Thursday, December 31, 2020

Mwaka 2020 Unaisha leo Mwaka Mpya 2021 ni Kesho Unajisikiaje?

"Pale unapohisi ni mwisho mara nyingi ndio mwanzo wa kitu kipya" ~ CYPRIDION MUSHONGI


Napenda kutoa shukrani zangu kwako, hii ni kutokana na ukweli kwamba wewe binafsi umekuwa pamoja na mimi na MAARIFSHOP kwa ujumla. Hakika tumekua na kuishi kwenye jumuia moja kama siyo kabila moja linaloitwa.. MAARIFASHOP.

Wakati huu tunapoelekea kufika ukingoni mwa mwaka 2020, napenda kukukumbusha kwamba njia ya mafanikio imejaa jasho na vumbi.

Kutokana na jasho na vumbi hili katika njia yetu hii ya mafanikio inatupasa kuzingatia utamaduni wa kupenda kufanyakazi kwa juhudi kubwa na maarifa, ubunifu na kujituma.

Ni rahisi sana kutupia wenzako lawama kwasababu zenyewe ni tamu kutoka mdomoni, lakini peke yake hazitapeleka mkono kinywani badala yake zitazidi kukatisha tamaa wale ambao pengine wangekusaidia katika safari yako. 

Ni vizuri sana kuhakikisha kuwa linapojitokeza jambo lolote ambalo ni hasi kuwa mvumilivu kidogo ili upate kutafakari ili kutambua wewe katika hilo lililotokea umechangia kiasi gani. 

Ukishajua mchango wako kwenye tatitzo lililopo hakika wale wahusika wengine utaweza kuwatendea haki kwa kuwapa au kuwalaumu kwa kile kiwango halisi walichochangia kwenye kusababisha tatizo.

Katika kujituma kila mtafuta mafanikio akumbuke kuwa LA muhimu si muda anaoutumia kufanyakazi bali ni kiasi cha kazi anayoweza kuifanya kazi katika muda uliopangwa.

Mwaka 2021 unakaribia, jitahidi usipanic kama ulipanga kufanya kitu fulani mwaka huu wa 2020 na hakijakamilika, hakikisha mwaka mpya ukianza endelea kufanya hicho hicho mpaka kitakapokamilika.

Ili kuondoa panic ya kila mwaka, jitahidi kuwa na mipango ya muda mrefu MF. Miaka 10 na kuendelea. 

Kwa wale ambao hawana mipango ya muda mlefu, mwaka ujao wa 2021 ni muhafaka kuwa na malengo ya mika 10 ijayo yaani 2021-2030.

Kama nilivyosema kwenye salaam zangu Christmas, wengi wanatumia mwaka mpya kutangaza biashara zao na hivyo kukuweka kwenye panic kiasi cha kukufanya ujione umechelewa!!..

..Nasema hapana kwani wewe bado ni yuleyule mpenda mafanikio na ndoto yako ndiyo itatakiwa ikutie hamasa. 

MAARIFASHOP itaendelea kuwepo mwaka kesho 2021, ili kujenga na kukuza uwezo wako wa kutafuta mafanikio kwa kupata makala mpya kila zinapochapishwa bonyeza kiungo hiki sasa hivi; NITUMIE MAKALA .

Pia jiunge na WHATSAP kupata MAFUNZO ya kila siku. 

NAKUTAKIA HERI YA MWAKA MPYA 2021, GOODBYE 2020 TUKUTANE MWAKA KESHO







No comments: