Biashara


Biashara Yako Inakutaka Ufanye Yafuatayo:
 "Kila utakapoona biashara iliyofanikiwa ujue kuna mtu alifanya maamuzi ya kijasiri" ~ Peter F. Drucker
Watu wengi tunatamani sana kuwa matajiri, lakini wengi wanakata tamaa. Mojawapo ya njia muhafaka itakayotufikisha kwenye utajiri ni “biashara”. Biashara ni
kundi mojawapo la “viingiza-pesa” mfukoni. Ziko aina nyingi za biashara, ambazo unaweza ukafanya kulingana na chaguo lako.

Biashara siyo lazima iwe ile tuliyozoea yaani “kununua vitu kwa bei ya chini na kuuza kwa bei ya juu” BALI ni zaidi ya hapo. Hapa ninamaanisha kuwa “biashara” ni hali yoyote ile ambayo unaweza ukaunganisha nguvu, nyenzo na vitu mbalimbali, kutengeneza mfumo wa uzalishaji wa bidhaa au huduma mbalimbali. Mwisho wa siku, mfumo huu wa uzalishaji ndio ambao uvuta au kutiririsha pesa nyingi kuingia mfukoni mwako. Mara nyingi pesa hii ambayo utiririka kuja kwako, huwa ni nyingi zaidi ya ile uliyowekeza awali.

Biashara imara inajengwa na aina ya wamiliki ambao wako tayari kufanya kazi bila ya kudai malipo (wanafanya kazi bure). Mojawapo ya sababu za kukufanya wewe ufanye kazi bure au bila kudai malipo, ni kukuwezesha wewe kujifunza tabia ya kujitolea kwa muda na kujenga VIINGIZA-PESA kabla ya kupokea au kupata faida.

Biashara yenye kuleta mafanikio makubwa inajengwa na vitu vitano muhimu, yaani: kiingiza pesa, wafanyakazi, wataalam, wawekezaji na mmiliki wa biashara.

Katika vitu 5 vinavyounda mfumo wa biashara kuna vitu vinatakiwa kulipwa kwanza na kuna vingine vinalipwa mwishoni. Hapa chini kuna orodha ya nani anatakiwa kulipwa kwanza na nani anatakiwa kulipwa akiwa mwisho:

1. Viingiza-Pesa (Biashara au Uwekezaji)
2. Wafanyakazi (Uliowaajiri)
3. Wataalam (Wahasibu, Wanasheria, Mtaalam mwelekezi)
4. Wawekezaji (wenye hisa)
5. Mmiliki wa biashara (wewe)

Wewe kama mmiliki wa biashara lazima ukilipe “Kiingiza-Pesa” kwanza. Maana yake ni kuendelea kuwekeza pesa kiasi cha kutosha na rasilimali, ili kutunza na kufanya Kiingiza-Pesa chako kuwa imara na kukua zaidi.

Wamiliki wengi wa biashara, mara nyingi ujiweka mbele kuliko au zaidi ya kiingiza-pesa, wafanyakazi, na watu wengine wote. Ndiyo maana biashara nyingi ushindwa kuendelea na hatimaye kufa.

Mmiliki wa biashara ni mmojawapo wa watu wanaotakiwa kulipwa mwishoni. Hii ni kutokana na ukweli kwamba lengo kuu la yeye kuanzisha biashara ni kulipwa zaidi ya mtu yeyote. Lakini, ili kuweza kulipwa zaidi ya wengine, lazima mmiliki wa biashara ahakikishe watu wote na vitu vingine vinalipwa kwanza.

SOMA; Mwajiriwa Jilipe Kwanza Mjasiriamali Ufanye Nini?

Lengo la kuandika makala hii, ni kukufundisha wewe usije kufanya kazi kwaajili ya kulipwa pesa. Nataka ujifunze tabia ya kuchelewesha ujiko, heshima, sifa n.k. Pia, ujifunze kufanya kazi kwaajili ya kujenga VIINGIZA-PESA ambavyo thamani yake huwa inakua. Nataka ujifunze kujenga VIINGIZA-PESA na siyo KUFANYA KAZI kwaajili ya pesa.

Biashara nyingi zinazoanzishwa huwa zinashindwa kufuata orodha hii au ushauri kama huu ninaoutoa leo. Nimekutana na watu wengi ambao huwa wanaanzisha biashara kwa kukopa pesa au kupata michango kutoka kwa marafiki, familia na kwa wawekezaji wengine. Mara moja huwa wanakodi ofisi kubwa, wananunua magari ya kifahari, na kujilipa mishahara mikubwa kutoka kwenye mtaji wa wanahisa au wawekezaji badala ya faida inayotoka kwenye biashara yenyewe.

Matokeo yake anajikuta kumebaki pesa kidogo sana, hapo ndipo ujaribu kulipa biashara, wataalam kiasi kidogo sana cha pesa. Katika biashara ya namna hiyo, ni mara nyingi wawekezaji ndio ukwama kwa kushindwa kulipa gharama za uendeshaji wa biashara kama ilivyo biashara nyingi zinazoanza siku hizi.

Ukilipa wengine kwanza kwenye biashara unayomiliki, ni kwamba pesa yote uliyowalipa wengine pamoja na faida lazima zirudi. Lakini ukijijali wewe kwanza na kulipa wengine mwishoni, basi ujue kuwa pesa nyingi uliyotumia haitarudi kamwe na huo ndio utakuwa mwisho wako kwenye ulimwengu wa biashara.

Ukweli ni kwamba, watu wote ambao huwa ni lazima kulipwa kwanza, mwisho na mwisho huwa ndio wanalipwa kidogo. Mmiliki wa biashara lazima ujilipe wa mwisho, kwasababu huko katika biashara kwa lengo la kujenga KIINGIZA-PESA. Kama huko katika biashara kwaajili ya kupata mshahara mkubwa, basi usiwe katika biashara. Kwa maneno mengine ni kwamba unatakiwa kuanza kutafuta kazi ya “kuajiliwa”.

Kama mmiliki wa biashara amefanya kazi nzuri na kutimiza majukumu yako yote ya kulipa wengine wote kwanza, ili wakujengee VIINGIZA-PESA, tunategemea kwamba kiingiza pesa kilichojengwa na wengine waliolipwa kwanza kitakuwa na thamani kubwa zaidi kuliko pesa ambayo angepata kama angeamua kujilipa kwanza kabla ya wengine.

Uzoefu unaonyesha kwamba “watu wengi hawako kwenye ulimwengu wa biashara ili kujenga au kupata VIINGIZA-PESA. Watu wengi wapo katika ulimwengu wa biashara kama “waajiliwa au wataalam waliojiajili” kwasababu wanapeda maisha ya mshahara na ujira. Hii ndiyo mojawapo ya sababu kubwa ya kuwa na matajiri wachache (chini ya asilimia 5) nchini Tanzania na kwingineko duniani. Ni asilimia 5 ya watu katika jamii wanaotambua thamani ya VIINGIZA-PESA kuliko MSHAHARA.

Mmiliki wa biashara au mjasiriamali upata pesa nyingi mwisho wa siku kwasababu mwanzo wa siku ni lazima awe mtu wa kujitoa kwaajili ya wengine (mwenye roho nzuri). Mmiliki wa biashara, ndiye uchukua au kukabiliana na hatari kubwa na pia kuwa wa mwisho kulipwa.

Kama wamefanya kazi nzuri, kiasi cha pesa kinaweza kuwa kikubwa ajabu. Ndiyo maana ni muhimu kufuata orodha hii (kiingiza-pesa, wafanyakazi, wataalam, wawekezaji na mwisho ni mmiliki), kila wakati unapoanzisha biashara ni lazima uendelee kufanya kazi bila malipo (bure) kwanza.

Siku hizi, napendelea mtindo wa kufanya kazi bure, kwasababu ninataka pesa kubwa mwisho wa siku. Watu wengi ambao bado tuko kwenye ajira na waliojiajiri tuna kikomo au mipaka juu ya ni watu wangapi tunaweza kuwahudumia. Kwahiyo, pesa au kipato chetu kina ukomo na ni kidogo sana.

Mjasiriamali au mfanyabiashara ambaye anaelekeza nguvu zake kwenye kujenga biashara ambayo inatoa suruhisho kwa watu wengi zaidi, atazidi kuwa tajiri zaidi na zaidi. Wafanyabiashara wa aina hii wanapata zawadi kubwa kwasababu wao ujenga “mfumo au Kiingiza-pesakwaajili ya kuhudumia watu wengi zaidi na zaidi. Ndiyo maana wamiliki wa biashara wanaweza kuwa matajiri wakubwa kwa haraka sana, na watu amabao ufanyia mshahara, upata utajiri kwa mwendo wa kinyonga.

Katika maisha kuna sheria inayosema kwamba “pokea halafu na wewe utoe kwa wengine” Ni sheria ambayo imekuwepo kwa miaka mingi na itaendelea kuwepo kwani bado inakidhi mahitaji ya sasa. Leo hii, kuliko ilivyowahi kutokea, ni muhimu kutaka kujijali mwenyewe na wale unaowapenda.

Lakini, kama unataka kuwa tajiri ni lazima kwanza ufikirie kutoa mchango wako wenye kukidhi mahitaji ya watu wengi kadiri unavyoweza kwanza. Ni sheria. Ninaamini katika sheria ya msaada sawa kutoka pande zote mbili na wazo la kutoa msaada bila kuhitaji malipo ni njia nzuri sana ya wewe kuwa tajiri mkubwa.

Tunakumbushwa kuwa watu wema na wenye kujali wengine ndio watapata neema ya utajiri. Hii ni sawa na kusema kuwa “kama unataka kutabasamu, kuwa wa kwanza kuachia tabasamu. Kama unataka mapenzi, kuwa wa kwanza kutoa mapenzi. Kama unataka kueleweka basi kuwa mtu kwanza kuwaelewa wengine.



JE? UMEISHA FUNGUKA KUHUSU BIASHARA YA MTANDAO? AU NA WEWE NI KATI YA WALE WANAOFIKIRI NI BIASHARA YA KUTUMIA MTANDAO WA INTERNET?
Ukichagua kufanya biashara ya mtandao, kama njia ya kujiongezea kipato cha ziada, ama kama fani yako mpaya, utakuwa umejionyesha kuwa kiongozi wa maisha yako. Pia kama wewe hufurahishwi na hali yako uliyokuwa nayo kwa sasa, katika kipato, kiafya n.k, basi hunabudi kuanza kufanya Biashara hii ambayo Ndiyo Biashara ya zama hizi (karne ya 21). Biashara hii imejionyesha dhahiri na wazi kuwa ndiyo muhimili sahii katika kujiendeleza kifikra na kibiashara na kukujengea uwezo wa kujitegemea. Kinachohitajika ni kuchukulia biashara yako kwa umakini. Kuwekeza mtaji wa pesa kidogo, kusikufanye ukadharau biashara hii. Kuwekeza kidogo katika biashara hii hakuamanishi kwamba huwezi kupata mapato makubwa.  “Hakuna biashara ndogo duniani! Bali kuna wafanyabiashara wenye mitizamo midogo”

Ukiifanya biashara yako kama shughuli ya kupoteza muda wako wa ziada, utapata kipato cha kupoteza muda wa ziada. Ukiifanya kama biashara kwa umakini, utapata kipato cha biashara kikubwa cha umakini. Kwahiyo, ni mpaka utakapo amua kuchukua hatua kwa vitendo ndipo utakapo weza kuona matunda yoyote katika biashara yako.

Kwanini Uipende Biashara ya Mtandao?
Ø  Umilikaji: Inakupa fursa ya kumiliki biashara yako mwenyewe kwa mtaji mdogo wa kuanzia, na hakuna kitu kinachoweza kumpatia faraja mwanadamu kama kuweza kuyamiliki na kuyaendesha maisha yake na shughuli zake mwenyewe bila ya kupangiwa na mtu.
Ø  Msaada: Ingawa unamiliki biashara yako, lakini unakuwa haupo peke yako, unakuwa mmojawapo katika timu ya watu, kunakuwa na watu juu yako waliokutangulia na watu chini yako uliowaingiza. Utapata msaada wa kuongozwa ambao hautaupata katika biashara nyingi tulizozizoea. Biashara hii ni biashara ya kushirikiana na watu
Ø  Mafunzo: Huitaji kuwa na ujuzi wa kuuza wala biashara ili uweze kufanikiwa katika  biashara hii, watu tuliokutangulia katika biashara hii tunapaswa kukusaidia na kukushauri ili kupata uelewa na mafunzo yote utakayohitaji ili uweze na wewe kufanikiwa. Vilevile wewe yakupasa kuwafundisha watu wako chini yako. Kuna vitabu vingi na mafunzo mengi yanayoweza kukufanikishia biashara yako kama utakuwa na moyo wa kujifunza.
Ø  Ni ya kila mtu: Biashara hii ni ya kila mtu, wazee kwa vijana, biashara hii imeisha wakomboa wengi sana duniani kuanzia wababa na wamama wa majumbani, walimu, wasiokuwa na ajira, wauguzi, watu wenye ujuzi mbalimbali kama wanasheria, wahandisi na madaktari. Hii inatuhakikishia biashara hii inamfaa mtu yeyote ambaye yupo tayari kufanya kazi kwa ajili ya matokeo na mafanikio.
Ø  Muda wa ziada au muda wote: Unaweza kuanza kufanya kwanza kwa muda wako baada ya ajira yako au shughuli zako nyingine na baadaye kuipeleka katika kuifanya kwa muda wako wote. Uzuri wa biashara hii ni kwamba unajipangia wewe mwenyewe kasi ya mafanikio yako
Ø  Gharama Ndogo za Uendeshaji: Biashara hii inakuwa na gharama ndogo za uendeshaji, tofauti na biashara nyingine tulizozizoe, Gharama zako zitakuwa kadri biashara yako inavyokuwa, hakuna gharama za kuwa na ofisi.
Ø  Time Leverage (rasilimali muda): Ndiyo biashara inayohusisha kugawa muda wako na juhudi zako kwa watu wengine.

Mfano:: WEWE + 2 + 4 + 8 + 16 = 30
Ama badala ya kuunganisha watu wawili unaweza kufanya kazi ya ziada na kuwaunganisha watu watatu kama mfano unavyoonyesha hapa chini
WEWE + 3 + 9 + 27 + 81 = 120
Sasa;
Chukulia mfano:
Umeweza kujenga timu ya watu 120 lakini mimi binafsi nimewaunganisha watu 3 tu katika majina ya watu ninao fahamiana nao. Kila mmoja wetu akiwa anafanya masaa 2 tu kwa siku tunapata masaa;

Masaa 2/siku x siku 5 = Masaa 10 kwa wiki x watu 120 = Masaa 1200/wiki
Mwaka una wiki 52 chukua wiki 2 ni za likizo;
Masaa 1200/wiki x wiki 50 = Masaa 60,000 kwa mwaka
Wakati ambapo mtu aliyeajiriwa kazini, katika ajira ambayo haimiliki, ajira ambayo muda wowote ina uwezo wa kutoa mbawa, ajira ambayo huwezi kuwarithisha wanafamilia yako, kwanza unatumikishwa kwa masaa 8 kwa siku zaidi….

Masaa 8/siku x siku 5 = Masaa 40 kwa wiki
Masaa 40/wiki x wiki 50 = Masaa 2,000 kwa mwaka
Ili uweze kufanikiwa kufikisha masaa 60,000 itakulazimu kufanya kazi kwa muda wa miaka 30 yani masaa 60,000 kwa mwaka ukiyagawanya kwa masaa 2000 kwa mwaka = Miaka 30. Kwa nini ufanye kazi kwa miaka 30 wakati unauwezo wa kuifanya kazi hiyo hiyo kwa mwaka mmoja.

Au mfano mwingine ni mathalani, wewe unalipwa mshahara wa TSh. 500,000 kwa mwezi. N a unaajiriwa kwa kipindi cha miaka 40 katika maisha yako kabla ya kustaafu na mwili kutokuwa na nguvu tena za uzalishaji mali.
500,000 x Miezi 12 = 6,000,000 kwa mwaka….. kwa kipindi chote cha ajira huyu mwajiriwa ametengeneza 6,000,000 x Miaka 40 = 240,000,000/-
Ukimtafuta mtu huyu baada ya miaka 40 na kumuomba akuonyeshe akiba zake sidhani kama utaikuta hiyo million 240 baada ya ajira yake ya miaka 40.

Sasa kwanini ufanye kazi kwa muda wa miaka 40 na ukiwa maskini wakati ambapo unauwezo wa kutumia mfumo wa biashara ya mtandao na kufikia mafanikio ya kutengeneza kipato hicho hicho kwa muda wa miaka 4 tu!
5,000,000 x Miezi 12 = 60,000,000 kwa mwaka….. kwa kipindi cha miaka 4 tu! Nitakuwa nimetengeneza;
60,000,000 x Miaka 4 = 240,000,000/=




Tunafanya Nini Katika Biashara ya Mtandao?
a)      Tunatumia Bidhaa: Hii ni hatua ya kwanza kabisa ya kukufanya uamini bidhaa na kuisambaza Biashara yako. Inakufanya uwe na shauku ya kuelezea bidhaa. Pia ukitumia bidhaa watu wataona maadiliko na kukufanya uweze kuanza kujenga wateja. Cha kusikitisha wagavi wengi hawatumii bidhaa wanauza tu na kuweka ubaili kwenye miili yao. Wakati ni sasa, tumia bidhaa bora, hata ukipata pesa nyingi kama huna afya bora haina maana. Jenga mazoea ya kuamka na kutumia bidhaa. Kumbuka unahitaji nguvu ya kutosha ili ufanye Biashara vizuri, mwili wako ukiwa dhaifu Biashara yako itasuasua. Jiuzie mwenyewe kwanza kabla ujaanza kuwauzia wengine. Weka malengo ya kutumia bidhaa zote moja baada ya nyingine, ili uzifahamu Zaidi.
b)      Shirikisha watu bidhaa, fursa ya Biashara na kuuza bidhaa: Hatua hii huifanya Biashara yako ianze kufahamika na kukua. Msingi mkubwa wa biashara ya mtandao “si kuuza”. Kama kila mtu atauza je! Biashara itajengeka vipi? Kuuza ni muhimu pia kwa sababu kuna kusaidia kupata faida ya mara moja itakayo kusaidia kwa Mahitaji ya kila siku. Mfumo huu wa uuzaji hujenga wateja walioridhika na huduma na bidhaa. Kila mgavi ni lazima wateja wa mara kwa mara wasiopungua 20.
c)      Waingize watu kwenye mtandao (sponsoring new distributors): Hii ndio njia ya ukuzaji wa Biashara. Unawashirikisha rafiki zako wanaohitaji kujiongezea kipato au wale wanopenda kuwa watumiaji wa bidhaa. Mara nyingi watumiaji wengi wa bidhaa wakiridhika huwa wanajiunga kufanya biashara. Kupitia kuwaingiza watu, kuwafundisha njia na mbinu za kujenga biashara, utakuza timu yako na kuwa na watu wengi. Katika biashara ya mtandao kuna mambo mawili tunayoyafanya, kuuza Rejareja na kutafuta watu watakao jiunga kwenye kampuni chini yako ambao nao watauza Rejareja na kujenga kikundi kitakachofanya unayoyafanya). “Kwa nini uwasiliane na watu na kuwaonyesha umuhimu wa Biashara ya mtandao? Kwa sababu Biashara hii inahitaji utumie muda mchache kwenye Kuuza na muda mwingi kwenye kuwaonyesha wengine wafanye unachofanya.
d)      Kuwaelimisha na kuwaongoza waliojiunga chini yako: Mtu akisha jiunga na Biashara yako, hapo kazi ndipo inakuwa imeanza. Ni sawa na mtoto mchanga, inakupasa kuweka taratibu za kumuelimisha.
·        Muache mtu aamue yeye mwenyewe
·        Mfundishe jinsi ya kutengeneza manunuzi yake na kuhesabu point zake
·        Mwambie akupigie simu akipata utata wowote
·        Panga naye mikakati ya namna nzuri ya kufanya Biashara bila ya kupoteza muda mwingi.
·        Biashara yako itakuwa kubwa na imara kama utafanikiwa kuijenga kwa ku-siponsor wajengaji Biashara walioelewa sera za Biashara ya mtandao katika kampuni husika!
·        Anza kuwa na sehemu za kukutana na watu uliowaingiza ili waweze kujijenga vema
·        Hakikisha unawashirikisha uliowaingiza kuhudhuria semina na kuwajenga wawe viongozi
·        Biashara kubwa ujengwa kwa kuwaelimisha watu juu ya mfumo wa Biashara na siyo kwa kuuza tu bidhaa za kampuni
·        Waulize unaowaingiza kwa nini wamejiunga na kisha uweke nao malengo ya kufikia ndoto zao bila kukata tamaa
·        Waongoze na waambukize watu wako wafanye kama unavyo wafanyia na Zaidi:

“Maisha si rahisi kwa kila mtu. Lakini inatupasa kuwa wavumilivu na kikubwa Zaidi kujiamini. Inabidi kuamini kwamba sisi tuna kipaji/kipawa Fulani tulicho zawadiwa na mwenezi Mungu”
e)      Jiendeleze na Kulisha Akili Yako: Kumbuka elimu haina mwisho. Katika Biashara ya mtandao kuna mambo mengi ya kujifunza kutoka kwa waliotangulia na kufanikiwa Katika Biashara hii. Kujiendeleza kutakufanya utoke Katika mazingira uliyoyazoea, na kujituma Zaidi kufanya maamuzi bila woga, kukabiliana na vikwazo, kujiamini, kujitoa na kuwa na shauku mara zote. Wanaoongoza Katika Biashara Katika Biashara ya mtandao wanasoma vitabu, kusikiliza CD au DVD za uhamasishaji, na kujifunza kutoka Katika tovuti mbalimbali. Tenga muda wa kujisomea”: Kuna vitabu vingi vya Biashara ya mtandao mfano;
*      Make that call by – Jan Ruhe
*      Become a Network Marketing Superstar by – Mary Christine
*      Your first year in Network Marketing by Mike Yernel
*      It’s time for Network Marketing by – John Milton Fogg
*      The ultimate Guide to Network Marketing by Dr. Joe Rubino
*      Become a Recruiting Superstar by – Mary Christine
*      45 second Presentation by – Don Filla
*      More Feet on the street by – Jan Ruhe
*      Effective Sponsoring by – David Goh
*      52 ways to make more money in Network Marketing by – David Goh

1 comment:

AbuuTwaha said...
This comment has been removed by the author.