“Utajiri unapendelea wale walio na ujasiri!” ~ Cypridion Mushongi
Mjasiriamali wa kweli sharti ajiongoze mwenyewe katika kufanya maamuzi juu ya biashara yake au maisha yake kwa ujumla. Ili, mjasiriamali ajiongoze vyema, ni muhimu ajitahidi kujifunza masuala mbalimbali yanayogusa kile ambacho anakifanya au anatarajia kukifanya. Kwa kawaida, hatutegemei mjasiriamali wa kweli afanye kazi kwa...
kutarajia kupongezwa, kupewa motisha wala kupandishwa cheo. Hii ni kwasababu wewe ndiye mwanzo na mwisho wa biashara unayoifanya.
Ni imani yangu kuwa, hata kama wewe ni mwajiriwa leo, mpango wako wa kupata uhuru wa kipato na maisha bora kwa ujumla, hauusishi kupanda vyeo au ngazi kama ilivyo kawaida kwenye ulimwengu wa ajira na waajiriwa kwenye makampuni na taasisi. Ili kuwa mjasiriamali mwenye kuishi maisha ya kujipangia mwenyewe, unahitajika kufanya vitu vichache ili kufikia malengo makubwa ya utajiri.
Leo ninapenda kukushirikisha mambo makuu manne, ambayo unahitaji kuyafahamu na kuyafanyia kazi ikibidi. Mambo hayo ni pamoja na “kutosubili bidhaa ikamilike, jali sana mtiririko wa pesa, fanya makosa yenye maana na bobea kwenye elimu ya mawasiliano na mahusiano”:

1. Usiogope kuzindua bidhaa mapema: Huwa hakuna kitu kama bidhaa iliyokamilika. Bidhaa au huduma zote unazoziona zimefanikiwa na zinaonekana pale nje, ni kwamba bado zinaendelea kuboreshwa, lakini huwa “hazikamilki”. Kama bidhaa yako inatoa thamani kwa wateja wako unaowalenga, basi iko tayari kuzinduliwa. Vitu vingine vilivyobaki vitakuja au kukamilika muda si mrefu. Hii haimaanishi kwamba unaanzisha biashara katika mazingira ambapo bidhaa haijakamilika au iko nusu, lakini siyo lazima kusubili mpaka itakapokamilika.
2. Ona mtiririko wa pesa taslimu kama mfalme: Utahitaji pesa ya kutosha siyo tu kuanzisha biashara, lakini ili kujiwezesha wewe wakati wa miezi ile ya mwanzoni, pia wakati ambapo hujaanza kuingiza faida. Mara tu ukianza kuona pesa inaanza kuingia, hakikisha unaanza kuiwekeza tena kwenye biashara yako. Hii inaweza kutokea au kufanyika kwa njia nyingi, kama vile masoko, kukuza biashara, au hata wewe mwenyewe.
3. Fanya makosa yenye maana: Watu wengi huwa wanajitahidi kupunguza kushindwa kwenye maisha yao. Kwahiyo, huwa hawako tayari kujaribu kufanya vitu ambavyo wanahisi vinaweza kuleta hasara.
Watu waliofanikiwa, huwa hawaogopi kushindwa lakini wanafahamu na kuelewa kuwa ni muhimu kujifunza na kukua kutokana na makosa au kushindwa. Huwa wanajaribu kufanya mambo makubwa, huku wakijua kuwa wanaweza kushindwa kuliko wakati wowote ule. Ingawaje, wanaweza kufanikiwa zaidi ya walivyowahi kuwazia hapo awali.
Kufanikiwa au kushindwa, yote hayo huwa yanajulikana baada ya mtu kuwa amejaribu kufanya. Kwa maneno mengine wajasiriamali walio wengi, ujifunza kutokana na makosa yao wenyewe na ya wajasiriamali wengine na hii ndiyo njia kuu ya kujifunza. Kwa mjasiriamali makini, kujifunza kisawasawa kunaanza pale ambapo unathubutu kuanza kufanya kwa vitendo.
SOMA; Elimu ya Ujasiriamali Haipo Chuoni Iko Wapi?
4. Kuwa mahili katika mahusiano na mawasiliano
Mawasiliano ni kazi namba moja ya mjasiriamali yeyote. Kumiliki biashara, lazima ubobee katika sanaa ya mawasiliano pamoja na kujenga mahusiano na watu wa aina tofauti tofauti: Mfano, wateja, wafanyakazi, wakandarasi, wachuuzi, wawekezaji, wazalishaji na pengine watu wengine zaidi ya hao niliowataja. Mawasiliano na mahusiano ya uhakika yatapelekea kuongezeka kwa mtiririko wa pesa inayoingia kwako, mtaji zaidi na baadae biashara yako kuwa nzuri.
Unahitaji kuanza leo kuyafanyia kazi kwa vitendo mambo haya manne na mengine, kwani hayo ndiyo yatakuwa kichocheo cha wewe kujifunza na kupata elimu halisi ya ujasiriamali. Kama unataka kujifunza na kupata mwongozo wa ujasiriamali na biashara tukutane kila siku hapa “MAARIFA SHOP” kwa elimu na kujifunza zaidi.
KWA MWONGOZO WA ZAIDI, TUWASILIANE KUPITIA
Simu: 0788 855 409
Barua Pepe: mchumieconomist2009@gmail.com
Ukurasa Facebook: Maarifashop@Mushongi.Blog

No comments:
Post a Comment