Thursday, July 11, 2024

Mikopo na Mifugo ni Marafiki Kwasababu Hii Hapa:


Mikopo ilianza zamani sana takribani miaka 3,000 iliyopita. Tangu kuanza kwa ustaarabu wa binadamu, mikopo imekuwepo katika sura mbalimbali kwa kipindi chote cha maisha ya binadamu. Historia ya ukopeshaji inatuonyesha kuwa.. maendeleo makubwa tuliyonayo hivi sasa yasingefikiwa bila uwepo wa mikopo.

Kwa upande mwingine, mikopo imekuwa kama mafuta kwenye gari kwakuwa kama kuchochea cha ukuaji wa uchumi na maendeleo ya kijamii.

Mikopo mingi huko nyuma, ilitolewa katika sura ya vitu halisi, hasa kupitia mavuno ya “nafaka” na “mifugo”.

Mifugo kama vile ng’ombe iliwekwa kama dhamana ya mikopo ya sarafu za dhahabu, fedha na hata shaba.

Wafanyabiashara hasa kutoka Bara la Ulaya, walitumia ng’ombe zao kama dhamana kukopa dhahabu, shaba na fedha kama mtaji wa biashara.

Baada ya kupata mikopo walisafiri kwa meli hadi nchi za mbali kutafuta bidhaa zilizohitajika kwa wingi barani Ulaya.

Walipofika katika nchi hizo za mbali, walinunua mizigo ya bidhaa na kisha kuipakia kwenye meli ili kusafirisha hadi Ulaya.

Endapo meli hiyo ya mizigo ilifanikiwa kurudi salama, wale wafanyabiashara waliokuwa wamekopa walimlipa riba mkopeshaji kwa njia ya 'ndama' wote waliozaliwa kutoka kwa 'ng’ombe' ambao awali waliwekwa kama dhamana kwa kipindi hicho chote cha mkopo kabla ya kurejeshwa.

Ulipaji wa riba kwa kutumia mali badala ya pesa, ndiyo ulijulikana kwa lugha ya kingereza kama “in kind".

Neno hili la “kind” linatokana na neno “kinder” linalomaanisha watoto, wawe ni binadamu au wanyama. Kwa lugha ya wafugaji, “Kinder” Ni ndama au watoto wa ng’ombe.

Ilipofika wakati fulani, mabenki yakaamua kuachana na utaratibu wa kutumia ng’ombe hai kama dhamana. 

Hapo mabenki yalianza kushughulika na madini ya dhahabu, fedha na shaba peke yake.

Wakati huo hakukuwa na sarafu za 'dhahabu' ambazo zingeweza kuzalisha sarafu nyingine kama ambavyo ng’ombe walizaa ndama.

Kwahiyo, 'riba' ilichukuliwa kutoka kwenye mtaji wa dhahabu, kwa kupunguza mtaji wa mkopaji pale wakati alipolipa Deni Lake. 

Riba ya mkopeshaji ilikatwa kutoka kwenye mtaji. 

Maana yake ni kwamba riba, ilikatwa kutoka kwenye kiasi cha dhahabu alichoweka mkopaji.

Habari njema kwa wafugaji ni kwamba, mifugo (mf. ng’ombe, mbuzi, kondoo n.k) zilivyo kwa uasili wake zinayo “riba” ndani yake.

Mtu yeyote anaweza kupata riba hii kwa kufuga. Kwahiyo, ukiwa na mifugo unakuwa sawa na yule tajiri anayemiliki benki.

Kama tunavyofahamu, moja ya kazi za benki ni kufanya biashara ya kuweka na kukopa pesa, ambapo mkopaji anatakiwa kurudisha pesa ikiwemo na riba…

Hivyobasi mmiliki wa mifugo anatakiwa kujua kuwa yeye anamiliki benki na riba yake ni watoto wanaozaliwa n.k.

Kwa maana mfugaji anaikopesha mifugo; muda wake, matibabu, malisho n.k halafu mifugo inamlipa watoto wanaozaliwa – mfano ndama.

Niseme tu kuwa waliodhani kuwa hawawezi kumiliki benki, sasa waondoe hofu na wajue kuwa tayari wameanza safari ya kumiliki benki.

Changamoto inayowakabili wafugaji wengi ni jinsi gani ya kufuga kibiashara. Maana benki yenye tija kwa mmiliki ni ile inayofanya biashara.

Utajiri wowote unaanza na pale unapoanza kumiliki vitu vyenye kukulipa riba ya mara kwa mara.

Nimetumia historia ya mifugo kuonyesha jinsi unavyoweza kumiliki vitegauchumi vyenye uwezo wa kukulipa riba.

Unaweza kufikiria au kubuni vitu vingine tofauti na mifugo, ambavyo vitasimama kama benki.

Unapoendelea kufanya yote haya tafadhali jibu swali hili Ni Nani ana Jukumu la Kutafuta Mali?

Wale walio katika harakati za kutafuta mali, jitahidi sana kujisomea makala za mtandao huu wa MAARIFASHOP ambao utakupatia maarifa na mbinu mbalimbali za kufikia maisha ya ndoto yako.

Ili kupata makala mpya kila zinapochapishwa, bofya kwenye neno MAKALA MPYA kisha sajiri barua pepe.

Kwa wale wanaopenda kupata mafunzo kwa njia ya whatsap bofya kwenye neno MAFUNZO.


                        ðŸ’¢ðŸ’¢KARIBU TWENDE KAZI💢💢



 

 

No comments: