Monday, October 8, 2018

Sunday, September 9, 2018

Umezaliwa Leo Kama Mimi Unahitaji Kuingia Hapa “Kujaribu House”

HAPPY BIRTH DAY TO ME

"Ukijaribu na Kushindwa Mara Nyingi Sana Kinachobaki ni Kufanikiwa" ~ Cypridion Mushongi
Leo (09/09/2018) ni siku yangu ya kuzaliwa. Siku hii ni muhimu sana kwangu kutokana na ukweli kwamba inanipa fursa ya kujitathimini mwenendo wa maisha yangu na familia yangu LAKINI pia napata kutathimini mchango wangu kwenye jamii. Tangu mwaka 2016 nilianza utaratibu wa kuadhimisha siku yangu ya kuzaliwa kwa kuandika makala maalumu kuhusu mambo mbalimbali. 

Mwaka 2016 tarehe kama ya leo, niliandika juu ya tofauti ya KUKUA na..

Friday, April 27, 2018

Pesa na Hifadhi ya Nishati Mwilini Vinahusiana Namna Hii


Pesa yoyote halali inapatikana kwa kufanya kazi halali. Kufanya kazi kwa juhudi na maarifa kutategemea sana uwepo wa nishati au nguvu mwilini. Nishati mwilini ni kitu cha kwanza na cha msingi katika kuleta ubora wa maisha yetu. Nishati au nguvu mwilini inapatikana kutokana na vyakula tunavyokula. Pia, tufahamu kuwa nishati ipatikanayo mwilini utumika katika kufanya shughuli za ndani ya mwili na shughuli za nje ya mwili kama zile za uzalishaji mali. Tatizo lililopo kwasasa ni...

Friday, April 13, 2018

Huu Ndio Muujiza wa Vyakula Vinavyoishi



Wewe kama binadamu anayejitambua na kujipenda, unahitaji kufahamu kuwa wewe ni matokeo ya kile ulacho kila siku. Kwa kufanya mageuzi katika lishe yako, unaweza kabisa kubadili maisha yako kuanzia muonekano, nishati/nguvu ya mwili hadi uchumi. Wengi wetu tayari tunafahamu juu ya ulaji wa kunenepesha mwili au kupunguza mwili, lakini ni watu wachache sana ambao wanatambua jinsi ya

Tuesday, March 27, 2018

Umuhimu wa Kutambua Kabila Lako Jipya ni Huu



Kabila ni kundi la kipekee ambalo linajitegemea katika kuendesha maisha yake. Kwa kiasi kikubwa kabila, ni kundi ambalo linajitosheleza, na watu wake wanachangamana kwa kiasi kidogo sana na jamii pana ya kitaifa. Pia, kabila ni mgawanyiko wa..

Tuesday, February 27, 2018

Andika Mawazo Yako na Ukae Kimya

Watu wengi wana mawazo mazuri, wana ndoto kubwa, lakini mojawapo ya sababu ya kwanini hakuna kinachofanyika ni kwamba wengi tunaongea sana. Utakuta mtu ndo kwanza amepata wazo la kufanya kitu fulani, lakini saa hiyo hiyo anaanza kuwashirikisha anaowaita marafiki zake. Na kuanzia hapo inakuwa kila siku ni...

Friday, February 23, 2018

Thamani ya Maisha Kabla ya Kifungua kinywa ni Ipi?


“Fikra ni viumbe hai” ~ Swami Sivananda
Siku zote, maisha ni kile ufanyacho kuanzia pale unapoamka kitandani asubuhi hadi pale unapokwenda kulala au unapomaliza siku yako. Kwa maneno mengine ni kwamba, kila unapoamka mapema asubuhi, maana yake umeanza maisha upya. Wengi wetu hatujaweza kutambua thamani kubwa iliyopo katika masaa haya ya kuanzia tunapoamka kitandani hadi pale tunapopata kifunguakinywa. Ukweli ni kwamba, masaa ya kabla ya kifunguakinywa ni

Friday, January 26, 2018

Mali Hizi Tatu Tayari Unazimiliki Japo Hujui



 
Kama kuna kitu nakipenda kukifanya katika maisha ni pamoja na kujitahidi kila mara kurahisisha mambo yanayoonekana kuwa magumu kwenye jamii. Napenda kulifanya suala la kupata pesa kuwa rahisi, ndiyo maana nimeandika makala nyingi juu ya pesa, ikiwa ni pamoja na kuendesha semina za mafunzo. Lengo kuu limekuwa ni kusaidia watu wengi kufahamu na kuelewa mambo ya msingi juu ya pesa. Kitu ambacho huwa nasisitiza kila mara ninapoandika makala na kufundisha watu wengine, ni...