Saturday, December 31, 2016

Fungua Mwaka ya Uchumi ni Hii Hapa



 
Mahitaji ya binadamu ni mengi sana na hayana kikomo. Mahitaji haya yamegawanyika katika makundi makuu mawili yaani “Vitu/Bidhaa” na “Huduma”. Pamoja na mahitaji mengi ya binadamu, mtu mmoja mmoja hawezi kuzalisha na kujitoshereza kwa kila kitu. Ndiyo maana binadamu wengi uendesha maisha yao kwa

kutegemea zaidi mfumo wa “kubadilishana” vitu na huduma.

Hapa duniani kila mmoja wetu anajikuta akikabiliwa na jukumu zito la kuzalisha “ziada”, yaani zaidi ya kile kinachotoshereza familia yako. Bila kuzalisha ziada hakuna namna endelevu ya wewe kuweza kupata mahitaji mengine kutoka kwa watu wengine.

Uzalishaji wa ziada ambao ni kwaajili ya kubadilishana ndiko kunatupeleka kwenye dhana nzima ya “uchumi” . Neno “uchumi” linatokana na neno “kuchuma” kwa maana nyingine tunaweza kusema kuwa kuchuma ni sawa na “kuvuna”. Unaposikia uchumi kukua (Kaya, Kijiji, Kata, Wilaya..Taifa) ina maana kinachovunwa au kuchumwa ni kingi na kikubwa.

Tunavuna kile tulichoangaikia kukizalisha (mf. uzalishaji wa zao la muhogo). Tukishavuna kinachofuata ni kaya kutumia au “kubadilishana” na watu wengine. Kitu pekee kinachotuwezesha kubadilishana bidhaa au mali tuliyonayo ni “PESA”.

Bidhaa/mali unazomiliki ndizo “zinaita na kuvuta” pesa kuja kwako. Bidhaa au mali zako ufanya kazi ya kuvuta pesa kama “sumaku”. Kaya iliyo na bidhaa zinazokidhi mahitaji ya watu wengine, mf. muhogo itavuta pesa nyingi kwake.

Kwahiyo, ndio kusema kwamba pesa inapokuja kwako inakuwa imetumwa kufuata vitu au bidhaa. Usiangaike kutafuta pesa BALI jiulize kwako pesa itatumwa kufuata nini? Kila ukijiuliza ni nini pesa itafuata kwako, basi jibu utakalopata ndiyo pesa yenyewe

Umuhimu wa pesa kijijini: Kukiwa na pesa kijijini watu wengine kutoka nje ya kijiji au kata watafuata pesa kwa wao kuwapatia nguvukazi. Nguvukazi ikitumika kwenye shughuli za uzalishaji mali tunapata pesa nyingi zaidi ya kiasi tulicholipa vibarua.

Kwakuwa ziada uuzwa, kupungua kwa uzalishaji kunasababisha kupotea kwa pato la kaya. Kupungua kwa uzalishaji kunasababisha kutoweka kwa usalama wa chakula na kipato ~ hatari kuu. Kitendo cha mazao kutokuwepo kinasababisha uchumi kuporomoka kuanzia kaya…..hadi Wilaya.

Endapo uchumi wa kaya ukiporomoka, watu wengi uanza kuuza “nguvukazi” (mtaji mkuu) kwa wazalishaji wengine hasa nje ya kijiji. Kaya inapotegemea mapato (pesa) yatokanayo na uuzaji wa nguvukazi ni hatari sana, kwasababu utendaji kazi kwenye mashamba yao unapungua sana. Na pia, uzalishaji ndani ya mashamba yao unashuka sana. Mwisho, kaya nyingi tegemezi ambazo ni ombaomba (maskini) zitazidi kuongezeka.
TUKUTANE MWAKANI 2017 muda mfupi ujao. 

No comments: