Kitu
pekee cha kukuhakikishia mafanikio makubwa siyo wewe kuwa smart bali ni tabia
ya kuwa chanya, na kufanya/kuweka nguvu kidogo kidogo kila siku na kwa muda
mrefu.
Kumbe
wakati mwingine tumekuwa tukitamani sana kufanikiwa Katika maisha lakini mara
nyingi tumejikita Katika kufanya vitu au kuwekeza kwenye miradi mikubwa na
midogo na wakati huohuo kutaka hayo mafanikio yaje ndani ya muda mfupi. Lakini,
wakati tukitafuta mafaniakio hayo, tumekuwa hatuna utamaduni wa kubadili mambo
madogo madogo ambayo huwa tunachagua kuyafanya kila siku tunapoamka mpaka
wakati wa kulala. Watu wengi waliofanikiwa, wanatufundisha kwamba ni lazima
tubadili hayo mambo tunayo chagua kufanya
kila siku, ili yaweze kuendana na mafaniko au malengo yetu. Mafanikio
yanatokana na kuchagua kufanya vitu Fulani Fulani kila siku na kuhakikisha
unarudia kuvianya kwa muda mrefu.
Katika
maisha kuna mambo madogo madogo unayochagua kufanya kila siku, na mambo hayo
huwa yana tabia ya kujidurufu aidha kwa kukurudisha nyuma au kukupeleka mbele. Ukweli
ni kwamba, maisha tuliyonayo sasa ni malimbikizo ya chaguo (choices) tunazofanya
kila siku. Mfano: uamuzi wa kula nyama tena za mafuta kila siku; uamuzi wa
kununua vitu vya anasa kawanza kabla ya kutumia pesa kuwekeza kwenye miradi ya
uzalishaji, vyote hivi ni chaguo ambazo ni sahihi kwako binafsi. Chaguo pamoja
ma maamuzi yetu tunayofanya kila siku yamekuwa aidha ni rafiki au adui yetu
mkubwa Katika kuleta mafanikio.
Chaguo
tunazofanya kila siku, zinanikumbusha kisa alichowahi kunisimulia rafiki yangu
mmoja; kwamba kulikuwa na bwana mmoja ambaye alichagua kumkopesha rafiki Kiasi
cha shilingi 120,000/- kwa makubaliano kwamba angezirudisha baada ya mwezi
mmoja lakini mwezi ulipoisha, Yule rafiki hakurejesha ile pesa mpaka jamaa
alikaa karibia mwaka mzima ndipo akaamua kudai pesa ile kwa namna ya pekee.
Lakini kabla alijitafakari ili kuona kama alishiriki Katika kusababisha kero
hiyo ya kutolipwa pesa yake au la!. Alipotafakari sana aligundua kuwa naye
alihusika; kivipi wakati yeye ni mdai? Kumbe kuhusika kwake ni pale tu alipofanya
uchaguzi wa kukubali kumkopesha huyo rafiki yake. Baada ya kutambua ukweli huu,
aliamua kumpa rafiki ya muda wa wiki moja, na kwamba kwa namna yoyote ile
asipokuwa amemlipa, hasilipe tena na deni hilo litakuwa limefutwa na hakuna
kudaiana tena. Rafiki yake kusikia hivyo aliweza kulipa pesa hiyo ndani ya muda
wa siku tatu kabla ya muda aliopewa kuisha.
Katika
stori hii tunajifunza viu vingi sana, moja ni kwamba ni vizuri kukumbuka chaguzi
unazofanya ili baadae uweze kuwajibika kwa matokeo yake; pili iwapo unatambua uchaguzi
ulio ufanya huko nyuma ni rahisi kujiepusha na kuwatwisha lawama asilimia 100%
watu wengine, kwani tumeona baada ya huyo mtu kutambua kuwa alihusika kwenye
sakata zima la kero hii ya kutolipwa, aliamua kuwajibika kwa kufanya maamuzi ya
kuweka muda wa kulifuta deni hilo ili aweze kuendelea na mambo mengine. Kingine
cha kujifuza ni kwamba mara nyingi hizi chaguzi tunazofanya kila siku bila
kujitambua kama tumefanya hivyo, huwa zinasahaurika haraka kiasi kwamba
yanapotoka matokeo mabaya, haraka haraka huwa tunadhani ni kwasababu ya watu
wengine na matokeo yake tunaingia kwenye mivutano na migongano ya kimasirahi na
watu mbalimbali waliotuzunguka.
Makosa
yanayotokana na chaguzi za kufanya mambo madogo madogo tunayofanya kila siku,
huwa yanaleta madhara makubwa kutokana na ukweli kwamba, wakati tunapofanya chaguzi
hizi huwa hazionekani haraka – Kiasi cha kuona kama vile hakuna jambo
lililofanyika. Kwahiyo, ili tuweze kutambua na kudhibiti chaguzi na maamuzi
yetu wenyewe, hatua ya kwanza kuelekea kwenye mafanikio ni kujitambua kwanza,
hii ikiwa ni pamoja na kutambua na kubaini chaguzi zote tunazofanya kila siku
kuanzia tunapo amka hadi tunapo lala. Kwa kufanya utambuzi huu tutaweza
kufahamu chaguzi na maamuzi gani ni mazuri na yapi ni mabaya; halafu yale
mazuri tuchague tena kuendeleza kwa kuyafanya kila siku ili baadae higeuke kuwa
tabia yetu itakayofanana na aina ya maisha tuyatakayo.
Mpendwa msomaji, endelea kuitumia vizuri MAARIFASHOP ili kujifunza mambo mbalimbali yatakayokuwezesha kupata mafanikio. Ili kupata makala mpya kila zinapochapishwa, bonyeza neno TUMA MAKALA MAARIFASHOP kisha sajiri barua pepe yako. Na kama unapenda kupata mafunzo ya kila siku kwa njia ya whatsap bonyeza neno MAFUNZO.
~ TWENDE KAZI
PAMOJA ~
No comments:
Post a Comment