Tuesday, February 10, 2015

UNAPOAMUA KUANDIKA HISTORIA YA MAISHA YAKO USIKUBALI MTU MWINGINE AKUSHIKIE KALAMU



Kwakuwa maisha ni safari ambayo unasafiri muda mrefu kabla ya kufika unakokwenda au kufikia maisha ya ndoto yako. Wakati ukiendelea na safari yako ya maisha, usikubali kushawishiwa na mtu yeyote wala kundi lolote lile kwani wao ni vigumu sana kufahamu unakotaka kwenda. Usijaribu hata siku moja kuchagua njia au cha kufanya kutokana na matakwa ya watu wengine.
 Mtu kikundi Fulani kufanya jambo Fulani na wakashindwa haimanishi kwamba na wewe utashindwa kumbuka wewe unajifanana wewe peke yako, hakikisha haugopi kupigwa mishale kutoka kila kona ambayo ni kejeli, matusi, kubaguliwa, kutengwa, kusemwa vibaya n.k. Jitahidi kuwa na uamzi pamoja na uchaguzi binafsi kama njia mojawapo ya kufikia mafanikio unayoyahitaji. Kwahiyo nilazima ujifunze kusema hapana kwa baadhi ya vitu, hata kama vinafanywa na watu wengi. Jambo la kuwa na uchaguzi na uhamzi binafsi ni muhimu sana kwani usipojifunza kufanya hivyo, basi wewe kila wakati utakuwa mfanyakazi au mtumwa wa kutumikia uchaguzi na uhamzi wa watu wengine. Ili uweze kuwa na uchaguzi sahii wa jambo la kufanya ili kupata mafanikio na maisha mazuri ni lazima kujifunza kutofautisha kilicho muhimu na kisicho na umuhimu. Watu waliowengi wanafanya vitu vingi, hata kama vingine siyo vya muhimu ilimradi tu watu wengine kama marafiki ndugu n.k wanafanya basin aye atafanya.
Matokeo ya kufanya kila kitu eti kwa sababu wengi wanafanya, ni kujikuta muda wako mwingi unautumia Katika vitu au shughuli ambazo zinaleta mafankio kidogo sana. Mwandishi “Richard Koch” Katika kitabu chake cha “Living the 80/20 Way: Work Less, Succeed More, Enjoy More”anasema kwamba ili uweze kupata mafanikio makubwa maishani ni lazima utumie Asilimia 20% ya muda kupata mafanikio ya Asilimia 80%; Kwahiyo, mwandishi huyu anatufundisha kuwa iwapo utakuwa mtu wa kufanya kila kitu ili mradi wanafanya marafiki zako, basi ujue wewe utakuwa unatumia Asilimia 80% ya muda wako ili kupata mafanikio ya Asilimia 20% tu! Kwa maana nyingine wewe utakuwa mtu unayehangaika kila siku mpaka unakufa.
Ikumbukwe kuwa Katika maisha unapoamua kuchagua kufanya kitu kimoja kati ya vingi ulivyonavyo, siyo kwamba hivyo vingine huvihitaji bali unachagua kilicho bora zaidi. Kufanya maamuzi ni mwanzo tu wa vitu kutokea na inampelekea mtu kupata nguvu halisi ambayo itampeleka mahali ambapo ni pazuri na hata unakuta mwanzoni ukupafikiri wakati ulipoamua kufanya mabadiliko hayo.
Katika kuandika historia ya maisha yako, uwezi kumfurahisha kila mtu, hivyo huwezi kukamilisha kila kazi unayo paswa kuifanya. Kwahiyo katka kila kazi au majukumu ni vizuri ukaweka malengo na utendaji wako ukawa unaongozwa na malengo uliyojiwekea wewe mwenyewe,  hivyo kipimo cha kufanikiwa au kutokufanikiwa kwako kitakuwa ni kwako kuweza kujipima kwa kutimiza au kushindwa kutimiza malengo yako na si kusikiliza watu wanasema nini kuhusu kufanikiwa au kutofanikiwa kwako.

Mpendwa msomaji, endelea kuitumia vizuri MAARIFASHOP ili kujifunza mambo mbalimbali yatakayokuwezesha kupata mafanikio. Ili kupata makala mpya kila zinapochapishwa, bonyeza neno TUMA MAKALA MAARIFASHOP kisha sajiri barua pepe yako. Na kama unapenda kupata mafunzo ya kila siku kwa njia ya whatsap bonyeza neno MAFUNZO

KARIBU TUCHUKUE HATUA PAMOJA!

Monday, February 9, 2015

UNAKUWA MASKINI KADILI UNAVYOCHELEWA KUPATA FEDHA INAYOFUATA BAADA YA KUPATA LEO



Ukifuatilia na kutafakari suala zima la mapato na matumizi ya pesa kwa watu walio wengi, utagundua kuwa kuna tatizo kubwa la msingi. Fikiria mkulima wa Tanzania ambaye amebahatika kuishi maeneo yenye misimu miwili ya mvua wanapata Mazao mara mbili kwa mwaka, hii ikiwa na maana kwamba, anapata fedha mara mbili kwa mwaka, maana yake mtu huyu akipata pesa leo, pesa nyingine itapatikana baada ya miezi sita. Lakini kwa mkulima anayeishi maeneo yenye msimu mmoja wa mvua, wanapata mavuno mara moja kwa mwaka mzima, hii ikimaanisha kuwa huyu mtu anapata pesa mara moja kwa mwaka. Wafanyakazi na hasa wa serikali na makampuni binafsi wana pata fedha kila mwezi. Wafanyabiashara wadogo na wa kati wanapata pesa kwa wiki na wengine kila siku. Wafanyabiashara wakubwa na matajiri wengine wanapata pesa kwa saa, dakika na wengine kama makampuni ya simu wanapata hadi kwa sekunde.

Uzoefu umeonyesha kuwa unapochukua muda mrefu kuingiza pesa nyingine ndivyo unakuwa maskini wa kutupwa na maisha yanakuwa magumu kweli kweli. Sababu kubwa ya umaskini huo ni kutokana na ukweli kwamba mahitaji au matumizi ya mtu yeyote huwa ni kila siku na wakati huo huo mapato ni kwa mwaka au kila baada ya miezi sita kwa Wakulima walio wengi. Kutokana na hali hii tunaona kuwa hakuna ulinganifu ulio sawa kati ya kupata na kutumia pesa. Kupishana kwa mapato na matumizi ndiko kunakofanya watu wengi na hasa Wakulima kuishi Katika madeni makubwa ambapo inapofika msimu wa mavuno Wakulima hawa tayari wanakuwa wanadaiwa, kiasi kwamba inapotokea msimu haukwenda vizuri wengine ulazimika kuuza hata vipande vya ardhi waliyokuwa nayo ili kulipa madeni, wengine huwa hawasubili kuvuna ndipo wauze badala yake wanauza Mazao yao ya yakiwa bado kukomaa shambani.

Katika wilaya za Karagwe, Bukoba na Muleba ambako zao la kahawa linalimwa kwa wingi Wakulima wengi uchukua fedha kama mkopo kutoka kwa wafanyabiashara kabla ya kahawa kukomaa wenyeji wanaita “Butura”. Biashara ya “Butura” ni maarufu sana mkoani Kagera. Watu upewa pesa kabla ya Mazao kukomaa huku wakikubaliana kulipana Mazao pindi yakikomaa. Katika Wilaya ya Ngara wao huuza mahindi yakiwa hata bado kubeba, maeneo ya usukumani suala hili liko sana kwenye zao la mpunga japo wengi uwa wanakopa pesa kutoka kwa wafanyabiashara ili kupata pesa ya palizi na kuhemea ndege“kumoja” n.k.

Kwasababu wanachukua muda mrefu kupata pesa, ndiyo maana wakishapata pesa wanachangamka sana kuzidi kipimo na hii ni kutokana na sababu kuwa mara nyingi wakati wa msimu, pesa uja kwa mkupuo, hali ambayo huwafanya kuzitumia ovyoovyo na wengine ujaribu na kuongeza mke wa pili, kunywa pombe kupindukia, harusi na sherehe nyingi. Kutokana na matumizi ambayo uambatana na mihemuko ya kila aina, watu uweza kuishiwa pesa walizokuwa nazo mara tu baada ya takribani mwezi mmoja hadi miwili.

Baada ya watu kuishiwa pesa zilizotokana na mavuno, watu wengi hurudia hali yao ya kutokuwa na pesa na hapa ndipo, utaanza kusikia lugha za “hakuna mzunguko wa pesa” Eti kila mmoja anaanza kusema pesa hakuna siku siku hizi; Kumbe kiuhalisia siyo kwamba hakuna pesa, isipokuwa ni kwamba hakuna cha kuuza wakati huo. Pesa huwa inafuata vitu vilipo pamoja na huduma zilipo. Hali hii ujenga hofu sana miongoni mwa wanajamii hasa kutoka Katika kaya masikni na pia kukata tamaa. 

Kutokana na hofu na imani kwamba kijjini hakuna pesa, wengi wao na hasa vijana uchukua uamzi wa kukimbilia mijini wanakoamini kuna mzunguko wa pesa wasijue kuwa hata huko wanakoamini kuwa na mzunguko mzuri wa pesa bado utalazimika kuwa na vitu au huduma ndipo uzipate, bila kuwa na vitu/huduma – wewe hata kama uko mjini unakoamini kuwa kuna mzunguko wa pesa, bado pesa utaziona tu kwa wengine na si kwako!!!!.

Kwahiyo kama wewe ni mmoja wa wadau wa maendeleo, njia pekee ya kuwakomboa Wakulima ni pamoja na kutafuta njia ya kufupisha muda wa kupata fedha nyingine angalau ukiweza kushuka kutoka miezi sita mpaka mwezi mmoja. Hikiwa hivi ndivyo, basi itakuwa ni hatua moja muhimu sana Katika kupambana na umaskini hasa Wakulima.

Mpendwa msomaji endelea kuitumia vizuri MAARIFASHOP, ili kujifunza mambo mbalimbali yatakayokuwezesha kufanikiwa. Kupata makala mpya kila zinapochapishwa, bonyeza sasahivi neno- hivi; TUMA MAKALA MAARIFASHOP kisha sajiri barua pepe yako na kama unapenda kupata mafunzo ya kila siku na makala mpya kwa njia ya whatsap bonyeza neno MAFUNZO

KARIBU TUCHUKUE HATUA PAMOJA!!

Sunday, February 8, 2015

UMUHIMU WA KUWA KIONGOZI WA MAISHA YAKO



AMUA KUWA RAIS WA MAISHA YAKO LEO
Maisha unayoishi sasa ni maisha yako, kama kuna sehemu yoyote ya maisha yako ambayo huipendi wewe ndio una jukumu la kuibadilisha. Hakuna mtu mwingine yeyote ambaye anaweza kuwa na uchungu na maisha yako ila wewe mwenyewe. Na wala hakuna mtu yeyote anayeweza kuyabadili maisha yako bila yaw ewe mwenyewe kuwa tayari kwa mabadiliko.

Kuanzia sasa jichukulie wewe kama raisi wa maisha yako, na jichukulie wewe ndio mtu wa mwisho wa kufanya maamuzi juu ya maisha yako. Na sio tu unajichukulia hivi, bali ndio ukweli wenyewe. Wewe kama raisi maamuzi yako yanaweza kusababisha mafanikio au yakasababisha kushindwa. Kama tulivyoona kwenye siku ya kwanza upo hapo ulipo kutokana na maamuzi uliyofanya na machaguo uliyofanya. Ili kwenda mbele zaidi unahitaji kufanya maamuzi bora zaidi na kuboresha machaguo yako.

Miasha ni kuchagua, ukichagua kufanikiwa ndiyo utakachokipata, ukichagua kuwa wa matatizo na kushindwa ndicho kitakachotokea. Usipochagua kabisa utapata kile kilicho kibovu kabisa ambacho ni kushindwa. Kipato unachopata leo ndio kipato ulichoamua kupokea, kama kipato unachopata sasa hakikuridhishi amua kupata zaidi ya hapo. Fanya hilo kama lengo lako, weka mipango na anza kufanyia kazi mpango wako wa kujiongezea kipato. Ukikaa tu na kulalamika kwamba kipato hakikutoshi huku hufanyi chochote cha kukiongeza unapoteza muda wako.

Wewe ndio raisi wa maisha yako, wewe ndio mfanya maamuzi mkuu na wewe ndio unayetengeneza maisha yako. Kama utakuwa na mtizamo hasi utajenga maisha ya matatizo na kushindwa na kama ukiwa na mtizamo chanya wa kuona unaweza kubadili maisha yako utatengeneza maisha ya mafanikio na furaha. Yote haya yapo mikononi mwako ni wewe tu ufanye maamuzi sahihi na kuyasimamia.

Endelea kuwa karibu na mtandao wa MAARIFASHOP ili kujenga na kukuza uwezo wako wa kusaka na kupata mafanikio. Kupata makala mpya kila zinapochapishwa bonyeza kiungo hiki sasa hivi; NITUMIE MAKALA MAARIFASHOP kisha sajiri barua pepe yako na kama unapenda kupata mafunzo ya kila siku na makala mpya kwa njia ya whatsap bonyeza neno MAFUNZO