Tuesday, March 29, 2016

Unapata Faida Gani Kwenye Woga?



 "Kitu pekee tunachoweza kuogopa ni woga wenyewe" ~ Franklin D. Roosevelt



Jiulize leo: “Ni faida kiasi gani unaweza kutengeneza kutokana na woga?. Na hii ndiyo sababu ya kwanini nimelazimika kuangalia moja kwa moja kwenye macho ya “WOGA” bila woga.....

Neno woga...
linasikika mara kwa mara kuliko "imani na matumaini ya mambo mazuri".

Mwanaume na mkewe wanashirikishana neno “woga” ili kutoshereza hali ya mashaka waliyonayo kwa siku za baadae au mbeleni…

Wapenzi ambao ndo wameanza kupendana, mara nyingi wakati wa mahaba wanashirikishana zaidi “woga” kabla ya kukubaliana…

Wafanyabiashara nao pia wanaongelea sana juu ya WOGA wa kupata hasara zaidi bila sababu…...

Kwahiyo, WOGA ni nini?: Tunaweza kusema kuwa “woga” si kitu chochote zaidi ya hali ya muamko wa hisia za fikra ambazo zinahitaji marekebisho madogo ya mtazamo wa mhusika. Ni hivyo tu basi ndugu yangu!

Muamko wa hisia unatengenezwa ndani ya fikra au akiri yako, na unapewa nguvu na kuruhusiwa na sisi wenyewe.

Sasa tujiulize, ni watu wangapi waliwahi kufanikiwa kwa kujikita zaidi kwenye “Woga”?

Ebu tuchukulie watu wawili maarufu ambao walikuwa mawakala wa mabadiliko makubwa yaliyokuwa chanya:

Wa kwanza ni Thomas Edison: Kama mtu huyu angeangalia woga wake wa kushindwa mara 999 kabla ya kufauru ; leo hii wote tungekuwa bado kwenye giza mpaka leo.
 

Lakini pamoja na kushindwa mara 999; bado aliendelea kuamini na kujiamini kuwa anaweza kufanikiwa.

Ndiyo maana katika nukuu zake aliwahi kusema kuwa: “Sijashindwa, isipokuwa nimegundua njia 999 ambazo haziwezi kufanya kazi na wala haziwezi kufanikisha ndoto yangu”.

Kwasababu hakukata tamaa na hakuusikiliza woga wake unamwambia nini, leo hii wote tunaona na kufurahia mwanga wa umeme.

Wa pili ni Henry Ford: Huyu ni mtu mwingine ambaye ni mfano wa kusisimua abaye aligundua magari; Kama angekata tamaa na kuacha kutimiza ndoto zake, nani anajua pengine leo hii tungekuwa bado tunatembelea ngamia au farasi.

Lakini kwasababu, hakukubali “woga” umtawale, leo hii tunashuhudia watu wengi wakiendesha magari mazuri.

Kwasababu bwana Thomas Edison na Henry Ford hawakukata tamaa na wakaendelea na kazi ya kutimiza ndoto zao, leo hii tunafurahia mwanga wa umeme unaotuwezesha kuona wakati wa usiku huku tukiendesha magari yetu ...

Mpendwa msomaji wa mtandao wa Maarifa Shop, ukweli ni kwamba watu wote tunazo ndoto kubwa. LAKINI ni kwa namna gani tunaweza kuzitimza?

Je? Kukaa tumeangalia na kufikiria zaidi woga kutatufikisha karibu na ndoto zetu? Bilashaka jibu sahihi ni HAPANA!!!

Lazima tubadili fikra na mitazamo yetu kama kweli tunataka kushinda na kupata mafaikio.

Hakuna wakala wa mabadiliko aliyewahi kushinda kwakuwa muhahirishaji wa mambo...

Hakuna wakala wa mabadiliko aliyefanikiwa kwa kuangalia zaidi mambo hasi au kwa kuangalia zaidi juu ya namna gani na kwanini mambo hayatafanikiwa….

Tunahitaji tudanganye woga wetu na tuangalie zaidi kile kitakachozidi kutusogeza karibu na ndoto zetu kuliko kukaa tumeangalia zaidi yale tunayodhani hayawezekani.

Somo tunaloweza kujifunza kutoka kwa Thomas Edison na Henry Ford ni kuwa na tabia ya kuushinda woga.

Kuzidi kujali WOGA hakuwezi kutupeleka karibu na ndoto zetu. Kama ni lazima tushinde, lazima tuwe tayari kudanganya WOGA wetu leo.

Nitawezaje kuushinda “woga” unaonizuia kuwa mjasiriamali?

Suka upya ubongo wako: Kuusuka upya ubongo wako ni njia ambayo ni ya uhakika katika kukabiliana na woga ulionao na kujenga ujasiri unaohitajika ili uweze kwenda huko unakotaka kwenda. Jaribu kuadika maneno ya kiapo cha ushindi na ujiambie maneno hayo kila siku. Kiapo cha namna hii kinakujenga kuwa juu na kuongeza uwezo wako wa kujiamini. Pia, jisomee vitabu na machapisho mbalimbali ambayo yanakusaidia kuingilia kati sauti na mazungumzo hasi ambayo yamekuwa yakiendelea ndani ya akiri yako.

Tagu tukiwa watoto wadogo, tumeambiwa vitu ambavyo hatuwezi kuvifanya, hatuwezi kuwa navyo n.k. Kama hutafanya jitihada za kusuka upya ubongo na fikra zako kwa ujumla, woga utafanya kazi hiyo na matokeo yake yatakuwa mabaya kwako na jamii inayokuzunguka.

Tengeneza mpango wa kufanya yale unayohitaji kufanya: Mara nyingi huwa tunakuwa na woga hasa pale tunapokuwa hatuna taarifa na mpango madhubuti wa kile tuachotaka kukifanya. Weka malengo yako bayana yakiambatana na mpango madhubuti wa utekelezaji. Baada ya hapo chukua hatua kwa kuanza kufanyia kazi yale uliyoyapanga hatua kwa hatua. Kuchukua hatua dhidi ya malengo yetu kunatupunguzia msogo wa mawazo na kutukinga dhidi ya kuchanganyikiwa kunakochochewa na woga wa kushindwa.

Fanya kitu kimoja kila siku ambacho kinakutisha: Kuendelea kukukaa kwenye ukanda wa kujisikia vizuri au hali uliyoizoea, siyo njia nzuri ya kuishi. Bila kufanya vitu ambavyo vitakushitua kunaongeza uwezekano wa woga ndani yako kuwa mkubwa na baadae kuchukua sehemu kubwa ya maisha yako. Kinaweza kuwa kitu kidogo ambacho unakifanya kila siku, lakini fanya kitu kila siku ambacho kinakutisha.

Unapojenga tabia ya kufanya kitu cha kukutisha kila siku, taratibu taratibu ujasiri wako wa kushinda woga unaongezeka siku hadi siku. Muda si mrefu vizuizi ambavyo hapo mwanzo vilikuzuia kusonga mbele, vitapotea na uwezo mkubwa uliopo ndani yako utajitokeza kwa kiwango cha juu sana. Kitendo cha kufanya maamuzi ya kutoruhusu woga ukurudishe nyuma tena, ni mojawapo ya maamuzi bora sana ambayo unaweza kuyafanya ili kuhakikisha mafanikio makubwa mbeleni.

Kufanya maamuzi ya namna hii siyo kitu kinachoweza kutokea kwa siku moja, lakini kuchukua hatua za makusudi na kuukimbia woga wako kila siku, inakupa matumaini ya kupata matokeo mazuri siku za baadae.

Kila kitu kizuri unachotaka maishani kiko nje ya ukanda wako wa kujisikia vizuri au mazoea. Usiruhusu “woga” kuwa ndiyo sababu ya wewe kuishi maisha duni na yasiyokuwa huru. Kwa mbinu hizi tatu hapo juu,pamoja tutamshinda adui “WOGA”.
Endelea kuwa karibu na mtandao wa MAARIFA SHOP Kwa kubonyeza neno “KARIBU”, Kama njia muhafaka ya kujifunza kuushinda “woga”.

No comments: