Kwakuwa
maisha ni safari ambayo unasafiri muda mrefu kabla ya kufika unakokwenda au
kufikia maisha ya ndoto yako. Wakati ukiendelea na safari yako ya maisha,
usikubali kushawishiwa na mtu yeyote wala kundi lolote lile kwani wao ni vigumu
sana kufahamu unakotaka kwenda. Usijaribu hata siku moja kuchagua njia au cha
kufanya kutokana na matakwa ya watu wengine.
Mtu
kikundi Fulani kufanya jambo Fulani na wakashindwa haimanishi kwamba na wewe
utashindwa kumbuka wewe unajifanana wewe peke yako, hakikisha haugopi kupigwa
mishale kutoka kila kona ambayo ni kejeli, matusi, kubaguliwa, kutengwa,
kusemwa vibaya n.k. Jitahidi kuwa na uamzi pamoja na
uchaguzi binafsi kama njia mojawapo ya kufikia mafanikio unayoyahitaji. Kwahiyo
nilazima ujifunze kusema hapana kwa baadhi ya vitu, hata kama vinafanywa na
watu wengi. Jambo la kuwa na uchaguzi na uhamzi binafsi ni muhimu sana kwani
usipojifunza kufanya hivyo, basi wewe kila wakati utakuwa mfanyakazi au mtumwa
wa kutumikia uchaguzi na uhamzi wa watu wengine. Ili uweze kuwa na uchaguzi
sahii wa jambo la kufanya ili kupata mafanikio na maisha mazuri ni lazima
kujifunza kutofautisha kilicho muhimu na kisicho na umuhimu. Watu waliowengi
wanafanya vitu vingi, hata kama vingine siyo vya muhimu ilimradi tu watu
wengine kama marafiki ndugu n.k wanafanya basin aye atafanya.
Matokeo ya kufanya kila kitu eti
kwa sababu wengi wanafanya, ni kujikuta muda wako mwingi unautumia Katika vitu
au shughuli ambazo zinaleta mafankio kidogo sana. Mwandishi “Richard Koch” Katika
kitabu chake cha “Living the 80/20 Way:
Work Less, Succeed More, Enjoy More”anasema kwamba ili uweze kupata
mafanikio makubwa maishani ni lazima utumie Asilimia 20% ya muda kupata
mafanikio ya Asilimia 80%; Kwahiyo, mwandishi huyu anatufundisha kuwa iwapo
utakuwa mtu wa kufanya kila kitu ili mradi wanafanya marafiki zako, basi ujue
wewe utakuwa unatumia Asilimia 80% ya muda wako ili kupata mafanikio ya Asilimia
20% tu! Kwa maana nyingine wewe utakuwa mtu unayehangaika kila siku mpaka
unakufa.
Ikumbukwe kuwa Katika maisha unapoamua
kuchagua kufanya kitu kimoja kati ya vingi ulivyonavyo, siyo kwamba hivyo
vingine huvihitaji bali unachagua kilicho bora zaidi. Kufanya maamuzi ni mwanzo
tu wa vitu kutokea na inampelekea mtu kupata nguvu halisi ambayo itampeleka
mahali ambapo ni pazuri na hata unakuta mwanzoni ukupafikiri wakati ulipoamua
kufanya mabadiliko hayo.
Katika kuandika historia ya
maisha yako, uwezi kumfurahisha kila mtu, hivyo huwezi kukamilisha kila kazi
unayo paswa kuifanya. Kwahiyo katka kila kazi au majukumu ni vizuri ukaweka
malengo na utendaji wako ukawa unaongozwa na malengo uliyojiwekea wewe
mwenyewe, hivyo kipimo cha kufanikiwa au
kutokufanikiwa kwako kitakuwa ni kwako kuweza kujipima kwa kutimiza au
kushindwa kutimiza malengo yako na si kusikiliza watu wanasema nini kuhusu
kufanikiwa au kutofanikiwa kwako.
Mpendwa msomaji, endelea kuitumia vizuri MAARIFASHOP ili kujifunza mambo mbalimbali yatakayokuwezesha kupata mafanikio. Ili kupata makala mpya kila zinapochapishwa, bonyeza neno TUMA MAKALA MAARIFASHOP kisha sajiri barua pepe yako. Na kama unapenda kupata mafunzo ya kila siku kwa njia ya whatsap bonyeza neno MAFUNZO.
KARIBU TUCHUKUE HATUA PAMOJA!
No comments:
Post a Comment