- Mjasiriamali Ujikita Katika Kuzalisha Bidhaa/Huduma kwa Lengo la Kugusa Maisha ya Watu Wengine
- Uongozi ni Ujuzi Muhimu Sana Unaotakiwa kwa Mtu Anayetaka Kuwa Mjasiriamali
Nafahamu kuwa kuna watu wengi
wanatamani kuwa wajasiriamali na wengine hasa waliojiajiri wanadhani na kuamini
kuwa, wao ni wajasiriamali. Kuna dalili zinazoonyesha kuwa jambo hili la
ujasiriamali linachukuliwa kimzaa mzaa sana. Imekuwa kitu cha kawaida sana hapa
Tanzania, kusikia watu wengi wakijiita wajasiriamali, hasa wale wanaofanyakazi za
kujiajiri wenyewe. Lakini je? kitendo cha wewe kujiajiri tu peke yake, kinatosha
kukufanya huwe mjasiriamali?. Sasa huyu anayeitwa mjasiriamali ni mtu wa namna gani?
Mjasiriamali ni ujuzi na siyo mtu. Kazi
unayofanya, timu ya watu uliyonayo, maisha unayoishi, ukubwa wa kazi yako,
maamuzi unayofanya kila siku n.k. vyote hivi vina nafasi kubwa ya kukufanya wewe
kuwa mjasiriamali au vinginevyo!.
Mjasiriamali ni mtu anaona fursa, anaweka
timu ya watu pamoja na kujenga biashara ambayo uzalisha faida kutoka kwenye
fursa husika”. Ni wazi kwamba wapo watu wengi ambao wameweza kuona fursa na kuamua
kuzichangamkia kwa malengo ya kupata faida wao peke yao. Lakini, kama ukiona
fursa na ukaona una uwezo wa kuifanyia kazi wewe peke yako, basi ujue wewe ni
mfanyabiashara mdogo sana ambaye umejiajiri au umeajiliwa na biashara badala ya
wewe kumiliki biashara”
Kuna tofauti sana kati mtu
aliyejiajiri na mjasiriamali. Mtu aliyejiajiri, ni mtu ambaye anaweza kuzalisha
bidhaa au kutoa huduma yeye mwenyewe peke yake. Kwa mfano msanii anaweza kuchora picha yeye mwenyewe, daktari anaweza kukutibu jino mwenyewe, au mtu anafuga mifugo yeye mwenyewe. Mjasiriamali, hawezi kufanya vyote vinavyotakiwa kufanyika katika kuendesha biashara peke yake. Mjasiriamali ni lazima awe tayari kupata na kuunganisha vipaji vya watu wenye uwezo na ujuzi tofauti tofauti, ambapo huwaunganisha ili wafanye kazi pamoja kwaajili ya kukamilisha uzalishaji wa bidhaa au huduma fulani. Kwa maana nyigine, mjasiriamali ujenga timu ambayo ujikita katika kuzalisha bidhaa/huduma, kazi ambayo mtu mmoja mmoja hawezi kuifanya yeye peke yake.
bidhaa au kutoa huduma yeye mwenyewe peke yake. Kwa mfano msanii anaweza kuchora picha yeye mwenyewe, daktari anaweza kukutibu jino mwenyewe, au mtu anafuga mifugo yeye mwenyewe. Mjasiriamali, hawezi kufanya vyote vinavyotakiwa kufanyika katika kuendesha biashara peke yake. Mjasiriamali ni lazima awe tayari kupata na kuunganisha vipaji vya watu wenye uwezo na ujuzi tofauti tofauti, ambapo huwaunganisha ili wafanye kazi pamoja kwaajili ya kukamilisha uzalishaji wa bidhaa au huduma fulani. Kwa maana nyigine, mjasiriamali ujenga timu ambayo ujikita katika kuzalisha bidhaa/huduma, kazi ambayo mtu mmoja mmoja hawezi kuifanya yeye peke yake.
Mjasiriamali ni mtu ambaye anapoamua
kufanya biashara mara nyingi anakuwa analenga kutatua changamoto au kero fulani
kwenye jamii. Kwa maana nyingine “mjasiriamali
ujikita katika kuzalisha bidhaa au huduma mbalimbali kwa lengo la kugusa maisha
ya watu wengine na siyo yeye peke yake”.
Sababu kubwa ambayo huwafanya watu wengi kuendelea kuwa wadogo au kuwa na
biashara ndogo ni kwasababu biashara wanazoziendesha ni kwaajiri ya kutatua
matatizo yao peke yao. Ndiyo maana unakuta mtu anafanya biashara fulani miaka
20, lakini biashara haibadiliki, hiko vilevile na haijawahi kupanuka kwa miaka
yote. Watu wa namna hii ndio wengi wamejiajiri na ndio hawa wanaodhani na
kuamini kuwa na wao ni wajasiriamali.
Mjasiriamali ni mtu anayebeba
majukumu ambayo yanahitaji timu ya watu. Mjasiriamali ambaye utegemea timu ya
watu kufikia malengo, huwa halipwi mpaka
hapo timu yake ikishafanya kile kinachotakiwa kufanyika wa kama timu. Waajiriwa
wengi, na wale waliojiajiri wanalipwa kulingana na kile ambacho wanaweza
kufanya kama wao binafsi. Tofauti na waajiriwa/waliojiajiri, mjasiriamali
amejijengea tabia ya kufanya kazi bila kulipwa, kutegemeana na unachofanya
wakati mwingine unaweza kulazimika kukaa muda mrefu zaidi ya mwaka ndio unakuja
kulipwa kama umefanikisha kile ulicho kilenga.
Malipo ya mjasiriamali ni baada ya kukamilisha
kazi na timu, wakati malipo ya waajiriwa wengi ni kabla ya kuanza kazi. Kama
alivyo mkandarasi wa majengo, huwa anatumia watu kujenga nyumba; mfano: mafundi
bomba, umeme, seremara na wataalam wengine kama wasanifu majengo, wahasibu n.k.
na mjasiriamali utafuta watu tofauti tofauti kama vile, mafundi mchundo (technicians),
wasomi, na wataalam wengine katika kumsaidia kujenga biashara”. Kwahiyo, ni
muhimu tukatambua ndani ya fikra zetu kuwa, mjasiriamali ni mtu ambaye ni kiongozi, japo
wakati mwingine yawezekana wasifanye kazi na timu zao moja kwa moja. “Kadiri
utakavyoongoza timu ya watu ambao ni wazuri wenye uelewa, haulazimiki kufanya
kazi kama sehemu yao, ndiyo vizuri na ndiyo utafikia kiwango cha kuitwa mjasiriamali
mkubwa.
Kuna
watu wanamiliki makampuni mengi, lakini huwa hawafanyi kazi katika makampuni
hayo. Ndiyo maana wanaweza kutegeneza pesa zaidi na kufanya vitu vingi bila
kuwa wamefanya kazi. Ni kutokana na hali hii, tunakumbushwa kuwa, “Uongozi ni ujuzi muhimu sana unaotakiwa kwa
mtu anayetaka kuwa mjasiriamali”.” Uongozi siyo zawadi ni ujuzi na wala
hauzaliwi nao bali ni kitu ambacho ukiamua unajifunza. Ukitafakari kwa kina unagundua
kuwa sisi wote tuna chembe chembe za ujuzi wa uongozi. Tatizo lililopo kwa watu
waliowengi ni kwamba, watu wengi utumia maisha yao yote kukuza ujuzi katika
taaluma nyingine tofauti na uongozi, ndiyo, maana kuna watu wengi ni waajiriwa
na wengine wamejiajiri. Ni watu wachache sana, ambao wanatumia muda wa maisha
yao kukuza ujuzi wao wa uongozi, kwasababu, uongozi ndio ujuzi ambao unatakiwa kwa wajasiriamali (wamiliki
wa biashara). Kwahiyo, ni vizuri watu tukaamua kuwa wajasiriamali na kujikita
katika kusaka kila aina ya ujuzi utakaotuwezesha kuongoza timu zetu, hili
hatimaye tuweze kumiliki biashara kubwa na mwisho kufikia maisha ya ndoto yetu.
Mpendwa msomaji, endelea kuitumia vizuri MAARIFASHOP ili kujifunza mambo mbalimbali yatakayokuwezesha kupata mafanikio. Ili kupata makala mpya kila zinapochapishwa, bonyeza neno TUMA MAKALA MAARIFASHOP kisha sajiri barua pepe yako. Na kama unapenda kupata mafunzo ya kila siku kwa njia ya whatsap bonyeza neno MAFUNZO.
No comments:
Post a Comment