Mara
zote ukishakupata pesa (kuingia mfukoni), kinachofuata huwa ni kuzitumia hata
kama ukizitunza kwanza, mwisho wake huwa ni kutumika kwaajili ya kukidhi mahitaji
ya vitu na huduma mbalimbali. Watu wengine upenda kusema kwamba “pesa ni mzunguko”. Mzunguko wa pesa una
vipengele viwili ambavyo ni “Kuingia na
Kutoka”. Kwa lugha rahisi tunaweza kusema kuwa pesa ina milango miwili,
kuna mlango wa pesa kuingia na kutoka kwako.
Kwa
yeyote anayetafuta mafanikio makubwa ni lazima kuangalia milango hii miwili
(kuingia na kutoka) na hapa ndipo kuna tokea makundi mawili ya watu ambao ni
masikini na tajiri. Kwa upande wa maskini tayari wamejenga hofu kubwa sana na
muda wote wana wasiwasi ya pesa kutoka na kupotea. Kutokana na hofu hii,
maskini wengi sana wemejijengea tabia ya kuibana pesa ikisha ingia mifukoni
mwao, huku wakidhani kuwa hilo ni suluhisho la wao kutoishiwa na pesa. Matokeo
yake linapokuja suala la kuwekeza au kuchangamkia fursa kubwa wanakuwa waoga
sana wa kuthubutu kutokana na hofu ambayo imejengeka kwa muda mrefu ndani ya
fikra zao.
Wenzao
ambao ni matajiri wao, mara tu pesa inapoingia, kitu cha kwanza ujiuliza ni
kitu gani wanaweza kukitoa ili kuondoa kero kwenye jamii ikiwemo le
iliyowazunguka. Kwahiyo, wao uweza kuiachia pesa yao kutoka lakini kwa malengo
ya kuituma malighafi ambayo pengine ikiunganishwa na mambo mengine uweza kurudi
na bidhaa au Huduma ambayo ni hitaji muhimu kwenye jamii. Kwa kufanya hivyo,
hata wale maskini walioogopa kuiachia pesa yao mwanzoni, wakati huu uweza
kuituma kwa matajiri hao na mzunguko uendelea hivyo hivyo na mwisho ni umaskini
uliokithiri.
Kama
tulivyoona kuwa kuna milango miwili ya pesa kuingia na kutoka. Mlango wa kwanza
ni wa kuingilia (pesa inaingia mfukoni) na wa pili ni wa kutokea (pesa inatoka
nje ya mfuko wako). Pesa ikishatoka nje ya mfuko wako, kuna mambo mawili ambayo
yanatokea; kwanza pesa inaweza kutumwa mali ambayo iwapo itaongezewa thamani na
kutoa bidhaa au huduma ambayo ikiuzwa tena inarudisha ile pesa iliyotoka
mwanzoni na nyongeza juu (faida) na hii yongeza ni kwasababu ya thamani
iliyoongezeka. Pili pesa inaweza kutoka
nje ili kufuata vitu ambavyo kwako wewe unakuwa ni mtumiaji wa mwisho; kiasi
kwamba pesa iliyotumwa vitu vya aina hii, kamwe haiwezi kurudi hata
ungefanyaje.
Watu
wengi hasa waajiriwa pamoja na wakulima, huwa pesa zao zikishatoka kwa
mwenyewe, mara nyingi huwa hazirudi kwasababu ya kutumwa vitu ambavyo wewe
ndiye mtumiaji wa mwisho. Sababu kubwa ya waajiriwa ufanya hivyo ni kwasababu
ya kutegemea mshahara mwisho wa mwezi. Hali hii humfanya mtumishi pamoja na mkulima
kuishi maisha ya kawaida sana ambayo huwa hayabadiliki miaka nenda rudi. Baadhi
ya vitu ambavyo pesa ikitumwa kuvifuata yenyewe hairudi ni vingi sana; mfano:
Runinga Redio, Karo za wanafunzi, gari la kutembelea, n.k.
Bila
kuingilia mipangilio mbalimbali ya watu walionayo, unaweza kuona kuwa pindi tu
tunapoanza kazi ya kuajiriwa tunaanza vizuri lakini muda mfupi tu! tunawahi
kutekwa na utamaduni wa kupeleka pesa kule ambako huwa hairudi. Na kwenye jamii
tulizomo watu wanahamasishana kufanya hivyo. Na mpaka sasa watu wengi wamekuwa
wakiishi kwa mazoea, kwamba unapopata ajira eti unashauriwa na wenzako kununua
kiwanja na kujenga nyumba ya kuishi na vitu vingine vyenye kupeleka pesa bila
kurudi.
Watanzania,
tunahitaji kubadili tabia pamoja na mtazamo wetu juu ya mapato na matumizi ya
pesa; tunahitaji kujifunza ni jinsi ya kutuma pesa ikarudi pamoja na vitu. Pia,
tunahitaji kuwa na mikakati na mbinu za namna ya kuifanya iwe nyingi badala ya
utaratibu uliozoeleka wa kubana matumizi. Tukiweza kuyafanyia kazi yote haya
hakika tutakuwa tumepiga hatua moja muhimu sana ya kutufikisha kwenye mafanikio
tuyatakayo.
Mpendwa msomaji, endelea kuitumia vizuri MAARIFASHOP ili kujifunza mambo mbalimbali yatakayokuwezesha kupata mafanikio. Ili kupata makala mpya kila zinapochapishwa, bonyeza neno TUMA MAKALA MAARIFASHOP kisha sajiri barua pepe yako. Na kama unapenda kupata mafunzo ya kila siku kwa njia ya whatsap bonyeza neno MAFUNZO.