Tuesday, July 28, 2020

Faida ya Kufanyakazi Bure ni Hii Hapa

“Tembo pamoja na kuwa myama mkubwa hang’ati LAKINI mbu anang’ata”~ Darren Hardy

Unaanzaje kufanyakazi bure bila malipo yoyote?; katika hali ya sasa ambayo watu wengi tayali ni waumini wa mfumo wa pesa taslim au mfumo wa nipe nikupe. Hivi sasa watu wengi wanajitahidi kufanya vitu vitakavyowaletea pesa haraka (chapuchapu). Kiashiria mojawapo cha watu kupenda malipo ya chapuchapu ni uwepo wa watu wengi wanaofanya shughuli za kuchuuza bidhaa ~ inakuhakishia kupata pesa za chapuchapu. 

Kundi la wachuuzi wa bidhaa linapanga kulipwa kwa kufuata vigezo vya waajiriwa katika sekta ya umma na binafsi. 

Ndiyo maana waangalia zimeingia shilingi ngapi mwisho wa siku/wiki au mwezi; na endapo pesa inayoingia kwa siku/wiki/mwezi ni ndogo basi haraka haraka mtu anasema biashara hii hailipi. 

Mtu huyu anasema biashara hailipi kwasababu wengi wanapima biashara zao kwakufuata mtazamo wa “fanyakazi leo na lipwa leo”. 

Watu wenye mtazamo wa namna hii ni vigumu kuelewa dhana ya “KUFANYAKAZI BURE”~ waliofanikiwa ni wale wenye mtazamo huu wa kufanyakazi bure. 

Unaposikia habari ya KUFANYAKAZI BURE sijui unaipokeaje, yewezekana sasa unajisemea kuwa haiwezekani kufanya kitu kama hicho; pengine unajiuliza ikiwa nitafanyakazi bure, nani atanilipa? 

Bilashaka umewahi kusikia watu Fulani wakilalamika kuwa “mimi naharibu muda wangu kufanya jambo fulani” ukisikia hivyo ujue kuwa huyo tayari anaumia sana kuona anafanyakazi yote hiyo bila kulipwa chochote. 

Watu wanaofanya biashara wakiwa na mtazamo wa kulipwa kwa siku/wiki/mwezi, mara nyingi ujikuta wakibadilisha biashara zao kila baada ya muda mfupi na hivyo kukosa fursa ya kufanikiwa. 

Je? Kufanya kazi bure maana yake ni nini? 
Kufanyakazi bure haimaanishi wewe utakuwa unafanyakazi bila ya kuingiza chochote HAPANA; hapa ninamaanisha kwamba unakuwa ni mtu wa kuzama katika kufanya kitu fulani kwa muda Fulani hata bila kujali kama pesa inaingia wakati huo au la! 

Kwa maana nyingine ni kwamba unafanya kazi leo haulipwi chochote mpaka siku ambayo matokeo ya kazi yako (thamani) yataanza kuonekana na hapo ndipo watu watakuletea pesa ili kubadilishana na thamani ya hicho ambacho umekuwa ukikifanya. 

Uzuri ni kwamba ukianza kupata mapato hata hizo siku ambazo hukuwahi kulipwa zote utalipwa na itafikia wakati kila ukifanya kidogo tu unalipwa kikubwa lakini mwanzoni ulikuwa ukifanya kikubwa unalipwa kidogo sana. 

KUFANYAKAZI BURE maana yake ni kufanyakazi kwa kipindi Fulani bila kulipwa mpaka hapo matokeo yaliyotarajiwa au kulengwa yatakapopatikana. 

Kwa maneno mengine ninawezakusema kuwa biashara ya KUFANYAKAZI BURE ni biashara ambayo inafanyika kwa kulenga mbali au inafanyika kwa malengo ya muda mrefu, siyo ya kukurupuka umepata au umekosa maisha yanaenda. Biashara hii ya KUFANYAKAZI BURE ni Mpangokazi wa kuanzia miaka 2 - 5 na kuendelea. 

Ni biashara ambayo unajikita katika kufanya shughuli ndogo ndogo kwa kila siku ilimradi ziwe zinachangia chochote katika lengo kuu. 

Mwandishi Darren Hardy katika kitabu chake cha “The compound effect” anasema “Tembo huwa hang’ati pamoja kwamba ni myama mkubwa LAKINI mbu anang’ata” akimaanisha kwamba mambo madogomadogo tunayofanya kila siku ndiyo yanajikusanya na kuleta mafanikio tuliyoyalega kwenye mpangokazi wetu wa miaka 2-5. 

KUFANYAKAZI BURE kunatufundisha umuhimu wa kupenda kazi unayofanya, kujimotisha mwenyewe, na pia nafsi yako inaanza kulidhishwa na vitu zaidi ya pesa…..LAKINI kikubwa ni kujenga tabia ya kusubili malipo, huku ukizidi kufanyakazi kwa juhudi na maarifa. 

Kuvumilia bila kulipwa mpaka hapo matokeo chanya yatakapopatikana ndiyo nguzo kuu kwa mjasiriamali wa kweli. 

Kila juhudi utakayoiweka kwenye biashara itakulipa pesa siku za mbeleni na siyo siku hihiyo. Ili upate mafanikio endelevu lazima ufikie hatua hii ya KUFANYAKAZI BURE. 

Watu wengi ukiwambia umuhimu wa KUFANYAKAZI BURE wanakushangaa wakidhani wewe haupendi pesa, wasijue kuwa pesa nyingi inawasubili wale waliotayari KUFANYAKAZI BURE-waliofanikiwa kwenye biashara ya mtandao wanalielewa sana hili. 

Unashangaa KUFANYAKAZI BURE kwasababu umekulia katika mazingira ya wanaojali zaidi mapato ya leo leo; ndiyo maana ndoto na mipango yako vyote ni vya muda mfupi na havina mwendelezo wa mwaka hadi mwaka. 

Kazi unayofanya leo haina uhusino na kile utakachokifanya kesho, unakuwa mtu wa maisha ya kazi za kukatishakatisha na ndiyo maana unaungana na watu wa kutesa kwa zamu – sisi tunaelekea kuingia kundi la kutesa siku zote. 

Chukua hatua kila siku kujenga biashara yako, huku ukizidi kutambua kuwa “ROMA haikujengwa kwa siku moja” ukiamua kufanya biashara Fulani, jitahidi uifanye kila siku hadi kufikia miaka miwili au zaidi kabla ya kuacha au kuanza kuwa na mashaka. 

Unapoendelea kujenga tabia ya KUFANYAKAZI BURE ukumbuke kuwa vitu vizuri vyote vinachukua muda hadi kufanikiwa. 

Endelea kupata elimu kutoka MAARIFASHOP ili kujenga na kukuza uwezo wako wa kusubili matunda ya kazi yako yafike. Kama unapenda kupata makala kila zinapochapishwa bonyeza kiungo hiki; TUMA MAKALA kisha sajiri barua pepe yako. 

Pia, unaweza kujiunga na kundi la WHATSAP kwa kubonyeza MAFUNZO, ili kupata mafunzo ya kila siku na pale makala zinapochapishwa. 

No comments: