Moja ya sababu kubwa inayofanya watu
wengi kushindwa kufikia ndoto za maisha wayatakayo ni kuishi kwenye jamii ambayo
imejaa watu wengi wenye mawazo ya Wastani
(watu wa kawaida), na watu hawa, kila mara wanakulazimisha uwe kama wao. Na kosa kubwa
unalolifanya au ambalo unatarajia kulifanya ni kuwa kama wao. Madhara ya kuwa
kama wao ni kwamba kila mara unapotaka kufanya kitu chochote kikubwa inabidi
upate ruhusa au ushauri kutoka kwao, ukifikia hatua hii basi ujue anayepanga
uishije ni wao na siyo wewe tena.
Kila unapofikiria kufanya kitu na mara
tu ukagundua kiko tofauti na wenzako, ghafla utapata washauri huria, ambao
hawakuwahi kuwazia au kufanya hicho kitu unachopanga kufanya. Watu hawa
watakwambia, hicho kitu hakijawahi kutokea na wewe utawezaje? Eti mtu
anakwambia husifanye jambo fulani kwasababu hakuna aliyewahi kufanya hivyo. Mtu
wa namna hii msikilize mpaka mwisho akimaliza muage na uondoke na kuanzia hapo
punguza mazoea naye. Kadili utakavyopunguza mahusiano/mazoe na watu hasa wenye
mawazo ya Wastani na hasi, ndivyo maisha yako yatakavyoanza kuboreka.
Jiulize ni mara ngapi umetamani kufanya
biashara lakini umeshindwa kwasababu watu wengi unaowajua walifanya biashara
wakashindwa? Kwahiyo, na wewe unaogopa hasara! Mara nyingi woga unaoupata unatokana
na kuzungukwa na watu wengi wenye mawazo ya Wastani (mawazo yanayofanana) na wengi
wao hufanya vitu vinavyofanana. Endapo huko katika hali hii ni wazi kwamba,
kila utakapo kuwa na ndoto ya kuwa na maisha ya tofauti na hao rafiki zako
waliokuzunguka, utapata majibu ya wewe huwezi!,
wakishakwambia hivyo, basi na wewe unapata hofu ya kushindwa ambayo huzaa woga
na mwisho unashindwa kuthubutu. Unapaswa kufahamu kuwa unapokutana na mtu na
ukamshirikisha ndoto yako akakwambia uwezi basi ujue yeye kwa nafsi yake ndiye
hawezi, hivyo jibu lake usilichukulie kama ndiyo jibu lako na usitumie majibu
yake kufanya maamuzi ya wewe kutokuanza kufanya mambo yanayokupeleka kwenye ndoto
ya maisha uyatakayo.
Watu wengi wanakwama kutimiza ndoto zao
kwasababu, walio wengi wanapenda kutazamia majibu kutoka kwa wengine, huku
wakisahau kuwa kila mmoja katika safari ya maisha anakuwa na mtihani wenye
maswali tofauti na ya mwingine. Kwahiyo, unapojaribu kutumia majibu ya maswali
ya mwingine kujibia maswali yako, basi ujue kuwa utashindwa tu! Cha muhimu hapa
ni kwamba tujitambue kuanzia leo kuwa kila mmoja ana maswali yake binafsi na
mwenye uwezo na ujuzi kuyapa majibu ya kweli ni wewe mwenyewe.
Kumbuka kuwa, ili mafanikio yoyote
yapatikane, yanaanza na fikra ambapo unahitaji kuanza kujifikilia na kujiona
wewe mwenyewe kama mafanikio. Kinachotakiwa ni wewe kufikiri na kutenda
kimyakimya bila kujali wengine wanakuonaje na mafanikio yakipatikana yatapiga
kelele ambazo kila mmoja atazisikia. Ukishafanikiwa, watu wataanza kushangaa na
wengi watadhani umefanikiwa siku hiyo, kumbe safari ulianza siku nyingi lakini
kwasababu ulikuwa unatekeleza ndoto yako Ndiyo maana walikuwa hawakuoni.
Kazi yako kubwa leo, ni wewe kuacha kuwa
mfungwa wa kundi hili la watu wenye mawazo ya wastani, na utambue kuwa
kulifanikisha hili, unahitaji kufanya maamuzi magumu na kuwa jasiri. Fanya vitu
ambavyo ni muhimu kwako siyo kwasababu kila mmoja anavifanya, na huu ndiyo utakuwa
mwanzo wa safari yako kuelekea kwenye mafanikio makubwa. Ili uweze kufanya
mambo ambayo ni muhimu kwako ni vizuri ukaongozwa na imani ya vitu viwili
ambavyo ni: maisha yatakuwa mazuri wakati ujao kuliko sasa na mimi nina uwezo
na nguvu wa kuweza kufikia maisha mazuri!
Mpendwa msomaji, endelea kuitumia vizuri MAARIFASHOP ili kujifunza mambo mbalimbali yatakayokuwezesha kupata mafanikio. Ili kupata makala mpya kila zinapochapishwa, bonyeza neno TUMA MAKALA MAARIFASHOP kisha sajiri barua pepe yako. Na kama unapenda kupata mafunzo ya kila siku kwa njia ya whatsap bonyeza neno MAFUNZO.