"Fahamu Sababu 5 Kwanini Wewe Hutakiwi Kuwa Mjasiriamali"
Mpendwa msomaji wa mtandao huu wa MAARIFASHOP, utakumbuka kuwa ni mara nyingi nimekuwa nikiandika sana juu ya ujasiriamali, na sababu za kufanya hivyo kwa sehemu kubwa ni kwamba ujasiriamali ndiyo njia ya uhakika ya mtu yeyote kuweza kuwa kiongozi wa maisha yake. Lakini...pia ni kwamba, mjasiriamali ana uwezo wa kufanya chochote.
Kuwa mwajiri na bosi wako mwenyewe kunatoa fursa zaidi ya kupata uhuru binafsi. Kuwa mjasiriamali kunakupa uhuru wa kipato na maisha mazuri ya mbeleni.
Kuna sababu nyingi za kwanini mtu anatakiwa kuwa mjasiriamali, lakini kumbuka kuwa ujasiriamali siyo kwa kila mtu. Kuna mambo kama 5 hivi ambayo ukiwa nayo ni ama husiwe mjasiriamali au huyabadili kuwa mjasiriamali, “chaguo ni lako”
1. Wewe una ngozi laini: Mara nyingi imeonekana kuwa mara tu unapotangaza kuwa unaanzisha biashara, kila mmoja ni mtaalamu wa kuanzisha biashara. Ukweli ni kwamba katika mazingira haya ambayo kila mmoja anajaribu kukushawishi na wengine kukuogopesha kwa hoja zao, unatakiwa kuwa na ngozi ngumu.
Ili kuweza kusimama kikamilifu kutimiza wazo lako au ndoto yako. Ama sivyo hutaweza kufika mbali kwasababu utakosa mwelekeo sahii wa kukamilisha wazo lako. Siyo, kila mmoja atapenda wazo lako hilo la biashara na hawataogopa kukwambia wewe juu ya mambo mabaya yanayohusu wazo lako jipya.
Sikwambii kuwa husiwasikilize wale wote watakao toa maoni juu ya biashara yako unayotarajia kuianza, LAKINI ni lazima huwe tayari kuchuja na ujiandae kifkra kusikia na kuvumilia yale mabaya yatakayosemwa juu ya mradi wako mpya. Bila hiyo utaishia kuogopa na mwisho wake hutaweza kuchukua hatua yoyote.
2. Hautaki kujenga mtandao na watu wengine: Wewe kama mjasiriamali, huwezi kufanya biashara kwa kujitenga na dunia. Kwa mjasiriamali tunaweza kusema kwamba hakuna kitu kama hicho kinachoitwa “kujitenga” na dunia , hasa pale mwanzoni unapoanza biashara.
Mwanzoni utakuwa unaishi na kupumua biashara yako mpya, kwasababu unajaribu kutaka kila mmoja afahamu juu ya biashara yako. Kila wakati utakuwa unafikiria jinsi na namna ya kuboresha, kupunguza gharama na kuuza zaidi.
Kwahiyo, kwa mjasiriamali ni lazima biashara yako iende sawa na dunia inavyokwenda, maana bila hivyo biashara yako itakufa kabla hata ya kushuhudia matunda ya uwekezaji ulioufanya.
3. Unapenda kupongezwa kwa juhudi zako: Kama wewe ni mwajiriwa, bila shaka umezoea kupata mrejesho juu ya utendaji wako wa kazi, kuimizwa juu ya utekelezaji wa majukumu uliyopangiwa. Waajiriwa wengi sana wamezoea,kuambiwa na waajiri wao jinsi walivyo wachapa kazi hata kama wanajua kuwa si wachapa kazi hodari.
Kwa mjasiriamali hakuna kitu kama hicho “kupongezwa”. Ukiwa mjasiriamali huwezi kusikia kitu chochote cha kupongezwa, labda ujipongeze wewe mwenyewe. Pongezi zako kama mjasiriamali, zinakuja kwa njia ya pesa unayotengeneza kwa kufanya kazi husika. Na itachukua muda kabla ya wewe kuanza kupata pongezi ambazo unazitafuta.

Soma: Maisha ya Ajira Yamtesayo Mjasiriamali ni Haya Hapa
4. Wewe unataka awepo mtu wa kukupa hamasa: Kama ilivyo kwa pongezi, kama unahitaji hamasa kutoka nje, basi hautakiwi kabisa kuwa mjasiriamali. Pindi unapoamka asubuhi, kama mjasiriamali, hakuna mtu yeyote anayesimama kwako kukupangia au kukupa ratiba ya kazi za siku hiyo. Mambo yote yako juu yako.
Mjasiriamali lazima ujipangie, ujisukume, ujitume, ujitoe na kujiamrisha mwenyewe. Kwa maana nyingine ujasiriamali unamtaka kila mtu aliyeamua kufanikiwa, awe kiongozi wa maisha yake na hapa hatukutegemei, huwe mtu wa kulalamikia wengine isipokuwa wewe mwenyewe.
5. Unajisikia vizuri unapovaa kofia moja: Kuna watu wengi unawafahamu ambao wanajisikia vizuri kwakuwa wahasibu, waandishi, au wapanga mipango ya matukio mbalimbali n.k. Watu hawa wanafurahi na kujiona wamefika kwa kufanya kitu kimoja na hawatakiwi wawe wajasiriamali. Kama mjasiriamali, ni lazima kila mara ujitahidi kuvaa kofia tofauti, huku ukifanya maamuzi mengi mbalimbali na unatakiwa kujiamini kwa kufanya hivyo.
Kama unafikiria kuanzisha na kumiliki biashara yako mwenyewe au kuwa mjasiriamali, lazima ufahamu kwanza kuwa mafanikio yako yanakutegemea wewe. Utakutana na changamoto nyingi na vikwazo vingi. Jinsi unavyokabiliana na changamoto hizo ndivyo utakavyoweza kufanikiwa au kuendelea mbele ya safari yako ya mafanikio.
Mpendwa msomaji wa mtandao wa MAARIFASHOP; Kama kama umekuta thamani yoyote ndani ya makala hii, basi jaribu kuwashirikisha rafiki zako na familia. Kwani, mafaniko ni kitu cha kushirikishana, ili kufanya maisha yetu yawe mazuri zaidi.

Mpendwa msomaji, endelea kuitumia vizuri MAARIFASHOP ili kujifunza mambo mbalimbali yatakayokuwezesha kupata mafanikio. Ili kupata makala mpya kila zinapochapishwa, bonyeza neno TUMA MAKALA MAARIFASHOP kisha sajiri barua pepe yako. Na kama unapenda kupata mafunzo ya kila siku kwa njia ya whatsap bonyeza neno MAFUNZO.
No comments:
Post a Comment