Tuesday, January 26, 2016

Unataka Kutajirika Anza na Hili

“Uhuru wa kipato upo kwa wale tu waliotayari kujifunza na kufanya kazi” ~ Robert Kiyosaki
Watu wengi wanatafuta utajiri kwa hudi na uvumba, japo wengine wachache wanapata na waliowengi wanakosa na kukata tamaa. Jambo ambalo ni dhairi kabisa ni kwamba, watu wengi tunaanza safari ya kutafuta utajiri katika hatua au vituo tofauti tofauti. Kwahiyo, swali la kujiuliza ni je? Safari yetu ya kutafuta Utajiriinapaswa kuanzia...
wapi?.

Katika utafiti na uzoefu wangu nimegundua kwamba, UTAJIRI unaanzia kwenye fikra. Na “fikra ni nguvu pekee inayoweza kuzalisha utajiri wa kuonekana kutoka kwenye vitu visivyoonekana”. 

Kila kitu unachokifanya sasa hivi kimeanza kama wazo kutoka ndani yako. Hakuna matendo utakayotenda bila kuanzia kwenye fikra (mawazo).

Kwahiyo, ukiwaza kwa namna fulani, basi ujue kwamba utapata utajiri wa namna fulani sawa na ulivyowaza mwanzoni kabla ya kupata utajiri huo. Fikra au mawazo, ndio kitu pekee ambacho huweza kukusukuma kufanya vitu fulani fulani ambavyo ndivyo huweza kukuletea utajiri.

Utajiri sio dhambi, bali ni sehemu ya maisha, tumeletwa hapa duniani kuweza kutawala vilivyopo na kama ukiweza kuvitawala vizuri ni lazima utakuwa tajiri. Unachohitaji ni kuweza kugeuza ndoto yako kuwa kweli.

Wakati ukifanya yote hayo, kumbuka kuwa, wewe ni mtu mwenye thamani kubwa sana isiyokuwa na mwisho. Hata kama unajiona wewe sio mtu mbunifu, hata kama ulishashindwa huko nyuma, hata kama unafikiri umeshajaribu kila kitu ila ukashindwa, jua kwamba bado una nafasi kubwa ya kupata chochote unachotaka.

Huwezi kuishi maisha unayoyataka, huwezi kuishi maisha yenye uhuru kama huna utajiri. Huwezi kuinuka na kufikia juu kwenye chochote unachofanya kama kweli huna uhuru wa kipato.

Ndio maana ni muhimu sana kwako kuwa TAJIRI. Kwa kawaida binadamu wote tunazo nia tatu ambazo tunaishi nazo, yaani mwili, akiri na roho. Nia hizi ndizo utengeneza maeneo muhimu ambayo utuongoza kuishi ama maisha ya utajiri au maisha ya umaskini.

Maeneo hayo yote matatu ni muhimu sana katika kuishi maisha yenye mafanikio na furaha. Ni lazima mwili uwe na utajiri, akili iwe ya utajiri na roho pia iwe na utajiri, hapo ndipo itawezekana wewe kuifikia ndoto yako ya utajiri.

Lengo la maisha yetu ni maendeleo yaletwayo na utajiri na wala si kitu kingine. Msingi mkuu wa maisha ni kuendelea kupiga hatua. 


Kama kila kitu kwenye maisha kinakazana kuwa zaidi ya kilivyo sasa, iweje wewe leo uendelee kuwa pale pale miaka yote? Mti unakazana kukua zaidi ya ulivyo sasa. 

Na wewe binadamu pia ni lazima ukazane kuwa bora zaidi ya ulivyo sasa katika maeneo yote muhimu ya maisha yako.

Katika harakati zako za kutafuta utajiri, lazima kuhakikisha kuwa fikra zako zinakuwa safi muda wote. Unatakiwa kutumia nguvu ya utashi wako kuzuia akiri yako isirishwe mambo ya umasikini, na ifanye akili yako ibaki imeshikiria imani na kusudi la maono ya kile unachotaka kufanya au kuumba .

Kamwe usizungumze: Jitahidi usizungumzie kuhusu matatizo yako ya zamani ya kifedha kama ulikuwa nayo; usiyafikirie kabisa.Usizungumze kuhusu umaskini wa wazazi wako au ugumu wa maisha yako ya huko nyuma. Kufanya lolote kati ya hayo ni kujiweka kiakiri katika umaskini kwa wakati huu ulionao sasa.Weka umsakini na mambo yote yanayohusiana nao kado au nyuma yako kabisa.

Linda mazungumzo yako: Kamwe usizungumze kuhusu masuala yako au chochote kile katika namna ya kuvunja moyo au kukatisha tamaa. Kamwe usikubali uwezekano wa kushindwa au kuzungumza katika namana inayoashiria kushindwa. Unatakiwa kutozungumza kuhusu nyakati kuwa ngumu au mazingira ya biashara kama vile una mashaka.

Nyakati zinaonekana kuwa ngumu kwa wale wote walio katika usawa wakushindana na wenzao. Lakini, wewe unayetafuta utajiri wako hunabudi kuanza kujifunza maisha yale ambayo unashindana na malengo yako au ndoto zako basi. 


Mwisho lakini siyo kwa umuhimu nipende kusema kuwa Mafanikio ni mchakato siyo tukio. Kwahiyo, kama wewe umeweza kujifunza kitu chochote kipya na cha thamani kutoka kwenye makala hii ni wazi kwamba tayari umeanza mchakato wa kuelekea mafanikio. 

Kitu kikubwa kingine unachoweza kufanya ni kuwashirikisha marafiki zako wanaopenda kujifunza namna bora ya kufanikiwa na hapa wanahitaji tu kubonyeza neno “NITUMIE MAKALA MPYA”.

No comments: