Sunday, February 8, 2015

UMUHIMU WA KUWA KIONGOZI WA MAISHA YAKO



AMUA KUWA RAIS WA MAISHA YAKO LEO
Maisha unayoishi sasa ni maisha yako, kama kuna sehemu yoyote ya maisha yako ambayo huipendi wewe ndio una jukumu la kuibadilisha. Hakuna mtu mwingine yeyote ambaye anaweza kuwa na uchungu na maisha yako ila wewe mwenyewe. Na wala hakuna mtu yeyote anayeweza kuyabadili maisha yako bila yaw ewe mwenyewe kuwa tayari kwa mabadiliko.

Kuanzia sasa jichukulie wewe kama raisi wa maisha yako, na jichukulie wewe ndio mtu wa mwisho wa kufanya maamuzi juu ya maisha yako. Na sio tu unajichukulia hivi, bali ndio ukweli wenyewe. Wewe kama raisi maamuzi yako yanaweza kusababisha mafanikio au yakasababisha kushindwa. Kama tulivyoona kwenye siku ya kwanza upo hapo ulipo kutokana na maamuzi uliyofanya na machaguo uliyofanya. Ili kwenda mbele zaidi unahitaji kufanya maamuzi bora zaidi na kuboresha machaguo yako.

Miasha ni kuchagua, ukichagua kufanikiwa ndiyo utakachokipata, ukichagua kuwa wa matatizo na kushindwa ndicho kitakachotokea. Usipochagua kabisa utapata kile kilicho kibovu kabisa ambacho ni kushindwa. Kipato unachopata leo ndio kipato ulichoamua kupokea, kama kipato unachopata sasa hakikuridhishi amua kupata zaidi ya hapo. Fanya hilo kama lengo lako, weka mipango na anza kufanyia kazi mpango wako wa kujiongezea kipato. Ukikaa tu na kulalamika kwamba kipato hakikutoshi huku hufanyi chochote cha kukiongeza unapoteza muda wako.

Wewe ndio raisi wa maisha yako, wewe ndio mfanya maamuzi mkuu na wewe ndio unayetengeneza maisha yako. Kama utakuwa na mtizamo hasi utajenga maisha ya matatizo na kushindwa na kama ukiwa na mtizamo chanya wa kuona unaweza kubadili maisha yako utatengeneza maisha ya mafanikio na furaha. Yote haya yapo mikononi mwako ni wewe tu ufanye maamuzi sahihi na kuyasimamia.

Endelea kuwa karibu na mtandao wa MAARIFASHOP ili kujenga na kukuza uwezo wako wa kusaka na kupata mafanikio. Kupata makala mpya kila zinapochapishwa bonyeza kiungo hiki sasa hivi; NITUMIE MAKALA MAARIFASHOP kisha sajiri barua pepe yako na kama unapenda kupata mafunzo ya kila siku na makala mpya kwa njia ya whatsap bonyeza neno MAFUNZO


No comments: