao una thamani sana, kwani wao wanafanya vitu vingi wao wenyewe. Kwa wajasiriamali walio wengi, kujifunza kutokana na makosa yao wenyewe na wajasiriamali wengine ndiyo njia kuu ya kujifunza.

Kwa maana nyingine ni kwamba, kujifunza kisawasawa kunaanza pale ambapo unathubutu kuanza kufanya kwa vitendo. Hii ndiyo sababu, matukio ya kujenga mtandao na program za kufundwa na wajasiriamali wengine, kujifunza kutoka kwa watu waliofanikiwa, kujisomea vitabu unavyopenda mwenyewe ni sehemu muhafaka ya kupata na kukuza elimu yako juu ya umiliki biashara yako. Siyo tu kuwa sehemu hizi ni muhafaka kwa kwaajili ya kukutana na watu, bali ni sehemu muhimu na muhafaka kwa upatikanaji wa rasilimali kama fedha za mitaji, elimu ya mahesabu na umiliki wa fedha, masoko na teknolojia—vyote hivi ni vitu ambavyo wajasiriamali tunahitaji.

Kwahiyo, wajasiriamali tunahitaji kuwa “makini” ili kufanikiwa? Ndiyo … lakni siyo katika namna au njia ambayo wengi wanafikiri ndiyo “umakini”.

Anza kufanyia kazi mradi wako sasa, kwani huo ndio utakuwa kichocheo cha wewe kujifunza na kupata elimu halisi ya ujasiriamali. Tukutane hapa “MAARIFA SHOP”,kwa elimu na kujifunza zaidi.


Muda wa Ziada Utakukwamua Namna Hii
 
“Yale unayofanya wakati wa muda wako wa ziada ndiyo yanakuweka huru au utumwani” ~Jarod Kintz
 
Utafiti uliofanyika duniani umeonyesha kuwa wengi wa wajasiriamali waliofanikiwa, walianza biashara zao kwa kutumia muda wao wa ziada. Ni mara ngapi umesikia mtu akisema “ningependa kufanya biashara hii LAKINI tatizo sina muda?” Unapoona mtu akwambia sina muda maana yake ni kwamba huyo mtu hana motisha, nia wala shauku ya kufanya hicho kitu ambacho umemshirikisha.

Majuzi nilipata kuongea na mzee mmoja kati ya wale waliosoma zamani zile za miaka ya 86 katika chuo kikuu cha kilimo Sokoine, Morogoro. Katika mazungumzo yetu alimtaja sana muhadhiri Profesa Mmari juu ya kauli yake kuhusu MUDA, anasema profesa huyu alizoea kusema darasani “Huwezi kukosa muda wa kufanya kitu unachokipenda”.

Kwa maana nyingine ni kwamba ukiona hujapata muda wa kufanya jambo fulani, basi ujue kuwa bado hujapenda au hujataka kufanya hivyo. Wakati mwingine ni vizuri tukatambua kuwa kitu kinachoitwa muda ni kitu kinachotengenezwa na sisi binadamu na kiuhalisia ni kwamba mara nyingi mpangilio wa shughuli zetu ndio unaotufanya ama tuwe na muda au tusiwe na muda kabisa.

Kwa mfano: Katika kila wiki kuna masaa 168. Je? Uliwahi kujiuliza masaa yote haya huwa yanakwenda wapi? Hapa utaona kuwa matumizi ya masaa 168 ya wiki nzima yanatofautiana kulingana na mfumo wako wa maisha. 

Katika ulimwengu wa MUDA tunaweza kusema kwamba kuna mifumo ya maisha aina mbili. Moja ni lile kundi la watu wengi wanaofuata mfumo wa maisha ya KUUZA muda na wapo watu wengine wachache wanaofuata mfumo wa maisha ya KUWEKEZA muda wao.

Mfumo wa maisha ya KUUZA muda au “kubadilishana muda na pesa”, unafuatwa zaidi na watu ambao ni waajiriwa pamoja na wale waliojajiri au kuajiriwa na biashara zao. Wewe kama ni muajiriwa, biashara yako kubwa ni kuwapa muda watu wengine halafu wao wanakupa pesa na maisha yanakwenda.

Mgawanyo wa matumizi ya muda kwa wale wote wanaofuata mfumo wa maisha ya KUUZA muda ni kama hivi:

Katika wiki moja kuna masaa 168:
  • Masaa 56 – kulala
  • Masaa 42 – kula, kusafiri, muda na familia n.k.
  • Masaa 40 – Kazi ya ajira
  • Masaa 30 – muda wa ziada, starehe, n.k.
Kwa kuangalia mgawanyo wa matumizi ya muda hapo juu ni kwamba, sisi wenyewe tunao uwezo wa kubadilisha matumizi ya muda uliopo. Kwa mfano: tunaweza sana kubadilisha matumizi ya masaa 30 kwa wiki ambayo ni ya ziada na starehe, yakawa ni masaa ya kufanya kitu kwaajili ya kutimiza ndoto yako au kukuletea utajiri siku za mbeleni.

Katika maisha tunaambiwa kuwa kitu ambacho huwatofautisha matajiri na watu wengi wa kawaida (masikini) ni kwamba; watu masikini utumia zaidi “muda wao wa ziada” kwenye starehe. Matajiri wao, utumia sehemu kubwa ya muda wao wa ziada katika kujenga biashara zao. Hakika hali hii ndiyo imeleta mgawanyiko mkubwa na tofauti kubwa kimaisha kati ya walionacho na wasiokuwanacho.

Tafiti nyingi zilizowahi kufanyika duniani, zinaonyesha kuwa mtu wa kawaida anatumia zaidi ya masaa matano kwa siku kwenye starehe. Starehe tunazosema ni kama vile kuangalia runinga, kuangalia mambo mbalimbali kwenye simu yako ya “smart phone”, movies kwenye tablet, kuangalia michezo, kuangalia video za michezo mbalimbali, vikao vya harusi n.k.

LAKINI, hiyo haina maana kwamba usifurahie starehe yoyote, BALI inabidi kufanya hivyo kwa wastani au kiasi. Kimsingi starehe hazitakiwi kula muda wako wa karibu moja ya tatu ya muda wako wa kufanya kazi kila siku. Usifanye hivyo hata kidogo.

Kila wakati ujiulize ni gharama kiasi gani unazilipa kutokana na tabia yako ya kuendekeza starehe? “million 1 kwa mwaka? million 5 kwa mwaka? au Milioni 10 kwa mwaka? Au zaidi? Je utajisikiaje kama kuachana na tabia ya kuendekeza starehe itakufanya utajirike?.

Hapa tunaona kuwa tunapata hasara mara mbili; kwanza tunapoteza rasilimali muda na pili tunapoteza pesa wakati vitu hivi viwili tunavyovipoteza kila siku ndivyo vinahitajika sana katika kujenga mtaji wa kufanya mambo makubwa mazuri tunayoyatamani kila siku

Anza biashara katika muda wako wa ziada (masaa 30/wiki)’…
 
Ukweli ni kwamba, kama unataka kutajirika, utatakiwa pengine kuanza biashara kwa muda wako wa ziada. Huitajiki kuacha ajira au kazi yako ya ajira mara moja na pengine unaweza ukaamua kutokuacha ajira yako.

Anza leo kujiambia maneno haya kila siku “sasa hivi ninafanya kwa muda wa ziada kwenye ndoto yangu na muda wote kwenye ajira yangu, lakini haitachukua muda nitaanza kufanya muda wote kwenye ndoto yangu. Fikiria maisha yatakuwaje?

Kwahiyo inatosha kusema kuwa masaa 30 kila wiki yanapotea na wakati huo huo tunaendelea kuwa masikini na kuishi maisha ya kubangaiza kila siku. LAKINI ni masaa hayo hayo 30 kwa wiki ambayo yakiokolewa na kuwekezwa vizuri yatakuweka huru na mwisho wake utakuwa mtu wa kusema, “biashara yangu ya muda ilifanya vizuri kiasi kwamba niliweza kuacha ajira”.

Wakati kuanza harakati za uokoaji wa masaa 30 yanayoangamia kila wiki ni leo. Endapo tukiacha masaa hayo yakaendelea kuangamia basi, tujue kuwa hatutabaki salama.




Hii Ndiyo Hatari ya Kukwepa Kukataliwa
“Nachukulia kukataliwa kama mtu anayejaribu kupigia tarumbeta kwenye masikio yangu ili kuniamsha niendelee na safari badala ya kurudi nyuma”
~ Sylvester Stallone ~

Katika ulimwengu wa nafsi kuna watu wa aina mbili. Kundi la kwanza ni wale watu wenye kumiliki nafsi zao, kundi hili tunaweza kuwaita “Wamiliki”; na kundi la pili ni................
wale watu ambao nafsi zao zinamilikiwa na watu wengine, na hawa tunaweza kuwaita “Wamilikiwa”.
Mara nyingi watu ambao ni wamiliki huwa hawaogopi kuomba au kusema chochote wanachokitaka kutoka kwa watu wengine. Ndiyo maana wamiliki hufanya vizuri sana linapofika suala zima la kuuza bidhaa/huduma na kupata maafiki au wachumba.

Kwa upande mwingine, watu ambao ni wamilikiwa, siku zote ni watu wanaoogopa sana jibu la “HAPANA” na siku zote wanajitahidi kufanya vitu ambavyo vinawasaidia kukwepa kusikia “hapana”. Kwa watu ambao ni wamilikiwa, jibu la hapana kwao linamaanisha “kukataliwa” jumla.

Neno hapana kwa wamilikiwa linasikika kama , “hapana, hapana, hapana!; hauna kitu chochote cha maana au thamani”. Lakini kwa watu ambao ni “Wamiliki” hapana ni sehemu nyingine ya “ndiyo”. Kwa maana nyingine NDIYO na HAPANA siku zote ni vitu vinavyoishi pamoja.

Kila binadamu anayo haki kamili ya kusema ndiyo au hapana, na haki hii ya kusema hapana, kamwe haiwabugudhi watu ambao ni wamiliki. Watu ambao ni wamiliki wanaheshimu sana haki hiyo.

Kwahiyo, wamiliki wanaposikia hapana, hawafikirii kuwa kuna kitu ambacho siyo sahihi kwenye ulimwengu. Wao huchukulia kuwa ni hali ya kawaida sana kama ambavyo mtu angekwambia au kukupa jibu la ndiyo. Wamiliki wanapopewa jibu la hapana, moja kwa moja wao huenda kwenye ombi au pendekezo jingine. Kwa ufupi maisha ni kuomba na ahadi.

Watu ambao ni “Wamilikiwa”, utumia muda wao mwingi kujaribu kukwepa jibu la hapana, kwasababu, wao wameifanya hapana kumaanisha “kukataliwa —jumla”. Na kwamba ni kukataliwa wao binafsi.

Inashangaza kuona kuwa Wamilikiwa, wanatumia muda mwingi kutaka kukwepa hapana kila inapowezekana. Hatari yake ni kwamba, kwa kujaribu kukwepa “Hapana” pia hujikuta wakikwepa “Ndiyo”. Vyote viwili vinaenda pamoja na vinaishi pamoja.

Sababu kubwa ambayo huwafanya watu kushindwa kupata kitu wanachokitaka maishani ni kwamba wanaogopa kukiomba. Woga unaotokana na kuogopa “kukataliwa” umewafanya wao kuichukulia Hapana kuwa ni sawa na kuwakataa wao binafsi.

Hali hii ya kuogopa kuambiwa hapana inaanzia kwa vijana wengi hasa wanaosoma shule ngazi ya sekondari. Unakuta kijana wa kiume anaogopa sana “Hapana,” kiasi kwamba hawezi kuomba moja kwa moja urafiki kwa msichana bila kwanza kufahamu mapema kama msichana huyo atakubali ombi lake. Badala yake ataanza kutuma ujumbe kwenye simu huku akijaribu kutokuwa muwazi na mkweli.

Mara nyingi, unakuta kijana anamuomba rafiki yake wa kiume, ili amsaidie kumuuliza msichana rafiki yake kama anampenda na yuko tayari kutoka na yeye kwenda kwenye disiko au promosheni. Kinachokuja kutokea ni kwamba kwakuwa msichana husika hajaongea na kijana ana kwa ana, mara nyingi hukataa.

Lakini, unakuta kuna kijana mwingine wa kawaida sana shuleni ambaye ujikuta akikubalika sana na mara nyingine kwenda disko na wasichana warembo sana, huku vijana wenzake wakishangaa jinsi anavyoweza kuwashawishi na kukubalika.

Katika maisha yetu ya kawaida siyo rahisi kujua siri ya mafanikio ya huyu kijana kukubalika kwake. Sasa tambua kuwa kijana huyu ni miongoni mwa watu kutoka kundi la “Wamiliki” ambao huwa hawaogopi kuambiwa hapana, wao huendelea kuuliza bila kujari hapana zinazotolewa.

Wamiliki wa nafsi na roho wanafanikiwa kwasababu hawana woga kushindwa au kukosa. Wamiliki siku zote huwa wanaendelea kuwa wajasiri hata pale wanapoingia kwenye ardhi ya “hapana”. Mchezaji maarufu wa mpira wa kikapu duniani, Bwana Michael Jordan aliwahi kusema “Nimekosa zaidi ya mara 9,000 katika maisha yangu ya kucheza mpira; Nimepoteza zaidi ya michezo 300; Nimeshindwa tena na tena katika maisha yangu, ndiyo maana ninafaulu na kufanikiwa ”.

Kuna tofauti kubwa sana kati ya kupoteza na kushindwa. Watu ambao ni “Wamilikiwa” wanatumia kupoteza kama kisinagizio cha kuacha kushiriki mashindano au michezo. Lakini “Wamiliki” wanapopoteza hawakati tamaa na wanapokea kupoteza kama kitu cha kawaida sana. Wamiliki hutumia kupoteza kama kichocheo cha hamasa ya kufanya vitu vikubwa zaidi.

Kwahiyo, wewe uliyebahatika kusoma makala hii, ifanye siku ya leo kuwa muhimu kwa kuanza kuishi maisha kama ya “wamiliki”. Endapo wewe ni mjasiriamali au mzalishaji wa kitu chochote (bidhaa na huduma), ni wakati huu unapohitaji zaidi kuwa “mmiliki wa nafsi na roho yako” ili hatimaye uache kutumia muda wako mwingi kukwepa HAPANA. Ukiendelea na utaratibu wako wa kukwepa na kuchukia kusikia hapana basi ujue maisha yako kibiashara na kiujasiriamali yatakuwa mabaya muda wowote kuanzia sasa. Kwa maana nyingine kama wewe unaogopa kuambiwa hapana ujue hutakaa uuze kitu chako mtu yeyote.

Kwahiyo, chukua kalenda yako leo na kwa upande wa juu mwa ukurasa, andika neno “Ombi kubwa leo”. Usikubali ipite hata siku moja bila kuuliza watu wengine wafanye kile ambacho unapenda kifanyike. Nakuhaidi utashangaa jinsi utakavyo pata NDIYO nyingi ambazo hukuzitarajia!” Na utashangaa jinsi ambavyo utaanza kuidhibiti “Hapana”. Utajifunza kusikia “hapana” kwa uzuri na kwa upole na siyo kuichukulia hapana kama kitu chako binafsi tena.

Kwa kujifundisha na kujikumbusha kila siku kuwa “HAPANA” huwa haimdhuru mtu hata siku moja!; nguvu yako itakuwa zaidi kuliko matarajio yako. Utaanza kusema moyoni kuwa “Kitu ambacho akiniui unifanya kuwa imara zaidi”. Utarudi nyuma na kuona kuwa, kile kilichozoeleka kuwa ni kukataliwa wewe binafsi kumbe hakina uhusiano wowote na wewe kama wewe. Na kucheka kwa sauti kwa jinsi ambavyo umeweza kuruka zaidi ya hilo la hapana. Pale vitendo vinapochukua nafasi ya wewe binafsi, basi utakuwa umejifunza mchakato mpya wa kujitambua.

Mara zote vitendo huwa havijali kuwepo kwa ndiyo na hapana. Kwa mtu wa vitendo, NDIYO na HAPANA ni kama kibao kinachoonyesha kushoto na kulia, au juu na chini. Kibao hiki hakina maana yoyote ya kukukatisha tamaa. Kikubwa zaidi ni kuzidi kuheshimu vitendo, kwani hivi ndivyo vitakupatia haraka kile unachokihtaji. Mwisho napenda kusema kuwa “kukwepa kukataliwa ni kukwepa kukubalika”

Aksante kwa kusoma makala hii. Kama unataka kupewa taarifa za makala mpya kila zinapochapishwa bonyeza maneno ”NITUMIE MAKALA MPYA” .


Huu Ndio Muujiza wa Makosa
“Mtu yeyote ambaye hajawahi kufanya makosa, ni yule ambaye hajawahi kujaribu kitu chochote kipya” ~ Albert Einstein ~
 Mpendwa msomaji wa MAARIFA SHOP ni kwamba kuna kitu kama muujiza karibu kwenye kila kosa lifanyikalo katika maisha yetu ya kila siku. Na muujiza huu unaitwa....

kujifunza au mafunzo. Nimetumia muujiza LAKINI kuna sayansi nyuma mafunzo yatokanayo na makosa tunayoyafanya kila siku. Kiukweli, ni sehemu ya msingi ya kila mchakato wa mantiki ya kujifunza. – hata wanyama wana uwezo wa kujifunza kutokana na makosa. Wanajifunza pia kutoka kwenye makosa yanayofanywa na wanyama wenzao.

Huko shuleni huwa tunajifunza kwamba makosa ni kitu kibaya sana na mara nyingi huwa tunapewa adhabu kila tunapofanya makosa. Hatahivyo, ukingalia namna ambavyo binadamu ametengenezwa kujifunza ni kwamba, sisi huwa siku zote tunajifunza zaidi kwa kufanya makosa.

Fikiria wakati ukiwa mdogo, makosa uliyoyafanya wakati ulipokuwa ukijifunza namna a kuendesha baiskeli. Utakumbuka kuwa ulifanya kosa moja baada ya lingine. Na baada ya siku chache ghafla, hukuanguka tena na badala yake tairi la baisikeli liliendelea kuzunguka, huku wewe ukizidi kusonga mbele bila kuanguka tena na kama vile “muujiza” dunia mpya ilifunguka kwako. Huo ndio MUUJIZA unaopatikana kwenye MAKOSA.

Mwanasayansi (Fizikia) mashuhuri aliyejulikana kwa jina la Albert Einstein aliwahi kusema kuwa “Mtu yeyote ambaye hajawahi kufanya makosa, basi mtu huyo hajawahi kujaribu kitu chochote kipya”. Kama unajifunza kitu chochote kipya, basi unatakiwa kufanya makosa, ili kukifahamu na kukielewa vizuri kile ulichojifunza. Kwahiyo, jitokeze na ukajaribu fursa mpya. Fanya makosa…….

Ni jinsi gani tunaweza kukabiliana na maudhi yatokanayo na makosa yetu.

Watu waliofanikiwa huwa wanakabiliana kwa kujifunza kutokana na maudhi ya makosa yaliyofanywa ama na wao wenyewe au na watu wengine.

Nilipoanza kuwa na ndoto ya kuwa mjasiriamali mkubwa na wa kimataifa, rafiki yangu na kocha wangu katika masuala ya ujasiriamali na biashara alinishauri ya kwamba nitafute kazi ambayo itanifundisha jinsi ya kuuza. Baada ya muda nilianza kufanya biashara ya ubia na kampuni ya kimataifa ya FOREVER LIVING PRODUCTS. Mwanzoni, nilikuwa na aibu sana na kazi ya kuuza ilikuwa ni kitu cha mwisho kukipenda, LAKINI kumbe hiki kilikuwa ni kitu pekee nilichokihitaji.

Kwa miaka miwili, naweza kusema kuwa nilikuwa muuzaji mbovu nilipokuwa nikijilinganisha na watu wengine wanaofanya biashara na kampuni hii ya kimataifa ya Forever Living”. Muda wote nililaumu sababu nyinginezo juu ya kushindwa kwangu kuwa muuzaji bora. Kwa mfano; nililaumu sana hali mbaya ya uchumi, bidhaa, hata wateja wangu. Kocha wangu hakupenda hata kuyasikia hayo yote niliyokuwa nikilaumu. Kama kawaida alipenda kwenda moja kwa moja kwenye msingi wa tatizo zima. “Pindi watu wanaposhindwa wao wenyewe, alisema: huwa wanapenda kulaumu”

Kocha wangu wa ujasiriamali, alikuwa anajaribu kunifundisha kwamba hisia za maumivu ya kufanya makosa zina nguvu sana kiasi kwamba watu wengi huamua kusukuma maumivu kwenda kwa watu wengine kupitia “kulaumu”. Wanasaikolojia ya akili ya binadamu wanadai kwamba mtu anapofanya makosa akapata wa kumlaumu na akafanya hivyo anapata nafuu na kujifariji. Ili nijifunze kuuza, nililazimika kuvumilia na kukabiliana na maumivu ya kushindwa kuuza bidhaa. Kadiri mchakato ulivyoendelea, nilijifunza namna ya kubadili maudhi ya makosa kuwa kitegauchumi badala ya changamoto au madeni.

Je? woga wa kupata maumivu ya kukataliwa na watu unakurudisha nyuma?: Kila mara nikutanapo na watu ambao wanaogopa kujaribu kitu fulani kipya, mara nyingi sababu huwa ni kwamba wanaogopa sana kufanya makosa au kupata maumivu yatokanayo na kukataliwa na watu. LAKINI uhalisia wa mambo ni kwamba, ili huweze kufanikiwa katika maisha, siyo tu kubahatisha, unahitaji kujaribu vitu vipya. Na kama utafanya hivyo, basi ujiandae kupata maudhi au kukataliwa ~ “Maumivu”.

Watu wengi hubadili maumivu ya makosa kuwa hasara au madeni kwa kusema vitu kama: sitarudia kufanya jambo hili tena” au ningejua nitashindwa.” Kwa kufanya hivyo, huwa wanaruhusu maumivu ya makosa yawarudishe nyuma. Watu hawa kwa maana nyingine wameacha kujifunza. Wamejijengea ukuta wa kuwakinga badala ya kujega msingi wa kuendeleza zaidi hicho wanachokifanya.

Maumivu ya makosa ni sehemu ya mafanikio: Lakini kama ilivyo kawaida kila tatizo ndani yake kumelala fursa, ndani ya maudhi yoyote kuna busara ndani yake. Ufunguo wa yote ni jinsi ya kukabiliana na kujifunza kutoka kwenye maudhi.

Kocha wangu katika biashara na ujasiriamali, alinisaidia sana kujifunza namna ya kukabiliana na hisia kali za maumivu ya kushindwa. Alisema, “sababu ya kuwepo watu wachache waliofanikiwa ni kwasababu ni watu wachache wanaoweza kuvumilia maumivu yatokanayo na makosa. Badala ya kujifunza kuyakabili, wanatumia muda wao mwigi kukwepa maumivu ya kushindwa/makosa.”

Kocha wangu aliamini kwamba maumivu ya kushindwa ni sehemu muhimu sana ya mafunzo katika maisha yenye mafanikio. Kama tunavyozidi kujifunza kutokana na makosa tunayoyafanya, ndivyo tunavyozidi kupata tabia ya ujasiri katika kutafuta mali kutoka kwenye maudhi ya makosa.

Hapa ni sehemu tu ya ushauri alionipatia juu namna ya kukabiliana na maumivu kufanya makosa.

1. Tarajia maudhi au kukataliwa:
Ni mjinga pekee anayetarajia mambo yote yafanikiwe kama alivyopanga, alisema kocha. Lakini, kusema kuwa mtu atarajie kupata maudhi, haina maana kwamba akae tu bila kuchukua hatua au akishindwa akae tu bila kufanya chochote BALI maana yake ni kwamba mara nyingi tunahitaji kujiandaa kiakiri, kifikra na kihisia, ili kuwa tayari kukabiliana na hali yoyote itakayojitokeza nje ya matarajio yetu, ambayo pengine unaweza usiitake au usiipende. Hii inakuruhusu kuwa mtulivu na mwenye heshima pindi pale mambo yasipokwenda sawa na ulivyotarajia, hali ambayo baadae ukuruhusu wewe kufikiri vizuri zaidi.”

Mafanikio yanachukua muda, na katika safari yake kuna kero nyingi sana. Lazima huwe tayari na huwe na nia ya kuendelea mbele huku ukijifunza kutoka kwenye makosa mbalimbali utakayoendelea kuyafanya wakati ukielekea kwenye safari ya maisha ya ndoto zako.

2. Kuwa na kocha karibu yako
Pindi mambo yakienda vibaya, ni nani utamwita? Kama ambavyo tuna namba ya dharura kwa kikosi cha zima moto na polisi, basi tunahitaji mtu tutakayempigia simu pindi tunapohitaji msaada wa ushauri juu ya mambo ya kibiashara na kifedha.

Mara nyingi kabla ya kuingia kwenye deal au venture, huwa ninamuita mentors na kuwauliza au kupata ushauri. Hii uniwezesha kujifunza kutoka kwa wengine na kutumia yale ninayojifunza kutoka kwa wnzangu kwenye mazingira ya kwangu.

3. Kuwa mwema kwa wewe binafsi
Mojawapo ya jambo la maumivu ya kufanya makosa au kushindwa kufanya kitu fulani siyo yale wasemayo watu wengine, BALI ni namna gani sisi tunajiona na kujisikia baada ya kufanya makosa. Watu wengi hufanya makosa na kujipiga wenyewe zaidi kuliko wanavyopigwa na watu wengine.

Nimegundua kuwa watu ambao wanakuwa wakali kwa wao wenyewe binafsi kiakiri na kihisia mara nyingi ni watu wa tahadhari sana, hasa linapofika suala la kutenda mambo wanayohisi ni ya hatari; kuchukua mawazo mapya; na au kujaribu kitu na fursa mpya. Ni vigumu kujifunza chochote kama kila mara huwa unajipa adhabu. Kwahiyo, jitahidi kuwa mwema wa wewe mwenyewe binafsi.

4. Sema Ukweli
Mojawapo ya adhabu mbaya niliyowahi kuipata ni kiwa mtoto ni pale kwa bahati mbaya nilipompiga jiwe usoni karibu na jicho mtoto wa jirani yetu. Mtoto huyo alikimbia nyumbani kwao kumwambia baba yake, nilikimbia na kujificha lakini . Baada ya baba yangu kupewa taarifa hizo alikasirika sana, na alinipa kichapo kikali huku akisema “Sababu ya kukupa adhabu siyo kwasababu ya kumpiga jiwe mtoto mwenzako BALI “ninakupa adhabu kwasababu ya kukibia na kujificha”.

Kwa maana nyingine KIFEDHA, kuna mara nyingi watu tumekuwa tukikimbia makosa, LAKINI kukimbia ni kuchukua njia rahisi “shortcut”. Wote huwa tunafanya makosa na kukutana na kero pamoja na maudhi. Tofauti ni kwamba, ni jinsi tunavyokabiliana nazo. Hii inaanza kwa kuona au kukabiliana na madhara/athari za hatua tuchukuazo na kusema ukweli juu ya chanzo na sababu za sisi kushindwa. Ni kwa njia hii pekee ndio tunaweza kukua kibiashara na kujifunza mbinu za kisasa katika kukabiliana na changamoto zitokanazo na makosa tunayoyafanya.

Aksante kwa kusoma makala hii. Kama kawaida, ukiona kuna thamani yoyote uliyoipata ndani ya makala hii hapa MAARIFA SHOP, tafadhari washirikishe rafiki zako wote na wataarifu iwapo wanapenda kufaidi kama wewe, basi ni kubonyeza neno “KUJIUNGA”. Kumbuka kuwa Mafanikio ni kitu cha kushirikishana ili kufikia maisha bora.



Kupata Mapato Makubwa  Kunahitaji Jambo Moja Muhimu
   
“Hakuna aliyewahi kulipwa pesa nzuri kwa kugundua matatizo, isipokuwa wale wanaotatua matatizo ya watu wengine wengi”


Pesa huwa inatiririka zaidi kuelekea kwa mtu yeyote aliye na suruhisho ya matatizo au changamoto mbalimbali zilizoko kwenye jamii.

Kwa kawaida ni kwamba, thamani ya suruhisho lako ni sawa na ukubwa wa tatizo au changamoto uliyotatua. Na hii ndiyo kusema kwamba, kiasi cha pesa utakachopata ni sawa na ukubwa wa changamoto ulizozipatia suruhisho au ufumbuzi. 

Kwa maana nyingine, watu wanakulipa pesa wewe, kutokana na matatizo unayotatua. 

Kwa Mfano: ukitoa suruhisho la changamoto ndogo utapata pesa kidogo; ukitoa suruhisho ya changamoto ya wastani utapata pesa ya wastani; ukitoa suruhisho ya changamoto kubwa utapata pesa nyingi na ukitatua changamoto inayogusa nchi nzima utapata pesa nyingi kutoka kwa watu wa nchi nzima.
  
Ndiyo maana watu ambao wako kwenye kiwango cha uwekezaji hapa Tanzania na duniani kote wanaheshimika sana kwa serikali na jamii kwa ujumla. Serikali nyingi duniani, upendelea kuwapa wawekezaji misamaa na unafuu wa kodi kama njia ya kuwavutia na kuwapa motisha.

Lengo likiwa ni kuwajengea mazingira wezeshi yanayowasaidia kuendelea kutoa suruhisho za kukabiliana na matatizo au changamoto mbalimbali, kama vile ajira kwa vijana. 

Kwasababu hiyo, kutokana na mchango wa wawekezaji hawa, jamii yetu imejikuta ikitoa pesa ili kulipia suruhisho mbalimbali zilizotolewa na zinazoendelea kutolewa na wawekezaji ambao ni “wafumbuzi wa changamoto”.

Kama wewe uko kwenye kundi la watu wanaotoa suruhisho kwa matatizo madogo basi huwezi kuelewa haraka dhana hii ya matajiri kupewa unafuu wa kodi. Serikali inapoamua kuondoa unafuu wa kodi, basi inafanya hivyo kwa umakini mkubwa na pale inapogundua kuwa imekaribia kuwaumiza watoa ufumbuzi wa matatizo makubwa nchini basi mara moja lazima waanze kutoa misamaa ya kodi katika sekta fulani fulani zinazozalisha bidhaa na huduma zinazogusa watu wengi.

Kama wewe bado uko kwenye fikra za kijamaa, ambapo unaendelea kuiona serikali kama baba wa kukupa misaada hata kwenye mambo yako ya starehe, hili la matajiri wakubwa kusamehewa kodi huwezi kulielewa sasa hivi, LABDA utalielewa huko mbele ya safari, pale utakapoanza kujishughulisha na ujasiriamali kwaajiri ya uwekezaji.

Katika hali halisi ya maisha ya binadamu, hakuna aliyewahi kulipwa pesa nzuri kwa kugundua au kubaini
matatizo, isipokuwa wale tu wanaotatua matatizo yao na ya watu wengine.

Kwa maana nyingine ni kwamba, uwezo wako wa kugundua matatizo haukamiliki kama wewe hautatafuta suruhisho la matatizo hayo uliyoyagundua.

Watu wengi katika dunia ya leo ni wazuri sana katika kuona, kutambua, kuibua na kulalamika juu ya matatizo LAKINI bado wameendelea kubaki maskini, kwasababu kazi wanayoifanya ya kuongelea matatizo kamwe haivuti pesa kuja kwao, bali pesa itakuja kwao iwapo wataamua kuwa wafumbuzi wa matatizo na watoaji wa suruhisho ya matatizo yanayosumbua watu wengi.
Usizungumze, usitafiti kuhusu umaskini au kujisumbua sana nao. Usijali ni nini chanzo cha umaskini, huna chochote cha kufanya kuhusu chanzo chake, kile unachohitaji wewe ni kupata tiba ya ya umaskini. 

Umaskini unaweza kuondolewa   siyo kwa kuongeza idadi ya watu wenye uwezo wa watu ambao watawafikiria masikini, bali ni kwa kuongeza idadi ya watu masikini, ambao watakuwa na kusudi na imani ya kuwa matajiri. 

Kwahiyo, jitahidi kufikiri kwa kina juu ya matatizo yaliyoko kwenye jamii yako ili hatimaye uweze kugundua na kutafuta suruhisho la matatizo hayo. Basi kwakufanya hivyo, utapata pesa kiasi kinacholingana na ukubwa wa suruhisho ulilotatua.



Ni Marufuku Kuwa Mjasiriamali
Fahamu Sababu 5 Kwanini Wewe Hutakiwi Kuwa Mjasiriamali

Mpendwa msomaji wa mtandao huu wa MAARIFASHOP, utakumbuka kuwa ni mara nyingi nimekuwa nikiandika sana juu ya ujasiriamali, na sababu za kufanya hivyo kwa sehemu kubwa ni kwamba ujasiriamali ndiyo njia ya uhakika ya mtu yeyote kuweza kuwa kiongozi wa maisha yake. Lakini pia ni kwamba, mjasiriamali ana uwezo wa kufanya chochote.

Kuwa mwajiri na bosi wako mwenyewe kunatoa fursa zaidi ya kupata uhuru binafsi. Kuwa mjasiriamali kunakupa uhuru wa kipato na maisha mazuri ya mbeleni.

Kuna sababu nyingi za kwanini mtu anatakiwa kuwa mjasiriamali, lakini kumbuka kuwa ujasiriamali siyo kwa kila mtu. Kuna mambo kama 5 hivi ambayo ukiwa nayo ni ama husiwe mjasiriamali au huyabadili kuwa mjasiriamali, “chaguo ni lako”

1.      Wewe una ngozi laini: Mara nyingi imeonekana kuwa mara tu unapotangaza  kuwa unaanzisha biashara, kila mmoja ni mtaalamu wa kuanzisha biashara. Ukweli ni kwamba katika mazingira haya ambayo kila mmoja anajaribu kukushawishi na wengine kukuogopesha kwa hoja zao, unatakiwa kuwa na ngozi ngumu. 

Ili kuweza kusimama kikamilifu kutimiza wazo lako au ndoto yako. Ama sivyo hutaweza kufika mbali kwasababu utakosa mwelekeo sahii wa kukamilisha wazo lako. Siyo, kila mmoja atapenda wazo lako hilo la biashara na hawataogopa kukwambia wewe juu ya mambo mabaya yanayohusu wazo lako jipya.

Sikwambii kuwa husiwasikilize wale wote watakao toa maoni juu ya biashara yako unayotarajia kuianza, LAKINI ni lazima huwe tayari kuchuja na ujiandae kifkra kusikia na kuvumilia yale mabaya yatakayosemwa juu ya mradi wako mpya. Bila hiyo utaishia kuogopa na mwisho wake hutaweza kuchukua hatua yoyote.

2.      Hautaki kujenga mtandao na watu wengine: Wewe kama mjasiriamali, huwezi kufanya biashara kwa kujitenga na dunia. Kwa mjasiriamali tunaweza kusema kwamba hakuna kitu kama hicho kinachoitwa “kujitenga” na dunia , hasa pale mwanzoni unapoanza biashara. Mwanzoni utakuwa unaishi na kupumua biashara yako mpya, kwasababu unajaribu kutaka kila mmoja afahamu juu ya biashara yako. Kila wakati utakuwa unafikiria jinsi na namna ya kuboresha, kupunguza gharama na kuuza zaidi. Kwahiyo, kwa mjasiriamali ni lazima biashara yako iende sawa na dunia inavyokwenda, maana bila hivyo biashara yako itakufa kabla hata ya kushuhudia matunda ya uwekezaji ulioufanya.
  
3.      Unapenda kupongezwa kwa juhudi zako: Kama wewe ni mwajiriwa, bila shaka umezoea kupata mrejesho juu ya utendaji wako wa kazi, kuimizwa juu ya utekelezaji wa majukumu uliyopangiwa. Waajiriwa wengi sana wamezoea,kuambiwa na waajiri wao jinsi walivyo wachapa kazi hata kama wanajua kuwa si wachapa kazi hodari.

Kwa mjasiriamali hakuna kitu kama hicho “kupongezwa”.  Ukiwa mjasiriamali huwezi kusikia kitu chochote cha kupongezwa, labda ujipongeze wewe mwenyewe. Pongezi zako kama mjasiriamali, zinakuja kwa njia ya pesa unayotengeneza kwa kufanya kazi husika. Na itachukua muda kabla ya wewe kuanza kupata pongezi ambazo unazitafuta.

Soma: Maisha ya Ajira Yamtesayo Mjasiriamali ni Haya Hapa

4.      Wewe unataka awepo mtu wa kukupa hamasa. Kama ilivyo kwa pongezi, kama unahitaji hamasa kutoka nje, basi hautakiwi kabisa kuwa mjasiriamali. Pindi unapoamka asubuhi, kama mjasiriamali, hakuna mtu yeyote anayesimama kwako kukupangia au kukupa ratiba ya kazi za siku hiyo. Mambo yote yako juu yako. Mjasiriamali lazima ujipangie, ujisukume, ujitume, ujitoe na kujiamrisha mwenyewe. Kwa maana nyingine ujasiriamali unamtaka kila mtu aliyeamua kufanikiwa, awe kiongozi wa maisha yake na hapa hatukutegemei, huwe mtu wa kulalamikia wengine isipokuwa wewe mwenyewe.

5.      Unajisikia vizuri unapovaa kofia moja. Kuna watu wengi unawafahamu ambao wanajisikia vizuri kwakuwa wahasibu, waandishi, au wapanga mipango ya matukio mbalimbali n.k. Watu hawa wanafurahi na kujiona wamefika kwa kufanya kitu kimoja na hawatakiwi wawe wajasiriamali. Kama mjasiriamali, ni lazima kila mara ujitahidi kuvaa kofia tofauti, huku ukifanya maamuzi mengi mbalimbali na unatakiwa kujiamini kwa kufanya hivyo.

Kama unafikiria kuanzisha na kumiliki biashara yako mwenyewe au kuwa mjasiriamali, lazima ufahamu kwanza kuwa mafanikio yako yanakutegemea wewe. Utakutana na changamoto nyingi na vikwazo vingi. Jinsi unavyokabiliana na changamoto  hizo ndivyo utakavyoweza kufanikiwa au kuendelea mbele ya safari yako ya mafanikio.

Mpendwa msomaji wa mtandao wa MAARIFASHOP; Kama kama umekuta thamani yoyote ndani ya makala hii, basi jaribu kuwashirikisha rafiki zako na familia. Kwani, mafaniko ni kitu cha kushirikishana, ili kufanya maisha yetu yawe mazuri zaidi


Maisha ya Ajira YamtesayoMjasiriamali ni Haya Hapa
 

Ni ukweli usiopingika kuwa maisha tunayoishi sasa, kwa sehemu kubwa yameegemea zaidi mfumo wa ajira na waajiriwa. Sababu mojawapo ya kuzama katika mfumo wa ajira ni kwamba, baada ya ukoloni na baadae ukoloni mamboleo kujikita katika bara la Africa, moja kwa moja tulianza kuathirika na mapinduzi ya viwanda uko barani Ulaya. 

Zama za mapinduzi ya viwanda ndizo zilisimika mfumo wa ajira na kundi kubwa la waajiriwa tunaowashuhudia leo hii. Kundi hili la waajiriwa limekuwepo kwa muda mrefu sasa na limejijengea misingi imara na taratibu za kuendesha shughuli zake. Mfumo wa ajira umekomaa kiasi cha kuyafanya makundi mengine (wakulima na wajasiriamali), kuendesha mambo yao kwa kufuata mfumo huu wa ajira na waajiriwa.

Kwa hapa Tanzania, mfumo wa ajira umeathiri sana kundi jipya la wajasiriamali, ambalo linazidi kupanuka kadili siku zinavyozidi kwenda mbele. Hatahivyo, pamoja na kupanuka kwa kundi hili, bado watu waliowengi ndani ya kundi hili, hawajaonekana kufanya vizuri kimaisha, licha ya kwamba wao wenyewe wanazo funguo za mafanikio yao.

Zipo sababu nyingi zinazofanya wajasiriamali wengi kutokufanya vizuri, lakini kubwa zaidi ni kuendelea kufungwa na kukumbatia tabia na mifumo yote inayoongoza “ajira na waajiriwa” kwa ujumla. Kwa maana nyingine, wajasiriamali wengi wazoefu na wapya wanaendelea kufanya kazi zao kwa kufuata na kutumia mifumo, kanuni, taratibu na tabia za waajiriwa au “watu wanaopangiwa chakufanya” kila wakati.

Kitendo cha wajasiriamali kuendelea kuishi kwa kufuata mfumo mzima wa maisha ya waajiriwa, kimedhoofisha sana jitihada mbalimbali za kufanikiwa kimaisha. Wajasiriamali wengi wameshindwa kubadilika kwanza kifikra na kitabia, ili kuishi maisha halisi ya mjasiriamali. Watu wanaendesha biashara na miradi mingine ya kiuchumi huku wakiwa bado ndani ya mfumo wa ajira na waajiriwa..!! 

Mfumo wa maisha ya waajiriwa ni sawa na mnyororo mkubwa ambao tusipotumia nguvu za fikra kuufungua, basi itabidi tusahau kuyaona maisha ya ndoto zetu. Ili kuanza mchakato wa kufungua mnyororo huu, inabidi tutafute funguo nyingi na tujipe muda kufungua sehemu moja baada ya nyingine. Sehemu za kuanza kufungua ziko nyingi, lakini ebu tuanze kwa kuangalia maeneo 7 yatakayo kusaidia kulegeza au kufungua mnyororo wa mfumo mbovu wa maisha ya waajiriwa:

1.       Waajiriwa wana siku maalum za kupumzika: Waajiriwa wengi wana mikataba ya ajira (rasimi na isiyo rasimi). Mikataba imetaja kuwa siku za mapumziko, hutakuja kazini na badala yake utaendelea na shughuli zako binafsi. Siku hizo ni kama vile siku za jumamosi na jumapili; sikukuu za kitaifa (mf. nyerere na karume day); sikukuu za kidini n.k. Kwa mtazamo wa waajiriwa, hizi siku zote zinaitwa siku ambazo “siyo siku za kazi”.
 
Wajasiriamali na sisi tumelichukua hili kama lilivyo na tunaamini kwa dhati kwamba siku za mwisho wa wiki na sikukuu siyo siku za kazi. Mjasiriamali halisi hana siku (weekend) maalum ya kupumzika, anapumzika anapokuwa amekamilisha malengo aliyojipangia. Kwa mfano: Anaweza kupanga kazi ambazo zitamchukua wiki mbili au mwezi kuzikamilisha, na baada ya hapo akajipangia siku au masaa ya kupumzika.

2.       Waajiriwa wana masaa maalum ya kufanya kazi: Waajiriwa wengi wanaanza kazi saa moja hadi saa mbili asubuhi na kutoka kazini saa tisa arasiri hadi kumi na moja jioni. Wajasiriamali nao, wanafanya biashara zao kwa kufuata masaa ya jua sawa na waajiriwa. 

Kimsingi hakuna sababu ya wajasiriamali kufuata ratiba ya masaa ya kazi kama wafanyavyo waajiriwa, tunatakiwa kuwa huru kwa kuipanga siku yetu (masaa 24) vingine, ili ikidhi matakwa yetu kama wajasiriamali. Unaweza kuamua kuamka na kuanza kazi saa tisa usiku hadi saa nne asubuhi na kupumzika kama masaa matatu hivi na baadae kuendelea na ratiba zingine, hufungwi na wala hukatazwi na mtu yeyote.

Tutakapofikia kuipanga upya siku yetu na ikawa tofauti na mtindo uliozoeleka na unatumiwa na watu wengi, ni wazi kwamba tutaweza kuokoa masaa mengi tunayopoteza kwa siku. Ukiweza kuokoa masaa 4 kila siku, maana yake kwa wiki utakuwa umeokoa masaa 28 ambayo ni sawa na siku moja na robo. Kwa mwezi mmoja unaokoa siku 5 na kwa mwaka unaokoa siku 60 sawa na miezi miwili.

Tofauti na wengine, wewe kama mjasiriamali, utakuwa unaingiza pesa kwa muda wa miezi ya 14 ndani ya ziada kutoka kwenye miezi miwili unayofanya kazi za kuingiza kipato. 

3.       Waajiriwa wanapenda kufanya kitu kimoja tu: Waajiriwa wengi wanapenda kufanya kazi ya aina moja maisha yao yote, na hii ni kutokana na mfumo wa elimu ambao unakulazimisha kubobea katika fani moja, yaani “specialist”. Waajiriwa wengine wanakuwa ni wataalam waliobobea katika fani mbalimbali, na pindi wanapoajiriwa, wanatakiwa kutumia taaluma zao kuchangia katika kufanikisha ndoto au malengo ya mtu mwingine ambaye ni mwajiri au tajiri wao.

Wajasiriamali wengi wanafanya biashara ya aina moja na kwa kwango kile kile miaka nenda rudi. Unakuta mtu anafanya biashara ya kuuza mchele, lakini unashangaa mtu huyo kwa muda wa zaidi ya miaka 10 bado anauza gunia tatu kwa mwezi miaka yote.

Sababu ya mjasiriamali huyu kuendelea kubaki vile vile miaka yote, ni kwamba amegeuza biashara ya mchele kuwa “ajira” na si mradi wa kumtoa kimaisha. Kwa maana nyingine, tunaweza kusema mtu huyu anafanya biashara ya kuuza mchele lakini anaishi maisha kama mwajiriwa, kutokana na kweli kwamba yeye ni “mwajiriwa wa biashara” ya mchele. 

4.       Waajiriwa wanapenda kupongezwa: Kama wewe ni mwajiriwa, bila shaka umezoea kupata mrejesho juu ya utendaji wako wa kazi unazopangiwa mara kwa mara kuzifanya. Waajiriwa wengi tumezoea kuambiwa na waajiri wetu, jinsi tulivyo wachapa kazi, hata kama tunajua kuwa si wachapa kazi hodari.  Imekuwa ni kawaida ya waajiri wengi, kuwapongeza wafanyakazi wao; kwasababu, pongezi zinatia sana hamasa na hivyo kuwafanya waajiriwa wengi kuongeza bidii ya kazi na kujituma kujituma zaidi. 

Kama waajiriwa, kupongezwa na watu wengine pale tunapofanya kazi zetu vizuri ni jambo jema, kwasababu tunapopongezwa na waajiri wetu, ni kiashiria cha kwamba, waajiri wetu wanafurahishwa na kile tunachoendelea kukifanya. 

Pia, tunapopongezwa na wakubwa zetu inatufanya tuendelea kujiona kuwa wenye uhalali na stahiki ya kuwepo mahali petu pa kazi. Kutokana na hali hii, watu wengi tumezoea sana na tunapenda kupongezwa na watu wengine kwa kila kitu tunachofanya maishani mwetu na hata kama kitu hicho ni kwa manufaa yetu binafsi. Kasumba hii, ipo zaidi kwa watu wengi walioajiriwa. 

Wakati kwenye ajira kuna utaratibu wa kupongezwa na wale waliotuajiri, kwenye ujasiriamali hali ni tofauti kabisa. Ukiwa mjasiriamali, hutasikia kitu chochote cha “kupongezwa” na watu wengine, labda ujipongeze mwenyewe. 

Pongezi zako zinakuja katika mfumo wa pesa utakazotengeneza kutokana na kazi ulizokamilisha kufanya. Na inachukua muda kabla ya wewe kuanza kupata pongezi “pesa” hizo. Kwahiyo, pongezi za kweli kwa mjasiriamali ni zile tu zinazotoka ndani yako wewe unayetenda kazi fulani. 

Ukiona umefikia kiwango cha kuipongeza kazi uliyoifanya wewe mwenyewe, basi ujue umeshinda hatua moja ya kujiondolea mnyororo unaokufunga usiweze kufikia maisha bora ya ndoto yako.
Kukosekana kwa jambo la “kupongezwa” na watu wengine hasa unapokuwa mjasiriamali ndilo limesababisha watu wengi na hasa wasomi kuona kuwa ujasiriamali ni mgumu au kuonekana ni kitu chenye changamoto nyingi sana. 

Matokeo yake, wale waliowahi kuingia kwenye ujasiriamali, wamejikuta wakikabiliana na hali ngumu ya maisha, kiasi cha watu wengine kuamua tena kusaka ajira, hata kama zinawalipa kiasi kidogo kuliko kiasi walichoanza kupata kutoka kwenye biashara zao binafsi.

5.       Waajiriwa wanapenda kutumia uzoefu tu! Waajiriwa wanafanya kazi kwakutumia uzoefu wa mambo yaliyowahi kutokea huko nyuma. Kwenye mfumo wa ajira, vijana wanapata wakati mgumu kupenyeza mambo mapya, kutokana na kutothaminiwa michango yao eti kwasababu siyo wazoefu. 

Mfumo wa ajira, unatumia sana suala la uzoefu katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya kazi. Kadili tunavyozidi kukumbatia mfumo wa kutumia uzoefu kwa kila jambo ndivyo tunavyozidi kupalilia ugonjwa hatari wa “mazoea”

Mwajiriwa anaweza kuendelea kutumia mfumo wa uzoefu peke yake na bado mambo yakaenda, lakini si kwa mjasiriamali. Kwa mjasiriamali halisi, licha ya kutumia uzoefu, unatakiwa kwa kiasi kikubwa kuwa na uwezo wa kubuni mambo mapya na ni lazima uwe na uwezo wa kuona picha nzuri ya maisha siku za mbeleni. Na kikubwa zaidi, lazima uanze kuchukua hatua mbalimbali za kukufikisha kwenye maisha hayo mazuri unayoyaona au kuyatarajia siku za mbeleni (future). 

6.       Waajiriwa hawapendi kufikiri nje ya mfumo uliopo: Tangu unapoajiriwa unakuta tayari kuna mfumo utakaokuongoza kwenye utendaji wako wa kazi, kwahiyo, ili uweze kukamilisha kazi zako vizuri ni wewe kufuata maelekezo na si vinginevyo. Ukifikiria njia mbadala siajabu ukaambiwa umekiuka utaratibu. 

Kwahiyo, wengi wa waajiriwa tunakabiliwa na “hofu ya kuvunja utaratibu” wa kazi na hivyo kushindwa kuwa wabunifu katika maisha, hali ambayo utusababishia umaskini. Katika ujasiriamali unatakiwa kila siku kufikiri na kubuni mambo mapya, pia unatakiwa kujifunza kila siku, ili kujijengea uwezo wa kukabiliana na changamoto ambazo huibuka kila wakati.

7.       Waajiriwa wengi wanafanya kazi ambazo hawazipendi: Watu wengi katika maisha ya ajira wanafanya kazi ambazo hawazipendi hata kidogo kutokana na ukweli kwamba, wengi wanatumikia ili wapate pesa ya kujikimu. Kazi nyingi zinazofanywa na waajiriwa wengi, nyingi hazitokani na ndoto zao binafsi bali zinafanyika ili kufanikisha malengo ya mtu mwingine.

Mara nyingi, nimekuwa nikikutana na wajasiriamali wengi ambao hawapendi kazi wanazozifanya utadhani kuna mtu amewalazimisha. Kama wewe ni mjasiliamali wa ukweli unatakiwa na ni lazima upende kazi hiyo unayoifanya nje ya hapo inabidi uiache ukatafute kazi utakayopenda kuifanya. Wajasiriamali wengi wameshindwa kufanikiwa kwasababu ya kutoipenda kazi wanazofanya.

8.       Waajiriwa wanajenga urafiki na watu wenye taaluma kama zao tu: Waajiriwa wengi wanatumia sana kigezo cha taaluma kuchagua na kupanga marafiki. Unakuta mtu kama ni mwalimu rafiki zake wengi ni walimu, daktari rafiki zake ni madaktari, muhasibu rafiki zake ni wahasibu n.k. Kiasi kwamba inakuwa vigumu sana kukuta mtu mweye taaluma fulani kujenga urafiki na watu wengine nje ya taaluma aliyoisomea. 

Hali hii ni kutokana na ukweli kwamba watu wenye taaluma moja mara nyingi wanakabiliwa na changamoto zinazofanana hasa zile zitokanazo na waajiri wao. Kwahiyo lengo lao la kujenga urafiki pamoja ni kuimarisha mshikamano, ili kudai maslahi yao kwa mwajiri. 

Wajasiriamali nao wameiga na kujenga kasumba kama ya waajiriwa, kiasi kwamba unakuta mfanyabiashara wa sokoni marafiki zake ni hao wa sokoni tena wenye bidhaa kama yake tu. Tabia hii kwa wajasiriamali inatukumaliza kimya kimya na hatuwezi kusonga mbele hata kidogo. Ukiwa mjasiriamali ni muhimu ukaanza kujenga urafiki au tandao na wateja wako bila kujali taaluma au kazi wanazofanya. 

Tunaposema kujenga urafiki siyo kumchekea tu mteja pindi anapokuja kununua bidhaa bali tunatakiwa kwenda zaidi ya hapo. Mfano; kama mtu ni mteja wako mzuri tunakutegemea akifiwa mtumie walau salamu za pole; akiwa na sherehe mpe mchango, akiwa mgonjwa mtembelee hospitali n.k. Ukiweza kufanya hivyo hakika ujasiriamali utakuwa umeupatia sawa sawa. Kwa maana nyingine, wewe kama masiriamali unatakiwa kujenga mahusiano na watu wa aina mbalimbali ilimradi mnasaidiana kwa usawa mnaoridhika nao. 

Wakati sasa umefika kwako wewe mtanzania hasa kijana ambaye umeamua kujikita kwenye ujasiriamali kubadilika na kuanza kuishi maisha halisi ya kijasiriamali na kuachana na mfumo yote ya waajiriwa ambayo haiendani na biashara yako unayoifanya. 

Ewe mjasiriamali, unatakiwa kuanzia leo uache kufanya biashara kwa kukiendekeza mfumo wa maisha ya waajiriwa badala yake JIFUNZE kwanza undani wa mfumo wa maisha ya wajasiriamali na baadae maisha yako yafuate mfumo huo. 

Ili kujifunza mfumo wa maisha ya wajasiriamali waliofanikwa bonyeza neno KUJIFUNZAkisha weka barua pepe yako. Kuanzia hapo, utakuwa ukipata makala nzuri za ujasiriamali na mafanikio kila zikitolewa. Pia, itakuwia rahisi wewe kupata vitabu vizuri bure kulingana na utakavyoomba.

Kwa mawasiliano zaidi:
WhatsApp: +255 788 855 409

 

 

Fahamu Mambo Sita Kuelekea Kwenye Mabadiliko Chanya


Njia nzuri na ya pekee ya kuweza kusaidia maskini ni kutokuwa mmoja wapo 
  1.   Acha kuamini yale uliyodhania ni kweli: Bahati mbaya, kuna mambo mengi ambayo huwa tunayakukubali na kuamini kadiri tunavyozidi kukua ambayo yanaweza kudhoofisha matumaini na matarajio ya mafanikio, furaha, na kutimiza ndoto za maisha yetu ya baadae. Mojawapo ya vitu ya vitu vinavyokuzuia wewe binafsi kuchukua hatua fulani fulani katika maisha, ni pamoja na dhana iliyozama ndani ya fikra ambayo ni “mimi siyo mzuri kiasi cha kutosha katika hili”. Imani hii ni ya msingi na ni ya kwanza ambayo huwa inasababisha watu wengi, kujisikia kuwa hawawezi na pia kujiona wenye mapungufu kila mara, hasa pale wanapokabiliwa na changamoto za kimaisha.
    Ni kwa muda mrefu sasa, tumekuwa na tabia ya kujiona kuwa watu wengine ni bora zaidi kuliko sisi, eti kwasababu sasa hivi, wanafanya vizuri kuliko sisi. Tunajihisi kwamba wao lazima watakuwa na thamani kubwa kuliko sisi na kwahiyo, lazima sisi tutakuwa na thamani ndogo kuliko wao.

    Hali hii ya kujiona kuwa kila wakati sisi tuna thamani ndogo ina kwenda ndani zaidi kwenye mzizi wa ubongo au akiri zetu na kusababisha sisi kutojithamini na kujipambanua kama watu wa chini wasiokuwa na mvuto wowote mbele ya jamii inayotuzunguka. Matokeo yake, tunaanza kujihisi ulofa na kujiona wahitaji wakubwa wa misaada mingi ya kijamii.

    Kutokana na kujiona kuwa sisi ni watu wa hali ya chini, basi mara nyingi tumekuwa watu wa kuridhika na vitu vidogo sana kuliko vile ambavyo tuna uwezo wa kuvipata. Mwisho wa yote hatuna hata picha ya maisha mazuri na ndiyo maana hata huwa hatuweki malengo na wala kuwa na ndoto za kufanya na kumilik vitu vikubwa.

    Kitu cha msingi amabcho ni muhimu sana wewe kukielewa ni kwamba, ili kuendelea unahitaji kujenga imani mpya ya kwamba, wewe una uwezo na kipaji kikubwa sana na pia una uwezo wa kufanya vitu vikubwa katika kila nyanja ya maisha ambayo ni muhimu kwako.

    Tambua kuwa wewe unao uwezo ambao hauna kikomo na unaweza kufanyia kazi na kupata kila kitu ambacho hujawahi kuwa nacho leo hii. Kama mmoja wa waandishi wa vitabu “Shakespeare” aliwahi kusema kuwa “upepo mkali na mingurumo ya radi ni utangulizi wa mvua kubwa inayokuja kunyesha baadae”. Akimaanisha kwamba chochote ulichowahi kufanya au kukamilisha siku zilizopita ni kiashiria au fununu za kitu unachoweza kufanya mbeleni na siku za baadae. 

    2.      Jisemee maneno chanya moyoni: Mojawapo ya maneno yenye nguvu katika msamiati wako ni yale ambayo huwa unajisemea kimoyomoyo na kuyaamini. Kujiongelea mwenyewe, au majadiliano ya ndani kwa ndani ya akiri (ubongo), ndiyo uchangia asilimia 95% ya hisia ambazo mtu huwanazo kila siku.

    Ukizungumza na nafsi yako, sehemu ya ubongo inayotunza kumbukumbu inayakubali maneno haya kama amri au komandi. Baadae inarekebisha tabia yako, picha yako binafsi, na lugha yako ya mwili ili iweze kuendana na mfumo na utaratibu wako kwenye maneno hayo unayojiongelea mwenyewe kila siku.

    Kama unataka mabadiriko katika maisha, hakikisha kuanzia sasa na kuendelea, unajisemea maneno kwa kufuata mtazamo wa jinsi unavyotaka uwe, pamoja na vitu unavyotaka kufanya. Kataa kusema chochote kile kuhusu wewe ambacho kwa dhati haukipedi. 

    Maneno chanya ambayo unatakiwa kujiambia mara kwa mara ni kama vile, “Ninaweza kufanya!” tena na tena. Kabla ya kufanya kitu chako chochote cha muhimu, rudia kwa kujisemea maneno ya “ninaweza kujipenda mwenyewe!” Sema mimi ni bora! Mimi ni bora! Mimi ni bora!” tena na tena kama unavyomaanisha. Alafu simama wima na imara, weka tabasamu la kujiamini kwenye uso wako na kufanya kile kilicho bora ambacho unaweza kukifanya. Na muda si mrefu itakuwa tabia yako. 

    3.      Jua kuwa unastahili kila kilicho bora: Kutokana na tabia ya watu kupenda kukosoa wenzao, hali hii imesababisha watu wengi kujenga tabia mbaya ya “kujikana wenyewe na kujiona hawawezi”.  Ni kwamba, hawaamini kwa dhati kuwa wanastahili na ni haki yao kuwa na mafanikio. Tabia ya kujikana sisi wenyewe, imesababishwa pia na maneno tuliyoambiwa na wakubwa zetu tangu utotoni, kwamba kuwa maskini ni jambo la kawaida LAKINI kuwa tajiri ni dhambi.

    Kama umekua ukiwa na mawazo na hisia za kujiona hustahili vitu vizuri, kwa sababu yoyote hile na ukaweza kupata mafanikio katika eneo lako la kimaisha, basi unaweza kupatwa na kitu kinachoitwa “tabia ya kujidanganya”.

    Utajisikia kwamba wewe ni kinara/mahili katika mafanikio yako, na kwamba baadae jamii inayokuzunguka itakuja kupata ukweli halisi. Haijalishi kiwango chako cha mafanikio kutokana na kufanya kazi kwa bidii, lazima utakuwa na ile hali ya kuogopa, ambapo kila wakati utakuwa unawazia kuwa utajiri wako utachukuliwa na watu wengine.

    Kama ukijisikia kuwa kama mtu wa kujipa sifa bandia, kila wakati utajisikia vibaya kwa wewe kupata mafanikio makubwa kuliko wengine. Ili kuepuka hisia za kujisikia vibaya, watu wengi ujiingiza kwenye kujidhoofisha wenyewe. Mathalani, watu wa namna hii wanakula sana, wanakunywa pombe sana, wanaterekeza familia zao, wanajihusisha na tabia ambazo hazitabiriki, na mara nyingi uweza kupoteza pesa zao kwenye maisha ya anasa, ufujaji na uwekezaji usiokuwa makini. Huwa wanajisikia kwa ndani kuwa hawastahili kuwa na mafanikio waliyonayo. Matokeo yake, ujikuta wakipoteza utajiri mkubwa waliokwisha upata. 

    4.      Jielekeze katika  kusaidia watu wengine: Ukweli ni kwamba wewe unastahili kila kitu ambacho unakipata kwa haki kwa kufanya kazi nzuri sana na kuzalisha au kusambaza bidhaa/huduma, ambazo zinachangia katika kuboresha kazi na maisha ya watu wengine. Katika jamii iliyo katika mfumo wa uchumi wa soko (market economy), kama hii ya kwetu, mihamara (transactions) yote  ya pesa kati ya mtu na mtu ni kwa hiari.

    Watu ununua kitu fulani, kama tu wanajisikia kuwa mahitaji yao au maisha yao yataboreka baada ya kununua na kutumia kitu chako. Kwahiyo, unaweza kufanikiwa sana, kwa kutoa tu! vitu wanavyovitaka watu, ili kuboresha maisha yao na kazi zao. Kadili utakavyosaidia vizuri watu wengi, ndivyo utakavyozidi kustahili kuingiza kipato kikubwa sana.

    Watu wanaofanya vizuri kwenye jamii zetu ukiacha wale wachache, ni wale ambao wanatoa huduma au kusaidia wengine vizuri zaidi kuliko mtu mwingine au kitu chochote. Nguvu yako yote, lazima uielekeze kwenye kusaidia watu wengine vizuri. Alafu, utastahili kila shilingi utakayoipata.

    Raisi wa zamani wa Marekani Abraham Lincoln aliwahi kusema kuwa “njia nzuri na ya pekee ya kuweza kusaidia maskini ni kutokuwa mmoja wapo”. Katika jamii yetu, kadili unavyozidi kufanikiwa kifedha, ndivyo unavyozidi kutozwa kodi sana. Kodi hizi ndizo husaidia kulipia karo, matibabu, barabara, ulinzi na usalama, na vitu vingine muhimu ambavyo jamii yetu inazalisha.

    Unaweza kujivunia kuwa umefanikiwa kupata uhuru wa kipato. Kwa kuweza kupata pesa nyingi, unatoa mchango mkubwa kwa watu wengi. Kwa maana nyingine ni kwamba unafanya vizuri kwaajiri yako kwa kufanya vizuri kwa watu wengine. Basi kama unalitimiza hili, ni vizuri zaidi kurudia neno “Ninastahili kila shilingi ninayoipata kutokana na kutoa mchango wangu kwa watu wengine kwa kuwapa bidhaa na huduma wanazohitaji kuboresha maisha yao”. Ninajivunia mafanikio yangu.” 

    5.      Jiamini wewe ni mtu wa hali ya juu na wa pekee: Ili kujijengea tabia ya kujiamini, ni vizuri ukatambua haya kuwa wewe ni mtu makini na mzuri. Wewe ni mkweli, wewe ni mtu nadhifu na mchapa kazi. unajali watu wengine kwa heshima na uchangamfu. Wewe umejitoa na unapenda familia yako, marafiki, na kampuni yako.Wewe ni imara, unajiamini, na mwajibikaji. Wewe ni mwelewa sana, intelligent, na mwenye uzoefu.Wewe ni muhimu siyo tu kwa watu wa karibu bali na kwa wanajamii wengine. Ulizaliwa kwasababu maalumu, na unataka kutimiza  ndoto kubwa. Wewe ni mtu mzuri katika kila hali. 

    Kauli zote hapo juu ni tamko linalodhihirisha upekee wa mtu na maisha yake. Yawezekana isiwe hivyo kwako kwa asilimia 100, lakini ni maelezo mazuri juu ya wewe ulivyo ndani yako na huko unakokwenda kwenye maisha yako. Unapokuwa umekubali kwa hiari kuwa wewe kiukweli ni wa thamani na mtu mwenye kustahili, utaonyesha katika kila kitu unachosema na kutenda.

    Kadili muda unavyokwenda, itafikia kipindi itakuwa kweli kwako wewe na uhalisia wako utakuwa ukweli. Rudia kila mara kwa kujitamkia maneno haya, “ninajipenda mwenyewe na ninapenda maisha yangu”. “Mimi ni wa pekee na mtu mzuri katika kila hali na kila mara ninafanya vizuri kwa kila kitu ninachojaribu kufanya. 

    6.      Tembelea duka la programu za akiri: Fikiria kuwa kama kungekuwa na duka ambalo linauza programu za akiri; ungeweza kununua kila imani, fikra yoyote unayoitaka na kuiweka kwenye akiri yako, na ndo aina ya mtu ambaye ungefanana naye kuanzia hapo. Kama duka hilo lingepatikana, ambalo wewe ungeweza kununua aina yoyote ya kifurushi cha imani, fikra na tabia, wewe ungechagua kipi?: LAKINI ili duka liko wapi? Ili kuweza kuliona duka hili zingatia pendekezo hili ~ Jiangalie jinsi ulivyo na utafute ni kitu gani watu wenye furaha na mafanikio makubwa wanacho kama imani ya ndani kabisa, halafu jipatie kifurushi cha imani na tabia kama za watu waliofanikiwa kwaajili yako mwenyewe. Kisha ingiza kifurushi hicho kwenye ubongo wako.

    Imani ya ndani na ya msingi ambayo unaweza kuiga wewe binafsi ni hii “Mimi ni mtu mzuri jumla na nitakuja kuwa mwenye mafanikio makubwa katika maisha na kila kitu kinachotokea kwangu, kiwe kizuri au kibaya ni sehemu tu ya mchakato. Mchakato wa kupata mafanikio makubwa na furaha ni lazima kwangu mimi.”
Kama kwa dhati kabisa unaamini hilo, basi tayari umejihakikishia kuwa na furaha na mafanikio. Kwa maana hiyo kila changamoto unazokutana nazo, huwa zinakujia, ili kukufundisha somo muhimu ulilohitajika kulijua, ili kufanikisha malengo yako. Kwahiyo, ukilitambua hili, unakuwa mtu chanya na mwenye matumaini makubwa muda wote. Rai yangu kwako mtanzania mwenzetu, jifunze jinsi ya kujiprogram, ili dunia yako ya ndani ifanane na mtu unayetaka uwe au maisha unayotaka kuwa nayo, hakika utafanikiwa sana.

Iwapo unapenda kupata makala nzuri za mafunzo kila zinapotoka bonyeza KUJIUNGA .

Kwa maelezo zaidi wasiliana nami kwa namba:
WhatsApp: +255 788 855 409



Mafanikio Yako Yamejificha Ndani ya Thamani
  • Kadiri utakavyozidi kutengeneza thamani nyingi kwaajiri ya watu wengine, ndivyo utakavyozidi kupata pesa nyingi.

  • Kwa mtu ambaye ni mjasiriamali mahili, kitu thamani ni bora kuliko pesa!
Siku watu wengi wakigundua kuwa thamani ndiyo pesa yenyewe wataanza kuthamini sana “thamani” kuliko “pesa”; na ndipo kila mmoja atawekeza juhudi na maarifa katika kusaka thamani kwaajiri ya jamii, kuliko hivi sasa ambapo watu wengi wanakesha wakitafuta pesa. Iwapo, watu watajihusisha zaidi na kusaka thamani badala ya pesa, ni wazi kwamba dunia itajaa bidhaa na huduma bora zenye kukidhi mahitaji yote ya binadamu (maisha bora), na dunia itakuwa ni mahali pazuri pa kuishi. 

Je uliwahi kujiuliza hiki kitu kinachoitwa thamani ni nini hasa? Au na wewe unaendelea kukutana nalo kwenye maandishi au mazungumzo basi! Maana ni kawaida kusikia watu wengi wakiongea juu ya suala zima la kuongeza thamani. Unapowauliza watu juu ya maana yake, jibu la haraka haraka unaambiwa kwa kingereza, yaani “Value” ukiuliza tena maana ya “value” anaambiwa ni “thamani” mwisho inakuwa kama ule mchezo wa kuku na yai ni kipi kilitangulia!.

Mara nyingi, neno “thamani” linapewa tafsiri na maana ya juu juu, kiasi cha kuwafanya watu kushindwa kupata picha halisi juu ya umuhimu, ukubwa na upekee wa “thamani” katika maisha. Kutokana na tafsiri ya juu juu sana, thamani kama kitu halisi, imekuwa haithaminiwi kama ilivyo pesa.  Sababu mojawapo za kutothamini thamani ni kutokana na ukweli kwamba, thamani ni kitu ambacho hakionekani kwa macho na hakishikiki mkononi, hali ambayo huwafanya watu wengi kushindwa kutambua kuwa, pesa zote halali walizonazo zinatokana na thamani. Kwa maneno mengine “thamani ndiyo kila kitu” ambacho binadamu utumia kumaliza kero na changamoto mbalimbali za kimaisha”. 

Thamani ni kile kiwango cha umuhimu uliomo ndani ya bidhaa au huduma. Pia thamani ni ubora ambao huifanya bidhaa/huduma fulani kupendeka au kuhitajika. Kwa maneno mengine, thamani ni ule uhitaji, umuhimu, faida, urahisi ambao mara nyingi huwekwa kwenye bidhaa au huduma fulani fulani. Thamani ndani ya bidhaa au huduma ndiyo hasa huwafanya watu kutoa pesa yao waliyoitolea jasho kwa hiari, kwa lengo la kujipatia thamani ili kukidhi mahitaji. Kwahiyo, thamani ni matokeo ya kile akipatacho mtu baada ya kuwa ametumia bidhaa au huduma yako.


Kwa mtu ambaye ni mjasiriamali mahili, kitu thamani ni bora kuliko pesa, kwasababu kiasi cha pesa ambacho mtu ukipata, lazima kilinganishwe na thamani iliyoko ndani ya bidhaa au huduma. Watu wengi waliofanikiwa wanaangalia zaidi thamani ya vitu walivyotengeneza, tofauti na kwetu hapa ambapo wengi wanaangalia pesa tu!. Mwazoni kabla ya kutengeneza bidhaa, thamani yake inakuwa bado iko kichwani mwa mjasiriamali. Kinachotakiwa ni wewe kuitoa ndani yako na kuiweka katika hali ile ambayo unaweza kuwapa au kuwasaidia watu wengine ili watimize matakwa na haja zao. 

Kadiri utakavyozidi kutengeneza thamani kubwa kwaajiri ya watu wengine, ndivyo utakavyozidi kupata pesa nyingi. Na ukiona unapata pesa kidogo usianze kutafuta mchawi, bali jiulize maswali ya kwamba wewe umetoa thamani ya kiwango gani kwa watu wengine? Kwahiyo, wewe jikite katika kutoa thamani ya kiwango kikubwa kwa watu wengine. Thamani unayotengeneza na kuwapa watu wengine inawasaidia kukidhi mahitaji yao mbalimbali. Kwa mjasiriamali yeyote, ni muhimu kutambua kuwa kila unapofirkiria kutengeneza thamani yoyote ile, hakikisha hisiwe ni kwaajiri yako peke yako, bali iwe ni kwaajiri ya watu wengine. Endapo utatengeneza thamani inayokulenga wewe peke yako, basi ujue kuwa, hakuna atakayekuletea pesa yake, kwasababu thamani uliyonayo haimfai chochote mtu mwingine. 

Watu wengi wanaendelea kuishi maisha duni, kwasababu wanatumia muda wao mwingi kutengeneza thamani kwaajiri yao peke yao, na wala si kwa watu wengine. Kumbuka kuwa watu mpaka watume pesa kwako ni lazima kuwe na thamani fulani kwako. Ukweli ni kwamba, pesa aliyonayo mtu, mara nyingi ameitolea jasho kuipata, lakini mtu huyo yuko tayari kuiachia kwa hiari, iwapo kitu anachokitaka kutoka kwako kina thamani kubwa kuliko kiasi cha pesa unachomtaka atoe. Kwahiyo, tukitaka kutengeneza pesa kwa urahisi, ni lazima tujikite katika kutengeneza thamani kwa wengine. Na endapo utakuwa umechangia thamani yoyote kwa maisha ya watu wengine, na thamani hiyo ikawa na faida kubwa kwao, basi wewe tunastahili malipo. 

Binadamu siku zote huwa anatafuta thamani kwaajiri ya kukidhi mahitaji yake ya kimaisha. Kwahiyo, kwa yeyote yule atakayeweza kutengeneza thamani, ni wazi kwamba kila mara pesa itakuwa inamfuata alipo. Watu mara zote wananunua thamani kupitia bidhaa au huduma mbalimbali. Wewe kama mjasiriamali, ni muhimu ukatambua kuwa, watu wanaponunua bidhaa, kinachonunuliwa siyo bidhaa kama bidhaa bali ni thamani yake. Thamani ya kitu, ndiyo huwasukuma watu wengine kutuma pesa zao kwako wewe uliye na thamani fulani. Wajasiriamali tunatakiwa kutambua kuanzia mwanzo wa utengenezaji bidhaa kuwa, thamani iliyoko ndani ya bidhaa ndiyo wateja wanatafuta. Kwa mfano; unapoona mteja amekuja kwenye salooni yako usifikiri amekuja kusuka, kuseti au kunyoa nywele bali anacholenga ni kupendeza na kupendeza ndiyo thamani halisi ya kusuka au kunyoa nywele. 

Katika zama hizi tulizomo na huko mbele tuendako, maisha mazuri pamoja na ukuaji wa uchumi vitategemea sana uwezo na ujasiri wa watu katika kuhamisha thamani zote zilizoko ndani yao na kuziweka ndani ya bidhaa na huduma mbalimbali. Katika uwekaji wa thamani kwenye bidhaa, tulenge zaidi zile thamani ambazo zinatatua kero sugu kwenye jamii. Endapo thamani zilizotengenezwa zitatoa suluhisho la changamoto kwa watu waliowengi, moja kwa moja watu watakuwa tayari kutoa pesa yao kwa hiari kwenda kwa yule aliyetengeneza thamani.  Jambo la msingi hapa ni watu kuendelea kuelekeza nguvu na maarifa yao, katika kutengeneza na kuzalisha thamani nyingi kadiri inavyowezekana, kwani kwa kufanya hivyo, uchumi wa kaya na taifa kwa ujumla utakuwa sana na Tanzania itaendelea kuwa mahali pazuri pa kuishi.

BILA "MABORESHO" IMANI YAKO INAWEZA KUKUANGUSHA!
  •  Kila binadamu anapendelea kufanya kitu kadiri anvyotumwa na imani yake
  • Imani Mbaya = Matokeo Mabaya
Uzoefu katika maisha ya binadamu umeonyesha kuwa kile unachoamini zaidi ndicho ukuletea mafanikio uliyonayo. Siku za nyuma kidogo nilichukua likizo yangu ya mwaka, wakati nikiwa likizo nilibahatika kwenda Entebbe Uganda, nikiwa huko nilitembelea hoteli ya Imperial Botanical Beach, lengo langu lilikuwa ni kuamsha upya mwili na fikra zangu ndiyo maana niliweka jitihada za kuuzuria mafunzo ya jinsi ya kujenga na kutunza afya ya mwili. Hakika nilipata nilipata somo la thamani kubwa kwa maisha yangu yote.

Kila binadamu anapendelea kufanya kitu kadiri anvyotumwa na imani yake: Siku ya kwanza nilipokutana na mtaalamu wa mazoezi ya viungo na afya, aliniuliza kuhusu tabia na utaratibu wangu kwa ujumla juu ya ulaji wangu wa chakula kwa siku. Nilimwambia kuwa, mara nyingi huwa ninakula milo miwili kwa siku; yaani kifungua kinywa na au chakula cha mchana na usiku. Wakati nikimueleza hayo nilifanya hivyo huku nikiangalia saa yangu ya mkononi, ndipo nikashitukia ni saa kumi na mbili jioni na baadae kugundua kuwa sijala chochote kwa siku nzima. LAKINI bado nilijisemea kimoyomoyo “Kwangu mimi kula siyo kipaumbele ”.

Baada ya mtaalamu kusikia kuwa huwa na kula mara mbili kwa siku aliniangalia na kuonyesha kusikitika kidogo, lakini aliendelea kusema, “Unatakiwa kula milo mitatu kwa siku.”
Kusikia hivyo nilimjibu kwamba, habari hiyo ya milo mitatu kwa siku nilikwishaiskia kabla. Lakini pamoja na kusikia habali hiyo, mimi imani yangu ni kwamba, iwapo nitakula milo mitatu kila siku, unene wangu utaongezeka sana. 

Mtaalamu wangu alicheka, na akazidi kusisitiza kuwa ninatakiwa kula zaidi wakati wa mchana kwasababu mwili unakuwa unafanya kazi sana. Kwahiyo, miili yetu uhitaji chakula cha kutosha nyakati za asubuhi, na mapema kabla ya saa za mchana (adhuhuri), na pia tunahitaji chakula kidogo nyakati za usiku, kwani muda wa usiku mwili unakuwa na kazi kidogo sana kwa maana nyingine unakuwa umepumzika.
Niliambiwa kwamba kwa mtu ambaye bado yuko vizuri kiafya, asipokula chakula cha kutosha ni kwamba badala ya mwili kuunguza mafuta, mwili utaunguza misuli na ikitokea hali hii basi ujue hutakaa huwe na kiwango cha uimara wa mwili unaoutaka.

Mimi nilikuwa ninaendelea kupigana na imani yangu iliyozidikuniambia kuwa, milo mitatu kwa siku itaongeza kilo moja ya uzito. Lakini kwakuwa nilienda kwa mtaalamu kwaajiri ya afya yangu, nilijifikiria na kuamua kufuata ushauri niliopewa na mtaalamu.
Wasikilize wataalamu: Kwa muda wa siku sita, nilianza kufanyia kazi imani mpya na kuanzia siku ya kwanza nikaanza kupata milo mitatu kwa siku. Niliamua kufuata masharti kama nilivyoelekezwa na mtaalamu kwa kuanza kula milo mitatu kwa siku. Kitu kimoja kilichojitokeza ni kwamba nguvu ya mwili iliimarika zaidi. Kuanzia nyakati za asubuhi, nilijisikia mwenye nguvu ya kutosha siku nzima. Niliendelea na mpango huu mpaka mwisho wa siku ya sita, siyo tu kwamba sikuongezeka uzito, bali badala yake nilipugua kilo kadhaa.
Kitendo cha kuamua kuachana na imani yangu juu ya idadi ya milo kwa siku, na kuamua kumsikiliza mtaalamu, kilinisaidia sana kufikia malengo yangu ambayo nisingeyatimiza hata siku moja kama ningeendelea kufanya yale niliyoamini miaka yote.

Imani mbaya = matokeo mabaya: Hoja muhimu juu ya stori hii ni kwamba, nilikuwa na imani potofu ambayo ilijengeka siku nyingi na imani hii kimsingi ilinizuia kusonga mbele na hatimaye kushindwa kutimiza malengo yangu ya kiafya. Pamoja na kwamba nimesikia tangu nikiwa mdogo, kwamba mtu mzima anatakiwa kupata milo mitatu kwa siku, sikuwahi kuamini kama faida zitokanazo na kula milo mitatu kwa siku zilikuwa za kweli. Nilikuwa na taarifa, lakini, faida hizi sikuzipata mpaka pale nilipoamua kufunguka na kuamua kujaribu yale niliyoelekezwa na mtaalamu —ndipo nilipopata uzoefu na elimu ya kweli juu ya kile kilichoonekana kufanya vizuri kwangu.

Kwa vyovyote vile, ukweli huu ni rahisi na unaweza kutumika kwenye hali yoyote katika maisha. Sasa swali kwako, “ni imani zipi zinazokurudisha nyuma kiasi cha kushindwa kufikia mafanikio ya kipesa au ndoto zako? Na utafanya nini kuondoa imani hizo?

Iwapo utapenda kujifunza jinsi ya kutambua na kuondokana na imani ambazo siku zote zimekurudisha nyuma pale ulipojaribu kutafuta uhuru wa kipato na mafanikio kimaisha, bonyeza; http://eepurl.com/bkXr3r kuweka barua pepe yako, ili kujiunga na programu ya mafunzo juu ya mafanikio ya kifedha.

Mafunzo haya yatatolewa bure kupitia barua pepe utakayosajiri hapa: http://eepurl.com/bkXr3r

Mafunzo yataanza tarehe 15/Septemba/2015 hadi 30/Septemba/2015.  Kwa kujiunga na mafunzo haya utapata thamani kubwa sana, ikiwa ni pamoja na kubadili mitazamo hasi uliyonayo juu ya kupata pesa. Pia utapata kujua mbinu na njia za uhakika utakazozitumia kufikia maisha ya ndoto yako kwa uhakika na kwa muda mfupi zaidi. Kama unafikiri program yetu haikufai huko sahihi; LAKINI bado ninakushauri ujitahidi kutafuta mtu, ambaye atakufundisha na kukupa mwongozo wa jinsi ya kufikia uhuru wa kipato. 

Kwa maelezo zaidi juu ya prograu hii ya mafunzo whatsApp: +255 788 855 49 au E-mail: mchumieconomist2009@gmail.com.
KARIBU TWENDE KAZI PAMOJA

MAFANIKIO YAKO YAMEJIFICHA NDANI YA "THAMANI"
  • Kadiri utakavyozidi kutengeneza thamani nyingi kwaajiri ya watu wengine, ndivyo utakavyozidi kupata pesa nyingi.
  • Kwa mtu ambaye ni mjasiriamali mahili, kitu thamani ni bora kuliko pesa!
Siku watu wengi wakigundua kuwa thamani ndiyo pesa yenyewe wataanza kuthamini sana “thamani” kuliko “pesa”; na ndipo kila mmoja atawekeza juhudi na maarifa katika kusaka thamani kwaajiri ya jamii, kuliko hivi sasa ambapo watu wengi wanakesha wakitafuta pesa. Iwapo, watu watajihusisha zaidi na kusaka thamani badala ya pesa, ni wazi kwamba dunia itajaa bidhaa na huduma bora zenye kukidhi mahitaji yote ya binadamu (maisha bora), na dunia itakuwa ni mahali pazuri pa kuishi. 

Je uliwahi kujiuliza hiki kitu kinachoitwa thamani ni nini hasa? Au na wewe unaendelea kukutana nalo kwenye maandishi au mazungumzo basi! Maana ni kawaida kusikia watu wengi wakiongea juu ya suala zima la kuongeza thamani. Unapowauliza watu juu ya maana yake, jibu la haraka haraka unaambiwa kwa kingereza, yaani “Value” ukiuliza tena maana ya “value” anaambiwa ni “thamani” mwisho inakuwa kama ule mchezo wa kuku na yai ni kipi kilitangulia!.

Mara nyingi, neno “thamani” linapewa tafsiri na maana ya juu juu, kiasi cha kuwafanya watu kushindwa kupata picha halisi juu ya umuhimu, ukubwa na upekee wa “thamani” katika maisha. Kutokana na tafsiri ya juu juu sana, thamani kama kitu halisi, imekuwa haithaminiwi kama ilivyo pesa.  Sababu mojawapo za kutothamini thamani ni kutokana na ukweli kwamba, thamani ni kitu ambacho hakionekani kwa macho na hakishikiki mkononi, hali ambayo huwafanya watu wengi kushindwa kutambua kuwa, pesa zote halali walizonazo zinatokana na thamani. Kwa maneno mengine “thamani ndiyo kila kitu” ambacho binadamu utumia kumaliza kero na changamoto mbalimbali za kimaisha”. 

Thamani ni kile kiwango cha umuhimu uliomo ndani ya bidhaa au huduma. Pia thamani ni ubora ambao huifanya bidhaa/huduma fulani kupendeka au kuhitajika. Kwa maneno mengine, thamani ni ule uhitaji, umuhimu, faida, urahisi ambao mara nyingi huwekwa kwenye bidhaa au huduma fulani fulani. Thamani ndani ya bidhaa au huduma ndiyo hasa huwafanya watu kutoa pesa yao waliyoitolea jasho kwa hiari, kwa lengo la kujipatia thamani ili kukidhi mahitaji. Kwahiyo, thamani ni matokeo ya kile akipatacho mtu baada ya kuwa ametumia bidhaa au huduma yako.


Kwa mtu ambaye ni mjasiriamali mahili, kitu thamani ni bora kuliko pesa, kwasababu kiasi cha pesa ambacho mtu ukipata, lazima kilinganishwe na thamani iliyoko ndani ya bidhaa au huduma. Watu wengi waliofanikiwa wanaangalia zaidi thamani ya vitu walivyotengeneza, tofauti na kwetu hapa ambapo wengi wanaangalia pesa tu!. Mwazoni kabla ya kutengeneza bidhaa, thamani yake inakuwa bado iko kichwani mwa mjasiriamali. Kinachotakiwa ni wewe kuitoa ndani yako na kuiweka katika hali ile ambayo unaweza kuwapa au kuwasaidia watu wengine ili watimize matakwa na haja zao. 

Kadiri utakavyozidi kutengeneza thamani kubwa kwaajiri ya watu wengine, ndivyo utakavyozidi kupata pesa nyingi. Na ukiona unapata pesa kidogo usianze kutafuta mchawi, bali jiulize maswali ya kwamba wewe umetoa thamani ya kiwango gani kwa watu wengine? Kwahiyo, wewe jikite katika kutoa thamani ya kiwango kikubwa kwa watu wengine. Thamani unayotengeneza na kuwapa watu wengine inawasaidia kukidhi mahitaji yao mbalimbali. Kwa mjasiriamali yeyote, ni muhimu kutambua kuwa kila unapofirkiria kutengeneza thamani yoyote ile, hakikisha hisiwe ni kwaajiri yako peke yako, bali iwe ni kwaajiri ya watu wengine. Endapo utatengeneza thamani inayokulenga wewe peke yako, basi ujue kuwa, hakuna atakayekuletea pesa yake, kwasababu thamani uliyonayo haimfai chochote mtu mwingine. 

Watu wengi wanaendelea kuishi maisha duni, kwasababu wanatumia muda wao mwingi kutengeneza thamani kwaajiri yao peke yao, na wala si kwa watu wengine. Kumbuka kuwa watu mpaka watume pesa kwako ni lazima kuwe na thamani fulani kwako. Ukweli ni kwamba, pesa aliyonayo mtu, mara nyingi ameitolea jasho kuipata, lakini mtu huyo yuko tayari kuiachia kwa hiari, iwapo kitu anachokitaka kutoka kwako kina thamani kubwa kuliko kiasi cha pesa unachomtaka atoe. Kwahiyo, tukitaka kutengeneza pesa kwa urahisi, ni lazima tujikite katika kutengeneza thamani kwa wengine. Na endapo utakuwa umechangia thamani yoyote kwa maisha ya watu wengine, na thamani hiyo ikawa na faida kubwa kwao, basi wewe tunastahili malipo. 

Binadamu siku zote huwa anatafuta thamani kwaajiri ya kukidhi mahitaji yake ya kimaisha. Kwahiyo, kwa yeyote yule atakayeweza kutengeneza thamani, ni wazi kwamba kila mara pesa itakuwa inamfuata alipo. Watu mara zote wananunua thamani kupitia bidhaa au huduma mbalimbali. Wewe kama mjasiriamali, ni muhimu ukatambua kuwa, watu wanaponunua bidhaa, kinachonunuliwa siyo bidhaa kama bidhaa bali ni thamani yake. Thamani ya kitu, ndiyo huwasukuma watu wengine kutuma pesa zao kwako wewe uliye na thamani fulani. Wajasiriamali tunatakiwa kutambua kuanzia mwanzo wa utengenezaji bidhaa kuwa, thamani iliyoko ndani ya bidhaa ndiyo wateja wanatafuta. Kwa mfano; unapoona mteja amekuja kwenye salooni yako usifikiri amekuja kusuka, kuseti au kunyoa nywele bali anacholenga ni kupendeza na kupendeza ndiyo thamani halisi ya kusuka au kunyoa nywele. 

Katika zama hizi tulizomo na huko mbele tuendako, maisha mazuri pamoja na ukuaji wa uchumi vitategemea sana uwezo na ujasiri wa watu katika kuhamisha thamani zote zilizoko ndani yao na kuziweka ndani ya bidhaa na huduma mbalimbali. Katika uwekaji wa thamani kwenye bidhaa, tulenge zaidi zile thamani ambazo zinatatua kero sugu kwenye jamii. Endapo thamani zilizotengenezwa zitatoa suluhisho la changamoto kwa watu waliowengi, moja kwa moja watu watakuwa tayari kutoa pesa yao kwa hiari kwenda kwa yule aliyetengeneza thamani.  Jambo la msingi hapa ni watu kuendelea kuelekeza nguvu na maarifa yao, katika kutengeneza na kuzalisha thamani nyingi kadiri inavyowezekana, kwani kwa kufanya hivyo, uchumi wa kaya na taifa kwa ujumla utakuwa sana na Tanzania itaendelea kuwa mahali pazuri pa kuishi.


KAMA UKO HIVI SI "MJASIRIAMALI"
  • Mjasiriamali Ujikita Katika Kuzalisha Bidhaa/Huduma kwa Lengo la Kugusa Maisha ya Watu Wengine
  • Uongozi ni Ujuzi Muhimu Sana Unaotakiwa kwa Mtu Anayetaka Kuwa Mjasiriamali

Nafahamu kuwa kuna watu wengi wanatamani kuwa wajasiriamali na wengine hasa waliojiajiri wanadhani na kuamini kuwa, wao ni wajasiriamali. Kuna dalili zinazoonyesha kuwa jambo hili la ujasiriamali linachukuliwa kimzaa mzaa sana. Imekuwa kitu cha kawaida sana hapa Tanzania, kusikia watu wengi wakijiita wajasiriamali, hasa wale wanaofanyakazi za kujiajiri wenyewe. Lakini je? kitendo cha wewe kujiajiri tu peke yake, kinatosha kukufanya huwe mjasiriamali?. Sasa huyu anayeitwa mjasiriamali ni mtu wa namna gani?  Mjasiriamali ni ujuzi na siyo mtu. Kazi unayofanya, timu ya watu uliyonayo, maisha unayoishi, ukubwa wa kazi yako, maamuzi unayofanya kila siku n.k. vyote hivi vina nafasi kubwa ya kukufanya wewe kuwa mjasiriamali au vinginevyo!.

Mjasiriamali ni mtu anaona fursa, anaweka timu ya watu pamoja na kujenga biashara ambayo uzalisha faida kutoka kwenye fursa husika”. Ni wazi kwamba wapo watu wengi ambao wameweza kuona fursa na kuamua kuzichangamkia kwa malengo ya kupata faida wao peke yao. Lakini, kama ukiona fursa na ukaona una uwezo wa kuifanyia kazi wewe peke yako, basi ujue wewe ni mfanyabiashara mdogo sana ambaye umejiajiri au umeajiliwa na biashara badala ya wewe kumiliki biashara”

Kuna tofauti sana kati mtu aliyejiajiri na mjasiriamali. Mtu aliyejiajiri, ni mtu ambaye anaweza kuzalisha 
bidhaa au kutoa huduma yeye mwenyewe peke yake. Kwa mfano msanii anaweza kuchora picha yeye mwenyewe, daktari anaweza kukutibu jino mwenyewe, au mtu anafuga mifugo yeye mwenyewe. Mjasiriamali, hawezi kufanya vyote vinavyotakiwa kufanyika katika kuendesha biashara peke yake. Mjasiriamali ni lazima awe tayari kupata na kuunganisha vipaji vya watu wenye uwezo na ujuzi tofauti tofauti, ambapo huwaunganisha ili wafanye kazi pamoja kwaajili ya kukamilisha uzalishaji wa bidhaa au huduma fulani. Kwa maana nyigine, mjasiriamali ujenga timu ambayo ujikita katika kuzalisha bidhaa/huduma, kazi ambayo mtu mmoja mmoja hawezi kuifanya yeye peke yake.
Mjasiriamali ni mtu ambaye anapoamua kufanya biashara mara nyingi anakuwa analenga kutatua changamoto au kero fulani kwenye jamii. Kwa maana nyingine “mjasiriamali ujikita katika kuzalisha bidhaa au huduma mbalimbali kwa lengo la kugusa maisha ya watu wengine  na siyo yeye peke yake”. Sababu kubwa ambayo huwafanya watu wengi kuendelea kuwa wadogo au kuwa na biashara ndogo ni kwasababu biashara wanazoziendesha ni kwaajiri ya kutatua matatizo yao peke yao. Ndiyo maana unakuta mtu anafanya biashara fulani miaka 20, lakini biashara haibadiliki, hiko vilevile na haijawahi kupanuka kwa miaka yote. Watu wa namna hii ndio wengi wamejiajiri na ndio hawa wanaodhani na kuamini kuwa na wao ni wajasiriamali.

Mjasiriamali ni mtu anayebeba majukumu ambayo yanahitaji timu ya watu. Mjasiriamali ambaye utegemea timu ya watu  kufikia malengo, huwa halipwi mpaka hapo timu yake ikishafanya kile kinachotakiwa kufanyika wa kama timu. Waajiriwa wengi, na wale waliojiajiri wanalipwa kulingana na kile ambacho wanaweza kufanya kama wao binafsi. Tofauti na waajiriwa/waliojiajiri, mjasiriamali amejijengea tabia ya kufanya kazi bila kulipwa, kutegemeana na unachofanya wakati mwingine unaweza kulazimika kukaa muda mrefu zaidi ya mwaka ndio unakuja kulipwa kama umefanikisha kile ulicho kilenga. 

Malipo ya mjasiriamali ni baada ya kukamilisha kazi na timu, wakati malipo ya waajiriwa wengi ni kabla ya kuanza kazi. Kama alivyo mkandarasi wa majengo, huwa anatumia watu kujenga nyumba; mfano: mafundi bomba, umeme, seremara na wataalam wengine kama wasanifu majengo, wahasibu n.k. na mjasiriamali utafuta watu tofauti tofauti kama vile, mafundi mchundo (technicians), wasomi, na wataalam wengine katika kumsaidia kujenga biashara”. Kwahiyo, ni muhimu tukatambua ndani ya fikra zetu kuwa,  mjasiriamali ni mtu ambaye ni kiongozi, japo wakati mwingine yawezekana wasifanye kazi na timu zao moja kwa moja. “Kadiri utakavyoongoza timu ya watu ambao ni wazuri wenye uelewa, haulazimiki kufanya kazi kama sehemu yao, ndiyo vizuri na ndiyo utafikia kiwango cha kuitwa mjasiriamali mkubwa.

Kuna watu wanamiliki makampuni mengi, lakini huwa hawafanyi kazi katika makampuni hayo. Ndiyo maana wanaweza kutegeneza pesa zaidi na kufanya vitu vingi bila kuwa wamefanya kazi. Ni kutokana na hali hii, tunakumbushwa kuwa, “Uongozi ni ujuzi muhimu sana unaotakiwa kwa mtu anayetaka kuwa mjasiriamali”.” Uongozi siyo zawadi ni ujuzi na wala hauzaliwi nao bali ni kitu ambacho ukiamua unajifunza. Ukitafakari kwa kina unagundua kuwa sisi wote tuna chembe chembe za ujuzi wa uongozi. Tatizo lililopo kwa watu waliowengi ni kwamba, watu wengi utumia maisha yao yote kukuza ujuzi katika taaluma nyingine tofauti na uongozi, ndiyo, maana kuna watu wengi ni waajiriwa na wengine wamejiajiri. Ni watu wachache sana, ambao wanatumia muda wa maisha yao kukuza ujuzi wao wa uongozi, kwasababu, uongozi  ndio ujuzi ambao unatakiwa kwa wajasiriamali (wamiliki wa biashara). Kwahiyo, ni vizuri watu tukaamua kuwa wajasiriamali na kujikita katika kusaka kila aina ya ujuzi utakaotuwezesha kuongoza timu zetu, hili hatimaye tuweze kumiliki biashara kubwa na mwisho kufikia maisha ya ndoto yetu.

WEWE NI MJASIRIAMALI LAKINI PUNGUZA HILI
“Watu wengi tunatumia kitu cha bure “usingizi” kujikosesha fursa hadimu”
“Masaa (muda) tunayotumia kufanya kazi ndiyo pesa yenyewe”
Kitu kinachoitwa “usingizi” ni kitu ambacho kipo siku zote na muda wote, na wakati huo huo ni kitu ambacho unatakiwa kuwa makini nacho hasa kama unataka mafanikio makubwa. Usingizi ni kitu ambacho huwezi ukakitumia kikaisha, kwahiyo, hata ukiukosa kwa muda fulani, bado utaukuta muda wowote ukiutaka. Usingizi” ni zawadi ambayo kila mwanadamu amepewa kiasi cha kutosha na ni kitu ambacho hakina ukomo. 

Habari njema ni kwamba, usingizi wa mtu hauwezi kuibiwa na wala mtu akilala usingizi wake, si rahisi kutumia usingizi wako. Kwa maana nyingine, tunasema kwamba usingizi ni hazina ya kwako peke yako. Usingizi haununuliwi kutoka kwa mtu mwingine, kwasababu kila mmoja ana wa kwake. Usingizi wote tulionao ni kitu ambacho tunakipata bure na itoshe kusema “Mungu aksante kwa zawadi hii ambayo tunapata bure kwa kipindi chote cha maisha yetu”.

Ajabu ni kwamba, “watu wengi tunatumia kitu cha bure “usingizi” kujikosesha fursa” hadimu ya kutafuta maisha ya ndoto yao. Tabia ya kuendekeza usingizi, imesababisha kupoteza muda mwingi, ambao tungeutumia katika uzalishaji na hatimaye kupata kipato. Mara nyingi watu ambao wanaendekeza usingizi na uvivu, ndio hao hao ambao kila kukicha wanalalamika maisha magumu na kibaya zaidi wanawatwisha mzigo wa lawama watu wengine, eti hawakuwajibika ipasavyo!.

Ikumbukwe kuwa, mwili wako usipotumia nguvu katika kazi zenye kuzalisha mali, bado nguvu uliyonayo itatumika kupiga soga, kuangalia runinga, kupiga umbea, kuangalia mpira, n.k. ukishakuwa umefanya vyote hivi, pale nguvu ikikuishia moja kwa moja mwili wako utajisikia kupumzika na hivyo kupata usingizi utakao kulazimu kulala. Hali hii inapojirudia rudia, inakujengea mazoea ya uvivu, jambo ambalo litakukosesha nguvu na uwezo wa kupambana na umaskini.

Mjasiriamali ukishaanza kushindwa kuutawala usingizi wako, basi ujue kuwa mambo mengi mazuri yataanza kukupita. Mfano: unakuta kuna watu wengi wanaofahamu kuwa, ili kulinda afya zao ni muhimu kuamka mapema na kufanya mazoezi, lakini mpaka sasa ni watu wachache wanaoweza kufanya mazoezi masaa yale ya alfajiri. Utakuta mtu anakwambia mimi ninapenda kufanya mazoezi asubuhi lakini, usingizi wa saa kumi na moja huwa ni mtamu, siwezi kuuacha. Mtu huyohuyo, ambaye anashindwa kuacha usingizi wa alfajiri anajikuta akiambulia magonjwa. Ukishakupatwa na magojwa ni wazi kwamba kuna mengine yatakusababishia maumivu makali ambayo, yatakukosesha usingizi ule uliokuzuia mwanzoni kuamka mapema na sasa kuukosa tena kwa gharama kubwa.

Usingizi pamoja kwamba ni kitu kizuri, lakini kinachukua “masaa” yetu mengi ambayo tuna uwezo wa kuyatumia vizuri katika shughuli nyeti za uzalishaji mali. Ikumbukwe pia kuwa, pesa uliyonayo inatokana na muda uliowekeza kwenye shughuli za uzalishaji mali. “Masaa (muda) tunayotumia kufanya kazi ndiyo pesa yenyewe” kwasababu uzoefu unaonyesha kuwa mtu ambaye anaamka na kuanza kazi mapema (alfajiri) kila siku amepiga hatua kubwa sana kimaendeleo kuliko anayechelewa kuamka.

Kwahiyo kama kuna kazi ya muhimu katika maisha yako, acha usingizi ukafanye hiyo kazi, kwani unapomaliza kazi hiyo, utalala usingizi wako kwasababu usingizi ni kitu ambacho kipo na hakipotei kamwe. Tukiendelea kufanya kazi kwa bidii ni wazi kwamba tutapata mafanikio makubwa ndani ya muda mfupi na hapo tutakuwa na fursa na muda wa kutosha sana kulala usingizi. Wewe ndiye mwenye maamuzi juu ya matumizi ya muda na nguvu yako. Chagua kuwekeza muda na nguvu nyingi kwenye shughuli za uzalishaji mali na ufanye maamuzi kwa kuanza leo, maana ujachelewa. 




SHULE YA “MAISHA YAKO” INATAKA MALENGO NA MIPANGILIO YAKO IWE NI KWA MAANDISHI.

Kumbukumbu ni kitu muhimu sana katika kujenga misingi imara ya mafanikio yoyote yale. Watu tuna kumbukmbu nyingi na za kila  aina ndani ya vichwa vetu. Kutokana na hazina hii ya kumbukumbu, watu wengi uzitegemea sana katika kufanya maamuzi ya shughuli mbalimbali za kila siku. Lakini, utafiti umebaini kuwa, huwezi kupata mafanikio makubwa ambayo ni endelevu, kama huna ndoto ya aina ya maisha unayoyataka. Kwa walio wengi yawezekana wana ndoto kubwa, lakini ndoto hizo hazitimii kwasababu mbalimbali, na sababu mojawapo ambayo ni muhimu ni kuendekeza utamaduni na tabia ya kutekeleza mipango kutokea kichwani.

Kumbuka kuwa, kila siku ubongo wetu unapokea na kutunza kumbukumbu nyingi sana, kiasi kwamba, inakuwa vigumu kwako wewe kuweza kukumbuka mambo muhimu ambayo unahitaji kuyatimiza. Matokeo yake, unajikuta kila siku unashughulika na vitu vipya tu! Au kulingana na mambo yanavyojitokeza. Mara nyingi shughuli zako zilizo nyingi zinakuwa hazina mwendelezo wa pamoja. Hii ni hatari sana kwa mafanikio na pia, ni vizuri ukafahamu kuwa, kuendelea kukumbatia tabia hii ya kutegemea kumbukumbu ambazo ziko kichwani, itakuwa ni vigumu sana kufikia maisha ya ndoto yako.

Tunapoongelea kumbukumbu hatuamanishi zile za mapato na matumizi tu! bali ni kumbukumbu zile ambazo zimejikita kwenye mambo ya fursa, malengo ya muda mrefu na mfupi, aina ya maisha unayotaka kuishi miaka (mtano, kumi, ishirini au zaidi) ijayo, mambo yanayotakiwa kubadilishwa ili wewe uweze kusonga mbele, mambo unayohitaji kujifunza n.k. Ni wazi kwamba kumbukumbu za aina hii, nyingi tayari unazo kichwani, lakini hazijaweza kukusaidia pengie kwasababu, nyingine ukumbuki kama unazo kwenye kichwa chako.

Kwahiyo, mwanzo wa kuweza kupanga na kutimiza malengo makubwa katika maisha ni kuwa na kumbukumbu za mawazo mazuri lakini yaliyoandikwa kwenye karatasi, kwani huu ndiyo msingi mkubwa na mzizi mkuu wa mafanikio. Watu wengi waliofanikiwa wanasema kumbukumbu ambazo  “zimeandikwa kwenye karatasi” ndizo za uhakika na ambazo unaweza kuzitegemea  kukuongoza kwenye safari yako ya kuelekea maisha unayoyataka. Ili kuweza kupata na kutunza kumbukumbu, huitaji kuwa na kitu kingine zaidi ya “nidhamu” ya kufanya vitu rahisi na ambavyo ni vya kawaida kila siku.

Wajasiriamali waliofanikiwa wanakwambia kwamba, kama ukipata au kusikia wazo zuri kuhusu jambo fulani lenye mashiko kwenye ndoto zako, shika kalamu na daftari na uliandike maramoja. Alafu wakati wa jioni au usiku kukiwa kumetulia, jaribu kulipitia daftari lako. Fikiria wazo ambalo lilibadilisha maisha yako, wazo lililonusuru ndoa yako, wazo lililo kutoa kwenye wakati mgumu, wazo lililokusaidia ukafanikiwa. Kazi hii endelea kuifanya mara zote bila kuacha. Kwahiyo, uwe ni mkusanyaji wa mawazo mazuri, mkusanyaji wa uzoefu kwaajili ya biashara na mahusiano yako na kwa maisha yako ya mbeleni (future).

Tunahitaji kuanzia sasa tujenge utamaduni na tabia ya kuandika kila wazo zuri tunalolipata kila siku; iwe kulifikri wenyewe, kusikiaau kuona kwa marafiki au watu wengine, iwe ni kulisoma kutoka vitabuni n.k. Ili uweze kulifanikisha hili, ni vyema ukakumbuka kuwa tabia ya kuweka na kutunza kumbukumbu za mawazo mazuri katika maadishi haitakuja ghafla kwako, isipokuwa itakuja kama utaianza kuifanya taratibu lakini ukaifanya kila siku kwa kipindi kirefu, ili uweze kuizoea. Kumbuka tulipokuwa shuleni, walimu walitufundisha kuwa na daftari kwaajili ya kuandika notisi na kabla ya kuandika tulihimizwa kuanza tarehe. Na hapo mambo yote tuliyokuwa tukifundishwa tulikuwa tukiyaandika na ndiyo maana wakati wa mitihani ulipokaribia, ilikuwa ni rahisi sana kujikumbusha kwa kupitia notisi zilizoko kwenye daftari na hatimaye kuweza kufahuru mitihani.

Tunapokuwa tumemaliza shule na kuanza maisha ya kujitegemea na kujiongoza wenyewe, tunahitaji kuwa “wanafunzi wa maisha yetu” na hapa ndipo tunatakiwa kuwa na daftari maalumu la kuandika na kuweka kumbukumbu za mawazo na mipangilio mingine ya jinsi tulivyojipanga kufanikisha ndoto zetu. Uzuri wa kuwa na daftari hili, ni kwamba, ni rahisi sana kurithisha watoto wako pamoja na vizazi vingine. Ukweli ni kwamba, inaleta changamoto sana kuwa “mwanafunzi” wa maisha yako, maisha ya mbeleni, mwisho wako (unakotaka kufika). Kumbuka utakapo amua kuwa mwanafunzi katika shule iitwayo “maisha yako” ni tofauti na shule zingine ulizowahi kusoma. Hapa katika shule ya “maisha yako”, wewe mwanafunzi ndiye kila kitu, hakuna wa kukuamsha, wala wa kukuogoza bali wewe tu ndiye unajiongoza, unajihimiza na unajiwekea presha mwenyewe. Ni kutokana na yote haya ndiyo maana daftari la kumbukumbu za mipangilio ya maisha ya ndoto yako ni muhimu sasa kuliko siku zote. Ni muhimu tuamke, na tuweke msingi imara kwaajiri ya kufikia mafanikio makubwa.



KUMALIZA SIKU KABLA YA KUIANZA NDIYO SIRI YA KUPATA MAFANIKIO MAKUBWA MAISHANI
Watu wengi tunatamani kupata mafanikio kwa lengo la kupata fursa ya kuishi maisha mazuri, maisha yenye furaha, maisha ambayo unaweza kusaidia wasiojiweza n.k. Lakini, waliowengi ndoto hizo, zinaonekana kuendelea kufifia kadili umri unavyozidi kuwa mkubwa!. Kwa kuangalia mifano ya watu wengi waliofanikiwa, unagundua kuwa mafanikio si kitu chochote zaidi ya kuwa na nidhamu ya kufanya vitu vya kawaida kila siku.
Mafanikio hayatokani na miujiza bali ni kitu kinachojitokeza kutokana na mambo ya msingi ambayo ni madogo madogo yanayohitajika kupangwa na kufanyika kila siku. Kwahiyo, tunaweza kusema kwamba, mafanikio ni ujuzi au kusoma vitu vya kawaida— lakini wakati mwingine tunahitaji mtu fulani wa kutukumbusha na kutuonyesha njia ambayo ni rahisi kufuata na kuweza kufikia mafanikio tunayo yataka. Na hapa nitaeleza umuhimu wa kuwa na mpango mzuri kama hatua mojawapo ya kufuata ili kuweza kufika kwenye mafanikio makubwa kuliko unavyoweza kufikiri.
Kujenga maisha, kujenga kitu chochote kile, ni kama kujenga nyumba; unahitaji kuwa na mpango. Chukulia mfano, kama ungeanza kubeba na kuanza kuweka matofari kwenye msingi alafu akatokea mtu akakuuliza “Unajenga kitu gani?” Je? Utaweka chini matofari uliyobeba na kumwambia kuwa hujui unacho jenga?” au utamwambia unachotaka kujenga kuwa ni nyumba hata kama bado haijajengwa. Mfano huu unatufungua akili na kutufundisha kuwa, mara zote“nyumba inaanza kujengwa mara tu inapokuwa imekamilika”.
Tukirudi kwenye maisha tunaona kuwa imekuwa vigumu sana kwa watu walio wengi kuweza kuweka mipango madhubuti ya maisha ya ndoto yao. Kwasababu ni ukweli usiopingika kuwa wengi wetu hatujabainisha kwa dhati kuwa uko mbeleni tunataka maisha ya namna gani na kwakuwa hilo halipo katika maandishi tumejikuta hatuna cha kupanga kufanya kwa siku, wiki, mwezi, mwaka au zaidi. Tunaamka asubuhi na kufanya chochote kinachojitokeza kwenye akili na fikra zetu. Kwa maana nyingine tumekuwa watu wa kushughulikia mambo mapya na matukio tu! Hii ni hatari na ni changamoto kubwa sana iliyoko mbele yetu.
Kila mmoja wetu ambaye haliziki na maisha aliyonayo kwa sasa, inabidi kujenga utamaduni wa kuwa na nidhamu ya kufikiri kwanza juu ya jambo ambalo unatarajia kulifanya. Baada ya kufikiri, unahitaji kuandika mawazo yako juu ya aina ya maisha unayotamani kuyaishi miaka mitano, kumi na zaidi ijayo, kwa kufanya hivyo utakuwa tayari umekamilisha nyumba kabla ya kuanza kujenga.
Ukijaribu kutafakali mafundisho mbalimbali kutoka kwa watu waliofanikiwa, utagundua kitu kimoja ambacho kinasisitizwa sana ni “usianze siku yako mpaka itakapokuwa imemalizika vizuri”—angalau orodha ya mambo ya kufanya. Jitahidi kuwa na orodha ya mambo ya kufanya kabla ujaanza kutenda kazi za siku, na mengi yawe ni yale yenye mchango katika kukufikisha kwenye malengo yako ya muda mrefu (k.m: miaka 5, 10, 25 au zaidi). Katika kupanga orodha ya mambo ya kufanya, jaribu kuacha nafasi ya kufanya marekebisho kadili utakavyoendelea, acha nafasi kwaajili ya mikakati ya ziada, lakini kikubwa hapa cha kusisitiza ni kumaliza kwanza jambo unalotaka kulifanya kabla ya kulianza. Usiaze wiki mpaka iwe imekamilika. Chora ramani ya jinsi itakavyokuwa, iwekee sura na umbo au weka jengo lake, na baada ya hapo anza kuifanyia kazi.
Utaratibu huu ufanyike kwa mwezi ujao—Usianze mwezi, mpaka uwe na mpango tayari mezani. Na kubwa zaidi, usianze mwaka mpaka umalizike kwenye karatasi. Siyo wazo baya, ikifikia mwisho wa mwaka, ukakaa chini na familia kwaajili ya kuweka mpango binafsi kwa mwaka ujao, kaa chini na weka mpango kazi, kaa chini na mshauri wako wa mambo ya fedha kuweka ramani ya jinsi pesa itakavyopatikana. Panga kalenda yako na kwa vitu vyote vinavyowezesha maisha yako kwenda mbele hasa kule unakokutaka.

1 comment:

Peter said...

Duuuu, nimekuelewa sana