“Utasonga mbele tu pale utakapoacha kujibinafsisha matatizo yanayoendelea kutokea katika mchakato wa maisha yako” ~ Cypridion Mushongi
Njia mojawapo ambayo ni kisababishi kikubwa cha hisia hasi na hasira ni hali ya kupenda kujibinafsisha au kujimilikisha matatizo yanayoendelea kutokea. Tabia au hali hii ya kupenda kujibinafsisha ni...
hatari kama ilivyobainishwa na bwana Ouspensky kwenye kitabu chake cha “In Search of the Miraculous: Fragments of an Unknown Teaching”(“nitumie kitabu”).
Hali hii ya kujibinafsisha matatizo, mara nyingi utokea pale unapochukulia jambo lililotokea kama la kwako binafsi au unalihusisha moja kwa moja na mtu au kitu fulani. Kila mara unaona matokeo ya matukio ya kuudhi au hali mbaya kama ya kwako binafsi. Wakati mwingine unaona matokeo ya matukio ya kuudhi kama mashambulizi dhidi ya kile unachokiamini wewe. Unajikuta unajihusisha kwa hisia zako zote na kujitambulisha na hali hiyo, kiasi kwamba inakuathiri kihisia, kifikra na kimtazamo katika hali ambayo ni hasi.
Walimu wakubwa katika masuala ya kidini, kama vile Buddha na Yesu, wamesistiza umuhimu wa kujitenganisha wewe na matukio yanayoendelea kutokea, ili kupata utulivu na kudhibiti hisia ulizonazo.
Kwa upande mwingine mtaalam wa masuala ya saikolojia na falsafa bw. William James kutoka chuo kikuu cha Harvard (Marekani), aliwahi kuandika kuwa “hatua ya kwanza kwa tatizo au ugumu wowote ule ni kuwa tayari kulipokea kama lilivyo”. Pia mtaalam huyu aliwahamasisha watu kuwa kitu chochote ambacho hakiwezi kutibiwa lazima kivumiliwe. Kwa maneno mengine ni kwamba tunahitajika kujenga tabia ya kujitenganisha na mtu au hali ambayo inatufanya sisi kuwa na hasira au kuudhika. Inabidi tuondoe nguvu ya hisia zetu kwa mambo yanayotupa hasira, ili kupata utulivu na amani.
Njia hii haina maana kwamba ukubali kila kitu kibaya kinachokujia BADALA yake, inakuhamasisha kutumia nguvu yako ya akiri katika kudhibiti hisia hasi. Unajiwajibisha wewe binafsi kurudi nyuma kidogo na kukabiliana na matatizo au changamoto kwa akiri na busara zaidi. Unatumia akiri kuona hali halisi ilivyo na kufanya maamuzi mazuri ya kutatua tatizo lililopo. Hakuna watu wanaoweza kukudhibiti wewe labda kama kuna kitu fulani ambacho unahitaji kutoka kwao.
Lazima watu wengine wawe na kitu fulani ambacho bado wanaweza kukupatia au kuzuia usikipate. Mara moja utakapojitenga kihisia na mtu au kitu na ukawa hauhitaji chochote kutoka kwao, basi wewe huko huru. Hali hii ya kufanya mazoezi ya kujitenganisha na matukio au watu wanaokukwaza ni nguvu ambayo unaweza kuipata kwa kuijenga kupitia mazoezi ya kiakiri. Mazoezi haya yanaweza kukufanya ukawa mtaalam na bingwa wa kutatua matatizo yanayosababisha hasira.
Jambo moja unaloweza kulifanya ili kusaidia watu wengine, ni kuwatia moyo wao kuweza kujitenga na matukio ya matatizo na kutokushawishiwa na hisia katika kuliona na kulitatua tatizo. Wahamasishe, kuona ugumu na matatizo, kama vile yanatokea kwa wengine. Waulize ni ushauri gani wangeweza kutoa kwa mtu mwingine anayekabiliwa na tatizo kama hilo la kwao. Kwa kujitenga na hali inayotokana na hisia zilizoamshwa na tukio, wewe pamoja na wengine mtazidi kuwa na uwezo zaidi wa kutatua tatizo kwa ufanisi.
Kikubwa tunachojifunza hapa ni kwamba, wewe mtu binafsi ndiye mwenye uwezo wa kuamua ukubwa wa tatizo. Suala la tatizo kuwa kubwa au dogo ni la kihisia zaidi kuliko uhalisia. Na inaonekana kwamba matatizo tunayoyaita makubwa mengi ni yale tuliyosimuliwa na wakubwa zetu kuwa ni makubwa nasi tumeendelea kushikiria hisia hizo. Kwahiyo, inatupasa kila tukio tunalodhani ni tatizo kwetu tujenge utamaduni wakuwa tunalitafakari upya sisi kama sisi na tuliangalie na kulipima katika mazingira halisi ya wakati huo uliopo, ili kusudi tuweze kupata suruhisho lenye kuondoa tatizo lote kwa ujumla.
Ni muhimu sasa tutambue kuwa matatizo yataendelea kutokea kwa yeyote yule anayetaka na asiye taka, maskini na tajiri, aliyesoma na ambaye hakusoma, aliyejiajiri na aliyeajiriwa. Kitu cha msingi sana unachopaswa kukumbuka kila mara ni kwamba “wewe ni mkubwa sana kuliko matatizo uliyonayo”. Jambo la kushangaza ni kwamba watu wengi wameamua kuwa wadogo kuliko matatizo wanayokabiliana nayo na ndiyo maana wanajiona wana matatizo makubwa kuliko wenzao. Hali hii imesababisha watu wengi kukata tamaa ya maisha.
Mpendwa msomaji, yawezekana baada ya kusoma makala hii, umepata maswali mengi na pengine ungependelea kupata majibu na kuendelea kujifunza zaidi.
Hivyo, napenda kukutaarifu kuwa bado unayo fursa ya kuwa mmojawapo wa kundi la wasomaji wa mtandao wa maarifashop: ni rahisi kwani unahitaji tu kuweka e-mail yako kwa kubonyeza neno “INGIA” .
Ukimaliza kufanya hivyo, tayari wewe utakuwa na fursa ya kuwasiliana na mimi muda wowote na utaweza kupata makala, vitabu moja kwa moja kupitia e-mail yako kila mara vinapowekwa vitu vipya.
Pia unaweza kuniandikia au kupiga simu moja kwa moja ili kupata mafunzo mbalimbali kama vile uongozi wa biashara yako, kuifahamu pesa ni kitu gani, jinsi ya kutoka kwenye mkwamo kimaisha na mengine mengi yakiwemo ya jinsi ya kupambana na udhoofu wa mwili (afya na ustawi).
No comments:
Post a Comment