Katika makala hii, nimetumia maneno mawili yaani
CAPITALIST na CAPITAL kama yalivyo katika lugha ya kinngereza, lengo likiwa ni
kutaka kueleweka vizuri na kurahisisha uchambuzi wangu juu ya chuki
iliyojengeka kwa mtu anayeitwa “Bepari”
hapa Tanzania.
Katika nchi ya Tanzania ambayo iliwahi kuendesha siasa
na uchumi wake kwa kufuata sera za mlengo wa kijamaa (socialism), ukiambiwa
wewe ni “capitalist au bepari mkubwa”
kama
huna roho ya uvumilivu unaweza kuhisi umetukanwa, umedhalilishwa na wakati
mwingine kuona kama umekashifiwa (kashifa), eti tu kuitwa bepari!. Hii yote ni kwasababu mapokeo yetu kuhusu mtu ambaye ni capitalist , yamekuwa ni hasi kiasi cha
kuambiwa kuwa mtu wa namna hiyo ni mnyonyaji, mwizi, mwenye roho ya kinyama na majina
mengine mabaya unayoyajua hapa duniani. Ukijaribu kuongea na baadhi ya watu hapa
kwetu Tanzania, utakuta wapo watu wanaopenda kujisifu! Eti wao ni watu safi kwa
kigezo tu! cha kutokuwa ma-capitalist, jambo hili linashangaza sana.
Ukichukulia tafsiri ya kawaida, ni kwamba capitalist
ni mtu ambaye ni "Bepari". Ili
kuelewa vizuri maana pana ya mtu ambaye ni capitalist
ni vizuri kuelewa kuwa neno hili chimbuko lake ni neno “capital” lenye maana ya”
mtaji”. Kwahiyo, capital ni kitu chochote kinachotumika kuzalisha vitu au Huduma
na hivyo tunaweza kusema kuwa mifano ya capital ni kama vile trekta, mashine za kusaga, cherehani, ardhi,
pesa taslim, nguvu kazi n.k.
Hatahivyo, wakati mwingine ni vigumu kuzalisha
vitu au Huduma Fulani Fulani kwa kutumia aina moja ya capital. Kwa mfano: Iwapo mjasiriamali akiamua kuzalisha mahindi na
baadae unga, yawezekana mtu huyu akahitaji kuchanganya aina ya mtaji zaidi mmoja
(ardhi, mashine ya kusaga na kukoboa, nguvu-kazi, pesa taslimu n.k). Katika
kuchanganya aina tofauti za mitaji pamoja na vitu vingine vinavyohitajika
kufikia kupata unga wa mahindi, ndipo vitu vyote hivyo uwekwa katika mpangilio
maalumu kuanzia jinsi mahindi yatakavyolimwa,yatakavyosindikwa na jinsi unga utakavyo
uzwa kwa wateja. Mpangilio huu maalumu Ndio baadae huleta kitu kinachoitwa “mfumo
wa kuingiza na kutoa pesa taslim (system of cash flow). Kwahiyo, mtu yeyote
anayemiliki na kuhakikisha “mfumo” unafanya kazi kwa kiwango cha juu mpaka
kufikia kuzalisha bidhaa iliyokusudiwa (k.m. Unga) na hatimaye kuuzwa na kupata
pesa si mwingine bali ni "CAPITALIST (BEPARI)".
Hivyo basi, itoshe kusema kuwa, iwapo watanzania
wakianza kuwekeza na hatimaye kumiliki mfumo
wa uzalishaji bidhaa na huduma (pesa), ni wazi kwamba watakaofanya hivyo,
watakuwa watu wenye kuheshimika sana. Mtu ambaye ni capitalist hapa Tanzania ataheshimika sana kwasababu, ni capitalist huyohuyo, ndiye serikali inamtegemea
kupata kodi mbalimbali kwaajili ya kuendesha na kughalimikia Huduma mbalimbali
za kijamii kama vile matibabu, elimu, barabara, maji, pembejeo za kilimo n.k.
Kwa sasa ni vyema ukafurahi pindi
unapoitwa “capitalist” kwasababu kwakuwa mtu wa namna hiyo, tayari unakuwa
umesaidia familia nyingi kupata ajira na Mahitaji mengine mengi. Tofauti na
zamani ambapo tulifundishwa shuleni kuwa ubepari ni WIZI na kwa kufanya hivyo walimu
wetu hawakujua kuwa walikuwa wanaua kabisa fikra za kijasiriamali na vipaji tulivyopewa na
mwenyezi Mungu. Ili kurudisha vipaji na fikra za kijasiriamali, ni vyema watanzania
tukaanza kuchukua hatua na jitihada za dhati kabisa, ikiwa ni pamoja na kusoma
sana vitabu, kujifunza kila siku kutoka kwa waliofanikiwa na kuthubutu bila
kuogopa changamoto zinazoweza kujtokeza mbele ya safari ya mafanikio.
Mpendwa msomaji, endelea kuitumia vizuri MAARIFASHOP ili kujifunza mambo mbalimbali yatakayokuwezesha kupata mafanikio makubwa. Ili kupata makala mpya kila zinapochapishwa, bonyeza neno TUMA MAKALA MAARIFASHOP kisha sajiri barua pepe yako. Na kama unapenda kupata mafunzo ya kila siku kwa njia ya whatsap bonyeza neno MAFUNZO.
No comments:
Post a Comment