Matokeo ni kitu kizuri kwani kinapendwa karibu na kila mtu. Matokeo ni kitu cha mwisho kutokea baada ya hatua mbalimbali na shughuli nyingi kufanyika. Kwa maana nyingine tunaweza kusema kuwa pesa ni hitimisho. Matokeo yana sifa moja nayo ni... kuisha!. Kiasi cha matokeo kilichopo hakiwezi kuongezwa kwa muda huo, bali kinaweza kupungua kutokana na watu watakavyozidi kutumia matokeo bila kuongeza. Unapokuwa, umefurahia matokeo fulani, kwa vyovyote vile utaanza kuyatumia na mwisho yataisha!. Kwahiyo, ili upate matokeo mengine kama yale ya awali inakubidi uanze mchakato upya.
Pesa nayo ina sifa kama za matokeo kutokana na ukweli kwamba ni hitimisho la kazi ya binadamu. Unaposherekea kitu ambacho ni hitimisho, moja kwa moja unakuwa umefikia wa kupata pesa. Watu wengi tunapenda sana kusherekea na kujipongeza mara tunapofanikiwa kupata pesa, huku tusijue kuwa kufanya hivyo ni kusherekea mwisho wa utajiri wetu. Mara nyingi tunapenda kusherekea pindi tunapopata pesa kwasababu kinachofuatia baada ya hapo ni kuzitumia zaidi kwenye mambo ambayo hata hayahusiani na mchakato uliozileta.

Furaha ya namna hii, siku zote huwa inadumu kwa muda mfupi sana, BAADAE tunarudi kwenye dhiki tuliokuwa nayo awali. Watu waliofanikiwa (matajiri) hawapati mihemko kama wale ambao hawajafanikiwa kwasababu wao wanapopata pesa sehemu kubwa ya pesa hiyo wanaichukulia na kuiona kama mbegu ~ furaha yao siyo kubwa kama wengine!. Matajiri wao matokeo mazuri au pesa wanayoipata inawapa motisha wa kupanda mbegu (kuwekeza zaidi), ili kupata matokeo makubwa au pesa nyingi zaidi – hii ndio tofauti kubwa kati ya matajiri na maskini.
Watu wengi tunapenda matokeo, lakini hatupendi mchakato wa kupata matokeo. Tunapenda pesa lakini hatupendi mchakato wa kuleta pesa mfukoni. Hatuko tayari kurutubisha udongo ambao ndio utustawishia mazao yetu. Ukiona unashangilia sana unapopata pesa au matokeo mazuri, lazima kuwa mwangalifu sana, kwani kuna uwezekano mkubwa ukajikuta unasahau kuboresha ile michakato yote iliyokuwezesha wewe kupata hiyo pesa unayoifurahia leo hii.
Kitu kimoja cha kujifunza ni kwamba, huwezi kubadili matokeo inabidi uyapokee kama yalivyo. Matokeo siku zote yanabadilishwa na mchakato, na kiasi cha pesa unachopata kinabadilishwa na mchakato. Unahitaji kuendelea na michakato ya kuzalisha pesa bila kujali pesa uliyokwisha ipata. Ukiwa na pesa nyingi ni matokeo, ukiwa na pesa kidogo ni matokeo, ukiwa unaumwa ni matokeo, ukiwa na afya bora ni matokeo – jambo muhimu hapa ni kwamba kila mtu anao uwezo wa kuchagua aina ya matokeo anayoyataka.
Katika jamii yetu leo hii, kuna malalamiko mengi hasa kuhusu upungufu wa pesa kwenye mzunguko au uwepo wa pesa kidogo mfukoni. Wengine wanahusisha suala hili na viongozi wao, wengine wanalalamika kuwa wao wanapata pesa kidogo kuliko wengine. Lakini tutambue kuwa malalamiko ya kupata pesa kidogo ni matokeo ya mchakato na kazi tunazofanya kila siku. Sasa wakati umefika wa kufanya tathimini ya mfumo wa maisha yetu ambao tumekuwa tukiishi huko nyuma na ambao umetufikisha kwenye hali hii ya kutokuwa na pesa.
Ukweli ni kwamba sisi wote tumepewa uwezo wa kujipangia matokeo. Kwahiyo, ni muhimu kila mmoja wetu ambaye haliziki na hali ya ukata wa pesa aliyonayo kuanza na hatua moja ya kuiambia nafsi yake aina na kiasi cha pesa (matokeo) anayoyataka. Aina na kiasi cha pesa (matokeo) tarajiwa ndiyo yawe kichocheo cha kufanya zaidi.
Tunahitaji kutambua kuwa pesa tuliyonayo sasa ni matokeo ya yale yote tunayofanya kila siku. Yale yote tunayopanga na kufanya yanaanzia kwenye fikra. Fikra zetu ndizo uzaa hisia ambazo utupelekea kuchukua hatua fulani fulani za kutuletea pesa. Hatua tunazochukua dhidi ya pesa ndizo zimeleta kiasi cha pesa tuliyonayo sasa.
Pesa kama matokeo haziwezi kuja kama ajali na wala haziji kama bahati. Ukipanga zitokee zitatokea, ukipanga zije nyingi zitakuja nyingi n.k. Watanzania wengi leo hii tunaishi na kuamini kwamba kuna siku tutabahatisha kupata pesa nyingi – nasema hili haliwezi kutokea mpaka mwisho wa dunia.
Ndiyo maana tunapofanikiwa kupata pesa mara moja tunashangilia na kusherekea sana. Baada ya kusherekea matokeo, pesa uanza kupungua na hatimaye kuisha. Pindi pesa zinapoisha inakuwa ni uzuni na vigumu sana kuipata tena, kwasababu njia iliyoleta pesa mwanzoni hatukujishughulisha kuiboresha. Matokeo yake kila siku tunaanza mchakato mpya ambao hauna uhusiano na mchakato wa mwanzo ~ kwa njia hii ni vigumu kupanuka!.
Mtaani kuna kelele za malalamiko juu ya pesa kama vile; “pesa haipatikani, ni ngumu, kupata pesa ni kazi, pesa ina siri nzito”hadi majumbani kwetu. Kelele hizi zinakera kiasi kwamba ukikaa ukazisikiliza unajenga imani inayofanana na hayo malalamiko. Mwisho wake unakata tamaa na kudhani kwamba pesa haipatikani kirahisi ~ Nasema pesa inapatikana kirahisi!.
Sababu inayotufanya kuona kama kupata pesa ni ngumu ni kwamba watu wengi hatutaki kujua wala kusikia kuwa pesa ni matokeo ya fikra tulizonazo, hatuamini kwamba tunaweza kupata pesa kwa kubadilisha fikra tulizonazo juu ya pesa, hatutaki kusikia kuwa mchakato wa kukamilisha kitu chochote kikubwa huwa unachukua muda – yote hayo sisi hayana nafasi, tunachotaka ni pesa tu!.
Hatutaki kusikia kuwa pesa ni kitu kisichoonekana, sisi tunakataa na tunasema pesa inaonekana tena kwa rangi tofauti tofauti. Kumbe pesa ni mawazo ambayo yako vichwani mwetu na hayaonekani – “pesa iliyoko mawazoni mwetu ni nyingi kuliko hiyo tunayoiona”. Kumbe kazi yetu inatakiwa kuwa ni kuanzisha na kusimamia mchakato wa kuitoa kwenye hali ya kutoonekana hadi kuonekana. Hapa lazima tufanye kazi ya kuweka malengo yanayoambatana na mpango wa utekelezaji _ hayo yakifanyika “pesa” kama matokeo lazima itokee.
Watu waliofanikiwa siyo kweli kwamba huwa hawaishiwi pesa bali wanapoishiwa (kupata hasara), mara nyingi utulia kidogo na baadae uanza mara moja kushika ile njia waliyopitia mwanzoni na haiwachukui muda wanapata pesa zaidi ya ile waliyoipata awali.
Matajiri wengi hawana tabia ya kusherekea wanapopata pesa, badala yake uanzisha mchakato mwingine wa kupata pesa kabla hata ya ile pesa waliyonayo kuisha. Uhalisia unatuonyesha kwamba wewe binafsi unao uwezo wa kupanga kiasi cha pesa unachotaka kukipata na ukakipata.
Ushauri wangu leo ni kwamba kuanzia sasa acha kuwa mtu wa kusherekea pesa unayopata kwa kununua zaidi vitu ambavyo vinakufanya upate pesa nyingi zaidi. Inatakiwa unapopata shilingi moja iwe kichocheo cha wewe kuwekeza zaidi na zaidi. Lazima pesa unayoipata uione na kuichukulia kama mbegu ambayo ikipandwa inazalisha pesa nyingi zaidi.
Jitahidi kutenga asilimia fulani kutoka kwa kila pesa unayoingiza, ili iwe ni mbegu ya kupanda kila msimu unapowadia. Pesa hiyo inayotengwa kama mbegu, ikitunzwa vizuri inatosha kuwekezwa kwenye michakato mingine na hatimaye ikatengeneza chanzo kingine cha pesa.

Kwahiyo, tukienda kwa mpango huu tunajikuta tuna vyanzo vingi vya pesa. Tulianza na chanzo kimoja cha pesa na sasa tuna vyanzo viwili, vitatu, vinne……n.k. Mwisho wake tutafikia mahala ambapo tutakuwa watu wa kupata pesa kama matokeo kila siku na mwisho tunaingia kwenye kundi la wachache wenye uhuru wa kipato na mafanikio makubwa.
No comments:
Post a Comment