Wednesday, July 31, 2024

Biashara Ina Mshindani Hatari Huyu Hapa

 

“Miradi ya Biashara ni Viumbe Hai” ~ Cypridion Mushongi
Mwandishi wa vitabu anayejulikana kama 'Napoleon Hill' aliandika kwenye kitabu chake cha ‘THINK & GROW RICH’ kwamba “Mawazo ni vitu”. Ndiyo maana tunasema, miradi mingi ya biashara..

Tuesday, July 23, 2024

Kuna Uzuri Gani Katika Kushindwa?



Je, wewe ni kati ya wale wanaoshangaa kuona ‘kushindwa’ ni jambo zuri? Mmmh! Unaona kama utani hivi, Hapana! Siyo utani! Ni ukweli, watu wengi tunashindwa kila..

Thursday, July 11, 2024

Mikopo na Mifugo ni Marafiki Kwasababu Hii Hapa:


Mikopo ilianza zamani sana takribani miaka 3,000 iliyopita. Tangu kuanza kwa ustaarabu wa binadamu, mikopo imekuwepo katika sura mbalimbali kwa kipindi chote cha maisha ya binadamu. Historia ya ukopeshaji inatuonyesha kuwa..

Wednesday, July 3, 2024

Mjasiriamali Biashara yako Inakufa Kwasababu hizi

∞∞∞ "Ni bora kuishi na mtu aliyeshindwa kuliko mtu mwenye Mashaka ~ Cypridion Mushongi" ∞∞∞

Biashara ni mradi au mfumo unaotengenezwa na mjasiriamali kwa lengo la kuzalisha bidhaa au huduma inayokidhi mahitaji ya wanajamii (wateja) mbalimbali duniani. 

Wakati wote, biashara inapoendelea kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake, hapo tunasema kuwa “Biashara yako ni hai na inaishi”. Tunasema biashara “imekufa” endapo..

Sunday, January 7, 2024

Heri ya Mwaka Mpya Itapatikana Ukifanya Jambo Moja

“Kuipatia Dunia Kunalipa Kuliko Kuidai Dunia” ~ CYPRIDION MUSHONGI


Mwaka 2023 ulikuwa mwaka wa KUIDAI DUNIA kila kitu tulichokipenda. Hali hii imetokana na ukweli kwamba, kila binadamu anahakikisha anakuwa na maisha yenye Faraja – yaani maisha yenye kumpatia kila kitu anachohitaji.

Uhitaji wa maisha ya faraja, unaongozwa zaidi na matamanio au tamaa za kibinadamu, ambazo hazina ukomo. Tabia hii ya kupenda faraja, humfanya mtu..

Wednesday, March 1, 2023

UZIO WA MJI NANI ANAFUNGUA LANGO LAKE?

“Mahitaji ya lazima ni machache lakini vitu tunavyovitaka havina kikomo” ~ Cypridion Mushongi


Wengi tunafahamu nyumba nyingi zina uzio wa aina fulani na tumezoea kuona walinzi wakikaa langoni kwa lengo la kulinda usalama wa watu na mali. Anayekaa LANGONI ndiye anayeruhusu watu na vitu kuingia na kutoka.

Ukweli ni kwamba“Mji ni..

Tuesday, January 31, 2023

Elimu Rasmi Inatosheleza AJIRA Siyo KAZI ni Kweli?

“Kujiajiri na kuajiriwa yote ni AJIRA siyo KAZI”~ Cypridion Mushongi.


Kuna jitihada nyingi za kukuza elimu rasimi zinazowekwa na serikali pamoja na wadau wa maendeleo. 

Malengo hasa ni kuona watu wengi katika taifa wakipata elimu rasmi kwa matarajio ya..

Monday, January 16, 2023

Ujanja! Unajisikiaje Kuitwa Mjanja?

 

“Siku Rahisi Kuishi bila Ujanja Zimeisha” ~ Cypridion Mushongi





Hapa kwetu Tanzania neno “Ujanja” mara nyingi linatafsiriwa Zaidi kuwa ni ulaghai, uhuni au udanganyifu. Ni kawaida sana kusikia mtu akimsema mwenzake kuwa “yule bwana ni mjanja mjanja” usimuamini!

Watu wengi hawapendi kuitwa wajanja; eti kwasababu itaonekana kwamba wao siyo waaminifu machoni mwa umma.

Kwa taarifa yako “Ujanja” ni..

Sunday, January 8, 2023

Mpenzi wa Kutiwa Moyo Kuna Ujumbe Wako wa Mwaka Mpya



"Roho ya kujitegemea ni kinga dhidi ya wakatisha tamaa" ~ Cypridion Mushongi



Wakati huu tunapoanza mwaka mpya wa 2023, tukumbuke kuwa dunia ya sasa ina watu wengi wanaotukatisha tamaa kuliko wanaotutia moyo. Yawezekana wewe ni..

Wednesday, May 26, 2021

Kazi ya Kuzalisha Mali ni ya Nani?

 

“Kuajiriwa na kujiajiri yote ni AJIRA siyo KAZI” ~ CYPRIDION MUSHONGI

Kazi mojawapo ambayo tumekuja duniani kuifanya ni kuzalisha mali. Hii ni kazi muhimu sana ambayo inatakiwa kufanywa na kila mtu aliyefikia umri wa kujitegemea. Jambo la ajabu ni kwamba kazi hii wengi wanaikwepa, hasa wale tuliokaa darasani miaka mingi. Sababu za kukwepa jukumu hili ziko nyingi; moja ni..

Thursday, May 6, 2021

Roho ya Kujitegemea Iko Wapi? Itafutwe kwa Hali na Mali.

 “Haikugharimu chochote kujiunga na wengi, inakugharimu kila kitu kusimama peke yako” ~ CYPRIDION MUSHONGI


    Katika hali ya kibinadamu watu wote tunataka maisha mazuri. Maisha mazuri ni hali fulani ya kuishi, ambapo mtu binafsi anakidhi mahitaji yake na kuridhika na hiyo hali. Lakini, ukweli ni kwamba hali ya Maisha tunayoishi kwa kiasi kikubwa ni..

Saturday, May 1, 2021

KAZI Inaleta AJIRA na AJIRA Inamaliza KAZI ni Kweli?

"KAZI uzaa ajira lakini AJIRA haiwezi kuzaa kazi" ~ CYPRIDION MUSHONGI


    Mpaka sasa ajira bado ni tatizo kubwa kwa watu wengi hasa vijana nchini Tanzania na kwingineko duniani. Kukosekana kwa ajira kwa sehemu kubwa kunachangiwa na wadau wengi wa maendeleo kushindwa kubaini chimbuko halisi la ajira. Hali hii inafanya mikakati mingi ya kuongeza ajira kutofanikiwa. Wapo wngine wanaodhani suruhisho la ajira ni...

Thursday, December 31, 2020

Mwaka 2020 Unaisha leo Mwaka Mpya 2021 ni Kesho Unajisikiaje?

"Pale unapohisi ni mwisho mara nyingi ndio mwanzo wa kitu kipya" ~ CYPRIDION MUSHONGI


Napenda kutoa shukrani zangu kwako, hii ni kutokana na ukweli kwamba wewe binafsi umekuwa pamoja na mimi na MAARIFSHOP kwa ujumla. Hakika tumekua na kuishi kwenye jumuia moja kama siyo kabila moja linaloitwa..

Sunday, October 11, 2020

BIBLIA TAKATIFU-WEWE UNAPENDELEA KUSOMA VIFUNGU GANI JUU YA PESA?

 “Chanzo cha maovu duniani siyo pesa bali kukosa pesa mfukoni” ~ Cypridion Mushongi


Upatikanaji wa pesa kwa mtu yeyote unategemea sana imani na mtazamo wa mtu juu ya pesa.

Linapofika suala la pesa, watu tunagawanyika katika makundi makuu matatu; ambayo ni..

Monday, August 31, 2020

Pesa Yako ni Ishara ya Nini? Kama Unajua Usisome Hapa

 "Pesa ni Mwakilishi Shughulika na Anayewakilishwa" ~ CYPRIDION MUSHONGI



Pesa ni kitu gani mpaka karibu kila mtu anaitafuta? Kama pesa inatafutwa na kila mtu, lazima kujiuliza wapi hasa inapatikana. Je? Ni kweli wote tunafahamu sehemu au mahali inapopatikana? Kama mahali pesa ilipo hapajulikani tutawezaje kuipata? Maswali yote haya yanahitaji majibu kwanza kutoka kwa kila mmoja wetu ambaye anazitaka pesa kwa dhati.

Maswali yote haya pia ndiyo yanatoa

Tuesday, August 18, 2020

Biashara yako Inakuzwa na Mteja Yupi?

“Kama unawajali wateja wa zamani usihangaike kutafuta wateja wapya” ~ CYPRIDION MUSHONGI 



Nguzo muhimu katika biashara yoyote duniani ni wateja. Ninaweza kusema kwamba biashara inafanikishwa na watu wawili; yaani mfanyabiashara ambaye ndiye anauza bidhaa au huduma na wa pili ni mteja ambaye ananunua bidhaa. Kama unafanya biashara ambayo wateja wapo, tunasema biashara hiyo inalipa lakini kama wateja hawapo tunasema biashara yako hailipi. Kwahiyo, kuendelea kwa biashara yako ni

Tuesday, August 11, 2020

Ulimwengu Mpya wa Ajira Unamuhitaji Nani?


Ukosefu wa ajira ni miongoni mwa changamoto kubwa kwa jamii yetu na hasa vijana. Lakini pia, pamoja na kuwepo kwa changamoto hii, bado na wale wanaofanikiwa kupata ajira wanaipoteza muda mfupi. 

Pengine hali hii inatokana na ukweli kwamba tuko kwenye ulimwengu mpya wa ajira,

Tuesday, July 28, 2020

Faida ya Kufanyakazi Bure ni Hii Hapa

“Tembo pamoja na kuwa myama mkubwa hang’ati LAKINI mbu anang’ata”~ Darren Hardy

Unaanzaje kufanyakazi bure bila malipo yoyote?; katika hali ya sasa ambayo watu wengi tayali ni waumini wa mfumo wa pesa taslim au mfumo wa nipe nikupe. Hivi sasa watu wengi wanajitahidi kufanya vitu vitakavyowaletea pesa haraka (chapuchapu). Kiashiria mojawapo cha watu kupenda malipo ya chapuchapu ni

Monday, July 20, 2020

Motisha wa Kazi nani Anapaswa Kutoa?




Baada ya mapinduzi ya viwanda uko barani Ulaya mwishoni mwa karne ya 18, iliibuka na kujengeka dhana nzima ya kuajiriwa. 
Dhana hii ilikua kutokana na ukweli kwamba viwanda wakati huo vilihitaji sana nguvu kazi. Mabepari waliomiliki vitegauchumi walihitaji sana wafanyakazi, ili

Monday, July 13, 2020

Muda ni Wako Unaumiliki au Unakumiliki?


Nimesikia mara nyingi sana watu wakilalamika kuwa hawana muda. Kupitia malalamiko haya, nimejikuta nikijiuliza maswali mengi kama haya;”kwamba muda huwa unatoka wapi? Nani huwa anagawa muda? Nani ni mmiliki wa muda? Je mimi ndiye mmiliki wa muda? Au muda unanimiliki mimi. 

Katika kutafakari maswali yote haya nimegundua kwamba...