“Watu waliofanikiwa sana katika maisha ni wale ambao upenda kuuliza maswali. Wanajifunza kila wakati. Wanakua kila wakati. Wanajisukuma mbele kila wakati.” – Robert Kiyosaki
Mwaka 2013 nilialikwa na kushiriki katika sherehe ya jubilee ya Baba Askofu Dk. Benson Bagonza wa KKKT Dayosisi ya Karagwe. Jubilee hiyo ilikuwa ni ya kutimiza miaka 50 ya kuzaliwa kwake, miaka 20 ya ndoa na miaka 10 ya uaskofu. Sherehe hiyo ilitanguliwa na ibada maalum ambayo iliongozwa na Baba Askofu mwenyewe.
Katika mahubili yake siku hiyo.....
alihubili mambo mengi ya msingi sana hasa yanayohusiana na mchakato wa maisha. Nakumbuka siku hiyo, kuna jambo moja lilinigusa sana pale alipotoa ushuhuda wa kile ambacho kwa miaka 20 ameweza kujifunza kutoka kwa watoto wake; na hapa alisema “Nawashukuru pia watoto wangu kwani wamenifundisha "UVUMILIVU” .
Baada ya mimi kusikia maneno hayo nilitafakari na kuanza kuona kitu kingine kipya ambacho sikuwahi kukifikiria wala kuwazia. Hapa ndipo nilipoanza kutambua kuwa kumbe hata watoto wetu tuliowazaa wana vitu vingi vya kutufundisha, japokuwa wengi wetu (watu wazima) hatuko tayari kujifunza chochote kutoka kwao, kwasababu tunadhani wao ni watu wasiojua kitu chochote.
Kama Askofu Dk. Bagonza alivyoweza kutambua na kuthamini mchango wa watoto wake, ambao alisema wamemfundisha “Uvumilivu” basi na mimi niseme leo ni siku ambayo nimeweza kujifunza kitu muhimu sana ambacho nafikiri nikikifanyia kazi kwa vitendo nitaweza kufika mbali katika kutimiza ndoto kubwa niliyonayo.
Siku ya leo (16/02/2016), nimeweza kushuhudia kile alichohubili Baba Askofu miaka 3 iliyopita. Kwa ufupi ni kwamba mtoto wangu ambaye ni wa tatu kuzaliwa anaitwa “Bliss Mushongi”. Huyu kwa sasa anasoma shule ya awali ya “LEO LEO PRE-PRIMARY SCHOOL” iliyoko manispaa ya Bukoba.
Kama kawaida inabidi kumuamsha mapema ili aweze kuwahi shule kila siku. Sasa leo alipoamka asubuhi alikuta tayari niko mezani huku nikipanga ratiba ya kazi zangu za siku.
Baada tu ya kunisalimia, akaanza kuniuliza maswali mengi, mengine magumu na mengine ni rahisi. Mtoto huyu kama walivyo kaka zake na mdogo wake, amekuwa na tabia ya kuuliza hadi wakati mwingine ninasikia hasira kwa mbali. Baadhi ya maswali yalikuwa ni kama haya:
“Baba unafanya nini?.…. Napanga ratiba ya kazi za leo; Ratiba ya kufanyaje? …Ya kazi… Kazi gani?...Kazi ya ofisi. Ofisi ndiyo nini?" .......n.k.
Nimemsikiliza huku nikitafakari juu ya udadisi huu wa kijana wangu, na baada ya yeye kutosheka na majibu akaendelea kupata chai yake tayari kwa kwenda shule”.
Maswali haya ndiyo yamenifanya nikumbuke sehemu ya mahubili aliyoyatoa Baba Askofu miaka 3 iliyopita. Na hapa nikaanza kujiuliza ni kitu gani mtoto huyu amenifundisha? Achilia mbali utulivu unaohitajika hasa pale unapopanga ratiba yako ya siku/wiki/mwezi au mwaka.
Katika kutafakari ndipo nikagundua kuwa leo kutoka kwa mtoto BLISS nimejifunza “UMUHIMU WA KUULIZA MASWALI KILA SIKU”. Ukweli ni kwamba ukiwa mtu wa kujiuliza maswali kila siku, ni wazi kuwa utajifunza mambo mapya kila siku.
LAKINI tofauti ya watu wazima na watoto ni kwamba, watu wazima tunawajibika kujiuliza maswali sisi wenyewe na kuyajibu wenyewe; watoto wao mara nyingi upendelea kuuliza wakubwa zao, hii ni kutokana na ukweli kwamba wanajitambua kuwa hawajui.
Mwanzoni watoto wanaanza wakiwa hawajui kitu chochote, lakini kutokana na bidii yao ya kujifunza kwa kuuliza maswali kila siku, hujikuta wakikua kifikra kwa kasi kubwa sana. Kasi hii ya kukua kifikra huwawezesha kufahamu mambo mengi mapya kuliko watu wazima.
Maswali waulizayo kila siku ndiyo huwawezesha kupata majibu mengi mapya, ambayo ndiyo hasa uchochea mabadiliko katika kutawala mazingira yaliyomzunguka.
Kwa wewe unayesoma makala hii sasa, tambua kuwa wakati umefika wa kurudia maisha yako ya utoto, maisha ambayo yalitawaliwa na kipindi cha kuuliza maswali mengi na kutafuta majibu mengi kila siku.
Unayesaka mafanikio ya aina yoyote ile, lazima kuchukua hatua mbili stahiki, KWANZA ni kuwa mtu wa kujiuliza maswali kila siku na kutafuta majibu mapema iwezekanavyo. Hatua ya PILI ni kuyafanyia kazi majibu yako.
Unapoyafanyia kazi majibu yako, lazima utegemee matokeo ya aina mbili; kwanza ni pale unapopata matokeo “CHANYA” . Matokeo chanya yanakuonyesha kuwa majibu ya maswali yako yalikuwa sahihi, na kwa njia hiyo utakuwa umegundua mbinu mpya ya kutatua changamoto au kufikia mafanikio tarajiwa.
Aina ya pili ya matokeo ya majibu yako ni kupata matokeo “HASI”. Matokeo hasi yanakuonyesha kuwa majibu ya maswali yako hayakuwa sahihi – Hapa unakuwa umegudua kitu kikubwa sana, kwani kwa njia hii unakuwa umegundua njia au mbinu ambazo haziwezi kamwe kutatua changamoto ulizonazo na wala haziwezi kukufikisha kwenye maisha ya ndoto yako. Kwa maana nyingine ni kwamba, kitendo cha wewe kugundua njia au mbinu ambazo hazifai, kinakuwezesha wewe kupata sababu ya kuendelea kutafuta majibu sahihi na huo ndio “uzoefu”.
Mgunduzi na mfanyabiashara maarufu kutoka Marekani aliyeishi kati ya mwaka 1847 – 1931 bwana Thomas Edison, inasemekana kuwa, wakati akijaribu kutengeneza taa ya umeme “bulb” na mtandao wa kusambaza umeme, aliweza kushindwa mara 999. Lakini, alipoulizwa juu ya kushindwa kwake mara zote hizo, alijibu kwa kujiamini kuwa yeye hakuwahi kushindwa BALI amegundua njia 999 ambazo hakutakiwa kuzifuata tena kutimiza ndoto yake.
Mfano huo wa bwana Thomas Edson unatufundisha kuwa, pale tunapopata matokeo hasi, kisiwe ni kisingizio cha sisi kuacha kujaribu tena na tena, kwani kila jaribio linatusogeza karibu zaidi na kile tunachokitafuta. Na tunapopata matokeo hasi inatupasa kujiuliza maswali ya kwanini, ili kutafuta matokeo mengine mapya yanayokidhi matarajio yetu au wateja wetu. Matokeo ya kila jaribio siku zote huwa yanakuacha na majibu mapya ambayo ndiyo ukusukuma kwenda hatua zinazofuata hadi kufikia mafanikio unayoyatafuta.
Wasiliana nami:
WhatsApp: 0788 855 409
E-mail: mchumieconomist2009@gmail.com
Tovuti: http://maarifashop.blogspot.com

No comments:
Post a Comment