"Ili kufanikiwa ni lazima hamu yako ya kubadirika iwe kubwa kuliko hamu ya kubaki ulivyo sasa" ~ Cypridion Mushongi
Neno “hamu” limekuwa likitumika visivyo. Mara nyingi, hamu imeelezwa kuwa ni “kile kitu tunachofikiria kupata” Hapana. Hamu ni...
kuwa na tamaa ya kupata kitu kiasi cha kujitoa maisha yako yote, kwaajili hiyo. Ni mpaka huwe tayari kufa ndipo utapata kile tunachotafuta, bila hilo hakuna namna tutaishia kutamani na kutumaini basi! Hamu ni kuwa na tamaa au kiu ya kutosha kiasi cha kuwa tayari kujitoa muhanga kwaajili hiyo”.
Jiulize ni mara ngapi umekuwa na wazo zuri lakini ujafanya jitihada zozote, kwasababu hukutaka au hukuwa na hamu ya kutosha? Tunapotaka kupata kitu fulani kwa hali na mali lazima tuonje radha yake. Hii ni muhimu sana katika kujenga matumaini yako, kwasababu matumaini siku zote ni kile unachoomba kupata lakini hujakiona au hujakipata.
Hamu kubwa ukuwezesha wewe kusimama mpaka utakapoona kile ulichoamini kuwa kitatokea. Kuna watu wachache walio na ujasiri wa kutosha kuweza kuishi maisha ya namna hii. Yote haya yanategemea ni kwa kiasi gani una “hamu” na malengo ya maisha bora.
Wewe unayo mimba ya mambo mengi mazuri ambayo kwasasa hakionekani—ikiwemo maombi ufanyayo kila siku kupata pesa. Unapoomba kitu chochote kwa imani na matumaini, tayari kinakuwa njiani kukujia. Huwezi kukiona, lakini kama unaamini basi tayari kiko kwenye mchakato. Mungu anakutaka wewe kuomba vitu vingi kutoka kwake, kwasababu anazo baraka nyingi na uwezo anaotaka utoke nje, ili kusaidia jamii.
Kwahiyo, chochote utakachotaka unapofanya maombi lazima utapata—lakini utapata tu kile ulicho na hamu nacho. Siyo kile unachoomba kukipata bali unatakiwa kuwa na hamu ya kile kitu kila unapoomba. Kuna vitu vingi tunamuomba Mungu ambavyo kimsingi hatuna hamu ya kutosha kuwa navyo.
Hatuwi na tamaa kiasi cha kujitoa Maisha yetu yote kupata kile tunachotaka kuwa nacho. Mara nyingi hatuwi na hamu ya kutosha kiasi cha kuwa tayari kufa kwaajili ya mafanikio tunayoyataka. Wengi wetu tunatumaini Mungu atafanya. Kama ikitokea, basi mshukuru Mungu—kama haitatokea mshukuru Mungu.
Hamu uliyonayo ndiyo uongoza mwelekeo wa maisha yako. Watu wengi hukata tamaa katika Maisha, kwasababu huwa hawana hamu na kitu chochote kiasi cha kutosha kutafuta hicho kitu.
Kama hauweki malengo kwaajili ya uwezo wako na kusema kuwa sitajali watu wanasema nini juu yangu, basi ujue hutapata kuishi Maisha ya ndoto yako. Lazima useme “hivi ndivyo ninavyotaka kuwa”. Lazima huwe na malengo ambayo unatamani sana kuyatimiza kwa gharama yoyote.
Kama hauko tayari kufanya hivyo, tayari ujue kuwa umeishapoteza, kwasababu ni “hamu” yako ndiyo itaendelea kukuchochea na kukuwezesha wewe kuendelea na safari yako ya kuelekea kwenye mafanikio bila kuchoka.
Ili upate kile unachotaka kuwanacho, lazima huwe na shauku ya kukipata. Lazima kuwa na lengo ambalo una hamu nalo bila kujali gharama zake.
Maisha yanayotuzunguka bianadamu yamejaa sana matangazo kwaajili ya kuteka mawazo yetu au uangalifu wetu. Pia maisha yetu yana msongamano ulijaa vitu vingi ambavyo kila wakati utukatizakatiza, na hivyo kutufanya wakati mwingine kushindwa kufanya kile tunachofanya. Matangazo kutoka kila upande, yanajaribu kukutikisha, ili utoke kwenye malengo yako.

Kama huna malengo, matangazo yaliyopo yatakupatia lengo mojawapo ambalo ukilitimiza halitakuwa na manufaa kwako. Lazima ujue kabisa ni wapi unataka kwenda na unataka kuwa nani. Mahitaji yako yanakutaka uyape mwelekeo.
Unapotafuta kitu jitahidi kuwa na hamu ya kile unachotafuta. Kataa kukatizwakatizwa. Nguvu ya uwezo wako itaachiwa kadiri utakavyozidi kujitoa kwa kila hali katika kufikia kile unachotamani kupata.
Katika kujenga hamu kubwa kwa mambo yote unayopenda kuwa nayo, endelea kuwa karibu na MAARIFA SHOP ambako ujuzi na maarifa ya kukuwezesha kupata mafanikio makubwa ni halali yako.
No comments:
Post a Comment