Saturday, June 13, 2020

Kama Unadhani KUTAMANI ni Kitu Kibaya Soma Hapa!





KUTAMANI ni dhana ambayo inachukuliwa kirahisi sana na pia, uelewa juu ya dhana hii ni wa kiwango cha chini.

Kutokana na hali hii, dhana hii imejengewa picha ambayo..
inatoa nafasi finyu kwa watu kuweza kujua umuhimu wa KUTAMANI katika jamii inayoendelea na iliyoendelea.

Ukweli ni kwamba dhana nzima ya KUTAMANI inahusishwa zaidi na mapenzi au kutaka vitu au mali walizonazo wengine.

Lakini ni vizuri tukumbuke kuwa hapa siongelei yule mtu aneyetamani vitu kila dakika, kila siku au kila wakati, yaani yeye hatulii kwenye kitu kimoja anatamani tu ilimradi ana uhuru wa kufanya hivyo.

Leo nataka tujifunze pamoja dhana hii ya “KUTAMANI” ikimaanisha kusudio lako katika kutaka kufanya kitu fulani ili kufikia mafanikio fulani ambayo unataka kuwa nayo maishani.

Hivyo basi dhana hii tusiichukulie kama mzaa, kwasababu kwa hali yoyote ile KUTAMANI ndiyo kusema ni kama “ZEGE” linalotumika kujenga msingi wowote wa mafanikio.

Kutokana na uelewa finyu juu ya dhana nzima ya KUTAMANI, watu wengi wameshindwa kunufaika na dhana hii ambayo kimsingi ndio chimbuko la mafanikio makubwa ya binadamu duniani kote.

Kwenye jamii yetu, wengi hawajapata fursa ya kuendeleza kipaji cha KUTAMANI ili kukitumia kama kichocheo cha wao kuweza kufanya kile wanachopenda kuwa nacho katika maisha.
 

Ukweli ni kwamba KUTAMANI ndio hasa uzaa ndoto. NDOTO tunawezakusema kuwa ndiyo mbegu au miche ya uhalisia wa kile kinachokuja kutokea hapo baadae.

Je ni kwa namna gani mtu anaweza kuvuna nguvu ya KUTAMANI?

Kila binadamu aliyefikisha umri wa kutambua kusudi la pesa katika maisha, mara zote atatamani kuzipata ~ na “mimi nazitamani”.

Lakini kumbuka kuwa KUTAMANI pesa tu haitoshi, ni lazima KUTAMANI pesa huku ukihakikisha tamanio lako linazama ndani na kuchukua nafasi kubwa ya fikra zako ndani ya ubongo au akili yako.

Halafu upange njia dhahili ya namna utakavyozipata huku ukichanganya na uvumilivu ambao hautambui kushindwa.

Zipo mbinu ambazo unaweza kupitisha TAMANIO lako likabadilika kulingana na kiasi cha pesa unachokitaka. Hapa chini kuna hatua sita kwa vitendo ambazo zinakusaidia kubadilisha kile unacho TAMANI kuwa kitu halisi chenye kuonekana kwa macho.

Kwanza; kama wewe hitaji lako ni pesa kama mimi, weka kwenye akili yako kiasi cha pesa ambacho una TAMANI kukipata. Haitoshi kusema ‘mimi nitahitaji pesa nyingi’. Inabidi kuweka bayana na dhahili kiasi unachokitaka, kwasababu kuna sababu za kisaikolojia unapokuwa dhahili juu ya kitu UNACHOTAMANI

Pili; amua ni kitu gani hasa uko tayari kutoa AU ni kwa namna gani uko tayari kujitoa ili kupata kiasi hicho cha pesa unachotamani.

Tatu; Weka tarehe ya lini unapanga kuanza kumiliki pesa hiyo unayotamani kuwa nayo

Nne; tengeneza mpango dhahili wa namna ya kutekeleza TAMANIO lako, halafu anza kuufanyia kazi mara moja na uwe tayari kutekeleza mpango wako kwa vitendo.

Tano; andika kwa ufasaha na kwa ufupi maelezo juu ya kiasi cha pesa unachotamani kuwanacho, taja tarehe unayotaka kuanza kupata pesa na pia taja ukomo wa muda hadi kumiliki hiyo pesa, eleza uko tayari kutoa nini kupata hiyo pesa, na ueleze kwa ufasaha mpango mkakati utakaotumia kupata kiasi hicho cha pesa.

Sita; Soma maelezo uliyoandika kwa sauti mara mbili kwa siku (unapoamka mapema asubuhi na muda mfupi kabla ya kulala). KADILI UTAKAVYO SOMA, jaribu KUONA, KUWA NA HISIA HUKU UKIJIAMINI KUWA TAYARI UNAMILIKI PESA hiyo unayotamani kuwa nayo.

Ukifikiria kwa undani mbinu sita hizi, utagundua kwamba suala zima la kupata pesa haliwezi kuwa suala la bahati, lazima mtu atambue kuwa wote waliofanikiwa walianza kwanza na KUTAMANI baadae wakajawa na ndoto baadae mipango ambayo uzaa matumaini na uvumilivu kabla ya kupata mafanikio waliyonayo.

Pia tunajifunza kwamba hatuwezi kupata utajiri mkubwa bila kuwa na TAMANIO la kitu unachokitaka, na ukaamini kuwa utapata kitu hicho.

“Kama huwezi kuona pesa kwenye mawazo yako basi usitegemee kuona pesa kwenye mfuko wako”. Maana yake ni kwamba pesa zote lazima uanze kuwanazo akilini mwako ndipo ziweze kuonekana kwa macho mfukoni.

Dunia hii inayoendelea kubadilika inahitaji karibu kila kitu kipya… inahitaji mawazo mapya, njia mpya za kufanyakazi, viongozi wapya, mbinu mpya za kuuza vitu tulivyonavyo, vitabu vipya n.k. 

Pamoja na mahitaji ya vitu vipya katika dunia ya sasa bado kila mmoja anayejiandaa kushiriki mashindano atatakiwa kuwa na kitu kimoja muhimu ambacho ni KUSUDI LA MAISHA LILILO DHAHILI. 

Katika mazingira haya ya dunia hii iliyobadilika, tunahitaji waota ndoto ambao wataweza kuweka ndoto zao katika vitendo kwa maana ya kuchukua hatua za maksudi. 

Lakini uvumilivu na kuwa na akili iliyofunguka vitakuwa ni nyenzo muhimu sana kwa wale wote wenye ndoto za kupata utajiri na mafanikio mengine.

KUTAMANI ndiyo hasa uongoza mwelekeo wa maisha yako. Watu wengi wamekuwa wakikata tamaa katika maisha, kwasababu huwa hawana TAMANIO na kitu chochote akilini mwao. 

Ni lazima useme “hivi ndivyo ninavyotaka kuwa”. Lazima huwe na TAMANIO ambalo unataka sana kulitimiza kwa gharama yoyote.

Unapojipanga leo kupata gawio lako la utajiri, kamwe hasiwepo mtu wa kukushawishi au kukukejeli na kukudharau kwa ndoto uliyonayo. 

Kupata ushindi kwa kupata gawio lako kubwa kutoka katika dunia hii iliyobadilika, ni muhimu kujitahidi kuwa na roho kama ya watu wale wa zamani walioanzisha vitu amabavyo tunavitumia hadi leo.

Hapa tujikumbushe tu mtu mashuhuli aliyejulikana kama Christopher Columbus, huyu bwana alifanikiwa kugundua dunia ambayo ilikuwa haijulikani (America ya Kusini). 

Mtu mwingine aliitwa Bw. Copernicus (mtaalamu wa unajimu/masuala ya anga). Bwana MARCONI yeye kwakutumia sumaku aliweza kugundua nguvu ya umeme utokanao na sumaku ambao ndio uliozaa vitu kama RADIO na RUNINGA tunavyoviona hadi leo hii.

Kwahiyo mpendwa msomaji wa MAARIFASHOP, kama unawaza kufanya kitu na unaamini kuwa ni kitu sahihi basi endelea kukifanya, bila kujali watu wengine wanasema nini.

Kama hauko tayari kufanya hivyo, tayari ujue kuwa umeishapoteza, kwasababu ni “TAMANIO” lako ndilo litaendelea kukuchochea na kukuwezesha wewe kuendelea na safari yako ya kuelekea kwenye mafanikio bila kuchoka.

Ili upate kile unachotaka kuwanacho, lazima huwe na shauku ya kukipata. Lazima kuwa na TAMANIO ambalo una shauku nalo bila kujali gharama zake.

Unapotafuta kitu jitahidi kuwa na TAMANIO na hicho unachotafuta. Kataa kukatizwakatizwa. Nguvu ya uwezo wako itaachiwa kadiri utakavyozidi kujitoa kwa kila hali katika kufikia kile UNACHOTAMANI kupata.

Kwahiyo, kabla ya mambo yote unayofanya, amua sasa KUTAMANI na ndani ya akili yako washa moto wa matumaini, imani, ujasiri, na uvumilivu ukiongeza na elimu juu ya hicho unachotaka kukifanya megine yatajileta. 

Katika kujifunza namna ya kubadili TAMANIO lako kuwa mafanikio unayoyataka, bonyeza neno MAARIFA SHOP; ili kusajili barua pepe (e-mail) yako ambapo utaendelea kupata ujuzi na maarifa yatakayo kuwezesha kupata mafanikio makubwa. 

Kupata mafunzo kila siku kwa njia ya whasap bonyeza neno MAFUNZO

2 comments:

salimmsangi.blogspot.com said...

Kaka unakuwa kimya sana..!! Ndugu zako bado tuna uhitaj sana na taarifa uliyonayo

Masele kwiligwa Self Development Blog said...

kaka umepotea sana tunahamu na maarifa