“Watu wengine wameitwa wabahili kwasababu wameamua kudhibiti pesa zao zisichukuliwe kiholela na watu wengine”.
Imekuwa ni kawaida kusikia watu wakilalamikia wenzao kuwa ni wabahili. Wengine wanasema eti hawa wanaoitwa wabahili ni wagumu sana kupata pesa yao!; pia inasemekana kwamba watu hawa hawapendi pesa yao itoke kwenda kwa watu wengine ~hawataki kutoa riziki.
Pengine ni vizuri tujiulize ni kwa namna gani mtu anaitwa bahili?
Ukifuatilia utagundua kuwa, mtu anayeitwa bahili, mara nyingi ni mtu yule ambaye hapendi kutumia pesa yake kwa vitu ambavyo havimuhusu yeye moja kwa moja.
Kwa mfano ukimfuata akuchangie mchango wa harusi, jubilei, mahafari n.k. hachangi au anachanga kidogo sana; hanunui vitu kwa fasheni mpaka asukumwe na dhamira yake ya ndani, hanunui vitu kwa kushitukizwa na wauzaji, lazima awe amepanga hivyo tokea alipotoka nyumbani kwake.
Sababu ya watu hawa kuitwa wabahili ni kwamba, ili wakupe pesa yao lazima na wewe huwe na thamani ambayo inalingana au kubwa kuliko pesa waliyonayo. Endapo wakiona hakuna thamani watakayoipata, basi wabahili hufanya maamuzi ya kutokutoa pesa yao.
Ikumbukwe kuwa mahusiano katika maisha ya binadamu yanaongozwa na ubadilishanaji wa “thamani” .
Kinachofanya kuwe na umoja na mshikamano kati ya mtu na mtu au kikundi ni thamani aipatayo mhusika. Kwahiyo, inatosha kusema kuwa “thamani” ni manufaa au uhitaji na kwa mantiki hii watu utoa pesa zao mfukoni ili kununua thamani kwaajili ya kutatua kero mbalimbali.
Soma; Mafanikio Yako Yamejificha Ndani ya Thamani
Thamani ndiyo huwafanya watu wengine kupeleka pesa kwa watu wengine. Kwa maana nyingine, maisha yetu yote yanatawaliwa na jambo moja tu nalo ni “kubadilishana thamani”. Tunaposema kubadilishana thamani maana yake ni kwamba, kila mtu anamiliki thamani tofauti na mwingine na ni vigumu mtu mmoja kumiliki thamani za aina zote, ndiyo maana ni lazima na ni kwaida watu kununua thamani ambazo hawana kutoka kwa watu wengine.
Kimsingi suala la kubadilishana thamani huwa linakuwa hivi: mimi ninazalisha thamani nyingi ambazo nazitumia kukidhi matakwa yangu na wengine. Ili watu wengine waweze kupata thamani kutoka kwangu lazima wanipatie pesa (tubadilishane), na mimi utuia pesa hiyo hiyo kununulia thamani kutoka kwa watu wengine.
Maisha ya kubadilishana thamani yanatufundisha na kutuonyesha kwamba, ukiwa na thamani kwaajili ya watu wengine, huwezi kupata ugumu wa kupata pesa kutoka kwa mtu yeyote yule, ilimradi una thamani haitakayo. Kwa ujumla wewe uliye na thamani kubwa, hutamuona mtu anayeitwa “bahili”.
Sasa kama maisha yetu yanastawi kwa watu kubadilishana thamani, iweje leo watu wengine wawalalamikie wenzao juu ya ubahili? Na kama mtu ameamua kwa hiari yake kubania rasirimali zake, iweje alaumiwe? Kwasababu rasilimali alizonazo mtu siyo za kwako, wewe unawajibika kwenye rasilimali zako tu.
Ubahili unatokea mara nyingi katika mazingira ambayo kunakuwa hakuna kitu cha kubadilishana. Upande mmoja unajaribu kutumia nguvu ili kujipatia pesa au bidhaa kutoka upande mwingine bila kulipa au kuchangia chochote ~ hali hii ikiachwa na kuendelea mara nyingi ndiyo uzaa unyonyaji na hili limeingia kwenye jamii yetu bila kujua.
Watu wengine wameitwa wabahili kwasababu wameamua kudhibiti pesa zao zisichukuliwe kiholela na watu wengine. Kutokana na tamaa ya kutaka kupata pesa za watu wengine bure, ndiyo maana jamii yetu ya sasa haina tena upendo wowote kwa mtu ambaye ni bahili wa rasilimali zake binafsi na wala siyo za mtu.
Watu wengi leo wana chuki sana na matajiri eti! ni wabahili, hawataki kutoa misaada n.k. LAKINI kama wewe hutajikita katika kuzalisha thamani itakayogusa maisha ya huyo tajiri basi sahau kabisa kupata pesa ya huyo tajiri.
Ukiona unasifiwa kuwa wewe siyo bahili basi ujue kuwa, watu waliokuzunguka wanaweza kuipata pesa yako bila kulazimika kuwa na kitu cha kubadilishana na wewe. Wakiona hawajapata chochote cha bure kutoka kwako, hawachelewi wanaanza kukulalamikia kwamba wewe hutoi pesa na inapobidi wanakuita “bahili” mkubwa sana.
Waliofanikiwa katika maisha ni wale wanaobana pesa yao dhidi ya watu wengine ambao wako tayari kula pesa yako bila kukupatia chochote chenye thamani. Kwahiyo, ndugu wananchi, ni wakati muhafaka sasa wa kuamua kusimamia na kudhibiti kikamilifu matumizi ya pesa yetu hatakama ni kidogo. Kuanzia sasa tujitahidi na tuhakikishe asilimia kubwa ya pesa tunayoipata tuiwekeze vizuri katika miradi yenye kutuhakikishia kipato kisichokuwa na kikomo.
Tusitishwe wala kuogopeshwa na wale waliojpanga kutuita wabahili. Tunatambua kwamba wale wanaotuita majina ya ubahili, wana malengo ya kutaka kujipatia pesa na utajiri wetu bure bila ya kufanya kazi. Tuhakikishe tunajipanga kutowasikiliza, ili mipango yao ya utunyonya ikwame, ili hatimaye tuibuke washindi na kuishi maisha ya ndoto zetu.
Pengine uwezo wa kusimamia na kudhibiti mapato yako utaupata kwa kuendelea kujifunza kila siku juu ya masuala ya fedha na ujasiriamali. Kwahiyo, ukiamua kuwa unajipatia makala mpya kila zikitoka kwenye Blog ya www.maarifashop.blogspot.com, bonyeza “KUPATA MAKALA” kisha unaweka E-MAIL yako na hapo utaanza kujipatia makala nzuri za mafunzo moja kwa moja kila zikitoka.

No comments:
Post a Comment