“Lengo la biashara yoyote ni kutoa suruhisho ya matatizo ya watu-kwa FAIDA” ~ Paul Marsden
Pesa ambayo huwa tunapata mara zote utoka kwenye mifumo mikuu miwili ambayo ni “mfumo wa mshahara” na “mfumo wa FAIDA”. Kati ya mifumo hiyo, mfumo wa mshahara ndio unaotegemewa na kuaminiwa na watu wengi. Lakini...
pia ndio mfumo ambao unazalisha maskini wengi, na ni mfumo ambao watu wake uhangaika sana kutafuta pesa ya kujikimu.
pia ndio mfumo ambao unazalisha maskini wengi, na ni mfumo ambao watu wake uhangaika sana kutafuta pesa ya kujikimu.
Watu ambao huwa wanafanikiwa kupata uhuru wa kipato au pesa ni wale ambao wanapata pesa yao nyingi kutoka kwenye mfumo wa faida kuliko wale wanaotegemea pesa kutoka kwenye mfumo wa MSHAHARA.
Kwa wale wote ambao tunapata pesa kutoka kwenye “mfumo wa mshahara”, biashara yetu kubwa ni ya “KUUZA MUDA” kama ulivyo. Kama unamiliki mfumo wa faida, unaweza kuwekeza pesa yako tena na tena katika mfumo huo huo na hatimaye kupata pesa nyingi.
Mfumo wa mshahara unakupatia pesa mara moja kwa kipindi Fulani kilichopangwa. Mfano kwa waajiriwa wegi serikalini pamoja na makampuni makubwa ya binafsi, pesa inatoka mara moja kwa mwezi nje ya hapo hupati kitu hata kama una shida kiasi gani hakuna namna.
Wakati huo huo, mfumo wa faida unakuwezesha wewe kupata pesa kila siku. Unapoweza kupata mapato (pesa) kila siku inakusaidia kufikia ulinganifu wa mapato na matumizi.
Ukweli ni kwamba, watu wengi tunaopata pesa yetu kutoka kwenye mfumo wa mshahara tunakabiliwa na tatizo sugu la kutokuwa na ulinganifu wa mapato na matumizi yetu. Kutokuwepo kwa ulinganifu wa mapato na matumizi ndiko kunasababisha watu wengi kutumia zaidi kuliko mapato yao halisi.
Mfumo wa mshahara unatufanya tupate pesa mara moja kwa mwezi na wengine kama wakulima ni baada ya miezi miezi 4 hadi 6. Mfumo huu wa kupata pesa mara moja baada ya kipindi kirefu ndio unatufanya watu wengi kukabiliwa na mzigo wa madeni yasiyoisha.
Hali hii ndiyo inatufanya wengi hasa waajiriwa kushindwa kupata mitaji ambayo ingetuwezesha kuingia kwa urahisi kwenye “mfumo wa faida”. Kwa maana nyingine ni kwamba tayari tumejenga tabia au utamaduni wa kula bila ya kuwa na pesa.
Kitu kinachoitwa mshahara au ujira huwa siyo cha kudumu, muda wowote kinaweza kukoma. Inatosha kusema kwamba, maisha ya mshahara yanakutaka usiugue/usiuguze, usisafiri n.k.
Kwa maana nyingine ni kwamba ukisimama kufanya kazi, pesa nayo inakatika hapo hapo. Pesa yako itakoma au kushuka kama utakuwa unaumwa. Pale utakapostaafu, pesa yako itapungua..ingawaje unataka pesa nyingi hasa pale unapostaafu
Hatahivyo, kama utajikita na kuegemea zaidi upande FAIDA , badala ua mfumo wa mshahara basi ataweza kutengeneza pesa wakati akiwa amesinzia au huko kwenye gym n.k. Endapo akiugua bado atatengeneza pesa nyingi. ukistaafu, pesa yako itaendelea kama kwaida.
Maisha ya mshahara siyo rafiki kwa maana hayatoi mwanya kwako wewe kuweza kufanya shughuli au mambo yale unayoyapenda. Mfumo wa mshahara unatumia zaidi ya asilimia 90 ya muda wa mwajiriwa.
Kama mwajiriwa huna udhibiti wowote wa mshahara wako wa kila mwezi. Wale wanaokulipa ndio wanaojipangia wakate ushuru kiasi gani bila hata ya kukuuliza.
Siku zote waajiri wako wanakata pesa yao kwanza, alafu wanakupangia kiasi utakachotumia kuendesha maisha ambayo wao wanaona ni muhafaka kwako. Kimsingi maisha yako yote yanadhibitiwa hadi unakosa kuifurahia dunia hii yenye maziwa na asali.
Kwa ufupi ni kwamba mfumo wa mshahara unakusaidia tu! wewe upate kuishi LAKINI mfumo wa faida unakusaidia wewe kutajirika…jambo ambalo ni zuri zaidi.
Uzoefu umeonyesha kuwa hakuna mtu yeyote ambaye huwa anatajirika kwenye mfumo huu wa mshahara. Labda wanamichezo au wanariadha wachache wenye majina makubwa. Wengine ni wakurugenzi wa makampuni makubwa ambao pamoja na kuuza muda wao, pia, utajiri wao mkubwa unatoka kwenye mfumo wa faida kupitia mikataba yao, kwa mfano kuwekeza na kupewa kiasi fulani cha hisa za makampuni wanayoyaongoza.
Njia pekee ya kupata ukombozi na uhuru wa kipato ni kila mara wewe kutenga kiasi fulani kutoka kwenye mshahara wako, ili kuwekeza pesa hiyo kwenye “mfumo wa faida” kama biashara ya hisa, ardhi ya kukodisha, nyumba ya kupangisha, biashara ya kushirikisha rafiki zako taarifa za bidhaa au huduma (jenga mtandao) n.k. hapo utakuwa tayari kwenye mfumo wa faida.
Ili kupata usalama na uhuru wa kipato, ni wakati muhafaka sasa wa kutoka kwenye “mfumo wa kuuza muda” ili upate pesa yako na kwenda kwenye “mfumo wa faida”.
Ewe mtanzania, muda wa kuanza jitihada za kuingia na kupata pesa kutoka kwenye mfumo wa FAIDA ni leo. Ni muda muhafaka pia wa kuanza kujiuliza maswali magumu. Kwa mfano: inabidi ujiulize; utakuwa wapi miaka 10 ijayo, endapo utaendelea kukaa kwenye mfumo wa mshahara?, je? Ukiendelea kufanya biashara ya kuuza MUDA, utaacha miaka 10 ipite bila kutimiza malengo yako?
Kuna mengi ya kuzungumza kuhusu jinsi ya kuhama kutoka kwenye mfumo wa mshahara kwenda kwenye mfumo wa faida. LAKINI nimeona ni vizuri wewe msomaji wa MAARIFA SHOP, … ukatoa maoni yako juu a dhana hizi mbili yaani MSHAHARA na FAIDA……Endelea kutoa maoni juu ya hili…
No comments:
Post a Comment