Ukitaka kujua kama umeanza mradi wa maisha unaoitwa “Fanya mwenyewe”
sikiliza watu wanasema nini kuhusu wewe, ukiona husemwi basi huenda bado
ujaanza mradi huu wa “Fanya mwenyewe” ambao unalipa sana, na yawezekana maisha yako
ya mwaka jana na ya mwaka huu yako sawa, ila tatizo kubwa linakuja kutushinda
ni katika kuwasikiliza watu, watu wengi tunapenda kusikiliza sauti za kusifiwa
tu basi, hii inatufanya kupenda kufanya vitu rahisi rahisi, wanavyopenda watu
wengine na sio tunavyopenda sisi, matokeo yake tumebakia kuwa na maisha magumu
na yakawaida wanayofurahia wengine maana tuwe sawa sote tubaki kulalamikia
serikali na mishahara midogo.
Unapoamua kuanza kutafuta mafanikio yako binafsi wakati mwingine unaweza
kufanya vitu vigumu, ambavyo wengine wanaona haviwezekani na huenda wengine
walishafanya wakashindwa, na huenda watu wengi hawapendi kufanya vitu hivyo
maana vinahitaji kujitoa kwa hali ya juu na kuwa makini, kinachotokea hapa
wanakuja kukukatisha tamaa, wanaanza kukupa maneno yao, hiyo huwezi, hiyo ngumu
hata fulani alifanya akashindwa, yani na wewe msomi mzima unafuga kuku.
Chakushangaza watakupa tu mifano ya wote walioshindwa na kwakuwa wao ufikiria
mambo hasi tu hata listi na rekodi ya waliofanikiwa hawana.
Muda mwingine unaweza kujiona kama umekosea kufanya unachokifanya maana
huenda kikawa kinaleta mafanikio baada ya muda mrefu lakiniwewe usijali maisha
ni kutembea hatua moja moja mbele bila kurudi nyuma, kwa maana kwamba wewe
unatakiwa uwaache waseme maana hawajui kilichoko moyoni mwako siku moja
watakuita shujaa pale tu kilichoko moyoni na akilini mwako kitakapoonekana
machoni mwao.
Wewe kama mtu ambaye umekwisha kujitambua unatakiwa kushika usukani wa
maisha yako mwenyewe na kuwaacha waseme, kwani watakuwa wanapoteza muda wao
bure, waache waseme kuwa wewe unapoteza pesa unazotoa kujifunza na kusoma
vitabu, waache waseme umeanza kuishiwa, waache waseme unafanya biashara ni
ngumu na utafirisika na kupoteza muda, hata kama kweli unapitia changamoto leo
maisha ni mdogo mdogo hizo changamoto huwa siyo za kudumu, maana ni za muda
mfupi. Kumbuka kuwa ka kupambana na changamoto, zinakufanya uwe shujaa, usiache
kwasababu wanasema,acha waseme na ukweli halisi wa mambo yote unao moyoni mwako
na wewe ndio unajua machungu ya ndoto zako.
Kwa hiyo hakikisha unafanya kazi kwa
bidii na maarifa utafanikiwa tu, cha msingi ni kupenda kufanya unachofanya na
ikiwa utajiingiza Katika mchakato eti wa kutafuta kazi inayokufaa itakuchukua
muda.
Mpendwa msomaji, endelea kuitumia vizuri MAARIFASHOP ili kujifunza mambo mbalimbali yatakayokuwezesha kupata mafanikio. Ili kupata makala mpya kila zinapochapishwa, bonyeza neno TUMA MAKALA MAARIFASHOP kisha sajiri barua pepe yako. Na kama unapenda kupata mafunzo ya kila siku kwa njia ya whatsap bonyeza neno MAFUNZO.
~TWENDE KAZI PAMOJA~
No comments:
Post a Comment