"Mungu hakupi pesa kidogo au nyingi, anakupa tu kile kiasi unachohitaji”.
Kwasasa wapo watu wengi wanaodhani kuwa wao wanazo pesa kidogo na wangependelea Mungu awaongezee. Pia kuna wale wachache ambao wanadhani wanazo pesa nyingi lakini.......
na hawa wangependelea Mungu azidi kuwapa pesa nyingi zaidi. Ki-ukweli hakuna pesa kidogo wala pesa nyingi.
Ukimwambia mtu yoyote kuwa “pesa aliyonayo ni sawa na kiasi unachohitaji”, anakukatalia kata kata kwasababu, hisia zake zinamtuma kuamini kwamba yeye ana pesa kidogo na mpaka anafikia hatua ya kulaumu watu wegine anaodhani wana pesa nyingi.
Katikati ya mwezi wa December mwaka 2015 nikiwa kwenye likizo yangu ya mwaka nilikutana na rafiki yangu ambaye ni Mganda Bw. Sam Mpiira. Rafiki yangu huyu ni mjasiriamali anayechipukia jijini Kampala-Uganda.Tukiwa tumekutana kwenye viunga vya hotel ya Speak Resort Munyonyo, tuliongelea sana juu ya namna tunavyoweza kutajirika na hatimaye kusaidia watu wengine kutajirika. Katikati ya mazungumzo yetu alinieleza mojawapo ya falsafa yake kuhusu “KUPATA PESA” na hapa alisema “Mungu hakupi pesa kidogo au nyingi, anakupa tu kile kiasi unachohitaji”.
Ukiangalia kwa undani unaona kuwa Falsafa hii inatugusa wengi, na inatuonyesha umuhimu wa kuacha kulichukulia suala la pesa kuwa la HISIA, badala yake tuone ukweli juu ya pesa tuliyonayo kuwa ni matokeo ya fikra na jitihada zile tunazoziweka kila siku basi!. Endapo tukilitabua hilo basi tutakuwa tumeachana na fikra za kwamba kupata pesa ni “bahati”.
Kama nilivyotangulia kusema hapo awali kuwa watu wengi bado wana machungu na wanalalamika kila wakati kwamba wao hawafanikiwi kupata pesa ya kutosha. Kuwepo kwa hali ya malalamiko juu ya pesa kidogo kunaonyesha dhairi kuwa ufahamu uliopo ni kidogo, kwasababu mfumo wa elimu ya darasani hauna ajenda ya kufundisha pesa. Na pia watu wengi tumefanya utafutaji wa pesa kuwa wa HISIA zaidi kuliko ukweli ulivyo.
Ndugu msomaji wa MAARIFASHOP, siri unayotakiwa kuijua leo ni kwamba, suala la kiasi gani cha pesa huwenacho ni la binafsi zaidi kuliko unavyofikiria. Hali hii inatokana na uwepo wa mahitaji yanayo tofautiana kati ya mtu na mtu. Ni vigumu kwangu mimi kufahamu wewe una kiu kiasi gani ya pesa. Utofauti huu wa mahitaji ya pesa ndio uzaa shauku, nguvu, motisha na hamasa tofauti linapofika suala la kutafuta pesa.
Kwahiyo, wale ambao ndani ya nafsi zao wana sababu nzito ya kutafuta pesa ndio wanapata kiasi hicho ambacho kwako wewe uliye na sababu nyepesi unaona wamepata pesa nyingi. Napenda kurudia tena kusema kuwa “hakuna aliye na pesa nyingi bali kila mtu anacho kiasi ambacho ni hitaji lake kwa wakati huo”.
Kwahiyo, kila mtu kabla ya kuanza mchakato wa kutafuta pesa ni vizuri ukatenga muda wa kutafakari kwanza juu ya maisha yako wewe binafsi.Tafakari zako zielekeze kwenye vitu vizuri ambavyo ungependa kuwa navyo maishani au hali ya maisha ambayo unadhani ukiifikia utajisikia raha na mwenye furaha.
Kwa maana nyingine lazima huwe na picha au ndoto ya maisha mazuri kwanza kabla ya kuyafikia. Ndoto ya maisha mazuri ndiyo itakayo kujengea sababu na hamasa ya wewe kutafuta pesa ya kutimiza ndoto yako. Utaratibu wa namna hii, utakusaidia sana kuachana na malalamiko. Pia ukiwa na ndoto yako ya maisha mazuri itakuwa vigumu kuwaonea wivu watu wengine waliotimiza ndoto zao, yaani wale ambao sasa hivi unadhani wana pesa nyingi.
Kikubwa hapa ni kufikiri, kutafakari, kupanga na kutekeleza kwa vitendo. Ninaamini kama pesa ndiyo shida yako itapatikana tu japo itachukua muda. Ni muhimu kutokata tamaa na kuwa mvumilivu.
Kama unadhani ni muhimu kuwa na mawasiliano ya karibu na mtandao huu wa “MAARIFA SHOP”, ni kiasi cha kubonyeza maneno haya “KARIBU MAARIFASHOP, -tayari utaanza kupata moja kwa moja mambo mapya ya mtandao huu.

No comments:
Post a Comment