Saturday, October 31, 2015

Fahamu Mambo Sita Kuelekea Kwenye Mabadiliko Chanya



1. Acha kuamini yale uliyodhania ni kweli: Bahati mbaya, kuna mambo mengi ambayo huwa tunayakukubali na kuamini kadiri tunavyozidi kukua ambayo yanaweza....
kudhoofisha matumaini na matarajio ya mafanikio, furaha, na kutimiza ndoto za maisha yetu ya baadae. 

Mojawapo ya vitu ya vitu vinavyokuzuia wewe binafsi kuchukua hatua fulani fulani katika maisha, ni pamoja na dhana iliyozama ndani ya fikra ambayo ni “mimi siyo mzuri kiasi cha kutosha katika hili”. 

Imani hii ni ya msingi na ni ya kwanza ambayo huwa inasababisha watu wengi, kujisikia kuwa hawawezi na pia kujiona wenye mapungufu kila mara, hasa pale wanapokabiliwa na changamoto za kimaisha.
 

Ni kwa muda mrefu sasa, tumekuwa na tabia ya kujiona kuwa watu wengine ni bora zaidi kuliko sisi, eti kwasababu sasa hivi, wanafanya vizuri kuliko sisi. Tunajihisi kwamba wao lazima watakuwa na thamani kubwa kuliko sisi na kwahiyo, lazima sisi tutakuwa na thamani ndogo kuliko wao.

Hali hii ya kujiona kuwa kila wakati sisi tuna thamani ndogo ina kwenda ndani zaidi kwenye mzizi wa ubongo au akiri zetu na kusababisha sisi kutojithamini na kujipambanua kama watu wa chini wasiokuwa na mvuto wowote mbele ya jamii inayotuzunguka. Matokeo yake, tunaanza kujihisi ulofa na kujiona wahitaji wakubwa wa misaada mingi ya kijamii.

Kutokana na kujiona kuwa sisi ni watu wa hali ya chini, basi mara nyingi tumekuwa watu wa kuridhika na vitu vidogo sana kuliko vile ambavyo tuna uwezo wa kuvipata. Mwisho wa yote hatuna hata picha ya maisha mazuri na ndiyo maana hata huwa hatuweki malengo na wala kuwa na ndoto za kufanya na kumilik vitu vikubwa.

Kitu cha msingi amabcho ni muhimu sana wewe kukielewa ni kwamba, ili kuendelea unahitaji kujenga imani mpya ya kwamba, wewe una uwezo na kipaji kikubwa sana na pia una uwezo wa kufanya vitu vikubwa katika kila nyanja ya maisha ambayo ni muhimu kwako.

Tambua kuwa wewe unao uwezo ambao hauna kikomo na unaweza kufanyia kazi na kupata kila kitu ambacho hujawahi kuwa nacho leo hii. Kama mmoja wa waandishi wa vitabu “Shakespeare” aliwahi kusema kuwa “upepo mkali na mingurumo ya radi ni utangulizi wa mvua kubwa inayokuja kunyesha baadae”. Akimaanisha kwamba chochote ulichowahi kufanya au kukamilisha siku zilizopita ni kiashiria au fununu za kitu unachoweza kufanya mbeleni na siku za baadae.


2. Jisemee maneno chanya moyoni: Mojawapo ya maneno yenye nguvu katika msamiati wako ni yale ambayo huwa unajisemea kimoyomoyo na kuyaamini. Kujiongelea mwenyewe, au majadiliano ya ndani kwa ndani ya akiri (ubongo), ndiyo uchangia asilimia 95% ya hisia ambazo mtu huwanazo kila siku.

Ukizungumza na nafsi yako, sehemu ya ubongo inayotunza kumbukumbu inayakubali maneno haya kama amri au komandi. Baadae inarekebisha tabia yako, picha yako binafsi, na lugha yako ya mwili ili iweze kuendana na mfumo na utaratibu wako kwenye maneno hayo unayojiongelea mwenyewe kila siku.

Kama unataka mabadiriko katika maisha, hakikisha kuanzia sasa na kuendelea, unajisemea maneno kwa kufuata mtazamo wa jinsi unavyotaka uwe, pamoja na vitu unavyotaka kufanya. Kataa kusema chochote kile kuhusu wewe ambacho kwa dhati haukipedi.

Maneno chanya ambayo unatakiwa kujiambia mara kwa mara ni kama vile, “Ninaweza kufanya!” tena na tena. Kabla ya kufanya kitu chako chochote cha muhimu, rudia kwa kujisemea maneno ya “ninaweza kujipenda mwenyewe!” Sema mimi ni bora! Mimi ni bora! Mimi ni bora!” tena na tena kama unavyomaanisha. Alafu simama wima na imara, weka tabasamu la kujiamini kwenye uso wako na kufanya kile kilicho bora ambacho unaweza kukifanya. Na muda si mrefu itakuwa tabia yako.

3. Jua kuwa unastahili kila kilicho bora: Kutokana na tabia ya watu kupenda kukosoa wenzao, hali hii imesababisha watu wengi kujenga tabia mbaya ya “kujikana wenyewe na kujiona hawawezi”. Ni kwamba, hawaamini kwa dhati kuwa wanastahili na ni haki yao kuwa na mafanikio. Tabia ya kujikana sisi wenyewe, imesababishwa pia na maneno tuliyoambiwa na wakubwa zetu tangu utotoni, kwamba kuwa maskini ni jambo la kawaida LAKINI kuwa tajiri ni dhambi.

Kama umekua ukiwa na mawazo na hisia za kujiona hustahili vitu vizuri, kwa sababu yoyote hile na ukaweza kupata mafanikio katika eneo lako la kimaisha, basi unaweza kupatwa na kitu kinachoitwa “tabia ya kujidanganya”.

Utajisikia kwamba wewe ni kinara/mahili katika mafanikio yako, na kwamba baadae jamii inayokuzunguka itakuja kupata ukweli halisi. Haijalishi kiwango chako cha mafanikio kutokana na kufanya kazi kwa bidii, lazima utakuwa na ile hali ya kuogopa, ambapo kila wakati utakuwa unawazia kuwa utajiri wako utachukuliwa na watu wengine.

Kama ukijisikia kuwa kama mtu wa kujipa sifa bandia, kila wakati utajisikia vibaya kwa wewe kupata mafanikio makubwa kuliko wengine. Ili kuepuka hisia za kujisikia vibaya, watu wengi ujiingiza kwenye kujidhoofisha wenyewe. Mathalani, watu wa namna hii wanakula sana, wanakunywa pombe sana, wanaterekeza familia zao, wanajihusisha na tabia ambazo hazitabiriki, na mara nyingi uweza kupoteza pesa zao kwenye maisha ya anasa, ufujaji na uwekezaji usiokuwa makini. Huwa wanajisikia kwa ndani kuwa hawastahili kuwa na mafanikio waliyonayo. Matokeo yake, ujikuta wakipoteza utajiri mkubwa waliokwisha upata.

4. Jielekeze katika kusaidia watu wengine: Ukweli ni kwamba wewe unastahili kila kitu ambacho unakipata kwa haki kwa kufanya kazi nzuri sana na kuzalisha au kusambaza bidhaa/huduma, ambazo zinachangia katika kuboresha kazi na maisha ya watu wengine. Katika jamii iliyo katika mfumo wa uchumi wa soko (market economy), kama hii ya kwetu, mihamara (transactions) yote ya pesa kati ya mtu na mtu ni kwa hiari.

Watu ununua kitu fulani, kama tu wanajisikia kuwa mahitaji yao au maisha yao yataboreka baada ya kununua na kutumia kitu chako. Kwahiyo, unaweza kufanikiwa sana, kwa kutoa tu! vitu wanavyovitaka watu, ili kuboresha maisha yao na kazi zao. Kadili utakavyosaidia vizuri watu wengi, ndivyo utakavyozidi kustahili kuingiza kipato kikubwa sana.

Watu wanaofanya vizuri kwenye jamii zetu ukiacha wale wachache, ni wale ambao wanatoa huduma au kusaidia wengine vizuri zaidi kuliko mtu mwingine au kitu chochote. Nguvu yako yote, lazima uielekeze kwenye kusaidia watu wengine vizuri. Alafu, utastahili kila shilingi utakayoipata.

Raisi wa zamani wa Marekani Abraham Lincoln aliwahi kusema kuwa “njia nzuri na ya pekee ya kuweza kusaidia maskini ni kutokuwa mmoja wapo”. Katika jamii yetu, kadili unavyozidi kufanikiwa kifedha, ndivyo unavyozidi kutozwa kodi sana. Kodi hizi ndizo husaidia kulipia karo, matibabu, barabara, ulinzi na usalama, na vitu vingine muhimu ambavyo jamii yetu inazalisha.

Unaweza kujivunia kuwa umefanikiwa kupata uhuru wa kipato. Kwa kuweza kupata pesa nyingi, unatoa mchango mkubwa kwa watu wengi. Kwa maana nyingine ni kwamba unafanya vizuri kwaajiri yako kwa kufanya vizuri kwa watu wengine. Basi kama unalitimiza hili, ni vizuri zaidi kurudia neno “Ninastahili kila shilingi ninayoipata kutokana na kutoa mchango wangu kwa watu wengine kwa kuwapa bidhaa na huduma wanazohitaji kuboresha maisha yao”. Ninajivunia mafanikio yangu.”

5. Jiamini wewe ni mtu wa hali ya juu na wa pekee: Ili kujijengea tabia ya kujiamini, ni vizuri ukatambua haya kuwa wewe ni mtu makini na mzuri. Wewe ni mkweli, wewe ni mtu nadhifu na mchapa kazi. unajali watu wengine kwa heshima na uchangamfu. Wewe umejitoa na unapenda familia yako, marafiki, na kampuni yako.Wewe ni imara, unajiamini, na mwajibikaji. Wewe ni mwelewa sana, intelligent, na mwenye uzoefu.Wewe ni muhimu siyo tu kwa watu wa karibu bali na kwa wanajamii wengine. Ulizaliwa kwasababu maalumu, na unataka kutimiza ndoto kubwa. Wewe ni mtu mzuri katika kila hali.




Kauli zote hapo juu ni tamko linalodhihirisha upekee wa mtu na maisha yake. Yawezekana isiwe hivyo kwako kwa asilimia 100, lakini ni maelezo mazuri juu ya wewe ulivyo ndani yako na huko unakokwenda kwenye maisha yako. Unapokuwa umekubali kwa hiari kuwa wewe kiukweli ni wa thamani na mtu mwenye kustahili, utaonyesha katika kila kitu unachosema na kutenda.

Kadili muda unavyokwenda, itafikia kipindi itakuwa kweli kwako wewe na uhalisia wako utakuwa ukweli. Rudia kila mara kwa kujitamkia maneno haya, “ninajipenda mwenyewe na ninapenda maisha yangu”. “Mimi ni wa pekee na mtu mzuri katika kila hali na kila mara ninafanya vizuri kwa kila kitu ninachojaribu kufanya.

6. Tembelea duka la programu za akiri: Fikiria kuwa kama kungekuwa na duka ambalo linauza programu za akiri; ungeweza kununua kila imani, fikra yoyote unayoitaka na kuiweka kwenye akiri yako, na ndo aina ya mtu ambaye ungefanana naye kuanzia hapo. Kama duka hilo lingepatikana, ambalo wewe ungeweza kununua aina yoyote ya kifurushi cha imani, fikra na tabia, wewe ungechagua kipi?: 


LAKINI ili duka liko wapi? Ili kuweza kuliona duka hili zingatia pendekezo hili ~ Jiangalie jinsi ulivyo na utafute ni kitu gani watu wenye furaha na mafanikio makubwa wanacho kama imani ya ndani kabisa, halafu jipatie kifurushi cha imani na tabia kama za watu waliofanikiwa kwaajili yako mwenyewe. Kisha ingiza kifurushi hicho kwenye ubongo wako.

Imani ya ndani na ya msingi ambayo unaweza kuiga wewe binafsi ni hii “Mimi ni mtu mzuri jumla na nitakuja kuwa mwenye mafanikio makubwa katika maisha na kila kitu kinachotokea kwangu, kiwe kizuri au kibaya ni sehemu tu ya mchakato. Mchakato wa kupata mafanikio makubwa na furaha ni lazima kwangu mimi.”


Kama kwa dhati kabisa unaamini hilo, basi tayari umejihakikishia kuwa na furaha na mafanikio. Kwa maana hiyo kila changamoto unazokutana nazo, huwa zinakujia, ili kukufundisha somo muhimu ulilohitajika kulijua, ili kufanikisha malengo yako. 


Kwahiyo, ukilitambua hili, unakuwa mtu chanya na mwenye matumaini makubwa muda wote. Rai yangu kwako mtanzania mwenzetu, jifunze jinsi ya kujiprogram, ili dunia yako ya ndani ifanane na mtu unayetaka uwe au maisha unayotaka kuwa nayo, hakika utafanikiwa sana.

Mpendwa msomaji, endelea kuitumia vizuri MAARIFASHOP ili kujifunza mambo mbalimbali yatakayokuwezesha kupata mafanikio. Ili kupata makala mpya kila zinapochapishwa, bonyeza neno TUMA MAKALA MAARIFASHOP kisha sajiri barua pepe yako. Na kama unapenda kupata mafunzo ya kila siku kwa njia ya whatsap bonyeza neno MAFUNZO



No comments: