Kila mwaka serikali inaposoma bajeti yake, watu wengi ujenga matarajio makubwa, ikiwa ni pamoja na wengi kutarajia kupata unafuu fulani katika maisha yao. Wengi uiangalia na kutathimini bajeti kwa mtazamo wa kupata mguso wa moja kwa moja kwenye maisha yao.
Kikubwa kinachofuatiliwa kwenye kila bajeti, ni
pamoja na kuona kama inalenga kupunguza kodi kwenye vitu mbalimbali, ambapo kila mtu ujaribu kuangalia eneo alilopo. Kama ni mkulima, yeye uangalia zaidi suala la ushuru wa mazao, wafugaji wanaangalia mustakabli wao juu ya malisho, ardhi, miundombinu ya maji n.k. Kwahiyo, ndo kusema kuwa watu wengi wanataka unafuu wa kodi na wakati huo huo wanataka huduma zitolewazo na serikali yao.
Lakini, embu tuangalie chimbuko na historia ya kodi ambayo inaonekana kwa namna moja au nyingine inaumiza, kiasi cha makundi mbalimbali ya kijamii kutaka na kuiomba kila siku serikali iwapunguzie. Historia ya kodi katika nchi za Ulaya na Marekani, inatuonyesha kuwa hapo zamani kulikuwa hakuna kodi, labda pale serikali ilipokabiliwa na majanga ikiwemo vita ndipo wafalme katika nchi hizo, walijaribu kuwahamasisha watu wao kuweza kuchanga fedha kwa lengo la kukabiliana na vita.

Mfano mwaka 1799—1816, nchini Uingereza, serikali iliamua kuchangisha fedha kutoka kwa wananchi ili kupigana vita dhidi ya Napoleon. Mwaka 1861-1865, Marekani nayo ilichangisha pesa kwaajili ya vita. Kwahiyo, tunaona kuwa enzi hizo kodi ilikuwa ni kitu cha hiari na cha matukio ya muda.
Kadiri mahitaji ya fedha kwa serikali yalivyozidi kuongezeka kutokana na sababu mbalimbali, ndivyo watawala walivyofikiria kulifanya suala la ulipaji kodi kuwa kitu cha kudumu na lazima kwa kila mtu mzima. Mfano, mnamo mwaka 1874, nchi ya Uingereza ilipitisha sheria iliyohalalisha kodi kuwa ya kudumu na ya lazima hasa kwa matajiri. Ilipofika mwaka 1913, Marekani nayo ilipitisha sheria ambayo ilifanya kodi kuwa jambo la kikatiba, na tangu hapo kodi ikawa ni lazima Marekani.
Hapa tunaona kuwa historia ya kodi inatuonyesha kuwa asilimia kubwa ya kodi inayokusanywa na serikali chanzo chake ni wananchi. Maana yake ni kwamba ni vigumu sana pesa ambayo ilitozwa kutoka kwa watu kuwarudia moja kwa moja. Kwahiyo, kuendelea kutegemea bajeti ya serikali ili kupata unafuu wa maisha siyo mkakati mzuri hata kidogo. Nasema siyo mkakati mzuri kwasababu, kama ulitozwa kodi kwaajili ya kuendesha mambo ya umma, iweje utegemee pesa moja kwa moja kutoka kwa yule yule aliyekutoza kodi? Sipendi kuamini kama wanaweza wakapanga kwenye bajeti, kukuletea pesa ambayo walishaichukua kutoka kwako. Na kama wakikuletea, kilichowafanya wakutoze pesa kitakuwa kimeisha?
Kuna wakati mwingine napenda kuamini kuwa, kodi ikishatozwa haiwezi kuja tena kwako moja kwa moja kama ilivyotozwa mwanzoni. Kwani mara tu baada ya pesa kwenda serikalini inakwenda kushughulika na mambo ya jumla (umma) zaidi ambayo ni ya kujenga mazingira rafiki kwako wewe kuweza kuishi na kufanya kazi zako sawa sawa.
Iwapo bajeti ni kwaajili ya mambo ya umma kwahiyo ni nani anapata unafuu wa kodi?
Kwa jinsi bajeti ilivyo, siku zote anayebeba mzigo mkubwa wa ongezeko la kodi ya kila mwaka ni MTUMIAJI/MLAJI. Kwahiyo, ili uweze kufaidi bajeti ya serikali duniani kote ni lazima uwe “mwekezaji” na kama huwezi uwekezaji basi jitahidi huwe “mzalishaji”. Nasema hivyo kwasababu, ukiwa mwekezaji na mzalishaji ni rahisi sana kuhamisha makali na machungu yatokanayo na ongezeko la kodi kwenda kwa mlaji au mtumiaji wa bidhaa/huduma. Endapo wewe unabakia kuwa mlaji, kwa vyovyote vile hauna namna lazima mzigo wote uubebe kadiri unavyokujia.
Kwa mfano; baada ya bajeti ya mwaka huu (2017/18) kusomwa bungeni, baadhi ya tozo/kodi (road license na motor vehicle) kwenye magari zimeondolewa na badala yake, serikali imeamua kuwa itaanza kutoza shilingi 40/- kwa kila lita ya mafuta (diesel na petrol). Maana yake ni kwamba hata wale ambao walikuwa hawana magari lakini wanatumia mafuta watatakiwa kulipa kodi hiyo. Hapa watumiaji wa mafuta ni kama wale wenye magari ya abiria, mashine za kusaga nafaka, mitambo ya kuzalisha umeme, wenye magari binafsi ya kutembelea n.k.
Mwenye kufanya biashara ya abiria, mara moja atatafuta namna ya kuihamishia kodi hii kwa wanaotakiwa kumlipa nauli. Mwenye mashine ya kusaga nafaka, atatafuta namna ya kuihamishia kodi hii kwa wale wanaokuja kununua unga na wale wanaokuja kupata huduma ya kusaga nafaka zao. Vilevile, kwa yule mwenye kufua umeme, ongezeko la tozo kwenye mafuta ataweza kuhamishia kwa wale wote watakaokuja kununua umeme. LAKINI, yule mwenye kutumia gari lake kwaajiri ya kutembelea au shughuli nyingine za kifamilia, yeye atakuwa hana namna yoyote ile ya kuweza kuhamisha ongezeko la tozo kwenye mafuta. Itabidi kulipa mwenyewe, kwasababu yeye anakuwa ndiye mlaji na mtumiaji wa mwisho wa mafuta.
Mfumo wa maisha ya kodi uko hivyo siku zote, ambapo bei nyingi wanazotozwa walaji, lazima ziwe ni zile zinazozingatia gharama zote alizotumia mwekezaji/mzalishaji na faida juu yake. Wahanga wakubwa maumivu yatokanayo na ongezeko la kodi za kila mwaka ni wale wote wanaotegemea kipato kitokanacho na mshahara. Maana yake ni kwamba, wengi walioajiriwa siyo rahisi kutajirika, kwasababu siku zote mahitaji makubwa ya kodi, lazima yawaguse na hakuna namna ya kuepuka mzigo huo. Hali ya kukatwa kodi mara tatu tatu, nne nne na hata tano tano ni jambo ambalo linawakumba waajiriwa wengi duniani kote.
Wakati wa kuacha kulalamikia bajeti na ongezeko la kodi ni leo, na unaweza kuacha kulalamika kwa kuanza kuelekeza nguvu na maarifa kwenye uwekezaji, kwani mwisho wake uwekezaji unakufanya kuwa mtu wa kugawa riziki kwa makundi mbalimbali. Kumbuka maisha yetu hapa duniani kwasasa yanategemea sana mwekezaji au mzalishaji—hawa ndio chimbuko la bidhaa na huduma ambazo ndiyo ukidhi mahitaji yetu ya kila siku.

No comments:
Post a Comment