Thursday, October 6, 2016

Utaweza Kuondoa Chuki na Hasira Ulizonazo Kwa Njia Hii


“Nimeamua kujikita kwenye UPENDO...Chuki ni mzigo mkubwa sana kuubeba” ~ Martin Luther King Jr.
Unapoona watu wanatembea, wanaongea na wanacheka, usidhani wengi wana furaha ya dhati. Ukweli ni kwamba watu wengi wana chuki, hasira, kinyogo na kero nyingi ndani yao. Kubwa zaidi ya yote ni kwamba..
muda mwingi hawana furaha. 

Hali hii ya watu kukaa muda mrefu bila kuwa na furaha, inatufanya kukosa msukumo na uwezo wa kufanya kazi kwa bidii na maarifa. Matokeo yake wanapata magonjwa na umaskini usioisha. Chanzo cha chuki na hasira miongoni mwetu ni kutokana na uwepo wa hisia hasi au mtazamo hasi ndani ya fikra zetu. 

Kimsingi kuna aina nne zinazosababisha hisia hasi au mtazamo hasi. Katika kitabu cha “In Search of the Miraculous: Fragments of an Unknown Teaching” cha Bwana Peter Ouspensky kutoka Urusi anasema kwamba, vyanzo vya mitazamo hasi ni pamoja na 1. Kuhalalisha matendo; 2. kujitambulisha binafsi au kujishikiza; 3. Kujari sana wanavyokuchukulia watu wengine; 4. Kulaumu watu wengine. 

Mpendwa msomaji wa MAARIFASHOP leo nitakushirikisha ili uweze kufahamu na kuelewa tabia ya “kuhalalisha matendo” ni kitu gani na unaweza kufanya nini ili kuondokana na kisababishi hiki cha mtazamo na hisia hasi ulizonazo hivi sasa kwenye maisha yako. 

Kuhalalisha matendo ni mojawapo ya kisababishi kikubwa cha chuki na hasira kwa watu walio wengi. Kitendo cha kuhalalisha matendo ni kama vile ambavyo huwa unafanya pale unapokuwa na visingizio au kutengeneza sababu ya hasira yako. Unajiambia wewe mwenyewe na watu wote wanaokusikiliza jinsi ambavyo hujatendewa haki. Wakati mwingine unajiambia jinsi ambavyo umetendewa vibaya sana au jinsi ambavyo watu wengine walivyofanya mambo ambayo hayakuwa ya kistaarabu/kiungwana. 

Kwahiyo,unaendelea kurudiarudia hali ile iliyotokea ndani ya akiri yako. Unarudia sababu zote zilizokufanya ujisikie vibaya. Kila mara unapojaribu kufikiri juu ya mtu yule unayesema amekutendea vibaya, ghafla unakasirika. Unajisikia na kujiona kama vile unastahili kuwa na hasira; unajiona kana kwamba jambo hili limekughalimu sana, na wewe katika kukadiria kwako unajiona ulikuwa mtu mzuri au muungwana sana. 

Je nitaondoaje tabia ya kuhalalisha matendo? Unaweza kuondokana na tabia ya kuhalalisha matendo na kuhakikisha unakataa kujihusisha nayo: 

1. Acha kuhalalisha matendo: Unapoacha “kuhalalisha matendo” maana yake ni kwamba, unatumia vizuri akiri yako kufikiri sababu halisi iliyotokea, na siyo kuhalarisha hisia hasi au hasira zako.
  Kumbuka kuwa hasira na hisia hasi, hazikufanyii jabo lolote jema, badala yake zinakuharibu kabisa. Hisia hasi na hasira, hazimdhuru mtu mwingine na wala hazibadili hali iliyopo au iliyojitokeza, BADALA yake zinadhohofisha furaha yako, zinapupunguza uwezo wako wa kujiamini. Kitendo cha wewe kuwa mnyonge na dhaifu kinakufanya kuwa na ufanisi kidogo sana katika utendaji wako wa kazi au nyanja zingine za maisha. 

Badala ya kuhalalisha hasira na hali yako ya kutokuwa na furaha, unatakiwa kutumia uwezo wako wa kufikiri na kupiga picha ndani ya akiri; Ili kuondoa lawama kwa mtu mwingine, au kuachana na hali ile ya kuchukia au kutokuwa na furaha. 

Kwa mfano: ukiwa unaendesha gari na ghafla mtu akakuingilia upande wako barabarani, badala ya kuchukia na kuwa na hasira, unatakiwa kusema, “haina shida ninatakiwa kuwa mwangalifu sana siku nyingine”, “ninadhani siku ya leo siyo nzuri kwake” au “lazima atakuwa anawahi ahadi muhimu kwake”. 

2. Ondoa lawama kwa watu wengine: Kwakuwa akiri ya binadamu inao uwezo wa kushikiria jambo moja baada ya lingine, ni kwamba kadili utakavyoanza kuondoa lawama kwa watu wengine ndivyo utakavyoanza kupunguza nguvu au mafuta ambayo hisia za hasira na chuki uzihitaji ili kuendelea kuwepo na kufukuta. 

Unarudisha uwezo wa kujihami. Unajiweka mpole na kujipa mtazamo chanya. Baada ya muda mfupi, hali hii ya sintofahamu huweza kupita na wewe kusahau yote yaliyotokea. Kwa kubadilisha fikra hasi, maana yake unaziondoa kabisa hisia zako hasi hata kama ni kubwa kiasi gani. 

Kama unayo matatizo makubwa kimaisha, kama vile mambo ya taraka na mkeo, kupoteza kazi au hasara kutokana na uwekezaji ulioufanya, njia ile ile ya kudhibiti hasira na chuki utumika. Acha kujiambia wewe na mtu mwingine yeyote anayekusikiliza kuhusu kwanini unastahili kuchukia au kutokuwa na furaha. 

Ondoa lawama kwa watu wengine kila mara unapofikiria hali fulani inayokunyima raha mpaka ile hali hasi ipotee. Pindi ule moto wa kuwa hasi unapoisha au kupungua, sasa unaweza kuelekeza nguvu yako kwa kitu kingine ambacho ni chanya. 

Kanuni mojawapo muhimu ya mafanikio na furaha ni “usiwe na hasira au kuwa na wasiwasi wala kuhofia kitu chochote ambacho huna uwezo wa kukibadilisha au huwezi kufanya chochote juu yake”. Usirumbane na kumlaumu mtu yeyote kwa kitu ambacho hana uwezo wa kukibadili. Sheria maarufu inasema kwamba, “Kama hakuna suruhisho, hakuna tatizo”
  3. Usiwekeze nguvu yako kwa mambo yaliyopita: Katika maisha huwa kuna vipindi viwili muhimu, yaani kipindi kilichopita na kipindi kijacho. Kipindi kilichopo ni kifupi sana, na kinatoweka haraka mara tu kinapotokea. 

Uamuzi ni wako, unaweza kuamua kuweka nguvu yako kwa mambo ambayo yametokea tayari, lakini huwezi kuyabadilisha. Au unaweza kuweka nguvu kwa mambo yajayo ambayo yanawezekana na unao uwezo kiasi fulani wa kuyafanya yatokee. 

Tatizo lililopo ni kwa watu wengi kutumia sana nguvu ya hisia zao kuchukia au kuwa na hasira kwa mambo ambayo yamekwishatokea. Niseme kuwa hii ni bahati mbaya, kwasababu nguvu yote hii inapotea bure. 

Hakuna jambo lolote zuri linaloweza kutokea kwa kuendelea kulalamikia mambo ya nyuma. Kibaya zaidi ni kwamba nguvu unayotumia kufikiria mambo mabaya yaliyopita inakupunguzia nguvu ambayo ungeitumia kufikiria jinsi ya kubadilisha au kuweka sawa hali ya maisha yako ya baadae.
  4. Acha liende: Watu wengi ambao hawana furaha ni kutokana na wao kurudishwa nyuma na mambo ambayo yalitokea na ambayo hawataki kuyasahau au kuyaacha yaende zake. Bado wana chuki, hasira na wanajisikia vibaya juu ya kile walichowahi kufanyiwa na watu wengine.
  Wana chuki na wazazi wao, ndugu, mahusiano mabaya ya ndoa, bosi au mahusiano mabaya ya kibiashara. Ukweli ni kwamba, maisha yako yatakuwa ni mwendelezo wa matatizo, changamoto, ugumu na kushindwa kwa muda. Haya yote ni mambo ambayo hatuyatarajii, japo muda wowote yanaweza kutokea na hayakwepeki. 

Kubadili fikra na kubadilisha maisha, lazima ufanye maamuzi ya kukabiliana na changamoto au matatizo yaliyopo, bila kujali ni makubwa kiasi gani. Mpaka utakapochukua hatua ndipo utakoma kuwa mtumwa wa mambo yote ya nyuma yanayokukwaza na ambayo kwa vyovyote vile huwezi kuyabadilisha. Fanya maamuzi leo kwamba kuanzia sasa na kuendelea utaondoa maneno yote ya kama isingekuwa hivi.....kwenye maisha yako. 

5. Kutafsiri matukio kwa njia tofauti: Mwandishi na mzungumzaji maarufu aitwaye “Wayne Dyer”, anasema hujachelewa kuwa na furaha ya wakati wa ujana”. Alimaanisha kwamba, muda wowote unaweza kutafsiri tukio lolote lililokuudhi au kukuchukiza siku za nyuma katika hali au njia ambayo ni chanya. 

Unaweza kujaribisha sheria ya kubadilishana, ambapo unaondoa kibaya na kuweka kitu kizuri na kuanza kuwazia kizuri badala ya mabaya yaliyowahi kutokea huko nyuma. 

Unaweza, kujikita juu ya ni jinsi gani jambo baya lingeweza kukufanya huwe bora zaidi, au mwenye busara zaidi. Kimsingi unaweza kuwa mwema kwa watu wote wale waliowahi kukukwaza huko nyuma, kwasababu, wameweza kukufanya huwe imara zaidi kwa wakati huu ulionao. Na kwa vyovyote vile, isingeweza kutokea vinginevyo. 

Wazazi wako hawakuwa na uzoefu wa kulea vizuri watoto. Na nyongeza ya hapo, walikuwa ni zao au matokeo ya jinsi wao walivyolelewa. Kama ilivyo kwa binadamu yeyote yule, waliingia kwenye malezi wakiwa na matatizo pamoja na udhaifu wao sawa na jinsi ulivyo wewe leo hii. 

Hatahivyo, walijitahidi, walifanya vizuri kile walichoweza kwa uwezo waliokuwa nao. Walifaya kazi jinsi walivyo na wasingeweza kukulea tofauti na wao walivyokuwa. Ni kutokufikri vizuri kuendelea kutokuwa na furaha kwa vitu ambayo walifanya au hawakufanya vile ambavyo hawakuweza, hawakuwa na namna ya kuvifanya tofauti.

Ngoja viede hivyo hivyo na wewe uendelee na maisha yako. Mpendwa msomaji wa makala hii yawezekana unapenda kusoma zaidi kitabu hiki “In Search of the Miraculous: Fragments of an Unknown Teaching” cha Bwana Peter Ouspensky: Weka e-mail yako kwa kubonyeza maneno haya: “NITUMIE KITABU” . Baada ya hapo nitakutumia nakala tete ya kitabu hicho ambacho mimi binafsi kimenijenga sana.
  KARIBU TWENDE KAZI PAMOJA

No comments: