Je? Na
wewe ni mmojawapo wa wanaotafuta pesa? Kama jibu ni ndiyo, hiyo pesa unajua ni nini?
mbali na kufahamu sura tu ya sarafu na noti? Ukiacha hilo, kuna cha zaidi unachojua
kuhusu pesa? Ikiwa jibu ni “hapana” sasa wewe pesa utazipataje wakati huzijui? Mara
nyingi watu husema kuwa, “huwezi kuona
kitu usichokijua”! Mpaka sasa, ufahamu na uelewa uliopo juu ya pesa ni mdogo
sana labda tu! ufahamu uliopo ni wa kujua jinsi pesa zinavyogawanyika na walio
wengi tunafahamu zaidi kutoa na kujumlisha pesa, hasa wakati wa kurudisha
chenji kwa mteja. Ukiacha hilo, taswira kubwa na ndefu iliyopo nyuma ya pesa (noti
na sarafu) haionekani kirahisi kwa watu walio wengi. Ufahamu na uelewa mdogo
juu ya maana pana ya pesa upo kwa watu wengi, na hali hii ni kwa wote waliokwenda
shule na wale ambao hawakwenda kabisa.
Ukweli
ni kwamba “Pesa ni kitu chochote kinachowezesha watu kubadilishana vitu na huduma.
Hapa ndo kuna mkanganyiko kwasababu watu wengi mpaka sasa wanaamini pesa ni
kitu halisi na hivyo kusababisha wao kuweza kuiabudu na kuamini pesa kama
inavyoonekana katika hali yake ya noti na sarafu. Mtazamo wa kuichukulia pesa
kama kitu halisi, unawafanya walio wengi kuwekeza nguvu kubwa Katika
kusaka/kutafuta pesa yenyewe kama ilivyo. Lakini wakisha ipata wanagundua kuwa,
hitaji lao siyo makaratasi ya noti bali ni vitu na huduma mbalimbali hapo ndipo
huzipeleka kwa wenye vitu na huduma, huku wakibakia tupu kabisa.
Katika
kutafuta pesa kunakuwa na dhamira tofauti kati ya maskini na tajiri; “Watu
maskini wanawekeza muda na nguvu yao kwa dhamira ya kutafuta pesa lakini watu
matajiri wanawekeza muda, akili na nguvu yao kwa dhamira ya kutafuta “vitu na huduma”.
Kwasababu maskini wengi waliamini kuwa mwisho wa utafutaji wao ni pesa, basi ndipo
ugundua kuwa sio mwisho, kumbe mwisho wao ni kupata vitu na Huduma (chakula,
dawa, mavazi; usafiri, elimu, utaalam, nguvukazi n.k.). Kwahiyo, pamoja na
kutafuta pesa hiyo kwa kutumia nguvu kubwa na muda mrefu, mtu huyo ujikuta
akilazimika kuzipeleka mwenyewe kwa tajiri ambaye wakati huo ana vitu na huduma
fulani fulani. Kwa maana nyingine tunaweza kusema kuwa watu hawa wanaishi kwa
kutafuta pesa na kisha kulipa bill! au madeni basi.
Mahitaji
ya mwanadamu ni mengi sana na hayana kikomo, lakini pamoja na hayo, mahitaji
haya yamegawanyika katika makundi makuu mawili: yaani “Vitu na Huduma”. Tunaposema “Vitu” inamaanisha vitu halisi na
vinavyoshikika kama vile nguo, meza, komputa simenti, gari, simu, vyombo,
spare, vitabu n.k); na tunaposema “Huduma” ni vitu ambavyo havishikiki
navyo ni kama; usafiri, habari, utaalam, ulinzi na usalama, maombi, ufundi n.k.
Kwahiyo, kutokana na ukweli huo hapo juu, ndiyo maana siku zote pesa itakwenda
kule kulipo na vitu au huduma hakuna sehemu nyingine.
Kutokana
na ukweli huu, ni wazi kwamba unapoona pesa imeingia mfukoni mwako, basi ujue
kuna mtu ametuma pesa hiyo kufuata kitu fulani kwako, na iwapo huna kitu chochote
ulichonacho basi hutapata pesa yoyote kwasababu hakuna kitu cha kufuata kwako.
Sasa unachotakiwa kufanya leo ni kuanza kubadili swali ambalo watu wengi
ujiuliza pindi wanapohitaji kupata pesa; swali lenyewe huwa ni hili hapa: “Nitapata pesa wapi?” na kwa kuwa wengi
ujiuliza swali hilo, ndiyo maana huishia
tu! kutafuta pesa bila mafanikio.
Iwapo utaendelea kujiuliza swali la nitapata
pesa wapi ndivyo itakavyozidi kuwa vigumu kupata jibu ambalo litakuongoza
kupata pesa. Kwahiyo, mtanzania mwenzangu ni wakati sasa wa kubadili swali lako
kutoka “nitapata pesa wapi?” kwenda “Pesa itakuja kwangu kufuata nini?”. Na
kila mara utakapojiuliza swali la pesa
itafuata nini kwako, basi jibu jibu lake tu! litakuwa ndiyo pesa yenyewe
kwa maana nyingine utaona watu wakibisha hodi mlangoni kwako, kwaajili ya kukuletea pesa ambayo miaka yote umekuwa
ukikimbia huku na huko kuitafuta bila mafanikio!. Sasa unachotakiwa kufanya ni utafiti
katika mazingira yanayo kuzunguka na maeneo mengine unayoweza kuyafikia ili kutambua
mahitaji, kero na changamoto zilizopo. Matokeo ya Utafiti yatakusaidia kubuni
na kuzalisha vitu au huduma ili kukidhi mahitaji ya jamii husika, na ukifikia
hapo ndipo utaona ndani muda mfupi watu wakituma pesa ili ikafuate vitu na huduma
kutoka kwako.
Kwahiyo,
uwanja ni wako wewe mtanzania unayetafuta mafanikio, kwani tuna imani kubwa
sana kuwa unaweza kupata pesa nyingi, iwapo utakubatia na kuifanyia kazi
falsafa hii ya “Pesa itakuja kwangu
kufuata nini?”.
Mpendwa msomaji, endelea kuitumia vizuri MAARIFASHOP ili kujifunza mambo mbalimbali yatakayokuwezesha kupata mafanikio. Ili kupata makala mpya kila zinapochapishwa, bonyeza neno TUMA MAKALA MAARIFASHOP kisha sajiri barua pepe yako. Na kama unapenda kupata mafunzo ya kila siku kwa njia ya whatsap bonyeza neno MAFUNZO.
No comments:
Post a Comment