Kila tupatapo pesa, akiri yetu ututuma kutumia mara moja. Wengi wakishapata pesa, hapo hapo ujihisi kutokuwa na nguvu tena ya kuvumilia shida walizokuwanazo, kabla ya kupata pesa. Kuna wengine hata hawawezi kuvumilia walau masaa mawili bila kuwa wameanza kutumia pesa waliyopata. Kwa maneno mengine ni kwamba,
mihemuko ya kupata pesa inakuwa juu kuliko fikra ya kusubiri.
Yote haya yanatendeka kwako kwasababu bado hujakaa chini na kutafakari juu ya hili. Ukweli ni kwamba suala hili la kutumia pesa hapo hapo baada ya kuipata ni kitu ambacho kimejengeka ndani ya fikra zetu na tuna mazoea nacho kwa muda mrefu.
Utamaduni wa kupata mshahara kila mwisho wa mwezi, tayari umetulemaza kiasi kwamba tunajikuta tunatumia pesa kabla hata ya kuipata. Kwa wale mnaofanya biashara ya kutembeza nyumba kwa nyumba, mtakubaliana na mimi kuwa watu wengi hasa waajiriwa, mara nyingi upenda kuchukua vitu na huduma kwa makubaliano kwamba watalipa mwisho wa mwezi.
Kila kitu kinasubirishwa mwisho wa mwezi; mchango wa harusi, mkopo, matoleo kanisani, bidhaa za mkopo n.k. Vyote hivyo na vingine vingi, mtu anahaidi kulipa mwisho wa mwezi. Sasa unajiuliza, huo mwisho wa mwezi unapata pesa kiasi gani za kuweza kulipia vyote hivyo? na wakati huo huo ukaweza kukidhi mahitaji ya mwezi ambao unauanza. Nadhani ni muda muhafaka sasa tulione kama changamoto kubwa inayotukabili.
Katika kutatua changamoto hii, yako mambo ambayo yanahitaji kufanywa na kila mtu mwenye kuwa na malengo au ndoto ya kutajirika. Lazima kufanya mambo tofauti kwa lengo la kujenga msimamo na utaratibu wa namna nzuri ya kujenga maisha bora na yasiyokuwa na madeni ya kupindukia.
Kitu kikubwa tunachohitajika kukifanya ni kuanza kujilazimisha kujenga moyo wa ujasiri na nidhamu ya kukaa na pesa kwa muda fulani kabla ya kuitumia. Kwa wewe unayetaka kuanza kujenga tabia ya “kusubiri kwanza” ni muhimu kuhakikisha kuwa pindi upatapo mshahara au pesa nyingine, anza kuvumilia kwa kukaa bila kununua au kulipia kitu chochote siku nne, baadae siku saba (wiki), na baadae siku kumi au zaidi kulingana na wewe ambavyo umeamua kufanya. Kumbuka kuwa, muda mzuri wa kukaa na pesa tangu uzipate bila kuzitumia inatakiwa kuwa angalau siku 10 na kuendelea.
Katika kipindi hicho inabidi ujitahidi kuishi maisha yako uliyokuwa ukiishi mwanzo, kabla ya kupata hiyo pesa mwisho wa mwezi. Badala ya kupata pesa na kuanza kutumia mara moja, wewe hakikisha unatumia siku hizo za “kusubiri” katika kupanga vipaumbele vya matumizi ya hiyo pesa ambayo tayari unayo mfukoni.
Nasisitiza vipaumbele kwasababu, siyo rahisi sana kuweza kutoshereza mahitaji yako yote kwa mwezi mmoja, hivyo ni lazima ujipange kuona ni kipi kinahitajika sasa na kipi kinaweza kusubiri. Hakikisha vipaumbele vya matumizi ya pesa yako, vinapangwa kulingana na kiasi cha pesa kinachobaki baada ya kuwa umeondoa fungu la kumi kwaajili ya akiba yako.
Kwa maana nyingine ni kwamba, akiba lazima itengwe kabla ya kufanya matumizi ya aina yoyote ile na kamwe usithubutu kutenga akiba baada ya matumizi mengine, kwasababu haitawezekana. Ukisubiri kutenga akiba baada ya matumizi mengine, kila mara utakuwa unajikuta huna cha kuweka akiba miezi nenda rudi.
SOMA; Hii Ndiyo Hasara ya Kulipa Kwanza Watu Wengine
Kwa wale ambao mishahara yao siku hizi inapatikana kati ya tarehe 22-25 ya kila mwezi, angalau kwa kuanzia, anza na kutotumia pesa yako kwa chochote kile mpaka ifike tarehe 30 yaani mwisho wa mwezi. Baada ya hapo unaweza ukawa unasubiri kutumia mpaka tarehe saba hivi.
Uzuri na faida za kusubili kwanza pindi upatapo pesa ni kwamba, hata madukani na sokoni bei zake zinakuwa zimeshuka siyo kama zile za mwisho wa mwezi. Ukijenga tabia ya kusubiri, taratibu taratibu unaanza kutumia pesa yako kwa vitu ambavyo ni mahitaji ya lazima tu kwa familia. Ukisubiri kwa muda bila kuitumia pesa, utaanza kuona unafika mwisho wa mwezi ukiwa haudaiwi na mtu. Tabia ya kusubiri ikikua zaidi, unaanza kuona akiba yako ikiongezeka mwezi hadi mwezi. Akiba ikikua na wewe unaanza kupata mawazo ya kuwekeza kidogo kidogo. Hali ya uwekezaji kidogo kidogo ndiyo itazaa uwekezaji mkubwa na baadae kuanza kupata kipato kikubwa kutoka vyanzo mbalimbali.
Ukibadili tabia na kuwa mtu wa “pata pesa subiri kwanza”, hapo utakuwa umepiga hatua kubwa na utakuwa tayari umeanza kujitoa kwenye mnyororo wa “tafuta—pata—tumia”. Ukishatoka kwenye mnyororo huu ni rahisi kuingia kwenye mfumo mpya wa Maisha ya pesa ambao ni “Tafuta—Pata—Akiba—Tumia". Uwepo wa “akiba ya pesa” ndio njia pekee ya kuingia kwenye maisha ya uwekezaji—huu ndio utengeneza mifereji mingine ya pesa kuja kwa wingi kwako. Ukianza kuishi maisha ya uwekezaji hapo mnyororo wako utaonekana hivi “Tafuta—Pata—Akiba—Wekeza—Tumia”.
Yote haya niliyoandika na mengine mengi yanawezekana endapo utaamua kutoka kwenye maisha ya “Pata—Tumia”. Maisha ya pata tumia hayatatufikisha kule tunakotaka kwenda. Lazima tuende zaidi ya hapa tulipo, ndiyo maana nasema tuanze kidogo kidogo kubadilika, ambapo leo uichukulie kama siku muhimu na muhafaka ya kuanza kujenga tabia mpya ya “Pata—Subiri—Tumia”.
Endelea kujifunza zaidi kupitia mtandao wako wa MAARIFA SHOP.

No comments:
Post a Comment