Thursday, January 19, 2017

Unafahamu ni Kwanini Uko Hivi Ulivyo?


“Uwezo wako wa kutawala na kupambana na changamoto za dunia, una uhusiano wa moja kwa moja na jitihada unazoziweka katika kukamilisha kazi~ Cypridion Mushongi

 

Kila binadamu amepewa uwezo mkubwa kama zawadi kwaajili ya kukuwezesha kupata kitu chochote atakacho maishani. Lakini, ili zawadi yako ya uwezo ikunufaishe, unahitaji kufanyia kazi uwezo wako. Ukweli ni kwamba tumepewa uwezo kama zawadi na wakati huo huo kama amri kwasababu,
ili tuweze kufaidi uwezo tulionao ni lazima tufanye kazi, ndipo matunda yake yapatikane. Tunapokiuka amri hiyo, ambayo hadi leo tunaendelea kuikiuka, adhabu yake ni umaskini uliokithiri.

Watanzania wenzangu nyie ni mashaidi ambao kwa miaka mingi mmeshuhudia jinsi ambavyo umaskini unazidi kukithiri kila kona ya nchi hii. Kwasasa, watu wengi wamekata tamaa na hawana matumaini kama umaskini unaweza kuondoka kwao. Wanadhani, watu wengine ndio wanaweza kuwaondolea umaskini. Jambo la kuondolewa umaskini na mtu mwingine, limekuwa ndiyo ndoto kuu kwa watu walio wengi. Lakini, kwa jinsi mambo yalivyo na yanavyokwenda, inaonekana ndoto hii haitatimia kamwe.

Leo tena nasema “tusikate tamaa” lakini wakati huohuo tubadiri fikra zetu. Tukiruhusu akiri yetu kufunguka tutakuja kugundua kuwa ni lazima tuwajibike kwa kufanyia kazi uwezo wetu wote ambao tulipewa kama zawadi, ndipo tutaweza kupata kile kilicho haki na wajibu wetu — “yaani maisha bora”.

Kile alichokupa Mungu ni “uwezo” na wewe ndiye mwenye kumiliki uwezo huo, lakini hutapata kile ulicho haidiwa yaani “maisha mazuri” kama hutafanya kazi ya kukidai. Kwahiyo, kama unahitaji pesa kulipa karo ya mtoto wako, usisubiri mtu mwingine akudondoshee shilingi mfukoni mwako. Amka na fanya kazi, ili kufaidi zawadi aliyokupa Mungu —“UWEZO.”

SOMA; Ajira Siyo Kazi ni Ajira na Kazi Siyo Ajira ni Kazi

Kazi tuliyonayo wale wote tuliodhamiria kutafuta maisha bora ikiwemo uhuru wa kipato ni kufanyia kazi “uwezo” ambao tunao tayari. Kwa maneno mengine kazi inaleta na kukuza uwezo wa kuendelea mbele na hatimaye kuboresha maisha--tajirika. Bila kazi ulichonacho ni uwezo tu. Kazi ni pale unapotumia uwezo wako na nguvu yako ya akiri kufanya au kutenda jambo fulani.

Mungu amekupa rasilimali nyingi mfano: utajiri wa maarifa, vipaji, na uwezo; kwahiyo, KAZI inakuwa ndiyo njia muhafaka kuweza kugundua rasilimali hizo. Kama hutafanya kazi, itakuwa vigumu kwako wewe kutambua rasilimali ulizonazo ambazo kimsingi ndizo zenye kukusaidia kuondokana na umaskini.

Ukifanya kazi na kugundua rasilimali hizo ni rahisi kujiamulia kuishi maisha unayoyataka. Kwa maneno mengine, kazi ni njia ya kuzalisha matokeo unayoyataka. Endapo utaamua kuchanganya “kazi” na akiri katika kufanya yale yote ufanyayo, ni lazima ushindi upatikane. Kwahiyo, kujitoa kwa kufanya kazi ni ufunguo wako wa mafanikio.

Kazi utoa fursa ya kutimiza lengo la maisha. Kama ukiona ufanyi kazi basi ujue hautatimiza malengo yako hapa duniani. Watu wengi ambao ni mzigo kwenye jamii --ni wale wanaopokea mshahara bure na huduma za jamii bure—siyo sehemu ya nguvu kazi. Elimu bure, matibabu bure, kodi ya nyumba bure, huwa wanapokea kutoka kwenye mifuko ya wale wanaofanyakazi na kulipa kodi. Kwahiyo, mtu yeyote anayetaka msaada kutoka serikalini ili kulipa umeme basi anaishi nje ya mfuko wake.

Katika mfumo wa maisha, kila mmoja anatakiwa kufanya kazi. Unatakiwa kufanya kazi. Uwezo wako wa kutawala na kupambana na changamoto za dunia, una uhusiano na jitihada unazoziweka kukamilisha au kumaliza kazi ulizopewa na Mungu. Ukikataa kutumia nguvukazi, hakuna matunda yatakayopatikana.

Yawezekana unayo mimba yenye majibu ya baadhi ya matatizo makubwa ya dunia. Kama unataka kuona ndoto yako inatimia, bora uwe tayari kufanya kazi. Mpaka utakapoanza kufanya kazi, nguvu yako ya kufaidi ubinadamu itaendelea kubaki bila kutumika.

Unaweza kuwa na ndoto na maono unayoyataka. Lakini, mpaka umue kufanyia kazi uwezo wako na kama siyo hivyo, maono yako yatabakia siyo kitu kingine zaidi ya mawazo ya matamanio basi! Kama haufanyi kazi basi jua kuwa una-matamanio au mawazo tu. Unapoteza muda wako kwa mawazo yasiyokuwa na thamani.

Kazi ni njia ya kutengeneza kile unachokiona kwa macho ya ubongo kuwa kile unachoonekana kwa macho yetu ya kawaida. Kazi ndiyo upanua rasilimali ulizonazo. Suala siyo rasilimali uliyonayo bali suala ni unazalisha kazi kiasi gani kwakutumia rasilimali uliznazo ambazo ndizo zitaleta umaskini au utajiri.

Kuwa na uwezo bila kufanya kazi ni umaskini kwasababu utashi wako wa kufanya kazi ni ufunguo katika kufaidi uwezo wako. Swali la uhalisia siyo kiasi gani cha uwezo unacho bali ni uwezo kiasi gani utafanya kuonyesha. Kila mmoja anao uwezo – ambao umejificha, lakini siyo kila mmoja anafanya kazi kutoa kile walichonacho akirini.

Kazi inaachia na kutengeneza mazingira. Watu wengi upendelea kuvutika kuelekea kwa wale watu wanaofikiri na kutenda kama wao wanavyofanya. Na hii ni kweli pia kwa wale wanaokwepa kazi. Wavivu, huwa hawapedi kuwa kwenye kundi la watu mahili kwasababu uvivu wao uonekana haraka.

Kwahiyo, kazi ni ufunguo katika kuanzisha mazingira chanya. Tabia yako ya kujitoa, kuvumilia, nidhamu ya kukamilisha kazi za ajira, kanisa, familia, biashara n.k vitavuta makundi ya watu wengine wanaopenda kufanya kazi kama wewe. Vile vile kutokuwa na kazi kutavutia upande wako watu ambao hawapendelei kufanya kazi. Kwahiyo, makundi ya watu utakaokuwanao yataonyesha na kukuhamasisha kupenda kufanya kazi au kutofanya kazi.

Je una kiu ya kufanya kitu fulani. Je? Uko tayari kujitoa ili kutimiza ndoto yako? Sasa tengeneza mpango kazi na uufuate. Kuna tofauti kati ya mpango na kutaka kutenda haraka. Kupenda kupata haraka ni pale unapojaribu kupata kitu fulani bure bila kufanya kazi. Hali hii inapelekea umaskini.

Lakini kufanya kazi kwa bidii ni kutengeneza mpango na kutumia jitihada kuona kwamba mipango hiyo inalipa. Mfano: unataka kuwa polisi, mwanasheria, mwekezaji, mvuvi? Wekeza nguvukazi kwenye ndoto yako hiyo. Anza urafiki na mtu ambaye anafanyia kazi kile unachopanga kufanya, alafu fanya kazi naye kujifunza, biashara, au utaalam.

Kukamilika kwa mpango wako kunahusiana na utashi wako ulionao wa kufanya kazi, kama ilivyo maendeleo yake. Vile vile, kuachiwa kwa uwezo wako kunategemea matumizi ya jitihada zote za lazima kuwa vitu vinavyoonekana. Anza mwenyewe kufanya kazi, usisubiri maisha yakusukume kufanya kazi. Mwisho lakini siyo kwa umuhimu napenda kusema kuwa, kazi ni ufunguo wako wa kuendelea binafsi, tija, kuridhika na mafanikio. Na kwahiyo, bila kazi, huwezi kukamilisha chochote na “kupitia kazi umekuwa kama ulivyo sasa!”

No comments: