Friday, January 15, 2016

Huu Ndio Muujiza wa Makosa



“Mtu yeyote ambaye hajawahi kufanya makosa, ni yule ambaye hajawahi kujaribu kitu chochote kipya” ~ Albert Einstein ~
 Mpendwa msomaji wa MAARIFA SHOP ni kwamba kuna kitu kama muujiza karibu kwenye kila kosa lifanyikalo katika maisha yetu ya kila siku. Na muujiza huu unaitwa....
kujifunza au mafunzo. Nimetumia muujiza LAKINI kuna sayansi nyuma mafunzo yatokanayo na makosa tunayoyafanya kila siku. Kiukweli, ni sehemu ya msingi ya kila mchakato wa mantiki ya kujifunza. – hata wanyama wana uwezo wa kujifunza kutokana na makosa. Wanajifunza pia kutoka kwenye makosa yanayofanywa na wanyama wenzao.

Huko shuleni huwa tunajifunza kwamba makosa ni kitu kibaya sana na mara nyingi huwa tunapewa adhabu kila tunapofanya makosa. Hatahivyo, ukingalia namna ambavyo binadamu ametengenezwa kujifunza ni kwamba, sisi huwa siku zote tunajifunza zaidi kwa kufanya makosa.

Fikiria wakati ukiwa mdogo, makosa uliyoyafanya wakati ulipokuwa ukijifunza namna a kuendesha baiskeli. Utakumbuka kuwa ulifanya kosa moja baada ya lingine. Na baada ya siku chache ghafla, hukuanguka tena na badala yake tairi la baisikeli liliendelea kuzunguka, huku wewe ukizidi kusonga mbele bila kuanguka tena na kama vile “muujiza” dunia mpya ilifunguka kwako. Huo ndio MUUJIZA unaopatikana kwenye MAKOSA.

Mwanasayansi (Fizikia) mashuhuri aliyejulikana kwa jina la Albert Einstein aliwahi kusema kuwa “Mtu yeyote ambaye hajawahi kufanya makosa, basi mtu huyo hajawahi kujaribu kitu chochote kipya”. Kama unajifunza kitu chochote kipya, basi unatakiwa kufanya makosa, ili kukifahamu na kukielewa vizuri kile ulichojifunza. Kwahiyo, jitokeze na ukajaribu fursa mpya. Fanya makosa…….

Ni jinsi gani tunaweza kukabiliana na maudhi yatokanayo na makosa yetu.

Watu waliofanikiwa huwa wanakabiliana kwa kujifunza kutokana na maudhi ya makosa yaliyofanywa ama na wao wenyewe au na watu wengine.

Nilipoanza kuwa na ndoto ya kuwa mjasiriamali mkubwa na wa kimataifa, rafiki yangu na kocha wangu katika masuala ya ujasiriamali na biashara alinishauri ya kwamba nitafute kazi ambayo itanifundisha jinsi ya kuuza. Baada ya muda nilianza kufanya biashara ya ubia na kampuni ya kimataifa ya FOREVER LIVING PRODUCTS. Mwanzoni, nilikuwa na aibu sana na kazi ya kuuza ilikuwa ni kitu cha mwisho kukipenda, LAKINI kumbe hiki kilikuwa ni kitu pekee nilichokihitaji.

Kwa miaka miwili, naweza kusema kuwa nilikuwa muuzaji mbovu nilipokuwa nikijilinganisha na watu wengine wanaofanya biashara na kampuni hii ya kimataifa ya Forever Living”. Muda wote nililaumu sababu nyinginezo juu ya kushindwa kwangu kuwa muuzaji bora. Kwa mfano; nililaumu sana hali mbaya ya uchumi, bidhaa, hata wateja wangu. Kocha wangu hakupenda hata kuyasikia hayo yote niliyokuwa nikilaumu. Kama kawaida alipenda kwenda moja kwa moja kwenye msingi wa tatizo zima. “Pindi watu wanaposhindwa wao wenyewe, alisema: huwa wanapenda kulaumu”

Kocha wangu wa ujasiriamali, alikuwa anajaribu kunifundisha kwamba hisia za maumivu ya kufanya makosa zina nguvu sana kiasi kwamba watu wengi huamua kusukuma maumivu kwenda kwa watu wengine kupitia “kulaumu”. Wanasaikolojia ya akili ya binadamu wanadai kwamba mtu anapofanya makosa akapata wa kumlaumu na akafanya hivyo anapata nafuu na kujifariji. Ili nijifunze kuuza, nililazimika kuvumilia na kukabiliana na maumivu ya kushindwa kuuza bidhaa. Kadiri mchakato ulivyoendelea, nilijifunza namna ya kubadili maudhi ya makosa kuwa kitegauchumi badala ya changamoto au madeni.

Je? woga wa kupata maumivu ya kukataliwa na watu unakurudisha nyuma?: Kila mara nikutanapo na watu ambao wanaogopa kujaribu kitu fulani kipya, mara nyingi sababu huwa ni kwamba wanaogopa sana kufanya makosa au kupata maumivu yatokanayo na kukataliwa na watu. LAKINI uhalisia wa mambo ni kwamba, ili huweze kufanikiwa katika maisha, siyo tu kubahatisha, unahitaji kujaribu vitu vipya. Na kama utafanya hivyo, basi ujiandae kupata maudhi au kukataliwa ~ “Maumivu”.

Watu wengi hubadili maumivu ya makosa kuwa hasara au madeni kwa kusema vitu kama: sitarudia kufanya jambo hili tena” au ningejua nitashindwa.” Kwa kufanya hivyo, huwa wanaruhusu maumivu ya makosa yawarudishe nyuma. Watu hawa kwa maana nyingine wameacha kujifunza. Wamejijengea ukuta wa kuwakinga badala ya kujega msingi wa kuendeleza zaidi hicho wanachokifanya.

Maumivu ya makosa ni sehemu ya mafanikio: Lakini kama ilivyo kawaida kila tatizo ndani yake kumelala fursa, ndani ya maudhi yoyote kuna busara ndani yake. Ufunguo wa yote ni jinsi ya kukabiliana na kujifunza kutoka kwenye maudhi.

Kocha wangu katika biashara na ujasiriamali, alinisaidia sana kujifunza namna ya kukabiliana na hisia kali za maumivu ya kushindwa. Alisema, “sababu ya kuwepo watu wachache waliofanikiwa ni kwasababu ni watu wachache wanaoweza kuvumilia maumivu yatokanayo na makosa. Badala ya kujifunza kuyakabili, wanatumia muda wao mwigi kukwepa maumivu ya kushindwa/makosa.”

Kocha wangu aliamini kwamba maumivu ya kushindwa ni sehemu muhimu sana ya mafunzo katika maisha yenye mafanikio. Kama tunavyozidi kujifunza kutokana na makosa tunayoyafanya, ndivyo tunavyozidi kupata tabia ya ujasiri katika kutafuta mali kutoka kwenye maudhi ya makosa.

Hapa ni sehemu tu ya ushauri alionipatia juu namna ya kukabiliana na maumivu kufanya makosa.

1. Tarajia maudhi au kukataliwa:
Ni mjinga pekee anayetarajia mambo yote yafanikiwe kama alivyopanga, alisema kocha. Lakini, kusema kuwa mtu atarajie kupata maudhi, haina maana kwamba akae tu bila kuchukua hatua au akishindwa akae tu bila kufanya chochote BALI maana yake ni kwamba mara nyingi tunahitaji kujiandaa kiakiri, kifikra na kihisia, ili kuwa tayari kukabiliana na hali yoyote itakayojitokeza nje ya matarajio yetu, ambayo pengine unaweza usiitake au usiipende. Hii inakuruhusu kuwa mtulivu na mwenye heshima pindi pale mambo yasipokwenda sawa na ulivyotarajia, hali ambayo baadae ukuruhusu wewe kufikiri vizuri zaidi.”

Mafanikio yanachukua muda, na katika safari yake kuna kero nyingi sana. Lazima huwe tayari na huwe na nia ya kuendelea mbele huku ukijifunza kutoka kwenye makosa mbalimbali utakayoendelea kuyafanya wakati ukielekea kwenye safari ya maisha ya ndoto zako.

2. Kuwa na kocha karibu yako
Pindi mambo yakienda vibaya, ni nani utamwita? Kama ambavyo tuna namba ya dharura kwa kikosi cha zima moto na polisi, basi tunahitaji mtu tutakayempigia simu pindi tunapohitaji msaada wa ushauri juu ya mambo ya kibiashara na kifedha.

Mara nyingi kabla ya kuingia kwenye deal au venture, huwa ninamuita mentors na kuwauliza au kupata ushauri. Hii uniwezesha kujifunza kutoka kwa wengine na kutumia yale ninayojifunza kutoka kwa wnzangu kwenye mazingira ya kwangu.

3. Kuwa mwema kwa wewe binafsi
Mojawapo ya jambo la maumivu ya kufanya makosa au kushindwa kufanya kitu fulani siyo yale wasemayo watu wengine, BALI ni namna gani sisi tunajiona na kujisikia baada ya kufanya makosa. Watu wengi hufanya makosa na kujipiga wenyewe zaidi kuliko wanavyopigwa na watu wengine.

Nimegundua kuwa watu ambao wanakuwa wakali kwa wao wenyewe binafsi kiakiri na kihisia mara nyingi ni watu wa tahadhari sana, hasa linapofika suala la kutenda mambo wanayohisi ni ya hatari; kuchukua mawazo mapya; na au kujaribu kitu na fursa mpya. Ni vigumu kujifunza chochote kama kila mara huwa unajipa adhabu. Kwahiyo, jitahidi kuwa mwema wa wewe mwenyewe binafsi.

4. Sema Ukweli
Mojawapo ya adhabu mbaya niliyowahi kuipata ni kiwa mtoto ni pale kwa bahati mbaya nilipompiga jiwe usoni karibu na jicho mtoto wa jirani yetu. Mtoto huyo alikimbia nyumbani kwao kumwambia baba yake, nilikimbia na kujificha lakini . Baada ya baba yangu kupewa taarifa hizo alikasirika sana, na alinipa kichapo kikali huku akisema “Sababu ya kukupa adhabu siyo kwasababu ya kumpiga jiwe mtoto mwenzako BALI “ninakupa adhabu kwasababu ya kukibia na kujificha”.

Kwa maana nyingine KIFEDHA, kuna mara nyingi watu tumekuwa tukikimbia makosa, LAKINI kukimbia ni kuchukua njia rahisi “shortcut”. Wote huwa tunafanya makosa na kukutana na kero pamoja na maudhi. Tofauti ni kwamba, ni jinsi tunavyokabiliana nazo. Hii inaanza kwa kuona au kukabiliana na madhara/athari za hatua tuchukuazo na kusema ukweli juu ya chanzo na sababu za sisi kushindwa. Ni kwa njia hii pekee ndio tunaweza kukua kibiashara na kujifunza mbinu za kisasa katika kukabiliana na changamoto zitokanazo na makosa tunayoyafanya.

Aksante kwa kusoma makala hii. Kama kawaida, ukiona kuna thamani yoyote uliyoipata ndani ya makala hii hapa MAARIFA SHOP, tafadhari washirikishe rafiki zako wote na wataarifu iwapo wanapenda kufaidi kama wewe, basi ni kubonyeza neno “KUJIUNGA”. Kumbuka kuwa Mafanikio ni kitu cha kushirikishana ili kufikia maisha bora.

No comments: