"Imetosha kusherekea 2016 – Twende Kazini!!"
– Leo wakati naamka asubuhi, nilijikuta nikijisemea maneno moyoni bila kutoa sauti yoyote. Maneno ambayo nilijisemea ni “sherehe za mwaka mpya zimeisha na sasa nikwenda kazini tayari kuanza utekelezaji wa malengo yangu ya 2016.
Hapa ninamaanisha – Haijalishi unayo mikakati ya namna gani au umejiwekea malengo makubwa kiasi gani mwaka huu, BADO hutaona mabadiliko ya kweli, iwapo....
HUTACHUKUA HATUA wewe mwenyewe binafsi.
Na hapa nimetengeneza orodha yangu ya mambo MATANO kama sehemu ya ushauri kutoka kwangu, ili kukusaidia na kukurahisishia wewe katika kutekeleza na kutimiza malengo yako ya mwaka 2016.
1. Uwajibikaji: Hapa ni lazima ujiwekee utaratibu wa kujiwajibisha mwenyewe kwa kuandika malengo yako ya mwaka kwenye kipande cha karatasi na ukibandike ukutani (chumbani, sebureni n.k.); Yaandike malengo yako na weka kwenye komputa yako sehemu ambayo kila ukiifungua ndiyo yanakuwa ya kwanza kusomeka; Weka malengo yako kwenye simu, intaneti au tovuti. Itakuwa vizuri zaidi, ukamwambia mshauri (mentor) wako au rafiki na familia yako juu ya malengo uliyojiwekea.
Lengo ni kuyaandika malengo yako na kuyaweka mbele yako au nje ya kichwa chako, ili huyaone na kuyasoma kila siku unapoamka. Utaratibu huu, utakufikisha hadi kwenye mafanikio unayoyataka kwa urahisi na haraka zaidi.
Hiki ni kitu ambacho huwa nakiongea mara nyingi kila ninapoendesha semina za mafunzo kwa wajasiriamali. Usikae na kuweka akiri yako kwenye PESA, bali ufikirie zaidi mafanikio na malengo. PESA itakuja kama utafanikiwa kutimiza malengo yako uliyojiwekea. Hii ni kutokana na ukweli kwamba “Pesa ni matokeo ya hatua zinazochukuliwa dhidi ya malengo”.
3. Mtazamo na Tabia: Haijalishi wewe ni makini kiasi katika dunia, kama wewe ni mtu mwenye mtazamo hasi na unayeamini katika kushindwa juu ya kile unachokifanya, basi ujue kuwa utahangaika sana na mwisho hutafanikisha malengo yako. Unahitaji kuwa na fikra sahihi, mtazamo sahihi na nguvu ya tabia, ili kuhakikisha unatimiza na kukamilisha malengo.
4. UPANGE mwaka wako wa 2016 sasa: Kutekeleza malengo kunahitaji mipango thabiti. Huwezi kuweka malengo bila mpango. Unahitajika kuchambua vizuri vikwazo na rasilimali zinazohitajika katika kukamilisha malengo yako. Nasema “Weka mpango sasahivi na uufuate”.
Ninashauri uweke malego madogo madogo kutoka kwenye malengo ya makubwa au ya jumla. Ukishajiridhisha kuwa malengo yako yanatekelezeka, basi fikiria hatua utakazozipitia hadi kukamilisha malengo. Ni rahisi kufikia kileleni mwa jengo lefu kwa kuanza kupanda ngazi moja baada ya nyingine kuliko kuruka au kukwea ukuta.
5. Jiandae kushindwa: Malengo siku zote hayawezi kuwa rahisi kuyatimiza. Kwahiyo, waweza kushindwa pia!. Lakini kumbuka kuwa siku zote mafanikio yanachangiwa na kile unachojifunza kutokana na kushindwa pamoja na jinsi utakavyo kabiliana na kushindwa. Unapokuwa umeanguka, jifunze namna ya kupangusa magoti, nyanyuka, simama na uzidi kusonga mbele kuelekea kwenye malengo yako ya mwaka 2016.
Kwahiyo, hivyo ndivyo ilivyo, baada ya kusema hayo nisema….. ANZA KAZI!!... tayari mwaka 2016 umeanza bila wewe! Kuwa na hisia za tabasam. Napenda kuwatakia wasomaji wangu wa mtandao wa MAARIFASHOP… Heri ya Mwaka Mpya!
Ni matumaini yangu kuwa ulijifunza mengi hapa MAARIFASHOP na kwamba ulisherekea vizuri sana ukiwa na marafiki pamoja na familia siku ya mkesha wa tarehe 01/01/2016!.
Kama unataka kutumiwa makala mpya moja kwa moja kila zitakapochapishwa ni rahisi, unahitaji kufanya jambo moja nalo ni kubonyeza neno “MAKALA”, kisha weka e-mail yako na jiunge na kundi la whatsap kwa masomo ya kila siku bonyeza neno WHATSAP group.

No comments:
Post a Comment