“Watu wengi wanatumia pesa walizopata..kununua vitu wasivyovihitaji..kufurahisha watu wasiowapenda” ~ Will Rogers
Mojawapo ya nguzo muhimu katika kupata maisha mazuri ni pesa ya kutosha kumudu gharama za maisha ya kila siku. Zaidi ya hilo, ni kwamba mafanikio binafsi ya kifedha ni chachu ya mafanikio ya aina nyinginezo. Lakini...
pesa ya kutosha haiwezi kupatikana eti kwasababu sisi ni wataalamu na wasomi wa fani mbalimbali. Suala la upatikanaji wa pesa ya kutosha ni pana sana, na siyo suala la kukurupuka. Tunahitaji kupata kwanza elimu juu ya fedha. Uhakika wa kupata pesa nyingi na endelevu, utakuwepo endapo tutafahamu na kuelewa kwanza lugha na maneno muhimu ya pesa.
Mambo mengi yasiyojulikana, ujulikana kwa urahisi na haraka zaidi pale tunapojifunza kwanza lugha na maneno yanayohusu kile tunachotaka kukifahamu na hatimaye kukifanyia kazi. Ndiyo maana, tulipoanza tu shule ya msingi, kitu cha kwanza kufundishwa ilikuwa ni jinsi ya kuandika na kusoma maneno. Baadae tulipozidi kukua, lugha na maneno vilitengwa katika makundi (masomo) kama vile jiografia, sayansi, hesabu, historia n.k. Kila kundi hapa lilikuwa na misamiati ya pekee ambayo ni nadra sana kupatikana kwenye kundi linguine. Kwahiyo, kama uliweza kufahuru masomo fulani fulani, basi ujue kuwa ufahuru huo ulitokana na wewe kuelewa vema maneno na misamiati ya masomo hayo.
Ukweli ni kwamba kila kitu unachopanga kufanya maishani kina lugha yake. Ndiyo maana kama ulikuwa unapanga kufanya kazi nchini Ujerumani, itakuwa vizuri kwanza ukijifunza kijerumani, kama unataka kujifunza uinjinia lazima utahitajika kujifunza kwanza lugha ya kihandisi au usanifu wa majengo n.k. Vivyo hivyo, ili tuweze kufanikiwa kupata uhuru wa kipato (pesa), lazima kwanza tuweke mkazo zaidi kwenye kujifunza lugha na maneno ya pesa. Kunahitajika kuweka mpango endelevu wa kujifunza kila siku, mpango ambao utatupa fursa ya kufahamu mambo mapya na ya kisasa yanayoendelea kutokea ndani ya ulimwengu wa pesa.
Habari mbaya ni kwamba mpaka dakika hii, lugha na maneno muhimu ya pesa havifundishwi mashuleni kwa kiwango cha kuweza kumsaidia mtu kupata utajiri. Ni ukweli usiopingika kuwa maneno mengi tuliyojifunza shuleni ni muhimu, lakini hayana uwezo wa kutuandaa kuwa na uhuru wa kipato au “pesa ya kutosha”.
Je kuna umuhimu wa kujifunza misamiati na maneno ya pesa?
Niseme kwamba kuna umuhimu mkubwa sana kwetu sisi wote kujifunza kwa undani maneno ya pesa, hasa kwa wale ambao tunaishi maisha ambayo hatuyapendi kwasasa. Sababu mojawapo za kujifunza maneno ya pesa ni kwamba, maneno yanabeba uhalisia na uhai kwenye ubongo wetu na ni nyenzo yenye nguvu kwa binadamu.
Maneno ya pesa ni nyenzo ambazo unifanya niwe tajiri, nyenzo ambazo unifanya kuingiza pesa bila kuwa na pesa yoyote. Pia, maneno kama nyenzo ya ubongo, ndiyo yanaruhusu ubongo wako uweze kuona “kile ambacho macho hayawezi kuona”. Kwa maana nyingine ni kwamba maneno ya pesa yanakusaidia kuona picha ya maisha mazuri.
Picha nzuri ya maisha ndiyo ukuongezea msukumo wa ndani wa kutafuta utajiri. Ndiyo maana tunasema kuwa makini sana na maneno ya pesa unayoyatumia kila siku. Kama ilivyo kawaida kuna maneno ambayo yatakufanya uwe tajiri, na kuna maneno yatakufanya uwe maskini.
Maneno ya pesa ni kama yapi?
Maisha yetu ya pesa yanaundwa na vitu viwili ambavyo ni pesa kuingia na kutoka. Kila siku, wiki, mwezi na mwaka kuna pesa nyingi imeingia na kutoka kwako!. Pesa inapoingia mfukoni kuna kitu fulani ambacho usababisha ije na kutoka ni hivyo hivyo, kuna kitu fulani kinasababisha pesa yako itoke mfukoni.
Kwahiyo, inatosha kusema kuwa kuna maneno kama “VIINGIZA-PESA" na “VITOA-PESA”. Tayari haya ni maneno mawili muhimu sana kuyajua na kuyaelewa kwa undani kama kweli unataka kupata uhuru wa kipato (utajiri).
Kwa wahasibu na wale wote ambao mna akaunti kwenye mabenki, mtakumbuka kuwa kuna kitu kinaitwa “taarifa ya mapato na matumizi”. Taarifa hii huwa inakuonyesha wewe mwenye akaunti benki kiasi cha pesa iliyoingia (mapato) na iliyotoka (matumizi). Taarifa hii maana yake ni kwamba, pindi upatapo pesa, kinachofuatia huwa ni kutumia pesa japo wengine wachache uzitunza kwanza kwa muda.
Hapa kwenye kutumia pesa ndipo watu wengi utofautiana sana na hapa ndipo kilipo kiwanda cha kuzalisha watu wengi wasiokuwa nacho (maskini). Katika kutumia pesa, kuna watu ama wanatumia pesa yao kununua “viingiza pesa” au wanatumia pesa kununua “Vichukua pesa”.
Jaribu kujiuliza wewe kwanza pesa yako yote unayopata kila mwezi, ni pesa kiasi gani inatumika kununua “viingiza pesa”? na ni kiasi gani cha pesa kinatumika kununua “vichukua pesa”? Uwezo wa kujiuliza na kujibu maswali hayo yote utakuwa nao kwasababu tayari umeanza kujifunza lugha na maneno mpya ya pesa.
Kama nilivyotangulia kusema hapo juu ni kwamba, pesa ina lugha yake na katika lugha hii kuna maneno mengi ambayo unahitaji kuyajua na kuyafahamu uhalisia wake. Lakini leo nitagusia kidogo maneno mawili muhimu ya pesa, yaani “Viingiza-Pesa” na “Vitoa-Pesa”.
Viingiza-Pesa” na “Vitoa-Pesa Ndio Nini?

Viingiza-Pesa: Hivi ni vitu vyote unavyovifanya na matokeo yake vinakuingizia pesa mfukoni. Viingiza-pesa vimegawanyika katika makundi makubwa manne kama ifuatavyo:
Kundi la kwanza ni biashara: Biashara ni kundi mojawapo la “viingiza-pesa” mfukoni. Na hapa ziko aina nyingi za biashara kulingana na chaguo lako. Tunapoongelea biashara siyo lazima iwe ile ya kununua vitu kwa bei ya chini na kuuza kwa bei ya juu BALI ni zaidi ya hapo.
Hapa tunaongelea hali yoyote ile ambayo unaweza ukaunganisha nguvu, nyenzo na vitu mbalimbali, kutengeneza mfumo wa uzalishaji wa bidhaa/huduma ambao utatiririsha pesa nyingi mfukoni mwako zaidi ya ile uliyowekeza awali.
Kama kawaida, biashara nayo ina lugha yake, na hapa unahitajika kujifunza lugha mbalimbali za biashara ikiwemo sheria, mahesabu, uhandisi, masoko, kuuza, uongozi, mtandao n.k. siyo lazima ubobee kama wataalam lakini angalau ujue vile vitu vya msingi basi. Kikubwa ni kufahamu lugha zipi zinahitajika kwenye kuendesha biashara yako. Mambo yatakayohitaji undani zaidi, ni rahisi kukodi wataalam waliobobea kwenye fani hizo.
Kundi la pili ni majumba/viwanja: Majumba na viwanja ni kundi la pili la “viingiza-pesa”. Kundi hili nalo lina faida, lakini pia lina changamoto zake. Miradi mingi ya majumba na viwanja inategemea zaidi mikopo ya mabenki na serikali, na kwa maana hiyo, tunaweza kusema kuwa miradi hii inaendeshwa kwa “madeni”. Madeni nayo yana lugha yake. Miradi ya majumba na viwanja inahitaji zaidi kujifunza lugha ya manejimenti ya majengo na mahusiano na watu.
Kundi la tatu ni hisa/hatifungani: Hili ni kundi la “viingiza-pesa” kwa watu wengi. Kupitia hisa au hatifungani, pesa inaingia bila wewe kuwa umefanya kazi. Kazi yako iliisha siku ile ulipokwenda kununua hisa. Ni rahisi kuwekeza kwenye hisa na hatifungani japo kuwa kunahitajika elimu ya fedha na maneno ya pesa, ili kuweza kupata faida kupitia uwekezaji huu.
Kundi la nne bidhaa za thamani: Hizi ni zile bidhaa zinazohusisha vitu kama madini ya dhahabu na fedha, makaa ya mawe, mafuta na chakula (mf: sukari, mahindi, mchele, maharage, nyama n.k). Kumbuka kuwa kila bidhaa hapa ina lugha yake. Kuna unafuu sana wa kodi kwa bidhaa hizi na hasa mafuta na chakula. Kwakuwa serikali inaendelea kuchapisha pesa, hivyo ni vizuri ukatunza pesa yako kwenye dhahabu na fedha kuliko pesa ambayo kiukweli siyo halisi ni makaratasi
Vitoa-pesa: Hivi ni vile vitu vyote vinavyotoa pesa yako mfukoni; mfano, mkopo wa elimu, gari la kutembelea, samani za nyumbani, nyumba yako ya kuishi n.k. Hivi vyote kila mara uchukua kiasi fulani cha pesa kutoka mfukoni mwako. Watu wengi tunanunua sana vitu hivi na tunatumia gharama kubwa kuvinunua na kuvitunza. Kwa maana nyingine ni kwamba watu wengi wananunua vitu vinavyowagharimu pesa.
Ukipata pesa na ukaamua kujenga nyumba ya kupangisha, ni wazi kwamba pesa itatoka mfukoni mwako lakini gharama za kutunza nyumba hiyo (mf: kodi, ukarabati n.k.), hazitakaa zitoke tena mfukoni mwako, badala yake zitalipwa kutoka kwa wapangaji. Kwahiyo, hivi ndivyo utajiri utiririka kuja kwako. Lakini kama wewe ni mjasiriamali makini.
Nitaanzaje kujifunza maneno ya pesa?
Kitu kitakacho kuchochea wewe kuaza kujifunza maneno na misamiati ya pesa ni “malengo na ndoto ya kutajirika”, vikiambatana na mpango mkakati wa kutajirika. Ni katika kutekeleza mpango huu ndipo utapata motisha, shauku na msukumo wa ndani wa wewe kujifunza maneno mapya ya pesa, elimu ya ujasiriamali, uwekezaji na fedha kwa ujumla. Pia utajifunza uzoefu unaotakiwa na mbinu madhubuti za kuweza kufikia uhuru wa kipato haraka.
Kwahiyo, jaribu kuwekeza muda kwa kuanza kuchagua mkakati wa kutoka kwenye hali ya maisha ambayo huyapendi kwa sasa na kisha anza kubuni na kutengeneza mpango wako binafsi ambao utahusisha elimu ya pesa, uzoefu, na misamiati au maneno; vyote ambavyo vinahitajika kwa wale wote tulioamua kutafuta uhuru wa kipato ili kuishi maisha mazuri.
Kwahiyo nifanye nini sasa?
Ni vyema sana ukazidi kufahamu kwa undani dhana hii ya pesa “kuingia na kutoka” kwako. Kwani siri kubwa ya kutajirika au kuwa masikini utaijua vyema endapo utaamua leo kuanza kujifunza lugha ya pesa kwa kuanza na maneno kama “kuingia na kutoka” kwa pesa mfukoni.
Upatikanaji wa uhuru wa kipato kwa mtu binafsi utategemea zaidi kasi yako ya kujifunza maneno yote muhimu ya pesa. Maneno ambayo yatakufanya wewe kupata vyema picha halisi ya pesa, na hivyo kukurahisisha upatikanaji wake tofauti na ilivyo sasa.
Kupitia kuyajua vizuri maneno ya pesa ambayo yanagusa ukweli na uhalisia wa maisha, ni rahisi wewe kuanza kupata mawazo mazuri ambayo yatakujengea tabia na uwezo wa kununua zaidi “viingiza-pesa” kuliko “vichukua pesa”. Na kwa kufanya hivyo, utakuwa umeruhusu pesa nyingi kuingia kwako kuliko ile inayotoka kuelekea kwa watu wengine.
Maisha mazuri yanayoambatana na uhuru wa kipato, vyote vinawezekana endapo utaamua kwa dhati kuanza leo safari yako ya matumaini kuelekea kwenye utajiri. Endelea kujitahidi kusoma makala mbalimbali hasa zinazopatikana hapa MAARIFA SHOP. Waweza pia kuwa karibu na blog hii kwa kubonyeza “NAJIUNGA” ili kujipatia makala nzuri moja kwa moja kupitia barua pepe yako.

No comments:
Post a Comment