Monday, July 20, 2020

Motisha wa Kazi nani Anapaswa Kutoa?




Baada ya mapinduzi ya viwanda uko barani Ulaya mwishoni mwa karne ya 18, iliibuka na kujengeka dhana nzima ya kuajiriwa. 
Dhana hii ilikua kutokana na ukweli kwamba viwanda wakati huo vilihitaji sana nguvu kazi. Mabepari waliomiliki vitegauchumi walihitaji sana wafanyakazi, ili kuweza kuzalisha bidhaa na huduma mbalimbali. 

Kwa mtu ambaye amekulia kwenye ajira kila wakati akikasirika au akapata changamoto, katika fikra zake anakuwa anajua kuna bosi mkuu ambaye atamuonea huruma na wakati mwingine kumtia moyo….Hali hii iliendelea na hatimaye ikasambaa duniani kote hadi huku kwetu Tanzania. 

Dhana hii imekua kiasi kwamba hata wale waliojiajiri nao pia wanataka mtu wa kuwatia moyo, wanataka mtu wa kuwapa MOTISHA. 

Kila mtu anatafuta mtu wa kumtia moyo na akimkosa anakasirika matokeo yake anakata tamaa kwa jambo hilo alilokuwa analifanya. 

Dunia ya sasa imejaa watu ambao wanasubili mtu fulani aje kuwapa motisha ili kufanya kile wanachotaka kukifanya au wapate mafanikio wanayo tamani kuyapata. 

Habari mbaya ni kwamba “hakuna mtu yeyote wa namna hiyo ambaye anakuja kufanya kazi hiyo”. Ni asilimia 2% tu ya watu ambao wanaweza kufanya mambo yao bila kuhitaji usimamizi. Watu hawa tunawaita viongozi. Na wewe umeumbwa kuwa huyo mtu. 

Kwahiyo hivi sasa, watu ambao ni adimu ni wale walio tayari kujimotisha wenyewe. Utakapoweza kujimotisha mwenyewe, utaanza kuona wengine wakikufuata kwasababu utaanza kuonekana mtu wa tofauti lakini mwenye thamani. 

Katika KUJIMOTISHA mwenyewe simaanishi kucheza dansi bali namaanisha KUJIMOTISHA huku ukitengeneza thamani (zalisha bidhaa na huduma). 

Kwahiyo, wakianza tu kukufuata maana yake wanafuata na ile thamani unayozalisha na wewe hapo unakuwa na kazi moja tu! “kuwapa bill”. 

Ni kwa namna gani nitaweza kujipa motisha? 
Ili kuhakikisha unajipa motisha wewe mwenyewe lazima ukate shauli ya kufanya yafuatayo: 

Weka malengo: Yawe yanapimika na kutekelezeka. Njia nzuri ni kuwa na malengo ya muda mrefu (miaka 10 na kuendelea), muda wakati (miaka 3-5), na muda mfupi 

Badili mtazamo juu ya kushindwa: Chukulia kushindwa kama njia ya kuelekea mafanikio: tambua kuwa kushindwa kunatoa mafunzo muhimu ya namna gani usahihishe mipango, mikakati na namna nzima ya kujipanga, ili kufikia mafanikio tarajiwa. 

Kushindwa kufanikiwa kunakupa fursa ya kubaini na hatimaye kukupa ni hatua gani uchukue ili kupata matokeo chanya. 

Soma vitabu: Soma vitabu vya waliofanikiwa. Utagundua kuwa changamoto unazopitia ni marudio kuna watu wengine walishapitia na wakapata suruhisho na wameandika walivyotatua changamoto zao 

Kuwa karibu na uwapendao: Tumia sehemu ya muda wako na wale uwapendao; kumbuka usemi usemao kuwa “fanya kazi ili kuishi na siyo kuishi ili ufanye kazi” 

Shauku juu ya kazi: Shauku inakufanya kuwa na MOTISHA ulio juu muda wote. 

Fanya tafakari na mazoezi: Tafakari inaleta maelewano na amani kichwani. Mazoezi pia, yatakusaidia kuwa na nguvu muda wote na ubunifu. Kwa maneno mengine tenga muda kwaajili ya afya na hili litakulipa sana huko mbeleni. 

Anza leo maisha ya KUJIMOTISHA yanalipa sana kwa watu wote wenye KAZI na walioko kwenye AJIRA. 

Endelea kutumia maarifa kutoka MAARIFASHOP ili kujenga na kukuza uwezo wako wa KUJIMOTISHA. Kama unapenda kupata makala kila zinapochapishwa bonyeza kiungo hiki; TUMA MAKALA kisha sajiri barua pepe yako. 

Na pia unaweza kujiunga na kundi la WHATSAP kwa kubonyeza MAFUNZO, ili kupata mafunzo ya kila siku na pale makala zinapochapishwa.

No comments: