Friday, January 8, 2016

Safari Mpya “2016” Imeanza Unasubiri Nini?


“Wakati wa kuvunja mfumo wa tabia zote zinazokuzuia kufanikiwa ni sasa hivi”

 

Mpendwa msomaji wa MAARIFA SHOP; Je! Unaweza kuamini kuwa tayari tumeishafyeka WIKI MOJA ya mwaka mpya wa 2016?
 ... Endapo na wewe huko kama lile kundi la wengi, basi yawezekana tayari umeanza kusahau yale yote uliyokuwa ukipanga kufanya pindi mwaka mpya wa 2016 utakapofika.  
Heee! Kumbe tayari tumo ndani ya meli iitwayo 2016 ambayo.......
iko kwenye mwendokasi wa ajabu kuelekea nyumbani kwetu! “mwaka 2017”.

Yawezekana wewe ni mmojawapo wa wale watu ambao walionekana kuwa na shauku na mihemko juu ya mipango na malengo mapya hasa kila inapofika mwisho wa mwaka (Novemba na December).

Lakini, chakushangaza ni kwamba mara baada ya sherehe za mwaka mpya kuisha, mpaka sasa hatukusikii ukiongelea tena malengo mapya na mipango mipya ya mwaka huu wa 2016. Ni nini kimetokea hadi ndani ya kipindi cha wiki moja sasa tangu mwaka mpya uanze tayari umeanza kusahau malengo yako ya mwaka huu?....

Ni dhairi kwamba, tayari ndani ya akiri yako, unayo malengo mengine na uenda ukatumia mfumo na utaratibu ule ule wa mwaka jana, ambapo uliishia kuwaza tu malengo wala hukuandika mahala popote na sasa UMESAHAU!! Lakini; Hiyo siyo tabia ya kuwa nayo.

Siyo muda wa kukata tamaa. Ndoto zako na malengo yako ni muhimu sana. Sasa ni muda wa kufanyia kazi malengo yako, ili kutengeneza maisha halisi unayoyataka.

Labda malengo yako ni kuanza biashara yako mpya. kupunguza uzito, kutoka kwenye madeni, kujenga mahusiano mapya na kuanza upya. Sawa malengo haya yanatekelezeka na mimi nina uhakika kwamba unaweza kutimiza malengo haya na zaidi!

Unaweza ukawa unashangaa na kujiuliza maswali ya kwanini huwa unashindwa kwenda na muda na baadae kushindwa kufikia na hatimaye kuishi maisha ya ndoto yako?

Je inawezekana hatuwi wakweli pale tunapoweka malengo na kupoteza nia na shauku ya kuyatekeleza? Je ni kweli tunamaanisha kuendelea na mfumo wa maisha ambao ni wa kuhangaika huku na kule? Ni kusudio letu kuendelea na mfumo wa maisha ambao kila mara tunajikuta tunakwama mwaka hadi mwaka? SIDHANI KABISA!.

Siku zote huwa tunaishi maisha yetu kwa kufuata mfumo wa imani au mtazamo fulani na kila mara vitu hivi (imani na mtazamo) tunakuwanavyo, na huwa ndivyo vinavyotuchochea kufanya maamuzi mbalimbali.

Imani na mtazamo wetu vimekuwepo kwa kipindi kirefu, na ndivyo utusaidia kutoa maana ya jinsi tutakavyo endesha maisha na kutambua sehemu yetu katika dunia. Kosa kubwa tunalolifanya ni KUTOJALI nguvu ya mtazamo na uwezo wake wa kukwamisha mawazo yetu hasa ya kile kinachowezekana katika maisha.

Pindi tunapoweka malengo ambayo yanaleta changamoto kwenye mfumo wetu wa imani au mtazamo, mara nyingi kuna uwezekano wa kushindwa na wakati huo huo tusijue ni kitu gani kimesababisha kushindwa.

Mfumo wetu wa kufikiri/imani hauna mantiki- mara nyingi ni kwamba, mfumo wetu huwa unapingana na mantiki na pia, huwa unatugeuka, hasa pale unapota mawazo ambayo yako nje ya mfumo wetu wa kufikiri au imani.

Ndiyo, maana mara nyingi huwa tunaweka malengo, lakini huwa tunajikuta tayari mwaka umepita bila kuwa tumefanya chochote na hakuna mabadiliko yoyote ya maana katika maisha!

Hatahivyo, bado tunayo nguvu na uwezo wa kubadilia LAKINI inahitajika HATUA mbili.
1. Fikiria kuanzisha utaratibu/mfumo mpya sasa hivi: Je utajisikiaje kuamka kila siku, huku ukijikita kwenye malengo uliyojiwekea hadi kuona matunda yake.

2. Chagua Kubadilika: Chagua kukabiliana na imani zote ziazokuzuia na ambazo zimekuwa zikikurudisha nyuma na ukashindwa kukidhi shauku na ndoto ulizokuwanazo. Usiangalie nyuma tena na kutamani vitu kuwa tofauti.

Chagua kubadilika na kuchukua hatua ili unachokitaka kiweze kutokea. Unayo nguvu na uwezo huo. Nakupa changamoto wewe kuacha kuishi kwa mbinu zile zile kila mwaka, badili mtazamo na leo upande mbegu ya mabadiliko.
 
Aksante kwa kusoma makala hii. Kama kawaida, ukiona thamani ndani ya makala za MAARIFA SHOP, tafadhari washirikishe rafiki zako wote na ukipenda nao wafaidi kama wewe wahimize kujiunga na mtandao huu kwa kubonyeza neno “KUJIUNGA”.
Kumbuka kuwa Mafanikio ni kitu cha kushirikishana ili kuleta maisha bora.

No comments: