Mojawapo ya vitu ambavyo utafutwa kila siku na watu wengi ni “unafuu”. Wakati mwingine tunalazimika kujiuliza “unafuu” huu ni kitu gani? Tunaweza kusema kuwa ni..
ile hali ya kupata kitu, huduma fulani ama kwa kulipa gharama kidogo kuliko thamani halisi ya kitu/huduma husika. Unafuu pia, waweza kuwa ni hali ya mtu kupata kitu bure, bila hata ya kufanya kazi.
Ukifuatilia kwa undani utaona kuwa, hivi sasa watu wengi wameelekeza zaidi mikakati yao mingi katika kutafuta unafuu wa maisha. Ni watu wachache sana ambao wanatumia muda wao mwingi kufikiri na kutengeneza bidhaa na huduma kwaajili ya wao wenyewe na watu wengine pia.
Kutokana na wengi kutumia rasilimali walizonazo katika kutafuta unafuu, kumekuwa na hali ya kuadimika kwa bidhaa na huduma mbalimbali, ikilinganishwa na mahitaji halisi ya watu. Kuadimika kwa bidhaa na huduma, kumepelekea kupanda kwa bei ya vitu, kiasi cha watu wengi kusindwa kumudu gharama za maisha—hiki hapa chanzo cha umaskni wa vitu na mali.
Ni muhimu sana tukatambua kuwa, katika maisha hakuna unafuu. Kila kitu ni gharama, lazima uzilipe ndipo upate kile unachotaka. Ukiona umepata unafuu leo, basi ujue kuna siku utalazimika kulipa, ndiyo maana tunahaswa kutokushangilia pale tunapopata unafuu.
Unafuu unapendwa kwasababu watu wengi ni wavivu, na kwasababu hiyo, wanataka utajiri uwaangukie badala ya wao kuutengeneza utajiri. Dalili mojawapo ya watu wanaopenda unafuu ni pamoja na wale wote wanaopenda kushiriki michezo ya bahati nasibu. Sasa hivi utakubaliana na mimi kuwa, michezo ya bahati nasibu hapa Tanzania ipo mingi, kutokana na watu wengi kuichangamkia.
Wanaojitosa kucheza michezo hiyo yawezekana wengi wamekata tamaa, na pengine hawana uhakika wa kipato kutoka kwenye shughuli zao ambazo wamekuwa wakizifanya. Wengi wao wanaona ni bora kujaribu bahati nasibu, ili kuona kama wanaweza kuibuka na mamilioni. Yote hayo yanatokana na "tabia ya kupenda unafuu" katika maisha. Kimsingi, hali hii ya kuwa na hamu ya kupata vitu bure (unafuu), imewagharimu na inaendelea kuwagharimu watu wengi sana.
Kwa mfano; unakuta mwanafunzi yuko busy na kutafuta mbinu za kumdanganya mwalimu ili apate unafuu wa kufaulu shuleni; Mkulima anamlilia kila mtu anayemtembelea, ili kupata unafuu wa pembejeo na nguvukazi kwaajili ya kilimo chake. Wazazi nao wanatafuta unafuu kutoka kwa watoto wao.

Unakuta mzazi anao watoto ambao wamemaliza shule, lakini hataki kuwajengea mfumo wa wao kuweza kuzalisha na kufaidi jasho lao, BADALA yake anawafanyisha kazi (kwake), alafu mavuno yakitoka akijitahidi atanunua nyama siku moja basi!.
Mfano halisi: chukulia mtu anao watoto wanne wakubwa, mara anaamua msimu huu kulima mpunga. Familia nzima (baba, mama, na watoto 4) jumla ni watu sita wanashiriki kulima ekari 6 za mpunga, bila kuajiri kibarua yeyote. Wakati wa mavuno, familia inapata kiasi cha jumla ya magunia 120 ya mpunga.
Baada ya mavuno, mkuu wa kaya anauza mpunga na kujipatia mamilioni. Hayo mamilioni ni pamoja na gharama za nguvukazi iliyotoka kwa wanafamilia 5 na mkuu wa kaya wa 6. Badala ya mkuu wa kaya kutoa gharama ya nguvukazi na kuwagawia familia, yeye anachukua mamilioni yote kama yalivyo, akidhani amepata pesa nyingi, kumbe ni "unafuu unaotokana na jasho la wanafamilia".
Mara tu watoto wanapoanza kujitegemea na kuwa na familia zao, ghafla uchumi wa familia walikotoka unaanza kushuka haraka sana na familia inaingia kwenye umaskini. Umaskini ukishamnyemelea mkuu wa kaya (mzazi), mara anaanza kulalamikia watoto kuwa hawamjali. Maana yake ni kwamba, muda huo anapoanza kulalamikia watoto, kimsingi huo ndio muda anapoanza kulipa gharama za ule unafuu alioupata enzi zile walipozalisha magunia 120 ya mpunga.
Mfano huu wa kilimo cha mpunga kwa wanafamilia 6, unatufundisha kuwa unapoona umepata "unafuu" wowote katika maisha, ujue kuna watu wameumia au kuna watu wamelipia. Kwa maneno mengine ni kwamba, katika maisha hali ya binadamu HAKUNA suala la unafuu; japokuwa sisi kila siku tumeamua kukataa ukweli huu. Ndiyo maana mpaka leo tunaendelea kuhangaika na maisha kwasababu, tumeendelea kuwa na kiburi cha kukataa ukweli huu juu ya suala zima la "unafuu".
Mahangaiko mengi tunayoshuhudia duniani, yanatokana na watu wengi kukwepa kulipa gharama zote za mwenendo wao wa maisha. Lakini pia, suala la kukosa uhuru, ambalo tunadai mpaka leo, linatokana na sisi kutokuwa tayari kulipa gharama za maisha yetu. Ndiyo maana wale wote wanaojitolea kutulipia gharama zetu ambazo tunazikwepa kila siku, wanatutawala mpaka leo. Kamwe tusiwalalamikie wanaotutawala kwasasa, bali tuamue sasa kuanza leo kulipa gharama zetu zote za maisha yale tunayopenda—hakika uhuru wetu utarejea.
Unafuu unawazuia na kuwafunga watu; unafuu unazuia vipaji, unafuu hauwezi kumfanya mtu kujitanua kulingana na uwezo alionao. Unafuu unawafanya watu kuwategemea watu wengine maisha yao yote. Unafuu unazuia uhuru na unaleta mzigo kwako. Unafuu unamfanya mtu kuishi maisha yasiyokuwa na mwelekeo. Rudisha uhuru wako kwa kuanza kulipa gharama zote za vitu vinavyokuhusu—ungana nasi kufanikisha mradi wa "Lipa gharama zako zote kupata huru wa kweli".
Endelea kujifunza mengi kupitia mtandao wako wa MAARIFA SHOP. Kupata makala mpya kila zinapotoka weka e-mail yako kwa kubonyeza neno hili: MAKALA.

No comments:
Post a Comment