Sunday, November 13, 2016

Je? Unatafuta Utajiri Au Unaangaika Kuwa Maskini


“Mtu aliye na tabia ya kuangaika vile vile ana tabia ya kutaka kila kitu apate leo leo, mwisho wake anaambulia kupata vitu vidogo vidogo” ~ Cypridion Mushongi
 
Leo wakati natafakari juu ya utajiri, nimekumbuka sana mwanzoni mwa miaka ya 2000. Miaka hiyo nilikuwa na rafiki yangu ambaye alizoea kusema “Mwaga mtama kumkamata kuku kirahisi na usiangaike kumkimbiza kuku unaweza kuvunjika mguu kabla ujamkamata”. Ni kawaida kukuta watu wakikimbiza kuku pindi wanapohitaji kitoweo. Hali hii huwafanya wengine kuumia kwasababu ya kutumia nguvu nyingi kupita kiasi.

Tabia ya kumkimbiza kuku kila mara tunapohitaji kitoweo, inafanana sana na tabia tuliyonayo katika kutafuta utajiri. Ukifuatilia kwa undani utagudua kuwa michakato yetu ya kutafuta utajiri ni

Sunday, November 6, 2016

Tofauti ya Kuwa Tajiri na Kuonekana Tajiri Iko Hapa


“Dawa ya kutibu ugonjwa wa kujiona tajiri ni kuweka ndoto ya maisha mazuri unayoyataka kwa maandishi” ~ Cypridion Mushongi
Katika mchakato wa kutafuta utajiri kuna dhamira kuu mbili zinazotuchochea kufanya kila tunachokifanya, ili kutimiza ndoto ya kutajirika. Dhamira ya kwanza ni ile mtu anapolenga kuonekana tajiri machoni mwa watu wengine na dhamira ya pili ni