“Falsafa
ya matajiri na masikini ni hii hapa: Matajiri wanawekeza pesa yao na
kutumia kiasi kinachobaki, Masikini wanatumia pesa yao na kuwekeza kiasi
kinachobaki” ~ Robert Kiyosaki
Hali
ya umaskini katika jamii yetu kwa kiasi kikubwa imesababishwa na watu
wengi kuuza muda wao kwa watu wengine. Dunia ya leo bado inatawaliwa
zaidi na kundi la watu ambao biashara yao ya kila siku ni kuuza muda kwa
lengo la kujikimu kimaisha. Katika ulimwengu wa kutafuta riziki
(kipato), tunapata kuona aina kuu tatu za kipato ambazo ni.....
kipato kutokana na ajira, kipato hai na kipato endelevu au kipato bila kikomo.
Karibu asilimia 90% ya watu duniani wanapata kipato chao kutoka kwenye ajira (mshahara) na kujiajiri (mapato hai). Ni chini ya asilimia 10% pekee ndio wanapata aina ya kipato abacho hakina kikomo –kikianza kuingia kinaendelea hata kama haupo kufanya kazi. Kwa maana nyingine ni kwamba, asilimia chini ya 10% ndio matajiri wanaomiliki asilimia 90 ya utajiri wote duniani.
Kimsingi mapato yanayotokana na kujiajiri (kipato hai) na ajira, yote ni mapato ambayo tunayapata baada ya “kuuza muda wetu” au kubadilishana muda (mwajiriwa) na pesa (mwajiri). Kutokana na hali hiyo ya kuuza na kununua muda, ndiyo maana watu wengi tuliokwenye ajira au tuliojiajiri mara nyingi hatuna muda wa kufanya vitu tunayovipenda hata kama vina maana na umuhimu mkubwa kwetu.
Kwa maana nyingine ni kwamba muda mwingi ambao tungeutumia katika kubuni vitu vipya tunakuwa tumeishiwa tayari kutokana na ukweli kwamba tumekwisha uza muda huo kwa watu wengine hasa waajiri –zaidi zaidi tunafanya biashara ya kuuza muda basi!
Kutokana na ukweli wa mambo ulivyo ni kwamba wauzaji wa muda kama mali tuko wengi sana kuliko wanunuzi (waajiri). Matokeo yake ni kwamba soko la MUDA linashuka au tuseme bei ya muda inashuka kila kukicha. Hali hii imetufanya wote wauza muda kuuza kwa bei ya chini ambayo hailingani na thamani ya kitu tunachokiuza. Leo hii, tunashuhudia migomo ya kila aina hasa kwa wafanyakazi wa viwandani na mashambani, hoja yao kubwa ikiwa ni maslahi duni au mishahara midogo “Kiduchu” isiyoweza kukidhi hata mahitaji ya lazima kama vile chakula na malazi.
Nataka kupata MAPATO YASIYO NA KIKOMO lakini siyajui ni kitu gani:
Unapoongelea suala zima la mapato yasiyo na kikomo ni sawa na wewe kufunga bomba la maji mtoni, ili kuleta maji nyumbani kwako. Maji yakishafika nyumbani wewe unayatumia unavyotaka na hayakatiki. Wale wote wasiofikiwa na mabomba ya maji majumbani mwao, wao wanachokifanya ni kuchota maji kwa kutumia vifaa kama ndoo, madumu n.k.
Watu hawa wakishapata maji, wanayatumia na inafika wakati yanaisha. Mara tu maji yanapoisha, inawabidi wafunge safari tena kwenda kuchota maji popote yalipo, na mzunguko unakuwa hivyo maisha yao yote. Ukichota maji yanakuwepo nyumbani, usipochota maji hayapo LAKINI yule mwenye bomba anaendelea kupata maji masaa yote, hata akiwa amesafiri maji yapo tu!.
Mfano huu wa maji ni sawa na mfumo wa mapato tunayoyapata. Kwa maana nyingine ni kwamba, wale wote tunaopata mapato hai au mapato ya ajira (mshahara), tunafanana kabisa na wale watu wanaochota maji mtoni kila siku kwa kutumia ndoo, madumu n.k. Kwa mfano: Mapato ya ajira -unalipwa siku unapofanya kazi, usipofanya kazi haulipwi, ukisafiri bila ruhusa haulipwi, ukiugua muda mrefu hulipwi n.k.
Kwahiyo, mapato bila kikomo ni mapato anayopata mtu pasipo kuwa na ulazima wa kushughulika au kufanya kazi kwa wakati huo. Mapato haya mara nyingi yanatokana na kazi au shughuli uliyokwisha kufanyika kitambo na kuendelea kupata mapato hayo “kimya kimya”, kutokana na ukweli kwamba watu wengine wanakuona tu umekaa lakini kumbe wewe unaingiza pesa nyingi mfukoni.
Kwa tafsiri nyingine ni kwamba mapato au pesa isiyo na kikomo ni ile ambayo mtu huipata mara kwa mara, lakini kwa kutumia nguvu kidogo sana katika kuiendeleza. Mfano; ni pesa itokanayo na haki miliki kama;k.m. pesa ya mrahaba au “royalties” kutokana na kuuza vitabu, album au kukodisha hakimiliki; faida benki; kodi ya majengo au mashine; au pesa kutoka kwenye biashara ambayo haikuhitaji tena wewe kuwepo moja kwa moja kama “biashara ya kupashana habari au mtandao”. Hii ni mifano tu ya vyanzo vya pesa isiyo na kikomo. Aina hii ya mapato inapatikana baada yaw ewe kufanyakazi kwa bidii sana kwa muda fulani (k.m. miaka 2 hadi 5), baadae unaendelea kupata pesa kwa muda mrefu bila hata wewe mwenyewe kushughulika tena au zaidi.
Uzuri wa mapato yasiyo na kikomo ni kwamba, unaendelea kupata pesa kwa muda mrefu baada ya kazi ya uzalishaji au ya awali kukamilika. Hali hii ya wewe kupata pesa bila kulazimika kufanya kazi tena ndiyo ukuwezesha wewe kupata MUDA wa ziada na hivyo kupata fursa ya kuwekeza muda huo kwenye mambo mengine. Uzuri mwingine wa mapato haya ni kwamba duniani kote hayatozwi kodi kubwa kama mapato ya aina nyingine.
Kwa wale wote tulio na ndoto ya kupata mafanikio makubwa kimaisha tunashauriwa kufanya kazi na kuwekeza kwenye miradi inayotuhakikishia kupata mapato yasiyo na kikomo. Hii ni kutokana na ukweli kwamba mapato ya aina hii, ndiyo mapato pekee ambayo ni imara, endelevu na yanarithishwa kizazi hadi kizazi. Sababu nyingine inayonituma nikushauri kupata mapato haya ni kwamba, watu wengi waliofanikiwa (matajiri) duniani, wamejipanga na kujikita katika kupata mapato haya.
Je? unawezaje kutumia mapato yasiyo na kikomo kununua tena muda wangu? Je? kununua muda wako tena kuna maana gani? Maana yake ni kwamba pesa ambayo unatengeneza kwa wiki kutoka kwenye biashara ambayo ni zaidi ya pesa uliyokuwa ukipata ulipokuwa ukimfanyia kazi mtu mwingine (mwajiri). Kwa upande mwingine, mapato bila kikomo yana tabia ya kununua muda wako tena kwakuwa yanarudisha kwako ule muda au masaa yote uliyokuwa ukiyatumia kufanya kazi za mwajiri.
Inapotokea biashara yako ikaanza kukupatia kipato kikubwa kisicho na kikomo na ambacho ni zaidi ya pesa (mshahara) uliyokuwa unaipata kutokana na kuuza muda wako kwa mwajiri, basi hapo utakuwa hulazimiki tena kuuza muda wako ili kupata mahitaji na badala yake hayo masaa yako uliyokuwa ukibadilishana awali na pesa, sasa unaanza kuyatumia (kuyawekeza) wewe mwenyewe katika kukuza faida na hatimaye kujijengea mikondo mingi ya kuingiza pesa –hii ndiyo namna ya kujenga utajiri.
Ukiona biashara au shughuli yako unayofanya inakuletea pesa isiyokuwa na kikomo, basi ujue kuwa biashara hiyo inaweza kukusaidia kununua muda wako na hatimaye ukajimilikisha tena muda huo. Kwa mantiki hiyo, ni wazi kwamba mapato yasiyo na kikomo ndiyo pekee yanaweza kukuwezesha wewe kurudisha au kununua tena muda wako.
Mwisho nipende kusema kuwa utakapoamua kwa dhati kujifunza undani wa mapato yasiyo na kikomo utakuwa ni sawa na mtu aliyepata dhahabu au aliyepata kujua suala nyeti. Kutokana na unyeti wa mapato ya aina hii, ndiyo maana ninapenda sana watu tuliowengi tuyafahamu na kuyajua kwa undani zaidi.
Tukisha elewa vizuri dhana nzima ya mapato yasiyo na kikomo; ni matarajio yangu kuwa tutaweza kuhama kutoka mfumo wa biashara ya kuuza muda (mshahara) kwenda biashara ya kuwekeza muda (faida). Nakusihi uanze mchakato wa kujifunza hatua wa hatua kupitia makala nzuri za ujasiriamali na mafanikio nyingi zikiwa zinapatikana hapa kwenye mtandao wa “MAARIFA SHOP”. Kama unapenda kuwa karibu na mtandao huu bonyeza KUWA KARIBU.
Kwa mawasiliano zaidi:
WhatsApp: 0788 855 409
E-mail: mchumieconomist2009@gmail.com
Tovuti: http://maarifashop.blogspot.com

No comments:
Post a Comment