“Mimi siyo zao la hali yangu ya maisha BALI ni zao la maamuzi nifanyayo kila siku”. ~ Stephen Covey ~
Ukibahatika kupata na kusoma kitabu cha “Are you fully charged?” Utajifunza mambo makubwa sana ambayo yatarahisisha kazi yako ya kusaka mafanikio makubwa.
Kutoka katika kitabu hiki na mimi nimejifunza mambo mengi sana LAKINI nimeona nikushirikishe mambo 5 kama sehemu ya mambo niliyojifunza kutoka katika kitabu hiki: Mambo 5 niliyojifunza mimi binafsi ni….
Ushindi katika maisha: Binadamu wengi wanadhani vitu pekee vinavyoweza kuwaletea ushindi mkubwa ni vile vikubwa tu! Lakini, mwandishi wa kitabu hiki cha “Are you fully charged?” anasema kuwa kitu kinacholeta ushindi mkubwa ni wewe kutengneneza maana kwa ushindi mdogo mdogo.
Unahitaji kujiuliza ni kitu gani hicho ambacho utakifanya leo kilete utofauti? Hata kama ni kidogo. Utofauti mdogo mdogo ndio unapelekea utofauti mkubwa, hivyo hivyo ushindi mdogo mdogo ukikusanyika kwa pamoja ndio unaleta ushindi mkubwa.
Usipuuzie jambo dogo ukadhani unapolifanikisha litakua halina utofauti mkubwa, HAPANA si kweli. Cha msingi ni wewe kuhakikisha kila unachofanya hata kama ni kidogo unakifanya vizuri ili kuleta maana. Siku zote maana inaletwa kwa kuunganisha ushindi mdogo mdogo na kisha kuwa ushindi mkubwa.
Hamasa ya kazi: Fanya vitu kutokana na msukmo wa ndani au hamasa ya ndani kuliko hamasa ya nje. Hamasa au msukumo wa nje huwa sio endelevu, hivyo ukiutegmea siku zote utapotea tu! Na huwa siyo wa kudumu. Hamasa ya ndani hua ni ya mtu binafsi.
Hamasa ya ndani ya mtu binafsi, ndio inayompa mtu nguvu ya kufanya zaidi na zaidi, hata anapokutana na vikwazo. Mfano kama unafanya biashara, hamasa ya nje inawezakuwa ni kutengneza faida kubwa, na hamasa ya ndani ikawa ni kuwafanya wateja wako kuwa na furaha au kutoa suruhisho la matatizo yanayowakabili wateja.
Faida ya kutambua mahitaji ya jamii/dunia: Unatengneza maana pale uwezo wako na vile unayovipenda vinapokutana na mahitaji ya jamii. Kufahamu vipaji vyako na kile upendacho katika maisha ni muhimu, lakini hilo halitoshi maana hilo ni nusu tu katika mlinganyo kuzalisha na kuhitaji vitu na huduma.
Kitu ambacho kinaweza kuwa cha muhimu zaidi ni kufahamu jamii yako au dunia inahitaji nini kutoka kwako na jinsi gani unavyoweza kutumia vipaji na uwezo wako katika kuzalisha kile unachopaswa kutoa kwa jamii au dunia.
Furaha katika Maisha: Katika safari ya maisha, tunatakiwa kusafiri na furaha muda wote na siku zote Kwa maana nyingine furaha siyo tukio la muda fulani bali inatakiwa kuwa sehemu ya maisha.
Lakini, kwenye kitabu hiki tunakumbushwa kuwa ili huweze kuwa na furaha ya kudumu ni vyema ukaacha kutafuta furaha kama furaha na badala yake ujikite katika kutafuta “Maana”.
Utafutaji wa maana ndio unaofanya maisha yawe ya thamani na sio utafutaji wa furaha. Watu wanaotumia muda mwingi katika maisha kujitafutia furaha yao binafsi, huwa hawaipati.
Furaha pasipo maana ni sawa na maisha yenye ubinafsi. Watu wanaoishi maisha yenye maana huwa wanapata furaha kubwa sana kwa kuwapa watu wengine.
Simamia vizuri muda wako: Matakwa ya wengine katika zama hizi za leo ambapo kuna taarifa kibao zisokuwa na kikomo. Pia kuna vizuizi vingi visivyoisha, ni rahisi kutumia muda mwingi katika mabishano na majibizano.
Ni rahisi sana kukosa umakini katika kazi kwasababu ya simu au radio, runinga n.k. Matakwa ya wengine yanayokuja kwako lazima yatatumia sehemu ya muda wako wa siku.
Mfano wapo watu watataka kuchati na wewe, kukupigia simu muongee, wapo watakaotaka mtoke wote n.k. Ila baada ya miaka kadhaa vitu utakavyokua unajivunia havitatokana na matokeo ya kufuata matakwa ya wengine.
Kitu kitakachokupeleka mbele katika maisha yako ya baadaye ni kile ulichoanzisha leo na sio ulichoanzishiwa. Usiishi maisha yako kwa kuwa mtu wa kujibu yanayoendelea kutendeka badala yake huwe ni mtu wa kuazisha vitu ambavyo baadaye utakua unajivunia.
Mambo hayo matano ni baadhi tu ya busara nilizozipata ndani ya kitabu hiki cha “Are you fully charged?” Kama unapenda kupata kutumiwa kitabu hiki kwa lengo la kukisoma kwa undani zaidi, basi bonyeza NITUMIE KITABU. Ndani ya masaa 48 utatumiwa kitabu hicho mara moja.
No comments:
Post a Comment